Dar es Salaam
MMILIKI wa jengo la hoteli iliyopo katika kiwanja namba 401
block ‘C’ Sinza jijini Dar es Salaam, Joanes Sanga, amekiuka agizo la
Manispaa ya Kinondoni kwa kujenga jengo la ghorofa tisa badala ya tano
kama alivyoomba.
Kutokana na kukiuka ujenzi huo uliopewa kibali namba 06809 kwenye
mpango namba K133/2009, tayari Manispaa ya Kinondoni imemwandikia barua
ya kumuelekeza taratibu za kufuata ili jengo hilo lipate baraka ya
kuendelea kujengwa.
Katika barua hiyo ya manispaa ya Aprili 17 mwaka huu, kwenda kwa
Sanga ikiwa imesainiwa na Mhandisi wa manispaa hiyo, Gerald Urio, kwa
niaba ya mkurugenzi wake, mmiliki huyo analezwa kuwa kwa taratibu za
viwango vya ujenzi mjini ukubwa wa kiwango kilichojengwa katika kiwanja
hicho hakitoshi kubeba uzito wa jengo unaoendelea.
“Wewe tayari umejenga kwa kibali hicho na kuongeza ghorofa nne, hivyo
jengo kuwa la ghorofa tisa (10 storey),” ilisomeka sehemu ya barua hiyo.
Pia barua hiyo inaelezea kuwa hakukuwa na aina yoyote ya ukaguzi
uliofanywa katika hatua zote za ujenzi ikiwamo kukagua vifaa
vilivyotumika.
Badala ya kuchukua hatua kwa ukiukwaji huo wa taratibu za ujenzi,
barua hiyo imemtaka mmiliki ahakikishe jengo hilo linafanyiwa vipimo
(structure assessment) kujua ubovu wake ambapo ametakiwa aende katika
taasisi ya serikali (BICO na DIT) na kisha majibu yarudishwe manispaa.
Alipotafutwa mmiliki wa jengo hilo kueleza sababu za kujenga bila
kufuata taratibu, alisema suala hilo waulizwe Manispaa ya Kinondoni.
Sanga alisema anachofanya ni suala la maendeleo na hajui kama amevunja taratibu.
Alipotakiwa kuelezea sababu ya kushindwa kukagua ujenzi huo, Mhandisi
wa Manispaa ya Kinondoni, Gerald Urio, alisema wao kama manispaa
hawawezi kukagua kila jengo katika wilaya hiyo.
Alisema sababu nyingine iliyowafanya wasiwe na wasiwasi na ujenzi huo
ni kutokana na vibao vinavyowaonesha wajenzi wa jengo hilo kuwa ni
wasomi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
Kuhusu athari inayoweza kujitokeza kutokana na ongezeko hilo, Urio alisema hilo si jambo la ajabu kwa kile alichoeleza kuwa kuna majengo mengi yanaongezwa baada ya ujenzi wa awali kukamilika.
Kuhusu athari inayoweza kujitokeza kutokana na ongezeko hilo, Urio alisema hilo si jambo la ajabu kwa kile alichoeleza kuwa kuna majengo mengi yanaongezwa baada ya ujenzi wa awali kukamilika.
No comments:
Post a Comment