Pages

Tuesday, April 21, 2015

WAKALA WA YAYA TOURE AIPIGA MKWARA MANCHESTER CITY

Wakala wa kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast, Yaya Toure amewaambia Manchester City kwamba kama hawana mpango na mteja wake waweke wazi kwani tayari kuna klabu mbili zinamtaka. "Kama City inataka Yaya aondoke ijitokeze na kusema. Klabu mbili kubwa tayari zimeniulizia kama anapatikana, na najua kwamba kama City watasema watamuuza, klabu nyingine 10 zitanipigia ndani ya saa 24.
 

“Kama City wana hofu na fedha zao basi wanaweza kuzitunza kwenye pochi yao, kwa sababu najua kwamba timu nyingine zinaweza kumlipa Yaya kile anachopata sasa,” alisema wakala huyo, Dimitri Seluk. Hata hivyo, Yaya akizungumza na gazeti la Evening News baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya West Ham mwishoni mwa wiki, alisema anaumizwa na shutuma juu ya kiwango chake msimu huu, lakini ataendelea kupigana hadi mwisho na anapenda kuichezea Man City.

No comments:

Post a Comment