Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Palycarp Kardinali Pengo amekema ndoa za jinsi moja na zile za mkataba kwa sababu ni kinyume cha maadili ya dini zote na zinachangia kuharibu familia.

Akizungumza katika sikukuu ya mapadri na kubariki mafuta ya krisma katika Kanisa la Mtakatifu. Joseph, Dar es Salaam, Pengo alisema ndoa za mkataba zinachangia kwa kiasi kikubwa wanandoa kutokuwa waaminifu na kujiingiza katika vitendo viovu ambavyo vinazaa familia ambazo hazina maadili.