Alisema kuwa Black Leopards ni timu nzuri na walipata mazoezi mazuri katika mechi ya kwanza iliyofanyika kwenye uwanja waTaifa jijini na kushinda kwa mabao 3-2.
“Ni mechi nzuri ambayo nadhani itakuwa ni kipimo
kikubwa kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, wachezaji wangu
wana viwango vizuri sana kwa sasa na naamini makosa yaliyofanyika katika
mechi ya kwanza hawatayafanya tena,” alisema Brandts.
Msemaji wa Klabu Yanga, Baraka Kizuguto
alisema jana kuwa pamoja na mechi hiyo kuwa ya maandalizi ya Ligi Kuu ya
Tanzania Bara, pia wameamua kuicheza ili kuwapa burudani mashabiki wa
Mwanza.
Kizuguto alisema kuwa Yanga haitakuwa na
mechi yoyote katika mzunguko wa pili Kanda ya ziwa na hiyo ndiyo nafasi
yao ya kuwaonesha uwezo wao mkubwa mashabiki wa Mwanza nini wamekipata
kutoka Uturuki.
“Tuna mashabiki wengi sana Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla, hii ni fursa kwetu kwani mahsbaiki na wanachama watapata fursa ya kuona kiwango na maandalizi ya timu yao kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili,” alisema Kizuguto.

No comments:
Post a Comment