EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, July 29, 2015

Wema skendo za ngono basi!

WEMA3 Staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ akiwa na mashabiki wake.
Waandishi Wetu
Kufuatia kupigwa mwereka kwenye Ubunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Singida, staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amekiri kwamba kilichomponza katika kinyang’anyiro hicho ni skendo za ngono hivyo kwa sasa atakuwa makini ili asichafuke.
MAPOKEZI
A photo posted by 👄wemasepetu👄 (@wemasepetu) on
Akizungumza na gazeti hili baada ya kupokelewa kishujaa na kuacha historia jijini Dar aliporejea kutoka Singida wikiendi iliyopita, Wema alisema mashabiki wake hawatamsikia tena na skendo hizo huku akiahidi kuibuka na bonge la ‘surprise’.
UMAKINI
“Shukurani zangu zipo palepale kwa mashabiki wote wanaonisapoti.
“Ninachowaahidi kwa sasa ni kuwa makini na skendo lakini pia kuna kitu cha kushtua nitafanya hivi karibuni ambacho kitaibua surprise (mshtuko) nzito kwa mashabiki wangu,” alisema Wema.
wemaMashabiki wakiwa na Wema wakati wa mapokezi.
TEAM WEMA
Katika mapokezi hayo ambayo gazeti hili lilikuwa mstari wa mbele, makundi ya mashabiki wake na yale ya Team Wema yalipeana taarifa kupitia mitandao ya kijamii kuwa kipenzi chao, Wema angefika Dar, Jumapili iliyopita ambapo taarifa zilisema kuwa walikutana kimyakimya na kuandaa mapokezi ya Madam.
Mishale ya saa 7:00 mchana ndipo Team Wema na mashabiki wake wengine walianza kumiminika maeneo ya Kimara-Baruti jijini Dar wakiwa na mabasi ya kukodisha, pikipiki na magari binafsi ambapo shamrashamra za kila aina zilifanyika.
KIBAO-KATA
Pia kulikuwa na ngoma ya Kibao-Kata, michezo ya pikipiki huku nyimbo za kumsifu Wema zikiimbwa.
Kama hiyo haitoshi, amshaamsha hiyo ilikuwa ikifanywa kila sehemu ambapo mastaa walikuwa wakitokea maeneo hayo kwa ajili ya kumsapoti Wema.
SHANGWE
Umati uliojitokeza walianza kulipuka kwa shangwe baada ya kumuona Meneja wa Wema, Martin Kadinda aliyeingia katika eneo hilo akifuatiwa na Petit Man ambaye alifuatana na wasanii wa Bongo Fleva, Mirror na Suma Mnazareti.
MJAMZITO
Mashabiki hao wa kila kada huku watoto wakifurika kumuona Wema walionekana kuwa na mapenzi ya hali ya juu huku mama mmoja mwenye ujauzito mkubwa akionekana akijichanganya kila kona bila kujali hali yake.
WEMA ENEO LA TUKIO
Wema aliingia katika maeneo hayo (Kimara-Baruti) akiwa ndani ya gari aina ya Toyota Land Cruiser ambapo alishuka na kuingia ndani ya BMW lililoletwa kumpokea ambapo alitokea kwenye paa na kuanza kusalimia mashabiki wake waliolipuka kwa furaha na wengine wakiangua kilio cha furaha.
MABUSU
Kuna wengine walishindwa kujizuia wakajikuta wakimfuata Wema wakimbusu na kumshika nywele zake kama vile siyo binadamu.
CHENI NA PETE
Wema alilazimika kugawa cheni na pete zake za dhahabu kwa mashabiki wake ili kuwatuliza huku akiwashukuru kwa kumpokea na kuwaaga kuwa anakwenda nyumbani kwake Kijitonyama ambapo msafara wake ulisababisha foleni ya zaidi ya robo saa njia nzima ambapo alikuwa akisindikizwa na pikipiki.
“Yaani Madam amepokelewa na watu kama rais vile, duh! Sijawahi kuona, amekosa ubunge lakini shamrashamra yake kama vile ameshinda!” Alisema mmoja wa mashabiki wa Wema aliyevalia fulana zenye nembo iliyoandikwa ‘Wema’.
KINACHOONEKANA
Habari zilieleza kwamba, kinachoonekana Wema anajipanga upya ili kujiimarisha kisiasa kwa ajili ya baadaye hivyo atajitahidi kuwa mbali na skendo hasa za wanaume.
TUJIKUMBUSHE
Huko nyuma Wema aliwahi kuripotiwa kubadili wanaume mbalimbali wakiwemo; Jumbe Yusuf Jumbe, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’ na CK.
Deogratius Mongela, Chande Abdallah na Musa Mateja

