EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA
Showing posts with label Mahusiano. Show all posts
Showing posts with label Mahusiano. Show all posts

Monday, July 6, 2015

MMEACHANA? HAKUNA SABABU YA KUCHUKIANA!

Mpenzi msomaji wa XXLove karibu kwenye Jumatatu nyingine mwanana katika ulimwengu wa uhusiano wa kimapenzi.Katika mada yetu tajwa hapo juu, nitazungumza na wale rakifi zangu walioachana au kuachwa na kuanza kumchukia mwenza wake.
Ni kweli kuachwa kunaumiza sana moyo. Kimsingi usiombe kukumbwa na maumivu ya kuachwa. Lakini kama hilo limekwishatokea, kwa nini uendelee kuumia na kumchukia aliyekuwa mpenzi wako?
Kitendo cha kukuacha wewe, kinaweza kumtokea hata yeye na kujikuta akilia na kuhuzunika kama wewe. Kama ndivyo basi mapenzi ndivyo yalivyo. Leo kwako, kesho kwake.
Hakuna sababu ya kuchukiana na kuwekeana visasi kwa sababu kama tutafanya hivyo, kwa dunia ya sasa iliyojaa uchepukaji, itakuwa dunia ya visasi kila kukicha.

Tuesday, May 26, 2015

‘NIMEKUMISS’ YA MWANAMKE, ‘NIMEKUMISS’ YA MWANAUME, TOFAUTI

NIJumanne tena! Tunakutana katika mada hii ya maisha na mapenzi. Ni somo ambalo litaweza kukusaidia katika kubadilika hususan kama wewe ni mwanandoa au upo katika uhusiano!
Leo katika makala haya nazungumzia neno maalum kabisa katika uhusiano linaloitwa miss! Miss yaani kosa, pia ‘kosana’ hutumiwa zaidi na watu wenye uhusiano wowote ule, iwe ndugu, wapenzi na hata marafiki walioshibana.
MATUMIZI YAKE
Ni neno la Kiingereza ambapo watumiaji wanapaswa kuwa Waingereza wenyewe lakini pia wasio Waingereza ambao wanajua maana yake.
Hutumika kwa watu waliopotezana kwa muda ambao mhusika amehisi kumkumbuka mwenzake kwa maana ya kuonana naye laivu.
“Shoga, upo?”
“Nipo shoga yangu, niambie, mzima?”
“Mi mzima tu, nimekumisi ‘miss’ ile mbaya.”
“Nimekumisi pia shoga yangu.”
Maneno hayo ni watu wawili walioshibana ambapo wamepotezana au hawajaonana kwa siku kadhaa. Idadi ya siku za ‘kumisiana’ hutegemea mtu na mtu na si kwamba ni kiwango cha kimataifa kuwa lazima ziwe siku mia moja!

Wednesday, May 13, 2015

ZIJUE SABABU ZA WANAUME KUCHEPUKA!

Mambo vipi msomaji wa safu hii. Bila shaka unaendelea vizuri na harakati zako za kimapenzi na kwa mara nyingine upo tena katika safu hii ili kufuatilia nini kimejiri.
Moja ya tatizo kubwa kabisa linalowasumbua wapenzi wengi ni tabia ya kutoaminiana baina yao. Kila mmoja hudhani mwenzake anakwenda kinyume na hili, mara nyingi lawama huenda zaidi kwa wanaume kwani ni wepesi kuchepuka.
Zifuatazo ni baadhi ya sababu zinazosababisha wanaume kutoka nje ya uhusiano wao wa kimapenzi.

Thursday, March 19, 2015

KAMA MKE NA MUME WANAPIGANA PICHA ZA UTUPU, WAPENZI JE?

Mapenzi ya sasa yamejaa sarakasi nyingi sana, kwa yule aliyebahatika kuingia kwenye uhusiano anatakiwa kuwa makini kuhakikisha mapenzi hayamtibulii maisha yake.Yapo mambo mengi ya kuwa nayo makini, changamoto kubwa na ya msingi ambayo wengi tunakumbana nayo ni uhakika kama kweli wanaodai wanatupenda wanamaanisha au wana zuga?Kwamba yule anayesema anakupenda ukimpasua kwenye moyo wake wewe utakuwa ndiye uliyechukua nafasi? Wengi wamebaki njia panda wanapofikiria hilo.Mbali na changamoto hiyo, pia wengi hufikiria namna ya kulinda penzi lisife. Wapo waliotokea kupendana sana lakini wakaishia njiani kwa kuachana.
Lakini pia wapo ambao mpaka leo hii wanajiuliza kama waliotokea kuwapenda wana nia njema? Kwamba anayekuambia anakupenda na anatamani siku moja uwe mwenza wake anamaanisha kweli au ana lake kichwani?
Kama ulikuwa hujui ni kwamba, wapo wanaume ambao wamejiwekea malengo ya kutembea na idadi flani ya wanawake kwa kipindi flani. Kwa hiyo wewe unayo changamoto ya kubaini kama huyo uliye naye siyo kati yao!

