EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, November 9, 2012

Sheikh Mukadam aunganishwa kwenye kesi ya Sheikh Ponda.


Habari imeandikwa na Happiness Katabazi 
KIONGOZI wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Mukadam Abdal Swalehe (45), jana alijikuta akifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, akiunganishwa  katika kesi ya jinai Na.245/2012 inayomkabili Katibu wa Jumuiya hiyo, Sheikh Issa Ponda Issa na wenzake 49 wanaokabiliwa na makosa ya uchochezi na wizi wa malighafi zenye thamani ya Sh. milioni 59 na hivyo kufanya sasa kesi hiyo kufikia idadi ya washtakiwa 51.

Sambamba na hiyo Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Dkt. Eliezer Feleshi aliwasilisha mahakamani hapo hati ya kumfungua dhamana Mukadamu kwaajili ya maslahi ya taifa chini ya kifungu cha 148(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002.

Mukadam alifikishwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Victoria Nongwa ambaye ndiye anayeisikiliza kesi hiyo tangu mwanzo  ambapo wakili Mwandamizi wa Serikali Tumaini Kweka  aliianza kwa kuieleza mahakama hiyo kuwa upande wa jamhuri unaomba kuifanyia marekebisho hati ya mashitaka ya kesi ya jinai Na. 245/2012 kwasababu imemuongeza mshitakiwa mmoja ambaye ni Mukadam  na kwamba Mukadamu anakabiliwa na makosa manne.

Wakili Kweka alidai kuwa kosa la kwanza ni la kuingia kwa nguvu kwenye kuingia kwa nguvu kwa nia ya kutenda kosa kinyume na kifungu cha  85 na 35 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002, kuwa Oktoba 12 mwaka huu huko Chang’ombe Markas, wasipokuwa na sababu za msingi waliingia kwa jinai kwenye kiwanja kinachomilikiwa na kampuni ya Agritanza Ltd, kujimilikisha kiwanja hicho kwa njia ya iloyopelekea uvunjifu wa amani,wizi ambapo baada ya kufamia waliiba vifaa na malighafi ikiwemo nondo, kokoto zenye jumla ya thamani ya Sh. 59,650,000 mali ya kampuni ya Agritanza na kosa la tano ni la uchochezi kinyume na kifungu cha 390 na 35 cah sheria ya Kanuni ya Adhabu, ambalo sasa kosa hili la uchochezi litamkabili Mukadamu na Ponda peke yao  kuwa akiwa ni kiongozi wa jumuiya hiyo , Oktoba 12 mwaka huu ,aliwashawishi katika eneo hilo ambapo aliwaamasisha washitakiwa hao watende kosa hilo.

Mshitakiwa huyo alikana mashitaka yote, Wakili Kweka alisema DPP. Feleshi amewasilisha hati ya kufunga dhamana ya Mukadamu na kwamba upelelezi wa kesi hiyo umekamilika tangu Novemba Mosi mwaka huu na kwamba Novemba 15 mwaka huu, kesi Mukadamu na wenzie 50 watakuja kusomewa maelezo ya awali.

Kwa upande wake hakimu Nongwa alisema makosa yanayomkabili mshtakiwa huyo yana dhamana ila kwakuw DPP-Feleshi amewasilisha hati ya kumfungia dhamana, mahakama imefungwa mikono,haiwezi kutoa dhamana kwasababu sheria iliyotumiwa na DPP kumfungia dhamana mshtakiwa huyo na Ponda zimetungwa na Bunge, mahakama yenye ipo kwaajili ya kuzifuata sheria hizo zilizotungwa na bunge katika kutoa uamuzi hivyo akaamuru mshitakiwa huyo amepelekwe gerezani hadi hadi Novemba 15 mwaka huu, kesi hiyo itakapokuja kwaajili ya washitakiwa kusomewa maelezo ya awali.

Jana washitakiwa 49 katika kesi hiyo waliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana isipokuwa Ponda peke yake ambaye naye dhamana yake imezuiwa na DPP ambapo hivi sasa  ni washtakiwa wawili kati ya 49 ndiyo dhamana zao zimefungwa na DPP, yaani Ponda na Mukadam ambao watakuwa wakiendelea kusota gerezani.
Mwandishi wa habari ana blogu kupitia: KatabaziHappy.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate