MSANII chipukizi kwenye tasnia ya filamu bongo, Miriam, ambaye ni mdogo wa msanii Jackine Wolper, ameuambia mtandao huu kuwa yupo kwenye wakati mgumu kwani wazazi wake wanamtaka aolewe
kilazima na mtu ambaye hana mahusiano naye huku wakiwa tayari
wameshachukua mahari.
Ishu hiyo awali kabisa ilidaiwa kuwa mwanaume ambaye amewekwa kwa ajili ya kumuoa ni mume wa mtu huku ndugu zake wakiwa wameshapokea nusu ya mahari tangu mwaka jana.
Ishu hiyo awali kabisa ilidaiwa kuwa mwanaume ambaye amewekwa kwa ajili ya kumuoa ni mume wa mtu huku ndugu zake wakiwa wameshapokea nusu ya mahari tangu mwaka jana.

Mwandishi wa habari hizi, alimtafuta msanii huyo ili kuzungumza naye kwa
kina juu ya hiyo, ndipo alipodai kuwa hawezi kusema lolote kwani
haitaji kuolewa kwa sasa na kitu kikubwa kinachomtatiza ni kwamba
mwanaume huyo tayari ni mume wa mtu.Alidai baadhi ya ndugu zake wanadai kuwa nusu ya mahari imeshatolewa kwa
ajili yake na endapo akikataa kufanya wanavyotaka hali itakuwa ngumu
kwani hakuna kitu wanachoweza kurudisha kwa mwanaume huyo zaidi ya yeye
kukubali kuolewa.
“Mimi siwezi kwa sababu sina mpango wa kuolewa kwa sasa lakini wazazi ndo kwanza wanataka mimi nifanye hivyo yani nashindwa kuelewa nifanye nini kwa hili, kila ndugu ninayemfuata kumbe anajua kila kitu juu ya hilo suala na walishindwa kunishirikisha mimi ili nitoe mawazo yangu,” alisema kwa unyonge.

No comments:
Post a Comment