Pages

Saturday, September 14, 2013

YANGA KUIVAA MBEYA CITY

Wachezaji wa Young Africans wakiwa mazoezini katika uwanja wa Sokoine Mbeya
Ligi Kuu ya 



Vodacom itaendelea katika viwanja saba nchini huku mabingwa watetezi timu ya Young Africans ikishuka dimbani kucheza na wenyeji Mbeya City katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya.

Young Africans imefanya mazoezi ya mwisho leo jioni katika uwanja wa Sokoine ikiwa na wachezaji wake wote wakiwa katika hali nzuri kiafya, morali na ari ya juu kuweza kuibuka na ushindi katika mchezo huo.

Mara baada ya mazoezi hayo kocha mkuu Ernie Brandts amesema kikosi chake kipo katika hali nzuri na hakuna mchezaji hata mmoja majeruhi kuelekea kwenye mchezo huo ulioteka hisia nyingi za wakazi wa mkoa wa Mbeya.

Watoto wa jangwani watashuka dimbani kuhakikisha wanapata pointi 3 katika mchezo huo ili kujiweka katika mazunguri mazuri ya kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu.

Young Africans inashia nafasi ya pili katika msimamo baada ya kufikisha pointi 4 na mabao sita ya kufunga na mabao mawili ya kufungwa kufuatia ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya wauza mitumba wa Ilala Ashanti United na kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Coastal Union.
Kiingilio cha mchezo huo kitakua ni TSHS 5,000/=
Mchezo utaanza majira ya saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki na tiketi zitaanza kuuzwa saa 2 asubuhi katika vituo vifuatavyo: 

1.Mwanjelwa Sokoni, 2.Kabwe, 3.Mbalizi, 4.Stand Kuu, 5.Uyole, 6.Stopa Enterprises, 7.Holiday, 8.Iyunga, 9.Uhindini, 10.Sokoine

No comments:

Post a Comment