Pages

Tuesday, January 29, 2013

Acheni kutukwaza kwa mavazi - mchungaji

KANISA la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Morogoro, limewataka wanawake wanaokwenda kufunga ndoa katika kanisa hilo kuacha kuvaa mavazi yanayoonyesha maungo yao hususan matiti na migongo ili kuepuka kuwakwaza wachungaji.
Akihubiri wakati wa misa maalumu ya harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa hilo usharika wa Kilakala iliyoongozwa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, msaidizi wa Askofu katika dayosisi hiyo, George Pindua, alisema kuwa baadhi ya wanawake wanaokwenda kufunga ndoa huvaa nguo zisizo na heshima.

“Nyie wanaume ambao mmepanga kufunga ndoa na wake zenu hakikisheni mnawanunulia nguo zenye heshima, atakayekuja na nguo zinazoonyesha matiti au mgongo hatutamfungisha ndoa,’’ alisema.

Alisema kuwa kina mama wa kanisa hilo wanapaswa kuandaa vitenge vya kuwafunika wanawake wanaovaa nguo zisizo na maadili ili kuepusha kanisa kupata aibu.
Naye Askofu wa KKKT Dayosisi ya Morogoro, Jacob ole Mameo, alisema kuwa wamekuwa wakitoa mahubiri mema ili kuhakikisha waumini wao wanadumisha amani na utulivu.
Alisema kuwa taifa hili limejengwa katika misingi ya kudumisha amani na utulivu hivyo kila muumini anapaswa kuilinda isipotee.

No comments:

Post a Comment