Pages

Tuesday, January 29, 2013

Castle Lite yataja watakaomshuhudia Kanye West

WATANZANIA watatu waliobahatika kuhudhuria tamasha kubwa la muziki lijulikanalo kama ‘Feel the Beet of Sub Zero’ wamejulikana.

Tamasha hilo la kimataifa linaloandaliwa na kinywaji cha Castle Lite, linatarajiwa kufanyika Johannesburg, Afrika Kusini Februari 2, mwaka huu.
                                                   Kim-Kardashian na Kanye West
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa bia ya Castle Lite, inayozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Pamela Kikuli, alisema watu hao watalipiwa kila kitu, ikiwa ni pamoja na nauli ya kwenda na wenza wao watakaowachagua.

Pamela aliwataja washindi hao ambao walipatikana kupitia shindano lililokuwa likiendeshwa katika ukurasa wa Castle Lite kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook, kuwa ni Caroline, Edger na Eric.

“Hii ina maana kuwa Castle Lite itawalipia watu sita ikiwa ni gharama za kwenda huko, kwani tulisema kila mmoja atakwenda na rafiki yake atakayemchagua.
Tumefanya hivi ikiwa ni kurudisha fadhila kwa jamii, maana kwa kiasi kikubwa imetuunga mkono katika mambo mbalimbali,” alisema.
Tamasha hilo litapambwa na burudani kutoka kwa mwanamuziki maarufu, Kanye West.

No comments:

Post a Comment