MTANGAZAJI kinara wa vipindi vya muziki wa kiafrika, Ben Kinyaiya leo usiku anatarajiwa kufanya kipindi chake cha kwanza kupitia kituo cha Clouds TValichojiunga nacho hivi karibuni.
Ben ameiambia www.saluti.com kuwa ataonekana kuanzia saa 2.05 usiku kupitia kipindi cha saa nzima cha Mamaland ambacho amesema amekifanyia mageuzi makubwa kwa kuongeza vionjo na vipengele (segment) vipya.

Kinyaia amewataka wapenzi wake na watazamaji wote kwa ujumla wategemee mambo mazuri. “Kwenye muziki wa kiafrika huwa sibahatishi” alisema mtangazaji huyo aliyewahi kuvitumikia vituo vya Channel 5 na TBC1.
Kwa ujio huo wa Kinyaiya katika Clouds TV kunaashiria mwisho wa kipindi cha Ben & Mai kilichokuwa kinarushwa na TBC1 chini ya Ben Kinyaiya na Maimatha.
Kinyaiya amesema umoja wake na Maimatha uliokuwepo tangu walipokuwa Channel 5 umefikia kikomo kwa nia njema kabisa bila mtafaruku wala mgongano.
“Tulikuwa katika mapumziko ya kujiandaa na season ya 3 lakini nikapata ofa kutoka Clouds TV, ofa ambayo nilishindwa kuikataa nkashauriana na Mai na hatimaye tukakubaliana kutofautiana” alisema Ben na kuongeza kuwa yeye na Mai bado wataendelea kushirikiana na kutegemeana kwa njia moja au nyingine.
Chanzo cha habari ni SALUTI5 (www.saluti5.com)
No comments:
Post a Comment