
Jennifer Lopez anaonekana kufuata ule msemo wa kati mti panda mti. Siku kadhaa baada ya kuachana na Serengeti boy wake Casper Smart tayari ameanza kuonekana akijiachia na dancer maarufu Maksim Chmerkovskiy.
Us Weekly limeripoti kuwa Jennifer na Masksim walioenekana Jumamosi katika Cassino ya Foxwoods Resort wakiwa karibu isivyo kawaida kwa watu marafiki na walikuwa wakicheza na kufanya kuongea kwa aina fulani.
Baada ya kutoka huko walihamia kwenye night club nyingine na kuendeleza bata la pamoja wakionesha ukaribu unaozua maswali.
Hii inakuja siku chache baada ya Jennifer kukanusha kuwa na mpenzi mwingine na kwamba bado yuko single.
Maskim ni mmoja kati ya dancers wanaompa kampani mara nyingi Jennifer Lopez anapokuwa jukwaani akifanya shows.
No comments:
Post a Comment