KIONGOZI wa kwanya katika Kanisa la St. Peter,
Oysterbay jijini Dar, Rogers Mgonja amemtetea mwanamitindo mahiri Bongo,
Jokate Mwegelo kuwa hajalikacha kanisa kama inavyodaiwa.
Hivi karibuni ziliibuka taarifa kuwa, Jokate amezuiwa kutinga kanisani hapo kutokana na kuvaa mavazi ya nusu utupu yasiyoendana na maadili.
“Jokate
ni mwanadada mwenye nidhamu sana kanisani, viongozi wote wanampenda ni
mpole na msikivu, Kama ni mavazi, kanisani anavaa mavazi ya heshima ni
ngumu sana kumfukuza kwa sababu ambazo haziingiliani na masuala ya
kanisa,” alisema Mgonja.
Hivi karibuni ziliibuka taarifa kuwa, Jokate amezuiwa kutinga kanisani hapo kutokana na kuvaa mavazi ya nusu utupu yasiyoendana na maadili.

No comments:
Post a Comment