Wednesday, February 25, 2015

STRESS HAZIPUNGUZWI KWA KUCHEPUKA!

LABDA haijawahi kukukuta, lakini maisha tunayoishi katika wakati wa sasa yanasababisha watu wengi wanapatwa na msongo wa mawazo, maarufu kama stress. Hali ni mbaya kwa wafanyakazi wenye mabosi wakorofi na hata wafanyabiashara wanaoyumba kiuchumi.
Lakini inakuwa mbaya zaidi mambo yanapoharibika ndani ya familia, kwa maana ya wanandoa au walio katika uhusiano wa kimapenzi. Ingawa sina takwimu kamili, lakini uzoefu unaonyesha tafrani katika ndoa zinasababisha watu wengi sana kuchanganyikiwa na hata kusababisha kukosa amani ndani ya mioyo yao.
Na siyo kukosa amani na kuchanganyikiwa tu, wengi pia wamepoteza maisha baada ya kushindwa kuhimili mikanganyiko iliyotokea. Mtu anaona mwenzake anakwenda ndivyo sivyo katika uhusiano wake anaamua kujimaliza mwenyewe, achilia mbali wanaoamua kujimaliza wote ili kila mmoja akose.

Thursday, January 22, 2015

MWANAMKE HANA JEURI YA KUMKATALIA MPENZI WAKE KUPIGA PICHA ZA UTUPU- JULIANA KANYOMOZI

Muimbaji wa Uganda, Juliana Kanyomozi amefunguka kwa urefu kuhusiana na masuala mbalimbali kwenye mahojiano aliyofanyiwa na mtandao wa SatisfashionUG.
 
Miongoni mwa mambo aliyohojiwa ni pamoja na kuvuja kwa picha za utupu za muimbaji mwenzie wa Uganda, Desire Luzinda. “Kwanza kabisa katika kesi nyingi kamwe huwa sio kosa la mwanamke,”anasema Juliana.
“Kama wewe ni mtu mzima na umempenda mtu unajua kuwa hakuna kikomo cha kipi kitatokea kwenye chumba binafsi cha watu wazima wawili. Kama hautaenda mbali zaidi kumfurahisha mwanaume wako, atakuacha na kisha utahukumiwa kwa hilo,” aliongeza.


Monday, January 19, 2015

KABULA AJUTA KUMPENDA BUSHOKE

Stori: Gladness Mallya/Ijumaa Wikienda
BAADA ya hivi karibuni kumwagana na aliyekuwa mpenzi wake wa muda mrefu, Maximilian Bushoke, msanii wa filamu Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ amefunguka kwamba hahitaji tena mwanaume kwa sasa.
Msanii wa filamu Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ akipozi.
Akipiga stori na paparazi wetu, Jini Kabula alisema kutokana na kwamba alikaa kwenye uhusiano wa kimapenzi muda mrefu na Bushoke na hakuona faida yoyote, anaujutia muda wake na sasa ameamua kuachana na masuala ya mapenzi na amejikita kwenye kazi zaidi.

NI LAZIMA MUACHANE KWA UGOMVI?

Nianze kwa kumshukuru Maulana kwa kunijalia kuiona siku hii ya leo nikiwa mzima wa afya. Ni matumaini yangu kwamba na wewe msomaji wangu uko poa kabisa, karibu jamvini tubadilishane mawazo na kujadili mambo mbalimbali yanayohusu uhusiano wa kimapenzi.
Imewahi kukutokea kwamba licha ya kuwahi kumpenda au kupendana na mtu fulani, imefika hatua mambo yote hayawezi kuendelea tena, moyo umekinai, hisia zimekufa na jambo pekee unalotaka litokee ni wewe na mwenzi wako kuachana?

Saturday, January 17, 2015

SHABIKI ZARI KUWA NA UJAUZITO, INA MAANA DIAMOND NA ZARI WALIFANYA NGONO BILA KINGA,WALIPIMA NA WALIJUANA KWA MUDA GANI ?

zari 56

Kupitia info za mashabiki wa sammisago.com, Shabiki wa Diamond ametuma mtazamo wake kuhusu issue ya Diamond na Zari kutegemea mtoto na kusema.
 
