Pages

Tuesday, January 29, 2013

Vodacom yaingia ubia na Fastjet

KAMPUNI ya mawasiliano ya simu za mikononi ya Vodacom Tanzania imeingia ubia na shirika la ndege la Fastjet ili wateja wanaosafiri na ndege hizo kuweza kulipia tiketi kupitia huduma ya M-pesa.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo jijini Dar es Saaam jana, meneja biashara wa Fastjet, Jean Uku, alisema kuwa ubia huo utaongeza ufanisi kwa kampuni hizo na wateja kupata unafuu wa kupata tiketi.

Alisema kuwa makubaliano hayo yamefikiwa kufuatia kampuni hizo kutambua umuhimu wa ongezeko la mahitaji ya usafiri katika bara la Afrika lenye idadi kubwa ya watu wanaokadiriwa kufikia bilioni moja.

Naye mkuu wa mawasiliano ya bidhaa na huduma za Vodacom, Kelvin Twissa, alisema kuwa wanajivunia kuwa suluhisho la mahitaji ya wateja wa masoko ya biashara mbalimbali nchini.
Twissa alisema kuwa kutokana na kuendelea kukua kwa huduma ya M-pesa tangu ilipoanzishwa mwaka 2008, Vodacom inajivunia kuwa wa kwanza nchini kuwezesha ulipiaji wa tiketi za mashirika ya ndege kwa njia ya haraka.

No comments:

Post a Comment