Pages

Saturday, April 12, 2014

MTOTO: LICHA YA ULEMAVU WANGU HUU, IPO SIKU TU NITAKUWA RAIS

“MATESO tumeumbiwa binadamu ila wakati mwingine unaweza kujiuliza kwanini matatizo yanamkumba hata mtu usiyetarajia kutokana na udogo wake,” ndivyo anavyosimulia Roswita Mhagama (48) mkazi wa Kibamba jijini Dar es Salaam.
Mwanamke huyo ni mama mzazi wa mtoto Aloyce Mhagama (6) ambaye alizaliwa Mrimba mkoani  Morogoro akiwa na ulemavu wa miguu na mkono.
KISA KAMILI
Mtoto Aloyce Mhagamaakiwa na mama yake mzazi aliyejulikana kwa jina la Roswita Mhagama
Mama Alo alisema kuwa, alipomzaa mtoto huyo mwaka 2008, baba mzazi alimkataa akidai  hayupo tayari kulea mtoto wa ajabu kutokana ulemavu huo.
“Mbali na baba yake, hata majirani wakati wa uchanga wa Aloyce, walimfananisha mtoto wangu na chura. Eti kwa sababu mguu mmoja umepinda, mwingine kipisi na mkono mmoja pia kipisi,” alisema mwanamke huyo.
Alisema kufuatia hali hiyo, mwaka 2010 aliamua kuhama Mrimba na kufika jijini Dar kuangalia jinsi gani angeweza kuishi na mtoto wake akiwa katika ulemavu huo.
“Riziki ni popote japo unafuu ninaoupata sasa hivi ni tofauti sana na nilipokuwa Mrimba lakini bado matatizo yapo. Mrimba jamii ilinitenga, Dar sivyo. Pengine ni kutokana na wakazi wake kuwa na uelewa mpana juu ya ulemavu,” alisema mwanamke huyo.

Akaendelea: “Maisha yangu kwa hapa nategemea zaidi kudura za Mwenyezi Mungu, leo ikipita kesho itajijua yenyewe.
“Kuna msamaria mwema mmoja alijitolea kuomsomesha mwanangu kwenye Shule ya Chekechea ya Saint Bernard, Kibamba (Dar) na alinilipia pango la nyumba, lakini sijui kama atanendelea maana
 pango linaisha mwezi huu wa nne na alionesha kukwama kwa kusema hana pesa ndiyo maana nimekuwa na wasiwasi.
ALOYCE AKITAKA KWENDA CHOONI
Mama Aloyce aliendelea kusema kuwa, mazingira anayoshi pia si rafiki kwa mwanaye kwa vile mvua ikinyesha maji machafu hutoka chooni na kusambaa hivyo kumsababishia mwanaye kuwa na homa za mara kwa mara kwa sababu ya kushika maji machafu.
KUHUSU WATANZANIA
Mama Aloyce alisema anawaomba Watanzania wamsaidie mtoto wake aweze kuendelea na shule, pia akaomba asaidiwe sehemu ya kuishi.
Kwa upande wake Aloyce alipozugumza na gazeti hili alisema anapenda sana kusoma na akiwa mkubwa ndoto zake ni kuwa rais ili aweze kuwakomboa watoto wanaoishi  katika mazingira magumu.
Mtoto Aloyce: “Pamoja na ulemavu wangu huu lakini nina imani kwamba iko siku nitakuwa rais, nitasoma sana, nitakuwa mwanasiasa mpaka nitafikia malengo hayo na ikitokea hivyo nitawasaidia zaidi watoto wanaoishi katika mazingira magumu.”
Kwa wale walioguswa kumsaidia mtoto huyu, wanaweza kutuma pesa kwa namba: 0713 612533. Kutoa ni moyo!

No comments:

Post a Comment