Mwanamke huyo ni mama mzazi wa mtoto Aloyce Mhagama (6) ambaye alizaliwa Mrimba mkoani Morogoro akiwa na ulemavu wa miguu na mkono.
KISA KAMILI
Mama Alo alisema kuwa, alipomzaa mtoto huyo mwaka 2008, baba mzazi alimkataa akidai hayupo tayari kulea mtoto wa ajabu kutokana ulemavu huo.
“Mbali na baba yake, hata majirani wakati wa uchanga wa Aloyce, walimfananisha mtoto wangu na chura. Eti kwa sababu mguu mmoja umepinda, mwingine kipisi na mkono mmoja pia kipisi,” alisema mwanamke huyo.
“Riziki ni popote japo unafuu ninaoupata sasa hivi ni tofauti sana na nilipokuwa Mrimba lakini bado matatizo yapo. Mrimba jamii ilinitenga, Dar sivyo. Pengine ni kutokana na wakazi wake kuwa na uelewa mpana juu ya ulemavu,” alisema mwanamke huyo.
Akaendelea: “Maisha yangu kwa hapa nategemea zaidi kudura za Mwenyezi Mungu, leo ikipita kesho itajijua yenyewe.
pango linaisha mwezi huu wa nne na alionesha kukwama kwa kusema hana pesa ndiyo maana nimekuwa na wasiwasi.
ALOYCE AKITAKA KWENDA CHOONI
Mama Aloyce aliendelea kusema kuwa, mazingira anayoshi pia si rafiki kwa mwanaye kwa vile mvua ikinyesha maji machafu hutoka chooni na kusambaa hivyo kumsababishia mwanaye kuwa na homa za mara kwa mara kwa sababu ya kushika maji machafu.
Mama Aloyce alisema anawaomba Watanzania wamsaidie mtoto wake aweze kuendelea na shule, pia akaomba asaidiwe sehemu ya kuishi.
Kwa upande wake Aloyce alipozugumza na gazeti hili alisema anapenda sana kusoma na akiwa mkubwa ndoto zake ni kuwa rais ili aweze kuwakomboa watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Mtoto Aloyce: “Pamoja na ulemavu wangu huu lakini nina imani kwamba iko siku nitakuwa rais, nitasoma sana, nitakuwa mwanasiasa mpaka nitafikia malengo hayo na ikitokea hivyo nitawasaidia zaidi watoto wanaoishi katika mazingira magumu.”
No comments:
Post a Comment