Pages

Friday, May 31, 2013

Sofapaka yazihofia Simba, Yanga.

UBORA wa klabu kongwe za Simba na Yanga, umeifanya timu ya Sofapaka kutoka Kenya kuleta kikosi chake chote ili kukabiliana nazo katika michezo ya kirafiki itakayopigwa hapa nchini.
                                                       Sofapaka kutoka Kenya.
Sofapaka inatarajiwa kutua nchini Juni 10 kwa ziara ya kimichezo, ikiwa na lengo la kuzipima klabu hizo kongwe zitakazokuwa katika maandalizi ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati maarufu kama Kombe la Kagame, itakayoanza kutimua vumbi Juni 18 hadi Julai 2, huko Sudan Kusini.

Akizungumza kwa simu kutoka Kenya, Meneja wa Sofapaka, Ngalambe Roberto, alisema kwamba hawana budi kuleta kikosi kamili ili kushinda michezo yake.

“Sisi tumejiandaa vizuri, tunazifahamu na kusoma kwenye mitandao kuhusu timu hizi, hivyo tutakuja na majeshi yote ili tushinde mechi zote mbili,” alisema Ngalambe.
Alisema Tanzania kuna timu nyingi nzuri zenye ushindani, lakini kwa Simba na Yanga ni zaidi, hasa kutokana na upinzani mkubwa uliopo kwa timu hizo mbili.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya Smartsports, iliyoandaa ziara hiyo, George Wakuganda, alisema Sofapaka itacheza mechi yake ya kwanza Juni 12 dhidi ya Simba, kabla ya Juni 13 kukwaana na Yanga. Mechi zote zitapigwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment