EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA
Showing posts with label Saikolojia. Show all posts
Showing posts with label Saikolojia. Show all posts

Saturday, February 1, 2014

MADENTI, PICHA ZA UTUPU ZA NINI?


Niwape hi kwa furaha sana wapendwa wasomaji wa safu hii, ingawa zaidi ningependa ziwafikie wanafunzi popote pale gazeti hili linaposomwa. Hawa jamaa ni wadau wangu wakubwa sana, hasa katika kubadilishana mawazo inapobidi.

Juzi nilikuwa naperuziperuzi kwenye mtandao, mara nikakutana na picha za aibu zilizopigwa na msichana ambaye ametambulishwa kama ni mwanafunzi, haikuelezwa kama ni denti wa sekondari au vyuo, lakini kwa uzoefu, inaonekana kabinti ni ka sekondari!

Nilipoziona, zikanikumbusha miaka kadhaa nyuma, kama minne au mitano hivi, wakati picha za msichana mmoja, aliyekuwa amevalia fulana zinazotumiwa na shule moja ya sekondari iliyopo Mbezi, jijini Dar es Salaam, zilipovuja na kufika gazetini. Binti huyo, alipigwa picha akiwa katika mikao mbalimbali akiwa mtupu!
 
Simulizi zilivuja kwamba kabla ya picha hizo kufika magazetini, ambako zilichapishwa, msichana huyo alishajaribu mara nyingi kuzuia zisisambae lakini bila mafanikio. Unajua ilikuwaje?

Mtu wa kwanza kuzidaka, alimfuata na kumuonyesha picha zake na kumtisha kuwa angezipeleka magazetini au kwa wazazi wake kama asingempa uroda. Kwa hofu, denti akalazimika kutii matakwa yale. Basi ikawa mchezo, picha zikaendelea kuhama kutoka kwa huyu hadi huyu na binti akajikuta akigeuka mtumwa wa ngono ili kulinda heshima yake, hadi alipokuja kugundua kuwa angetumika hadi mwisho wa dunia, akaamua kukataa, akisema liwalo na liwe, ndipo zilipofika gazetini na kutoka!

Wednesday, February 20, 2013

Pistorius alimuua mpenzi wake kimakosa

Oscar Pistorius

Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius alimuua mpenzi wake kimakosa baada ya kudhania kuwa alikuwa mwizi aliyekuwa amevamia nyumba yake.
Aliambia mahakama kuwa alimpenda mchumba Reeva Steenkamp na wala hakuwa na nia yoyote ya kumuua

Viongozi wa mashtaka wanamtuhumu Pistoriusa kwa mauaji wakisema alikuwa amepnga kumuua mchumba wake baada ya kumpiga risasi mara tatu na kumuua akiwa ndani ya bafu nyumbani kwake.

Taarifa kuhusu mauaji hayo zimeanza kujitokeza katika kesi ambapo jaji ataamua ikiwa atampa Pistorius dhamana au la.
Haya yamejitokeza kwenye maelezo ya viongozi wa mashtaka huku mazishi ya mwanamitindo huyo yakifanyika mjini Port Elizabeth

Viongozi wa mashtaka wanasema kuwa Oscar alimuua Reeva baada ya kupanga mauaji yake. Madai anayotarajiwa kuyapinga vikali.
Pistorius alibubujikwa na machozi alipokuwa anasikiliza maelezo ya viongozi wa mashtaka, lakini mawakili wake walisema kuwa mauaji hayo hayakupangwa.

Saturday, January 26, 2013

MSAADA PEKEE KWA WATU WENYE UFAHAMU MDOGO


KAMA wewe ni mmoja kati ya watu ambao wana tatizo la ufahamu mdogo au mwanao ana ufahamu mdogo, basi ungana nami upate ufumbuzi wa tatizo hili. Uchunguzi unaonesha kuwa mashuleni,  makazini na kwenye jamii kuna watu ambao wanadharaulika kwa sababu si wazima katika uelewa. Hali hii imekuwa ikiwauma wahusika hasa pale wanapojaribu kufanya mambo kwa uwezo wao wote na kupata matokeo dhaifu.
Wanafunzi wengi wamejaribu kusoma kwa bidii, lakini wamejikuta katika nafasi za chini,  wengine wametumia uwezo wao katika kazi, lakini ukaguzi wa bosi hukosoa walichokifanya. Kwa kifupi watu wenye kasoro hii wamejikuta wakipoteza dhamana mbele ya wenzao. Kutwa hubebeshwa kauli hizi: “Usimtume fulani hataweza.” “Somo gani, la Kiswahili? Hawezi.” “Hana uwezo wa kuoa.”
Kauli hizi zinauma na wengi zimewakatisha tamaa. Wazazi wamewatenga watoto wao kwa sababu wanashindwa kupata alama za juu katika mitihani yao. “Wewe shule huwezi labda usubiri kuolewa.” “Mtoto huyu hasara tupu haelewi kabisa unapomwambia.” Lakini je, saikolojia inaamini katika kushindwa? Jibu ni hapana kwa sababu historia inaonesha kuna watu wengi ambao walikuwa hawawezi lakini baadaye waliweza. Njia ya kufanya ni hii!

JUKUMU LA MHUSIKA
Jukumu la mhusika katika kushughulikia tatizo la ufahamu mdogo ni kujitambua. Atambue maeneo ambayo yanamkwaza na ayaorodheshe tayari kwa kuyaongezea umakini. Kama ni masomo, basi ajue ni yepi yanayomshinda, kama ni yote uchungu wake usiwe kuona aibu baada ya kudharauliwa bali kwa kushindwa kufanikiwa.
Mhusika atenge muda wa kutosha kujizoeza katika yale anayofundishwa na awe na wakati wa kuyarudia. Aepuke kuchanganya mambo kabla ya kutimiza alichokusudia kukifanya. Mbio zake ziwe ni kupata alichokilenga. Kwa wale ambao ufahamu wao ni mdogo kazini, nao vivyo hivyo wanatakiwa kujifunza kwa bidii na kuwaweka wenzao wanaoweza kama shabaha ya ukamilifu. Kujielimisha kupitia vyombo vya habari, kusoma vitabu na kuwa karibu na wenye uelewa mkubwa ni jambo la muhimu.
Mwisho wahusika wanatakiwa kuwa mbali na hali ya kukata tamaa, hasa pale wanapojaribu jambo na kujikuta wamekosea. Wawe karibu zaidi na waalimu wao, wawe tayari kukiri kushindwa kwa lengo la kutaka msaada na kuepuka ukimya na kufanya jambo huku wakiwa na hofu au uelewa mdogo.

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate