MWANAMUZIKI Stara Thomas juzikati aliwaacha watu hoi kwa kicheko pale alipoamua kumkatikia mauno Mzee Chillo walipokuwa wakicheza muziki.
Tukio hilo lililonogesha shughuli lilijiri kwenye uzinduzi wa kitabu
cha marehemu Steven Kanumba kilichopewa jina la The Great Fallen Tree
uliofanyika ndani ya Hoteli ya Landmark, Ubungo jijini Dar.
Ilikuwa hivi; wakati wa kucheza muziki, kila mmoja alimvutia karibu
yule aliyemvutia ambapo Stara aliamua kujongea kwa Mzee Chillo kisha
kuanza kucheza taratibu lakini kadiri mambo yalivyonoga, mwanamama huyo
alionesha umahiri wake wa kukata mauno na kumuacha mwezake akiangua
kicheko.
No comments:
Post a Comment