KATIBU MKUU WA CCM ABDULRAHMAN KINANA AENDELEA NA ZIARA YAKE MKOA MPYA SIMIYU SIKU YA JANA.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki
kupiga lipu katika jengo la ofisi ya Chama cha Mapinduzi CCM katika kata
ya Ngoboko, huku Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi
akishuhudia tukio hilo.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na
wanachama wa CCM kata ya Ngoboko mara baada ya kushiriki shughuli za
ujenzi wa jengo hilo.
Hili
ni Daraja la mto Mwanhuzi mjini Meatu ambalo limejengwa na serikali na
linatarajiwa kuzinduliwa siku chache zijazo baada ya kukamilika,Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pia alikagua
daraja hilo katika moja ya shughuli alizofanya katika ziara hiyo kama
wanavyoonekana mafundi wakiendelea na kazi ndogo ndogo zilizobaki.
Katibu
wa Itikadi, Siasa na Uenezi CCM ndugu Nape Nnauye katikati Mh. Luhaga
Mpina Mbunge wa Jimbo la Kisesa na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Simiyu Ndugu Dk Titus Kamani wakimsikilizaKatibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman wakati alipokuwa akizungumza na wanaCCM wa Kata ya Ngoboko. (PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE- MEATU SIMIYU).
No comments:
Post a Comment