Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiangalia mto Malagalasi ambao ni
mpaka kati ya Tanzania na Burundi alipokuwa katika ziara wilayani
Buhigwe mkoani Kigoma leo Alhamisi, Aprili 10, 2014. Kinana yupo katika
ziara ya siku tano mkoani humo ya kukagua uhai wa Chama na kusikiliza
kero za wananchi mkoani humo. Moja ya kero kwenye mpaka huo
unaokutanisha vijiji vya Kibande (Tanzania) na Murambi(Burundi) ni
Watanzania kulazimika kukumbana na adha ya kuvuka mto huo kwenda kufanya
biashara na kununua mahitaji kwenye soko lililopo upande wa Burundi. Wa
pili kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye

Eneo
la soko la Murambi, Burundi ambako Watanzania hulazimika kwenda
kufanyabiashara na kupata mahitaji huko kutokana na upande wa nchi yao
kutokuwa na soko ikiwemo la mifugo lililokuwepo zamani na sasa halipo
kutokana na kufungwa kwa sababu zisizojulikana, ambaopo Kinana alihoji
kwa nini lisiwepo soko upande wa Tanzania ili kuondoa kero ya watu
kuvuka mto kila siku kwenda ng'ambo.

Juu ya maelezo haya ni wananchi wakivuka mto Malagarasi kutoka upande wa Burundi kuingia Tanzania

Wananchi
wa Kijiji cha Buhigwe wakimlaki Kinana alipowasili kwenye Ofisi ya CCM
Kata ya Buhigwe, kuzungumza na Kamati ya Siasa ya CCM wilayani humo, leo

Katibu Mkuu wa CCm Abdulrahman Kinana akipokea zawadi mbalimbali kutoka kwa wananchi wa Buhigwe wakati wa mkutano huo
No comments:
Post a Comment