Sijawahi kuona mastaa hawa wakiwa hospitalini au kwenye kituo chochote wakipima afya zao, ukizingatia ni watu wakuweka hadharani mambo yao yote basi hata kupima wangeweka instagram au huko twitter

Ni vizuri staa kuzaa na staa mwenzake ila Diamond ana muda wa kuwa baba? mahusiano yake mengi ni kiki au drama a,bazo hata Kwa Zari tuliyedhani itakuwa tofauti kumbe ni yale yale, mimi ni shabiki tu ila nawatakia kila la heri kwenye familia yao wanayoanzisha
Shabiki alimaliza hivyo.Upi mtazamo wa juu comment za huyu shabiki ?

Wednesday, January 14, 2015

JIFUNGIENI, ELEZANENI!

KUNA msanii mmoja wa muziki wa kizazi kipya nchini anaitwa Rich Mavoko. Sijamfuatilia sana, lakini nyimbo chache alizoimba, zina ujumbe unaopaswa kupongezwa.
Kuna kibao chake kimoja kinasema Roho Yangu. Kwa sisi wapenzi wa Bongo Fleva, huu ni moja kati ya tunzi zenye kuelimisha, achilia mbali burudani nzuri inayopatikana ndani yake. Katika mstari mmoja miongoni mwa versi, unasema ‘Ukiwa mjanja kuchapiwa ni siri ya ndani.’

Thursday, January 1, 2015

USIWE MBULULA, UNA HAKI YA KUPENDA ILA ‘USIFOSI’ MAPENZI!

Awali ya yote nimshukuru Mungu kwa kunifanya kuwa miongoni mwa wale waliouona mwaka wa 2015 wakiwa wazima. Hili ni jambo la kumshukuru sana Mungu kwani najua wapo waliotamani kuuona mwaka huu wakiwa wazima lakini leo hii wameshatangulia mbele za haki huku wengine wakiwa hoi kwa magonjwa.
Kikubwa ni mimi na wewe ambao tumepata neema hii kuendelea kufanya yale yanayompendezesha Mungu na kuachana na yale yanayomchukiza. Kwa kufanya hivyo mwaka huu utakuwa ni wa furaha kwetu na hata kama mapenzi yamekuwa yakituliza kwa mwaka uliopita, tutafurahia maisha kama wengine.

Thursday, October 30, 2014

SIYO DHAMBI KUMPENDA MPENZI WA MWENZAKO ILA FANYA HIVI…

Utafiti ambao umefanyika unaonesha kuwa, asilimia kubwa wapo kwenye uhusiano na watu ambao siyo waliopangiwa na Mungu kuwa nao.Kutokana na hilo ndiyo maana utakubaliana na mimi kwamba, usaliti umekuwa ukishamiri, watu wamekuwa wakiachana kila siku na wengine kuendelea kuishi pamoja lakini si kwa amani.
Hii ni kwa sababu wameingia kwenye penzi na watu ambao si sahihi. Kutokana na mazingira hayo, haiwezi kuwa kitu cha ajabu mume wa mtu kutokea kumpenda sana mke wa mtu au kinyume chake.
Pia huwezi kuonekana mwendawazimu kwa kumpenda mtu ambaye tayari ana mpenzi wake. Hii ni kwa sababu inawezekana una mapenzi ya kweli zaidi kwake kuliko huyo aliye naye. Hata hivyo, hakuna kitu kibaya kama kuanzisha uhusiano na mtu ambaye tayari ana mpenzi wake au ameshaingia kwenye ndoa. Utakuwa unatafuta matatizo kama utamtongoza mke wa mtu au utaonesha kumzimikia mume wa mtu na kujikuta ukishawishika kutaka kumpasulia ukweli.

Wednesday, October 22, 2014

WEWE SIYO MZURI? NANI KAKUDANGANYA!

BINADAMU tumeumbwa kwa namna tofauti sana, ingawa kibaolojia, wote tuko sawa, bila kujali kama ni Wahindi, Waarabu, Wazungu, Waafrika, Wachina na makabila yote, siyo warefu, wafupi, wembamba wala wanene.
Tunatofautiana akili, uwezo wa kuelewa, uwezo wa kukabili changamoto na hata jinsi ya kuishi kwenye jamii inayotuzunguka. Kuna watu wengine hawaamini kama wao wako vile walivyo kwa sababu yao wenyewe, bali wanamsingizia Mungu.

Sunday, October 12, 2014

Duh, Aamua kujiua kisa kamfumania mpenzi wake akiwa na mwanaume mwingine

Mapenzi hatare sana!hayana cha wewe mzuri,au una cheo,au una pesa,ama hauna...yaani yakikukamata utajuta so mtu akifikiaga maamuzi ya hivi usimcheke kabisa!!....sawa na kumtukana mamba huku mto bado hujavuka Huyu ni mwanafunzi aliefahamika kwa jina moja la Moza alie mwaka wa kwanza katika chuo cha Uhasibu TIA Mkoani Singida amenusurika kufa baada ya jaribio la kutaka kujiua kwa kujichoma na kisu kushindikana,tukio hilo limetokea jana baada mwanafunzi huyo kumfumania mpenzi wake wa kiume akiwa na mwanamke mwingine.....sasa ni hivi huyu mwanafunzi akitoka hospt unaweza kumshauri vipi ili asirudie kufanya kitendo hicho??maana huwezi kujua labda bado anayo dhamira ya kujimalizia......ila wanaume mnapata dhambi sana kwa Mungu dah!hivi mwanaume akiwa na mwanamke mmoja itakuwaje??au ataonekana mshamba??....yaani tangu jana niliwaza hili tukio mpk basi...dwah ngachoka mie!!

Thursday, September 11, 2014

DIVA: ZITTO NI MUME WANGU


Na Shakoor Jongo MTANGAZAJI wa Kipindi cha Ala za Roho kinachorushwa kupitia Radio Clouds FM ya jijini Dar, Loveness Malinzi ‘Diva’ kwa mara ya kwanza, amejilipua kuzungumzia uhusiano wake na Zitto Kabwe kwamba walikuwa mke na mume.
Mtangazaji wa Kipindi cha Ala za Roho, Loveness Malinzi ‘Diva’ akipozi.
Katika mahojiano maalum na mwanahabari wetu jijini Dar juzi, Diva alisema anashangazwa na baadhi ya vyombo vya habari (siyo vya Global Publishers) kumnyima uhuru wa kuongelea suala lake na ‘zilipendwa’ wake huyo wakati kisheria yeye ni mke wake hivyo anapaswa kuzungumzia kutengana kwao.
MSIKIE DIVA
“Ninyi mnayaongelea mambo ya Zitto na mimi juu kwa juu tu hamjui kama mimi nimeishi naye kama mke na mume nyumbani kwake Masaki (Dar), sasa nini kilisababisha penzi letu kuvunjika watu hawajui, nina ushahidi wa kutosha lakini wanaongeaongea tu,” alisema Diva.Akaongeza: “Sasa ninavyojua mimi kwa sheria za nchi, mwanamke na mwanaume wakiishi pamoja kwa zaidi ya miezi sita tayari ni mke na mume. Hawezi kuniacha kirahisirahisi tu.”

Wednesday, September 10, 2014

UKIFANYA KAMA HUJALI, HUTASUMBUKA!

KUNA kelele nyingi sana kutoka kwa akina mama, wakilia kutendwa na wenza wao. Nimewahi kukutana nao wengi sana, wakilalamika na ukijaribu tu kuwagusia kuhusu nia yako ya kutaka urafiki nao, utawasikia: “Weee, tena sitaki hata kumsikia mtu anaitwa mwanaume.”
Na unapotaka kujua kulikoni, atakupa simulizi ndefu juu ya uhusiano wake wa kimapenzi ulivyokatishwa ghafla na mwenza wake kutokana na sababu mbalimbali, lakini kubwa huwa ni kukosa uaminifu.
Ninataka kuwapa siri, siyo tu wanawake, bali hata wanaume.Wakati mwingine tunajiumiza mioyo yetu sisi wenyewe, kwa sababu tunatumia muda mwingi kujipa mawazo ambayo yanatuondolea furaha tunayopaswa kuwa nayo kwa muda mwingi.
Kufikiri sana kuhusu mwenza wako ni ugonjwa ambao mwenye uwezo wa kuutibu siyo mwingine zaidi yako. Na ugonjwa huo unatokana na kosa ambalo wewe ulilifanya siku ile ya kwanza ulipoamua kuanzisha uhusiano wa kimapenzi naye.

Thursday, September 4, 2014

YANAYOWEZA KUMFANYA MPENZI WAKO AKATEMBEA NA RAFIKI YAKO!


Ni wiki nyingine tulivu kabisa tunakutana tena kupitia safu hii nikiamini umzima bukheri wa afya na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku kama kawaida.
Mimi namshukuru Muumba wa mbingu na ardhi kwa kuniwezesha kutimiza majukumu yangu ya kila siku likiwemo hili la kuelimishana na kukumbushana juu ya mambo yanayogusa maisha yetu ya kimapenzi.
Mpenzi msomaji wangu, wiki iliyopita nilikuwa na kazi kubwa ya kumshauri rafiki yangu ambaye aliniletea mashitaka ya mpenzi wake kutembea na rafiki yake.

Nilipata wakati mgumu sana kwani nilipoongea na msichana akaniambia wazi kwamba, amekuwa hapati penzi alilotarajia kutoka kwa rafiki yangu.

Monday, August 11, 2014

KWA NINI MAPENZI NI ASALI, VILEVILE NI SHUBIRI?


Kwa nini mapenzi ni tata? Unaweza kujiuliza swali hilo. Ni kwa faida ya kila mmoja kwa sababu yanamhusu kila mmoja wetu. Ni matamu lakini ndani yake hutokea kuwa na ukakasi kama siyo maumivu.Jiulize tena, kwa nini mapenzi yanasumbua? Mapenzi ni maumivu ya kichwa na moyo. Watu wengi waliomo ndani yake wanaweza kukupa ushuhuda wa mateso wanayoyapata kwenye uhusiano wao. Je, baada ya kuteseka huwa wanajiapiza kutorudi tena?
La hasha! Wanajaribu mara nyingi, hawakomi. Unaweza kujiuliza ni kwa nini lakini ukweli ni kwamba pamoja na maumivu ambayo mtu anaweza kuyapata kwenye mapenzi, bado yanabeba hisia kubwa kabisa katika maisha ya kila binadamu.

Thursday, March 20, 2014

KILA SAA MAPENZI…MAPENZI…HIVI HAMNA MENGINE YA KUFANYA?

Mpenzi msomaji wangu, wiki iliyopita utakumbuka nilizungumzia suala la kuwajali wapenzi wetu. Niligusia suala ya kuwapa nafasi watuchune.
 
apo walioshituka kuona kichwa kile cha habari lakini kiukweli sikumaanisha kuchuna kule ambako wanawake micharuko hufanya hasa kwa waume za watu, nilimaanisha utayari wa kila mmoja kumsaidia mwenzake kifedha. Mkeo akitaka pesa ili aende saluni kama zipo, mpe! Akihitaji pesa akanunulie vipodozi na nguo kama pesa zipo, mpatie.

Tusibaniane pale ambapo Mungu ametujaalia uwezo wa kuwafanya wenza wetu waonekane watu mbele ya wenzao. Hili ni kwa mke na mume na hata wapenzi wa kawaida. Baada ya kugusia hayo, nigeukie sasa kwenye mada yangu ya wiki hii.

Ndugu zangu, nimekuwa nikipokea malalamiko mengi kutoka kwa baadhi ya wanawake wakielezea kukerwa kwao na tabia za waume zao kuendekeza sana tendo la ndoa. Wanaume wanaoweka mbele suala hili husimamia kwenye ile pointi kwamba, kufanya mapenzi na wake zao kila wanapojisikia ni haki yao ya ndoa.

Saturday, February 8, 2014

VALENTINE’S DAY ISIWE CHANZO CHA MAUMIVU YA MOYO!

BADO siku tisa tu kuifikia Sikukuu ya Wapendanao ambayo hujulikana zaidi kama Valentine’s Day. Kila mwaka huadhimishwa Februari 14, duniani kote.
Umejiandaaje kwa ajili ya siku hiyo? Je, kwako  itakuwa siku ya furaha au chanzo cha mateso kwako na kwa mwenzi wako? Unadhani unatakiwa kufanya nini ili kuifanya siku hiyo kuwa nzuri kwako?
Yapo mengi ya kufanya, lakini kabla ya kuingia huko tuone kwanza maana yake, japo kwa kifupi sana. Marafiki, kuna watu mpaka leo hawafahamu chimbuko na maana halisi ya siku hiyo muhimu. Hapa kwenye All About Love ni mahali sahihi zaidi pa kupata elimu hiyo.
Nini maana yake?
Asili hasa ya siku hiyo ni Roma.
Inaelezwa siku hiyo huadhimishwa kama kumbukumbu ya Padre Valentino ambaye aliuawa na Utawala wa Kirumi uliokuwa chini ya Mfalme Claudia kwa kosa la kutetea waumini wake wafunge ndoa.

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate