EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, January 31, 2014

KENNETH KIDAGO WA EAST AFRICA RADIO AFARIKI DUNIA


 
Marehemu Kenneth Kidago Lyanga enzi ya uhai wake.
Mbunifu Msaidizi na Mtangazaji wa Habari za Michezo wa East Africa Radio Kenneth Kidago Lyanga amefariki dunia nyumbani kwake Mwenge Mlalakua, Jijini Dar es Salaam.
Mipango ya mazishi ya Kenneth Lyanga inafanywa na familia yake. 

IRENEJAMII Blog tunatoa pole kwa familia ya marehemu Kenneth.Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Kenneth Kidago Lyanga Mahala Pema Peponi, Amina.

WASTARA: NIKIKUMBATIWA NAKUWA HOI

MSANII wa filamu, Wastara Juma amefunguka kuwa starehe yake kubwa duniani ni kukumbatiwa na anapofanyiwa kitendo hicho na mtu wa jinsia yoyote huwa hoi.
 
Wastara Juma.
Akistorisha na paparazi wetu, Wastara alisema: “Mimi napenda sana kukumbatiwa au kukumbatia, awe ni mwanaume au mwanamke, ndugu yangu au hata kama siyo ndugu yangu, tukikumbatiana tu najisikia raha sana.
“Unajua kila mtu anakuwa na kitu anachokipenda duniani sasa mimi starehe yangu ndiyo hiyo hata marafiki zangu wanajua kwamba mimi napenda kukumbatiwa.”

TAMKO LA MZEE JOHN MALECELA KUHUSIANA NA GUMZO LA MBIO ZA URAIS 2015 HAPA NCHINI



Ndugu zangu waandishi wa habari, awali ya yote naomba niwasalimie na niwapongeze kwa kufika -mwaka mpya 2014, pia naomba niwapongeze kwa kazi kubwa ambayo mmekuwa mkiifanya hasa kuhakikisha watanzania wanapata habari kwa kila jambo linaloendelea kila kona ya taifa letu la Tanzania.

Ndugu waandishi wa habari nimewaita hapa ili kuzungumza nanyi na mnisaidie kufikisha ujumbe kwa watanzania hasa kuhusu jambo hili ambalo limekuwa gumzo kwa watanzania wengi la mbio za urais 2015 kwa baadhi ya watu ndani ya chama changu cha mapinduzi (CCM), kilichonisukuma zaidi na kupata hamu ya kuongea nanyi ni baada ya kumsikia -na kumuona kijana wetu ndani ya chama cha mapinduzi bwana Paul Makonda akiwa na ujasiri wa kukemea vitendo mambo haya yanayofanywa na baadhio ya viongozi bila uwoga wowote naomba tuchukue fursa hii kumpongeza sana kijana huyu.

JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS SASA!


Kuwa wa kwanza kupata Breaking News za wasanii, watu maarufu na zingine kutoka Magazeti Pendwa ya IJUMAA WIKIENDA, UWAZI, RISASI, AMANI, IJUMAA na CHAMPIONI moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa shilingi 100 tu kwa SIKU!

Kujiunga tuma GLOBAL kwenda 15778
Huduma hii ni kwa watumiaji wa Vodacom pekee.

TP MAZEMBE YATUA KWA MESSI


Kiungo nyota wa Simba, Ramadhani Singano ‘Messi’.
MAMBO yamekucha kwa kiungo nyota wa Simba, Ramadhani Singano ‘Messi’ baada ya klabu tajiri ya TP Mazembe ya Lubumbashi, DR Congo kuonyesha wazi kuwa inamtaka.
TP Mazembe tayari imetuma mtu ambaye amekuja nchini kwa ajili ya kumshuhudia Messi akiichezea Simba na ameeleza nia ya klabu hiyo.

Thursday, January 30, 2014

LEO NI SIKU YA KUZALIWA MWANAMUZIKI PHIL COLLINS


Phil Collins.
MWANAMUZIKI kutoka nchini England, Philip David Charles "Phil" Collins leo ametimiza umri wa miaka 63. Collins ambaye pia ni mwimbaji, mwandishi wa nyimbo, mpiga ala mbalimbali za muziki na mwigizaji  alizaliwa Januari 30, 1951 jijini London, England.
Baadhi ya nyimbo za msanii huyo zilizotamba ni pamoja na: "You Can't Hurry Love", "You Can't Hurry Love", "You Can't Hurry Love", "Against All Odds (Take a Look at Me Now)", "Easy Lover" (With Philip Bailey), "One More Night", "Sussudio", "Separate Lives" (With Marilyn Martin), "A Groovy Kind of Love", "A Groovy Kind of Love", "Two Hearts", "Another Day in Paradise"

WAPO MASUPASTAA, MASTAA NA WAIGIZAJI


NITAELEWEKA tu! Sina ubishi kwamba kwa sasa Bongo, fani ya sanaa ya uigizaji ndiyo imeshika kasi kukubalika katika jamii (anayebisha anyooshe mkono, najua hakuna).
Elizabeth Michael 'Lulu'.
Siku hizi ukikatisha kwenye mitaa mbalimbali nchini Tanzania, hasa uswahilini, utagundua wengi wanaangalia ‘filamu za akina Kanumba’ kama vile Uncle JJ, Ndoa Yangu, Mr. Ben, World of Benefit na nyingine nyingi.
Haya ni maendeleo kwa wasanii wetu ambao zamani walikuwa wakihaha kutoka lakini walishindwa kutokana na soko la filamu Bongo kushikwa na ‘muvi za akina Rambo’ na baadaye akina Noa Ramsey.
ANGALIZO LANGU
Pamoja na yote hayo, kuna angalizo langu. Ili sanaa hiyo izidi kukua nchini ni lazima kuwe na ushirikiano mkubwa kati ya wasanii wenyewe (waigizaji) na vyombo vya habari.
Aunt Ezekiel.
Vyombo vya habari ndivyo vinavyotangaza kazi zao mpaka zikajulikana na akina mama Nyakomba kule kijijini Songea (nyumbi hii, bomba hii).
Lakini kumekuwa na ugumu wa ushirikiano kutoka kwa baadhi ya waigizaji, hasa wale ambao wanajiita (hawaitwi) wanajiita masupastaa au mastaa wa Bongo (Bongo Movies).  
Hawa jamaa baada ya kuamini wamekuwa na majina makubwa kupitia filamu (ni vyombo vya habari vilivyowafanya wawe na majina makubwa) wamekuwa na dharau, wamekuwa bize, wamekuwa hawana nafasi, simu wamekuwa wakiziweka mbali na wao walipo au hazina chaji tangu jana usiku (si unajua umeme wa Tanesco?).
Jack Wolper.
MBAYA ZAIDI
Mbaya zaidi, hao ‘mastaa’ wapo hata wale waliokwishaonekana kwenye filamu tatu tu tena si ‘mastering’, waliigiza kwenye udereva, kufungua mageti, wakaribisha wageni maofisini au wasaidizi wa kazi za ndani ‘mahausigeli’.
NINAVYOJUA MIMI
Kwa mujibu wa ufahamu wangu mdogo ni kwamba, katika kila tasnia duniani kuna masupastaa na mastaa. Pia wapo wahusika wa fani husika. Kama filamu tunasema waigizaji.
Sasa hawa wa Bongo ambao nao pia wamejiweka kwenye kundi la masupastaa na mastaa wananitatiza kila kukicha, kwamba ni wagumu kupatikana, iwe laivu au kwa simu kwa sababu wao ni maarufu katika fani.
 
Jacob Steven 'JB'.
MASUPASTAA
Kufuatia lawama zangu hizi kwa wasanii wa fillamu Bongo, kama mtu ataniuliza ninavyojua mimi nani supastaa, staa na mwigizaji orodha yao ninayo na niko tayari kuiweka wazi.
Siwezi kusema Ray, JB, Aunt Ezekiel, Nora, Wolper, Johari, Natasha, Monalisa, Dk. Cheni, Riyama Ali, Lulu, Mzee Majuto, Mzee Small siyo mastaa wa filamu Bongo.
Wamecheza filamu nyingi, wamejenga majina makubwa kupitia sanaa hiyo. Japokuwa miongoni mwao wapo ambao ni wababaishaji kwenye kupokea simu na kujifanya ‘aghali’ kupatikana.
Lakini pia kuna kundi la mastaa wa filamu za Bongo; hawa ni akina Baba Haji, Kuambiana, Maya, Jini Kabula, Wastara, Mr. Chuz, Frank Mwikonge, Mzee Chilo, Mzee Magali, Cloud, Penina, Richie, Bi. Chau na Thea.
Wengine ambao kwangu ni mastaa ni, Jack wa Chuz, Cathy, Lucy Komba, Big, Chekibudi, Baba Haji, Kelvin, Odama, Rose Ndauka, William Mtitu, Tino, Flora Mvungi, Nisha, Shilole, Mainda, Shamsa Ford, Snura, Mlela, Shumileta, Hemed, Yusuf Mlela, Dude na Maya.
Mbali na makundi hayo, kuna ambao wamepitiliza usupastaa na sasa wameingia kwenye kundi la wakongwe wa sanaa. Hawa ni kama akina Natasha, Mzee Small, Mzee Majuto, Bi. Hindu, Bi. Mwenda, Bi. Chau, Kemmy na Muhogo Mchungu.
Mzee Majuto.
Lakini napata tabu kusema, Batuli, Zamda, Tiko, Slim, Skaina, Rachel Haule, Chikoka, Kupa, Mafufu, Badra na wengine wengi ambao kwenye fani hawana hata mwaka mmoja ni mastaa.
Kwa nchi za wenzetu ‘majuu’, vyombo vya habari havitambulishi kila mwigizaji kama staa, ila wanakuwa mastaa katika filamu walizocheza tu, hususan kama amecheza filamu mbili au tatu.
Mfano; wakitaka kumtambulisha Rachel Haule watasema: “Staa wa filamu ya…..(wataitaja jina), Rachel Haule amepata mchumba (mfano lakini).
Majuu staa, kama wa filamu ni yule aliyekwishacheza muvi zaidi ya 10 akiwa ni stering na zikatikisa. Kibongobongo, hata akicheza filamu moja halafu akavuma sana, tena wengine huvuma kwa mambo nje ya filamu, ni staa.
Makala haya ni mtazamo wangu.

Wednesday, January 29, 2014

Bunge lataka mgogoro Bukoba uishe

29/01/2014 | Posted by Happiness Mnale | Kitaifa | 0 comments | 184 views MAKAMU Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Benadetha Mshashu, ameitaka wizara husika kuhakikisha inasimamia na kuupatia ufumbuzi mgogoro wa uongozi katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba. Hatua hiyo inakuja zikiwa ni siku chache tangu aliyekuwa Meya wa manispaa hiyo, Anatory Amani, kutengua msimamo wake wa kujiuzulu baada ya taarifa ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kumtia hatiani kwa ubadhirifu wa miradi ya maendeleo aliyokuwa akiitekeleza. Akizungumza jana wakati kamati hiyo ilipokutana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Hawa Ghasia, Benadetha alisema Bukoba inafuka moshi, hivyo ni vyema wizara hiyo ikasimamia sheria ili kuinusuru halmashauri ifanye kazi. Alisema kuwa halmashauri hiyo ni vyema ikanusuriwa ili itende kazi kwani baada ya ripoti ya CAG kutoka nakala zake zimegawiwa hadi mitaani. Akijibu hoja hiyo Waziri Ghasia, alisema kuwa walishakutana na kuamua kuwa meya wa manispaa hiyo ajiuzulu ama madiwani wapige kura za kumuondoa au Baraza la Madiwani livunjwe na kueleza kuwa atalifanyia kazi suala hilo. Katika hatua nyingine, Ghasia alijitetea kuwa anaitwa waziri mzigo kwa sababu Tamisemi haina meno ya kuwashughulikia watendaji kutokana na sheria za nchi zilizopo. Ghasia alisema kuwa Baraza la Madiwani wakishindwa kuwachukulia hatua watendaji, Waziri wa Tamisemi hawezi kuchukua hatua kutokana na sheria zilizopo bali wakurugenzi wanachukuliwa hatua na Waziri Mkuu. Suala la mawaziri mizigo lilijitokeza jana baada ya Mwenyekiti wa kamati hiyo Dk. Khamis Kigwangalah, kueleza kuwa mfumo wa sheria katika kuwachukulia hatua za kinidhamu wakurugenzi ni tatizo. “Sheria ya Utumishi wa Umma namba 8 ya mwaka 2002 haiko sawa, ikiwezekana ijadiliwe upya, maana kila mtu kilio ni halmashauri, mawaziri wameambiwa mizigo, kombora zimepigwa kwao, madaraka waliyopewa madiwani, wakurugenzi hawawasilikizi, wananchi wamepewa mamlaka ya kiujanja ujanja tu ya kuwashughulikia wakurugenzi. Mfumo ni tatizo. “Ziangaliwe upya sheria kama madiwani hawawezi kuwasimamia, madaraka yapunguzwe na kama mfumo huu wa sasa wa uendeshaji wa halmashauri utaendelea nyie mawaziri mtaendelea kushambuliwa tu, maana usiri wa halmashauri unasababisha urahisi wa kuiba,” alisema. Katika maazimio yake, kamati hiyo ilitaka kikao hicho kihairishwe kwa wiki mbili ili wizara hiyo iwape majibu ya kina ya hoja zilizowakilishwa zitolewe kwa maandishi ikiwemo watu wa hazina wawepo, mtindo wa ripoti uonyeshe bajeti ni kiasi gani, kilichotolewa na asilimia ionekane. Maazimio mengine ni taarifa ya kesi zilizopo mahakamani, majina ya watuhumiwa, tuhuma na hatua zilizochukuliwa kwa wakurugenzi waliodaiwa kufanya ubadhirifu sh milioni 444 katika mradi wa maboresho ya serikali za mitaa ikiwemo wizara hiyo itoe ripoti za miradi ipi imetekelezwa katika sekta ya kilimo, afya, maji na elimu. Dk. Kigwangalah ambaye ni mbunge wa Nzega alisema kuwa kwa mwaka 2014, kuwajibishana ni lazima ili kuendana na mabadiliko chanya katika kuwaletea wananchi maendeleo.

NAPE AJICHANGANYA WA WANANCHI SOKO LA MWANJELWA MBEYA


 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa  Nape Nnauye akicheza draft na vijana wafanyabiashara wa soko la Sido Mwanjelwa jijini Mbeya. Nape yupo mjini Mbeya kwa ajili ya maandalizi ya sherehe za miaka 37 ya CCM ambazo kitaifa zitasheherekewa mkoani hapo.Katibu wa NEC alikutana na vijana mbali mbali ambao walifurahi sana kumuona kiongozi wao akiwa pamoja nao kiasi soko zima lilipuka kwa nyimbo za hamasa za CCM zilizoimbwa na Kapteni John Komba,Nape pia alipata fursa ya kusalimiana na baadhi ya madereva wa Taxi wa kituo maarufu cha Mafiati.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akila chakula cha mchana kwenye kibanda cha Mama Lishe anayefahamika kama Bi. Tandiwa Tewete kwenye soko la Sido Mwanjelwa mjini Mbeya.

NEW ARRIVALS @AK CLASSIC COSMETICs


 KILA SIKU WANAKUJA NA MAMBO TOFAUTI NA MAKUBWA ZAIDI.WALE MABINGWA WA COSMETICS ORIGINAL KABISA KUTOKA MBELE MBELE, @AK CLASSIC COSMETICS  WAMEWASHUSHIA TENA MADINI MAPYAA KABISA!!  KUANZIA PRODUCTs ZA KUPUNGUA,TIBA ZA CHUNUSI,PRODUCTs ZA KUNG'ARISHA NGOZI YAKO,DAWA ZA KUONDOA STRETCH MARKS, BODY SHAPERs,LACEWIGS...NA BIDHAAA ZINGINE LUKUKI MUPYAAAAAA!!EM TUONGOZANE HAPA..

 KWA MAELEZO YA KINA NA PICHA ZAIDI WATEMBELEE BLOGUNI www.akclassic.blogspot.com
 KUWEKA ODA NA KUFIKISHIWA BIDHAA MPAKA ULIPO PIGA  0753-482909/0713-468393.
WAPO KINONDONI KWA MANYANYA NA SINZA KUMEKUCHA.

KARIBUNI SANA.

MKUNGA WA JADI ALIYEFANIKIWA KUMZALISHA MWANAMKE WATOTO WATATU AOMBA MSAADA WA VIFAA VYA KUZALISHIA

WADAU wa sekta ya Afya nchini wametakiwa kuwajali na kuwathamini wakunga wa Jadi kwa kuwa wamekuwa wakombozi kwa wazazi waishio mbali na vituo vya afya pindi wanapohitaji huduma ya kujifungua. Mwito huo ulitolewa na Mkunga wa Jadi, Dotea Mwanakulya (60) Mkazi wa kijiji cha Magamba Wilayani Chunya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari waliomtembelea nyumbani kwake kujua changamoto anazokabiliana nazo. Mkunga huyo wa alisema anakabiliwa na changamoto za ukosefu wa vifaa vya kujifungulia kama kitanda,godoro,mipira ya kuvaa mikononi ili kuzuia maambukizi ya ugonjwa ambapo wagonjwa wengine hufika hapo wakiwa hawana vifaa  hivyo. Hata hivyo mkunga huyo amewaomba wadau mbali mbali kumsaidia kupata daftari ya kutunza kumbukumbu za watoto wanaozaliwa nyumbani kwake kwa kile alichodai kuwa hana kumbukumbu sahihi za idadi hali ya watoto waliozaliwa kwake. Mkunga huyo alilazimika kutoa kauli hizo kufuatia kuwepo kwa Mwanamke mmoja kujifunga watoto mapacha mfululizo kwa Mkunga huyo na watoto wake wakiendelea kukua vizuri. Mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina la Paskalia Adrofu (37)mkazi wa kijiji cha Magamba kata ya Magamba wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya,alijifungua salama watoto watatu hivi karibuni kwa mkunga wa Jadi huyo. Paskalia amejifungua watoto wawili jinsi ya kiume na mmoja wa kike ambapo amesaidiwa  na mkunga wa jadi  Dotea Mwanakulya (60)anayeishi kijiji cha Magamba. Paskalia alisema kwamba mume wake aitwaye Richard Saba (55) ni mkulima hivyo imekuwa vigumu kwake kumudu gharama za matunzo kwa watoto hao ambapo ana jumla ya watoto wanane,wakiwemo mapacha ambao wamemaliza shule ya msingi na hawajachaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari. Mama huyo alianza kujifungua mtoto wa kwanza mwaka 1995,wa pili ambao ni mapacha mwaka 1998 wa tatu mwaka 2006,wa nne mwaka 2009 na wa tano ambao wamezaliwa watatu amejifungua mwanzoni mwa mwaka huu ambao wana afya njema. Hata hivyo Paskalia alisema uongozi wa kata akiwemo Diwani wa kata ya Magamba  Chakupewa Kapalala wamefika kumtembelea na kumjulia hali yake na kumhimiza kuhudhuria kliniki mara kwa mara ili kufuatilia afya za watoto. Aidha mkazi mmoja wa kijiji hicho aitwaye Luhende Luhaga ametoa ng’ombe wawili wa maziwa ili mama huyo amudu kuwanyonyesha watoto hao bila shida kutokana na kulemewa na watoto hao. Watoto wawili wa mwanzo wamezaliwa na uzito wa kilo 2.8 na wa tatu amezaliwa na uzito wa kilo 2.0 ambapo Paskalia alisema kuwa watapofikia uzito wa kilo 3 ndipo watapatiwa chanjo katika zahanati ya Magamba. Baadhi ya changamoto anazokabiliwa nazo ni pamoja na nguo za watoto,chupa za kunyonyeshea,sabuni,mafuta na chupa za chai kwa ajili ya kuhifadhia maziwa ya watoto. Na Ezekiel Kamanga Mbeya yetu

HAPANA CHEZEA MCHAGA

MANGI NA MBINGUNI WAPI NA WAPI! Mangi alipokufa aliulizwa na MALAIKA:kulia kwako ni peponi, kushoto ni Jehanam. unapenda uende wapi? MANGI: Nitabaki katikati ya peponi na Jehanam MALAIKA:Kwanini?! MANGI:nikifungua duka hapo wote wa mbinguni na jehanam watafika kununua bidhaa. Chezea mchaga wewe,,,,

Tuesday, January 28, 2014

MWANDISHI ANNE WAITHERA WA BBC AFARIKI DUNIA

 
Mwandishi Anne Waithera enzi za uhai wake.
MWANDISHI wa BBC kutoka nchini Kenya, Anne Waithera amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu akisumbuliwa na maradhi ya saratani. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi!

USHAURI WA BURE KWA MABINTI

 1. Usimuulize mpenzi swali ambalo jibu lake litakuuma. Usilulize maswali kama, ‘Hivi Amina alikuwa mpenzi wako? Au je, eti mi mnene?’ Si maswali muafaka

2. Kama jamaa anaangalia mpira kwenye TV, aidha umuunge mkono na wewe anza kuangalia mpira au nenda kalale, hakuna mbadala

3.  Kiukweli una nguo na viatu vya kutosha siyo kila style ikija unamwambia mupenzi akununulie

4.  Kama ukitaka jamaa asisahau birthday yako mkumbushe siyo unaanza lawama baadae eti kwanini hakukumbuka

5. Ukiona mupenzi anaangalia wadada wengine ni jambo zuri, atajuaje kuwa wewe mzuri kuliko wao kama halinganishi?

MSIBA: MCD WA TWANGA PEPETA AFARIKI DUNIA!

 
Sudi Mohamed, 'MCD' (pichani, juu na chini) ambaye ni mpinga tumba maarufu nchini Tanzania amefariki dunia usiku huu akiwa Moshi ambako alikwenda kwa ajili ya matiabu zaidi yapata miezi mitatu iliyopita. Kwa mujibu wa kiongozi mmoja wa Bendi ya Twanga Pepeta, Meneja Hassani, MCD alipelekewa nauli ya kurudi jijini Dar esalaam leo ili arejee kesho lakini mauti yakamfika usiku mida ya saa tano na nusu. MCD amewahi kupiga katika bendi kadhaa za muziki wa dansi ikiwemo Mashujaa Band na African Stars ambako alirejea tena. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi - ameen!

MZEE DUDE AFARIKI DUNIA

Mzee Dude enzi za uhai wake.
MSANII wa kundi maarufu la vichekesho na uigizaji la Futuhi, Mzee Dude amefariki dunia akiwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando iliyopo jijini Mwanza siku ya jana jioni!
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN!

Monday, January 27, 2014

KIGOGO WA WEMA NOMA SANA!

NOMA sana! Baada ya kupigwa cha mbavu (kuachwa) na Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu huku akimnyang’anya vitu vyote vya ofisini, yule kigogo wa ikulu, Clement a.k.a CK, hivi sasa anadaiwa kutoka na shosti wa staa huyo, Naima Shaa.
Naima Shaa.
Kwa mujibu wa chanzo makini cha gazeti namba moja la burudani Bongo, Ijumaa Wikienda, Naima anatamba na kuwapiga vijembe wasichana wa mjini kuwa anatoka na CK mwenye mkwanja mrefu (bado fedha hazijaisha).
“Nakwambia hatunywi maji, mtoto kadata kabisa hadi ameamua kujichora ‘tatuu’ ya jina la Clement  kwenye bega lake la kulia. Inahusu?” kilihoji chanzo chetu.
Wema Sepetu.

WANAFUNZI 1725 WASHINDWA KURIPOTI SHULENI WILAYA YA KILOLO

Mkuu wa Wilaya ya Kilolo,Mh.Gerald Guninita akifungua kikao cha DCC katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya,Kushoto ni Mkurugenzi Ruukia Muwango na Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri  ya Wilaya,kikao kilichofanyika mwisho mwa wiki katika ukumbi wa halmashauri hiyo.
Mkurugenzi wa wilaya ya Kilolo Rukia Muwango akisoma taarifa ya wilaya hiyo mbele ya wajumbe wa kamati ya wilaya katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa wilaya mwishoni mwa wiki.
WANAFUNZI 1725  WASHINDWA KURIPOTI SHULENI WILAYA YA KILOLO
JUMLA ya wanafunzi 1725 waliotakiwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza katika shule mbalimbali zilizoko katika Wilaya ya Kilolo wameshindwa kuripoti kutokana na sababu mbalimbali.
 
Akizungumza katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kilolo mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi Mtendaji  wa Halmashauri hiyo, Rukia Muwango  alisema wanafunzi wasioripoti kati ya hao wavulana walikuwa 788 na wasichana 937 sawa na asilimia 56.1

Muwango alisema wanafunzi waliochaguliwa kwa halmashauri ya wilaya ya Kilolo ni wanafunzi 3101 wavulana 1442, wasichana 1658 kati ya hao wavulana 10 na wasichana 10 wamechaguliwa katika shule za bweni.
Alisema wanafunzi waliopangwa kwenda katika shule za ufundi walikuwa wavulana 6 na hakuna msichana aliyechaguliwa na wanafunzi 3074 walipangwa katika shule za serikali katika halmashauri ya wilaya ya Kilolo.

Aliongeza kuwa wanafunzi walioripoti hadi Januari 23 mwaka huu walikuwa wanafunzi 1349 wakiwemo wavulana 638 na wasichana 711 sawa na asilimia 43.
Muwango alizitaja shule ambazo zina asilimia ndogo ya wanafunzi walioripoti shuleni kuwa ni shule ya Sekondari Mawambala (5.2%), Mlafu (14%), Lukosi (19.3%),Udekwa (21%) na Mtitu yenye asilimia 29 ya wanafunzi walioripoti.

Aliwataka walimu wa wakuu shule za sekondari wawasilishe majina ya wanafunzi wa kidato cha kwanza 2014 waliojiunga katika shule zao ili halmashauri iweze kujua na kujiridhisha kuwa wanafunzi wote wapo shuleni na kutoa taarifa kwa wanafunzi wanaokwenda shule za zisizo za serikali kupata takwimu sahihi.
Alisema kuwa halmashauri imeandaa mikakati kwa wanafunzi wasioripoti kwa kuwaandikia barua waratibu wote kuwafatilia wanafunzi  hao na kuwahimiza kuhudhuria katika shule walizopangiwa.
 
Kwa upande wa ke Mkuu wa Wilaya hiyo Gerald Guninita amewataka watendaji wawasisitize wazazi kuwapeleka watoto shule bila kujali suala la ada na sare za shule.
Aliwataka watendaji kupeleka ripoti ndani ya siku 24 kwa wanafunzi wote ambao hawajaripoti shuleni hadi sasa katika ofisi ya wilaya na kuwachukulia hatua wazazi wakaidi.

“Haki ya mtoto kupata elimu ni muhimu sana na tusiache wazazi wanaowaficha watoto ndani hivyo wabanwe wazazi wao kwa kuwaficha kuna kitu nataka kuwaambia kumpeleka shule mtoto ni kumwongezea thamani mtoto na mzazi mwenye katika maisha yetu ya kila siku hivyo nawsisitiza sana watendaji wabaneni  sana wazazi wote wasiotaka kuwapeleka watoto wa kike shule” alisema Guninita.

MTIKISIKO WATOKEA KATIKA JENGO LENYE OFISI ZA TIGO MAKUMBUSHO JIJINI DAR

Taswira ya jengo la Derm lenye ofisi za Tigo ulipotokea mtikisiko leo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camilius Wambura.
Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga akiongea na wanahabari (hawapo pichani).
Makamanda kutoka Jeshi la Polisi wakiwa eneo hilo la tukio.
Eneo la jengo hilo likiwa limefungwa kwa usalama wa wafanyakazi na watu wanaopita eneo hilo kupisha uchunguzi.
(PICHA NA BALINABAS MANYILIZU / GPL)

Saturday, January 25, 2014

PENNY AZUNGUMZA UKWELI WA MAMBO

Penniel Mwingila 'VJ Penny'.
Mtangazaji na meneja wa vipindi wa kituo cha runinga cha DTV, Penniel Mwingila 'VJ Penny' amesema kuwa yeye na mpenzi wake, staa wa ‘My Number One’, Diamond Platnumz, wamepeana nafasi ili kila mmoja kutafakari anachotaka maishani.
Kauli ya Penny kwenye mahojiano maalum na Bongo5 TV, inajibu maswali ya wengi kuhusiana na kama wawili hao wapo pamoja au wameachana baada ya Diamond na mpenzi wake wa zamani, Wema Sepetu kurudiana tena. Katika interview hiyo, Penny ameongea pia kuanzia historia yake, namna alivyoingia kwenye utangazaji, alivyokutana na Diamond, mapenzi yao yalivyokuwa, alivyojisikia baada ya kuona picha za Wema na Diamond, maisha yake ya sasa na mipango yake ya mwaka huu.
CHANZO BONGO 5

KUMBE MIMBA YA ODAMA NI YA KIGOGO SERIKALINI!

Jennifer Kyaka ‘Odama’.
Stori: Musa Mateja
Imevuja! Kumbe kile ‘kibendi’ cha staa wa sinema za Kibongo, Jennifer Kyaka ‘Odama’ ni cha kigogo mmoja serikalini na ndiyo sababu kubwa ya mwigizaji huyo kufanya siri nzito juu ya ujauzito huo.
Kama mbu aenezavyo ugonjwa wa malaria, ndivyo rafiki wa karibu na msanii huyo alivyotunyetishia juu ya usiri huo huku akisisitiza hifadhi ya jina.
Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wetu mwanzoni mwa wiki hii, rafiki huyo alisema kwa sauti tulivu kuwa mimba ya Odama ni ya bosi mkubwa wa moja ya wizara nyeti hapa nchini (jina na wizara vinavunda kwenye droo zetu) na kwamba moja kati ya masharti magumu aliyompa ni kuhakikisha jambo hilo linabaki kuwa siri hadi Yesu atakaporudi.
 
Ilisemekana kuwa usiri huo unatokana na madai kwamba kigogo huyo ni mume wa mtu.
Akiendelea kumwaga mchele kwenye kuku wengi, ‘kikulacho’ huyo alisema licha ya Odama kupata huduma zote bora anazostahili mjamzito lakini hana raha kwani furaha ya mjamzito ni pamoja na kumnadi mhusika wa ‘mzigo’ jambo ambalo limekuwa likimnyima raha.

HAPPY BIRTHDAY NICOLAUS TRAC


BENKI YA CRDB TAWI LA UBUNGO YASHEREHEKEA KUTIMIZA MIAKA 2

 Keki iliyoandaliwa na uongozi wa Benki ya CRDB tawi la Ubungo kwa ajili ya sherehe za kutimiza miaka 2 tangu kuanzishwa kwa tawi hilo, ambapo wateja wa benki hiyo walijumuika na wafanyakazi wa tawi hilo kusherehekea kwa pamoja.
 Meneja Mwandamizi wa Benki ya CRDB anayeshughulika na wateja wadogo na wa Kati, Eribariki Masuke, akikata keki wakati wa hafla ya kutimiza miaka 2 kwa tawi la Benki ya CRDB Ubungo. Kulia ni Meneja wa CRDB tawi la Ubungo, Oswald Kweka na wa pili kulia ni Ofisa wa benki hiyo, Angelitha Msaki.
 Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Ubungo, Oswald Kweka akizungumza  na wateja wa tawi hilo wakati wa hafla ya kutimiza miaka  2 tangu kuanzishwa kwa tawi hilo. Hafla hiyo ilifanyika Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Meneja Mwandamizi wa Benki ya CRDB anayeshughulika na Wateja Wadogo na wa Kati, Eribariki Masuke. 
 Meneja Mwandamizi wa Benki ya CRDB anayeshughulika na wateja wadogo na wa Kati, Eribariki Masuke, akikata keki wakati wa hafla ya kutimiza miaka 2 kwa tawi la Benki ya CRDB Ubungo. Kulia ni Meneja wa CRDB tawi la Ubungo, Oswald Kweka na wa pili kulia ni Ofisa wa benki hiyo, Angelitha Msaki.
Meneja Mwandamizi wa Benki ya CRDB anayeshughulika na wateja wadogo na wa Kati, Eribariki Masuke (kulia), akimkabidhi zawadi mmoja wa wateja wa benki ya CRDB tawi la Ubungo, wakati wa hafla ya kutimiza mika 2 tangu kuanzishwa kwa tawi hilo. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
Meneja Mwandamizi wa Benki ya CRDB anayeshughulika na wateja wadogo na wa Kati, Eribariki Masuke (kulia), akimkabidhi zawadi mmoja wa wateja wa benki ya CRDB tawi la Ubungo, wakati wa hafla ya kutimiza mika 2 tangu kuanzishwa kwa tawi hilo. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
Mteja wa Benki ya CRDB, Ester Lawrance (kushoto), akipokea zawadi kutoka kwa Meneja Mwandamizi wa Benki ya CRDB anayeshughulika na wateja wadogo na wa Kati, Eribariki Masuke wakati wa hafla ya kutimiza miaka 2 tangu kuanzishwa kwa benki hiyo.
Maofisa wa Benki ya CRDB wakipata keki wakagti wa hafla hiyo.
Karibuni wateja wetu....Meneja Mwandamizi wa Benki ya CRDB anayeshughulika na wateja wadogo na wa Kati, Eribariki Masuke akiwapa keki wateja wa benki hiyo waliofika katika tawi la Ubungo.

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate