SIKU moja baada ya Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme
Tanzania (Tanesco), kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa
Shirika hilo, Mhandisi William Mhando, Kamati ya Bunge ya Mashirika ya
Umma (POAC), imeitisha kikao cha dharura kujadili uamuzi huo.
Juzi,
Bodi hiyo chini ya Uenyekiti wa Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Robert
Mboma, iliwasimamisha kazi, Mhando na viongozi wengine wa Tanesco ambao
ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma za Shirika, Robert Shemhilu, Ofisa
Mkuu wa Fedha, Lusekelo Kassanga na Meneja Mwandamizi, Ununuzi Harun
Mattambo.
Akizungumza na gazeti hili jana, Mwenyekiti wa Kamati
Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Zitto Kabwe alisema
kufuatia uamuzi huo wa Bodi ya Tanesco, ameomba ruhusa kwa Spika wa
Bunge, Anne Mkinda kuitisha kikao cha dharura na bodi hiyo ijieleze.
Zitto alisema kuwa, mbali na bodi hiyo wamemwita Mkaguzi na Mdhibiti
Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh na Mamlaka ya Udhibiti
wa Ununuzi wa Umma (PPRA).
“Siku ya Jumatano (kesho kutwa)
kamati imemwomba Spika ruhusa ya kuitisha kikao ili bodi nzima ya
Tenesco kuja kutupa maelezo ya nini kimetokea, maana taarifa ya CAG na
PPRA haina hizo tuhuma wanazosema watu wa Serikali,” alisema Zitto na
kuongeza:
“POAC tunahusika na usimamizi wa fedha za shirika,
tunataka kujua ubadhirifu na masuala ya kisheria na itahakikisha
uwajibikaji na tutasimamia hilo kwa nguvu zote kwani hatutaki uonevu na
tutalinda wanaoonewa. Hata hivyo, kauli hiyo ya Zitto inakuja wakati
baadhi ya wabunge akiwamo yeye mwenyewe hivi karibuni walishinikiza
mawaziri ambao wizara zao zilitajwa kuhusika na tuhuma za ufisadi katika
ripoti ya CAG wajiuzulu.
Zitto pia ndiye aliyeongoza zoezi la
kukusanya saini za wabunge kwa ajili ya kupiga kura za kutokuwa na imani
na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda baada ya ripoti ya CAG kuonyesha ufisadi
mkubwa serikalini. Akisoma ripoti ya POAC baada ya kutolewa ripoti na
CAG, Zitto alisema kuwa, Tanesco kulikuwa na ongezeko la gharama za
ununuzi kutoka Sh300 bilioni za mwaka juzi hadi Sh600 bilioni katika
ripoti ya mwaka huu na kuhoji, chanzo cha ongezeko la gharama hizo kwa
asilimia 100.
Hata hivyo, taarifa za ndani kutoka Wizara ya
Nishati na Madini zinaeleza kuwa uamuzi wa bodi hiyo kumng'oa Mhando na
wenzake unatokana na kushindwa kuwajibika kwa Mkurugenzi huyo kumaliza
mgawo wa umeme na kuendelea kuwapo kwa vitendo vya hujuma katika
uzalishaji wa umeme.
Kauli ya Utouh
Hata hivyo, akizungumzia suala hilo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh alisema hana taarifa zozote za kuitwa na Kamati ya POAC kuhusiana na sakata la kusimamishwa viongozi wa Tanesco.
“Sijapata taarifa za kuitwa na Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma, wewe ndiyo unanijulisha kuhusu hilo.”
Hata hivyo, akizungumzia suala hilo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh alisema hana taarifa zozote za kuitwa na Kamati ya POAC kuhusiana na sakata la kusimamishwa viongozi wa Tanesco.
“Sijapata taarifa za kuitwa na Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma, wewe ndiyo unanijulisha kuhusu hilo.”
Utouh
alisema kwa sasa hawezi kuzungumza kuhusu ripoti ya hesabu za Tanesco
kama walipata hati safi au hati chafu hadi aipitie upya ripoti hiyo.
“Kwa
harakaharaka siwezi kufahamu kama Tanesco walipata ripoti ya aina gani
inayohusu matumizi ya fedha hadi niisome upya ndipo ninaweza
kulizungumzia,” alisema Utouh.
CAG alisema taarifa za kusimamishwa viongozi wa Tanesco ameziona na kuzisoma katika vyombo vya habari.
Mwambalaswa
Mmoja wa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Victor Mwambalaswa alitaja
baadhi ya tuhuma zilizosababisha bodi hiyo kumsimamisha Mhando pamoja na
maofisa wenzake kuwa ni kuhusika katika matumizi mabaya ya fedha za
umma.
Mwambalaswa ambaye pia ni Mbunge wa Lupa (CCM), alizitaja
tuhuma nyingine kuwa, ni matumizi mabaya ya madaraka likiwamo la
kuongoza kwa upendeleo.
Alidai upandishwaji vyeo unafanywa kwa misingi ya ukabila.
“Msingi wa tuhumu hizo ni ziara aliyofanya Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Sospter
“Msingi wa tuhumu hizo ni ziara aliyofanya Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Sospter
Muhungo hivi karibu ambapo aliwataka
wafanyakazi wenye kero kuwasilisha malalamiko yake wizarani ili
yafanyiwa kazi,” alibainisha Mwambalaswa.
Pia, uamuzi wa kutaka
watendaji nao wawajibike ulitangazwa na Rais Jakaya Kikwete Ikulu Mei 4,
wakati akitangaza baraza jipya la mawaziri ambapo alisema kuwa, mbali
ya uwajibikaji kisiasa, bodi za wakurugenzi na watendaji ambao taasisi
zao zimetajwa katika ripoti ya CAG kuhusika na matumizi mabaya ya fedha
za umma, watapaswa kuwajibishwa.
Ilivyokuwa Hatua hiyo
ilitangazwa juzi jijini Dar es Salaam kufuatia kikao cha dharura cha
Bodi ya
Wakurugenzi ya Tanesco kilichofanyika Julai 13 mwaka huu,
ambacho kilijadili tuhuma mbalimbali dhidi ya menejimenti ya Tanesco.
Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wake, Jenerali Mstaafu Robert
Mboma na kuchukua uamuzi wa kumsimamisha kazi Mhando ili kupisha
uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka.
“Hivyo,
bodi iliazimia pamoja na mambo mengine kama ifuatavyo: Uchunguzi wa
tuhuma hizo uanze mara moja kwa kutumia uchunguzi huru na kumsimamisha
kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Mhandisi William Mhando ili kupisha
uchunguzi huo na kwa kuzingatia matakwa ya sheria za kazi nchini,”
ilieleza sehemu ya taarifa aliyoitoa Mboma kwa vyombo vya habari.
Mhando aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa
Tanesco kuanzia Juni Mosi Mwaka
2010.
Baada ya uteuzi huo, Mhando alisema atahakikisha wateja
wote wa Tanesco wanakuwa na mita za Luku. Kabla ya uteuzi huo, Mhando
alikuwa ni Meneja Mkuu Usambazaji Umeme na Masoko katika shirika hilo.
Mhando alichukua nafasi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa shirika hilo, Dk
Idris Rashid ambaye alimaliza muda wake wa uongozi.
No comments:
Post a Comment