Tuesday, July 28, 2015

Lowassa rasmi Chadema, akabidhiwa kadi, asema hausiki na Richmond



















https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi6e8KYhLudE3B-REXw0lhxrh5esCf1GfSrdW6oG7Wjo02yoJpPsm8Npte9tCJmuFXuV9TC5QJArAVQiz_NXK39GBP8G4j4R85_hZixsNsPqVQkWBPsvxUOIMA3dxURwJ0FkGICvLajdfuB/s1600/MMGL0450.jpg


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjDeOmP_aTfLoeabLvXLQ8INYWJds1OBXAdinGivkey1BDZOvW00ntLs6YxCjOX06duGExfPoTNMrTBurlc4x9kSmk2RjxuZMkZEiaZCgqAWdkgiIBn7y0ul_bG8z9K273cZK5pMox7XR8q/s1600/MMGL0364.jpg


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjDeOmP_aTfLoeabLvXLQ8INYWJds1OBXAdinGivkey1BDZOvW00ntLs6YxCjOX06duGExfPoTNMrTBurlc4x9kSmk2RjxuZMkZEiaZCgqAWdkgiIBn7y0ul_bG8z9K273cZK5pMox7XR8q/s1600/MMGL0364.jpg


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEifQLnkItPZnRhqLTDka06dwLir5a25mcJ9RwD-NLUzcxTJ3vGioVdgwn0fjSmAvif9KM3KkQ3AvSkWjf6y_uv0e4cNc8uyC4DbENdq8IxpIQlCJiYP1H6MLj9CZ9i7JARXX7NYd6KErkzk/s1600/MMGL0471.jpg


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj0_AtenT7xwWsCcaLV8LYC5jYMSluDGJGwwUBSQOOPWAgCuf3QcKtU6Jy7PccTWFTXkTD16FKewqilywjFEPc2tAjQdM8VVqp0kDwUdZAs4YwCKepDxxFg9m9oDc38p6RCGUw2KXw1p9BH/s1600/MMGL0516.jpg






BVR Dar, sasa ni mateso

AWananchi wakiwa katika foleni ya kujiandikisha kupiga kura. 
Na Shani Ramadhani
WAKATI zoezi la uandikishaji kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa kutumia mfumo wa kielekrtioniki uitwao Biometric Voters Registration (BVR), jijini Dar es Salaam ukiendelea, mengi yameibuka kwenye baadhi ya vituo vya uandikishaji na kuwafanya wananchi wengi kukata tamaa wakidai kuwa zoezi hilo kwao sasa ni mateso.
IMG_1067Wananchi kadhaa waliohojiwa na gazeti hili walisema zoezi hilo la uandikishaji ni gumu kwa sababu baadhi yao huamka saa sita usiku kuwahi vituoni lakini baadaye wanajikuta wakiandikishwa siku ya pili.
Mama mmoja aliyekutwa Kituo cha Shule ya Msingi Kisiwani, Ubungo Dar, Mariam Ally alisema katika kituo hicho Jumamosi iliyopita wananchi walipigana kutokana na mwingiliano wa namba zinazotolewa kwa kila anayefika kujiandikisha.
2 (4)Mwandikishaji akiandikisha wapiga kura kwenye mfumo wa BVR.
“Kuna watu walifika saa sita usiku, lakini asubuhi walipofika wakakuta waliochelewa wanaandikishwa, fujo ilitokea ikabidi polisi kuitwa wakaweka mambo sawa, kifupi ni kwamba haya ni mateso,” alisema Mariam.
Nao wananchi waliokutwa katika Kituo cha Kimara walisema kuwa katika kituo hicho watu hukesha.
2 (5)…Akichukuliwa alama za vidole.
Mkazi wa eneo hilo, Massawe J. Massawe alisema japokuwa amepata kitambulisho cha kupigia kura lakini alifika kituoni hapo saa tisa usiku.
 “Ilinibidi niamke mapema ili niwahi kupata kitambulisho lakini tangu saa 9 usiku nilivyoamka nimekuja kupata kitambulisho saa 6 mchana, kiukweli watu wanateseka sana hasa wale wenye watoto wadogo na wazee, hawapewi kipaumbele na wananchi.

Monday, July 27, 2015

Binti wa Whitney Houston, Bobbi Kristina afariki dunia

bobbi 2
Bobbi Kristina Brown amefariki akiwa na miaka 22.
BINTI wa marehemu Whitney Houston, Bobbi Kristina Brown amefariki dunia jana baada ya kupoteza fahamu kwa muda wa miezi sita tangu alipokutwa taabani bafuni.
bobbi na whitneyMama na mwana: Whitney Houston akiwa na Bobbi Kristina mwaka 2011.
Bobbi amekufa akiwa na umri wa miaka 22, huku akivutiwa kuwa muigizaji na mwimbaji mahiri na mwenye ubora wa aina yake.
Msemaji wa familia ya marehemu, Kristen Foster amesema Bobbi amefariki akiwa amezungukwa na familia yake,”hatimaye yuko salama sasa kwenye mikono ya Mwenyezi Mungu, tunawashukuru wote walioungana nasi katika maombi na kuonesha upendo kwa miezi michache iliyopita”.
bobbi na nickBobbi Kristina akiwa na mpenzi wake Nick Gordon mwaka 2012.
Bobbi ambaye alikuwa amepoteza fahamu tangu akutwe ameanguka bafuni Januari 31, mwaka huu na kuwekwa kwenye matibabu huku akiwa amepoteza fahamu na mpaka kifo chake kumkuta alikuwa hajapata fahamu bado.
bobbi 3
Itakumbukwa kuwa miaka mitatu iliyopita mama yake Bobbi, Whitney Houston alikutwa pia bafuni akiwa amepoteza fahamu baada ya kuzidisha kiwango cha dawa za kulevya na pombe na baadaye kupoteza maisha.
Bobbi alikuwa mtoto pekee wa Whitney Houston na Bobby Brown, magwiji wa muziki wa miondoko ya R&B.

Urais: Ukawa kimeeleweka

27th July 2015
Chapa
Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa.
Hatimaye mchakato wa kumpata mgombea urais kupitia vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) umefikia ukingoni na sasa jina la mgombea huyo linatarajiwa kuwekwa hadharani wakati wowote kuanzia sasa.
 
Taarifa kutoka chanzo kimoja miongoni mwa vigogo wa Ukawa ziliiambia NIPASHE jana kuwa, kazi kubwa ya uteuzi wa jina hilo iliyohusisha wakuu wa vyama vinavyounda Ukawa imeshakamilika na kwamba kilichokuwa kikisubiriwa kabla ya kutangazwa kwa jina la mgombea ni maridhiano ya ndani ya vyama; kazi ambayo pia ilikamilika mwishoni mwa wiki. Ukawa unaundwa na muungano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama cha Wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi na NLD.
 
"Watanzania wanaopenda mabadiliko hawana sababu ya kuwa na hofu. Wakati wowote kuanzia leo (jana) jina la mgombea wetu tutaliweka hadharani na baada ya hapo tutaendelea na maandalizi yetu kabambe kuhakikisha kuwa tunahitimisha utawala wa CCM," chanzo hicho kiliiambia NIPASHE jana kwa sharti la kutotajwa. Uhakika wa kuelekea ukingoni mwa maridhiano kuhusu jina la mgombea wa Ukawa umetokana pia na kile kinachodaiwa kutokea kwenye kikao cha Baraza Kuu la CUF kilichofanyika juzi visiwani Zanzibar na pia kikao cha Kamati Kuu Maalum ya Chadema kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam.
 
Inaelezwa kuwa wakuu wa CUF wamekwishajadili kwa kina suala la Ukawa na kimsingi wameridhia maamuzi kadhaa yatakayoupa nguvu umoja huo, huku Chadema kupitia kikao chake cha jana ikiridhia pia jina la mgombea kupitia majadiliano yao yaliyohusisha ajenda mbili kuu, ambazo ni maandalizi ya uchaguzi na taarifa za mchakato wa uteuzi wa wagombea wa nafasi za ubunge na udiwani unaoendelea nchini kote. Aidha, imeelezwa kuwa kilichobaki hivi sasa ni masuala madogo ambayo yanaendelea kufanyiwa kazi kupitia vikao mbalimbali vinavyoendelea miongoni mwa vyama vinavyounda Ukawa kabla ya kumtangaza mgombea huyo.
 
Hata hivyo, hakuna kiongozi yeyote kutoka miongoni mwa vyama vinavyounda Ukawa aliyepatikana kuzungumzia rasmi suala hilo. 

Nec, Msajili wa Vyama wamuogopa Magufuli

Dk. John Magufuli.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, vimepata kigugumizi na kutupiana mpira kuhusiana na ufafanuzi juu ya madai kuwa mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, anakiuka sheria na kanuni za uchaguzi mkuu kwa kuanza kampeni kabla ya wakati.
 
Dk. Magufuli amekuwa katika ziara kwenye maeneo mbalimbali nchini katika kile ambacho chama chake kinaeleza kuwa ni kumtambulisha kwa wananchi baada ya kuibuka mshindi katika mchakato mkali wa kumpata mgombea urais wa CCM uliohusisha makada 38 kitendo kinacholalamikiwa na baadhi ya wapinzani kwa madai kuwa huko ni kuanza kampeni kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanjyika Oktoba 25, mwaka huu.
 
Baada ya kuteuliwa kwake, Magufuli ameshafanya mikutano ya hadhara ya kujitambulisha katika mikoa ya Dodoma, Dar es Salaam, Mwanza, Geita, Shinyanga, Morogoro, visiwani Zanzibar na pia mkoani Pwani na mara kadhaa amesikika akiahidi mambo mazuri kwa Watanzania, huku ahadi yake kubwa kwa wanachama wa CCM na wananchi wengine ikiwa ni "Sitawaangusha".
 
Katika kufahamu kama kinachofanywa na mgombea huyo kipo ndani ya kanuni na sheria ya uchaguzi, NIPASHE iliwasiliana na viongozi wa Nec na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa nyakati tofauti, ambao walitoa maelezo ya kutupiana mpira.
 
 Mwenyekiti wa Nec, Jaji Mstaafu, Damian Lubuva, alipoulizwa kama kinachofanywa na mgombea urais huyo CCM ni sahihi, alisema mikutano inayofanywa na Dk. Magufuli ni ya ndani ya chama, hivyo tume hiyo haina mamlaka ya kuingilia.
 
 Lubuva alisema NEC itaanza kuzifuata sheria na kanuni za uchaguzi Agosti 21 baada ya tume hiyo kupitisha rasmi uteuzi wa wagombea wa vyama vyote kufanyika.
 
“Kinachofanywa na mgombea urais wa CCM ni suala ambalo lipo ndani ya chama chao, kama tume hatuwezi kuingilia ni mambo ya ndani ya chama, uteuzi ukifanyika ndipo tume itaanza kuangalia kama kanuni na sheria zinafuatwa na wagombea, wa kuwauliza kwa sasa ni Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa,” alisema.
 
Wakati Nec wakitoa maelezo hayo, Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, Sixtus Nyahoza, alisema suala la wagombea na kampeni siyo kazi ya ofisi yake bali ni  Nec.

Saturday, July 25, 2015

WEMA SEPETU ABWAGWA SINGIDA


Koleta: Nachukia wanaojirahisisha kwa wanaume

f28fpombeMsanii mkali wa filamu za Kibongo, Coletha Raymond ‘Koleta’.
WIKI hii katika Dukukudu la Staa, tupo na msanii mkali wa filamu za Kibongo, Coletha Raymond ‘Koleta’ akizungumzia tabia ya wanawake kujirahisisha kwa wanaume.
“Nachukia sana tabia ya wanawake kujirahisisha, kujibweteka kwa wanaume, sipendi wanawake wasiopenda maendeleo kwa kutafuta vya kwao. Nawachukia pia watu wanafiki, wapenda majungu, wanaojifanya wananifahamu zaidi na kuongea uongo juu yangu, wakati hawanifahamu,” aliweka nukta Koleta.

Wagombea Urais UKAWA bado? Wajawazito feki kwenye BVR, Rufaa ya akina Mramba


story_News-in-Brief
MWANANCHI
Wakati leo saa 10 jioni ndiyo muda wa mwisho uliopangwa kurejesha fomu za kuomba kuteuliwa kuwania Urais ndani ya CHADEMA, hadi sasa hakuna mwanachama hata mmoja aliyejitokeza kuzichukua.
Hali hiyo inazidisha sintofahamu iliyougubika mchakato wa Urais ndani ya chama hicho na ndani ya UKAWA, kuwa huenda kuna ‘mtu wa nne’ anayesubiriwa kutoka nje ya chama hicho japo kuhusu Viongozi na Wabunge wa chama hicho walisema Edward Lowassa anakaribishwa mradi tu afuate kanuni na taratibu.

Shamsa ajitetea skendo ya kuhongwa simu

shamsa_ford
Staa wa sinema za Kibongo, Shamsa Ford.
Gabriel Ng’osha
STAA wa sinema za Kibongo, Shamsa Ford amefunguka kuwa ameeleweka vibaya alipoandika mitandaoni kuwa hajawahi kununua simu za bei mbaya zaidi ya kupewa na watu.
Baada ya kuweka maneno hayo na watu kumnanga kuwa amezoea kuhongwa na hajawahi kununua simu za ‘maana’, alizungumza na mwanahabari wetu na kufafanua:
“Kiukweli simu nyingi za kisasa nimekuwa nikipewa na ndugu, jamaa na marafiki na si kuhongwa na mabwana kama wengi walivyomsema,” alisema Shamsa.

Utata mpya mtoto wa Diamond!

Diamond-Platnumz-na-Zari
Staa wa Bongo Fleva,  Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’,  akiwa katika pozi na mpenzi wake Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
MUSA MATEJA
Utata mpya umeibuka wakati mama kijacho wa staa wa Bongo Fleva,  Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’,  akitarajiwa kujifungua muda wowote kutoka sasa, ishu ni juu ya uraia wa mtoto atakayezaliwa.
TUJIUNGE NA MTU WA NDANI
Habari kutoka kwa mtu wa ndani wa familia hiyo zilidai kwamba, utata umezidi kuigubika familia hiyo kwa kile kinachodaiwa kuwa ndugu wa pande zote kuendelea kuvutana juu ya Zari ajifungulie nchi gani kati ya Tanzania, Uganda na Afrika Kusini ‘Sauz’.
DIAMONDZARI.jpg
Utata huo umevuja wakati paparazi wetu akiwa katika mishemishe za kutaka kujua Zari alipo kwa sasa na atajifungulia katika hospitali ipi ndipo alipopenyezewa ‘ubuyu’ kwamba hadi sasa kuna utata mkubwa katika familia hiyo.
MABISHANO YA URAIA
Chanzo kilimweleza mwanahabari wetu kuwa, kikubwa ni mabishano ya uraia na sehemu sahihi ya kujifungulia mtoto huyo.
Kilidai kwamba, suala hilo limekuja kufuatia ndugu wa Zari kutaka ajifungulie Sauz jambo ambalo Diamond na familia yake wamekuwa wakilipinga vikali.
ZARINADIAMOND4.jpg
ZARI NJIA PANDA
Ilisemekana kwamba, kwa upande wake Zari amekuwa njia panda kutokana na shinikizo hilo huku mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ naye akisisitiza kuwa lazima Zari ajifungulie Bongo ili amuhudumie mkwe wake huyo.
“Yaani ndugu wa Zari wanampa Diamond wakati mgumu sana kutokana na kuendelea kung’ang’ania Zari akajifungulie kwao (Sauz ambako kuna ndugu wengi) wakati furaha ya Diamond ni kuona mtoto akizaliwa Bongo.

RAIS OBAMA: NAFURAHI KUREJEA KENYA

Thursday, July 23, 2015

Rap Festival ndani ya Dar Live

HIP-HOP-FESTIVAL

Riyama Ally alilia ndoa!

11419100_1453341164968186_1138492146_n

Lowassa amtia hofu Wema!

DSC00401Wema Sepetu alipokuwaakikabidhiwa fomu za kuwania ubunge viti maalum mkoa wa Singida leo mwishoni mwa wiki iliyopita.
DU! Kazi kwelikweli! Habari ya mjini kwa sasa ni mtoto mzuri Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ kuwania Ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), lakini nyuma yake kuna habari zinazodai kuwa mrembo huyo ameingiwa na hofu ya kukatwa jina kama ilivyotokea kwa Mbunge wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa aliyekuwa mmoja wa watia nia ya kugombea urais, Amani lina mkanda kamili.
edward-lowassaAliyekuwa Mbunge wa Monduli na mmoja wa watia nia ya kugombea urais kwa tiketi ya CCM walioenguliwa, Edward Ngoyai Lowassa.

Download Shilole & Nuh Mziwanda – Ganda la Ndizi

Shiwonder-Ganda-la-Ndizi-1024x1024

Shamsa ford alinadi penzi lake!

11352043_1433727903613936_1212634612_n
Mwigizaji Shamsa Ford.
Brighton Masalu
Mwigizaji Shamsa Ford amefunguka kuwa kwa sasa hahitaji mwanaume asiyekuwa na mkwanja, hivyo anaangalia mwenye ‘mavumba’ huku akidai kuwa mwanaume lofa ni kujitwisha msongo.
Akistorisha na paparazi wetu hivi karibuni, Shamsa alisema kuwa, amekuwa akiingia kwenye uhusiano na wanaume wasiokuwa na ‘mpunga’ kwa muda mrefu na kuambulia maumivu na mawazo yasiyokuwa ya lazima hivyo ni bora aumizwe na mwanaume mwenye fedha.
11377440_1605623056347418_815159447_n
“Kwa sasa sihitaji kabisa mwanaume lofa, nataka mwenye ‘nyekundu’,  nipo tayari kwa muda wowote lakini si kurudi kwa wanaume wasiokuwa na kitu,” alisema Shamsa.

Chadema yaja na mbinu mpya kudhibiti mamluki

Kauli hiyo imetolewa jana na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod Slaa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya Magomeni, Jijini Mwanza.
 Mbunge wa Kahama Mjini, James Lembeli (kushoto) akiwa na Ester Bulaya aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Mara
“Mwaka huu hakuna kupita bila kupingwa, wagombea wetu wote tutawasainisha mahakamani na wakishindwa kurudisha fomu, tutawashughulikia mahakamani,” amesema Dk. Slaa na kuongeza;
“Waliochukua fomu hatutaki kesho mmoja amejitoa, kama unataka kujitoa ondoka leo, ruksa.”
Mkutano huo umehudhuriwa na wabunge na viongozi mbalimbali wa chama hicho akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika, Makamu Mwenyekiti Bara, Prof. Abdallah Safari; Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA), Halima Mdee.
Katika mkutano huo, wanachama wapya kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) walitambulishwa, wanachama hao ni James Lembeli aliyekuwa Mbunge wa Kahama Mjini na Ester Bulaya ambaye alikuwa Mbunge Viti Maalum kutoka Mkoa wa Mara.
Kwenye mkutano huo Dk. Slaa amesema, sasa hivi Chadema ipo sehemu yote ya nchi hivyo hakuna mahali ambapo chama hicho kitashindwa kusimamisha mgombea na kwamba, Ijumaa wiki hii watamaliza uteuzi kwenye majimbo yote Tanzania.

Stori zote zenye uzito kwenye #Magazeti ya Tanzania JULY23 2015 ziko hapa, Udaku, Michezo na Hardnews

DSC09931
Good morning mtu wangu..
Kutoka Dar es Salaam Tanzania leo Alhamisi July 23 2015 tayari nimeyakusanya Magazeti yote na stori zake kubwakubwa kukusogezea hapa, headlines baada ya headlines kwenye Magazeti ya Udaku, Michezo na Hardnews, zote ziko hapa.
DSC09929
DSC09930
DSC09931

Wednesday, July 22, 2015

Baada ya vuta vikuvute ya muda mrefu, hatimaye leo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinatarajia kumtangaza mgombea wake wa urais katika mkutano maalumu utakaofanyika jijini Mwanza. Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na viongozi wa chama hicho Kanda ya Ziwa Magharibi na makao makuu zilisema kuwa leo mgombea huyo atatangazwa mkoani hapa huku zikibainisha kuwa anayepewa nafasi kubwa ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa. Taarifa hizo zimekuja wakati kukiwa na tetesi kuwa chama hicho kilikuwa kinafanya mazungumzo na waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa aliyekuwa anawania urais kupitia CCM na kutemwa katika hatua za awali, huku vyanzo mbalimbali vikisema mazungumzo hayo yanachukua muda mrefu na kuna uwezekano mkubwa wa kutozaa matunda. Jana, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe pamoja na baadhi ya wabunge walikaririwa wakitoa matamko ya kumkaribisha Lowassa kuingia Chadema lakini kwa sharti la kufuata kanuni na taratibu za chama hicho, lakini Dk Slaa alisita kumzungumzia kiongozi huyo akiahidi kuzungumza mambo yatakapokuwa sawa. Mratibu wa Operesheni za Chadema Kanda ya Ziwa Magharibi, Tungaraza Njugu alisema mgombea huyo (bila kumtaja jina), atatangazwa katika mkutano wa hadhara utakaofanyika kwenye Viwanja vya Magomeni, Ilemela kuanzia saa nane mchana. Njugu alisema katika mkutano huo, viongozi wakuu wa Ukawa wanatarajia kuwapo na maandalizi yake yamekamilika. “Kesho (leo) tutakuwa na mkutano mkubwa kwenye viwanja vya Magomeni,” alisema Njugu na kuongeza: “Mgombea urais kupitia Ukawa atajulikana hapo, kwani tunatarajia viongozi wakuu wa Ukawa watamtangaza.” Katika mazingira tofauti, akihutubia mkutano wa hadhara mjini Geita juzi, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alidokeza jina la Dk Slaa kama mgombea urais wa chama hicho, kitendo kilichoibua hamasa na umati kumshangilia, lakini akawapoza akisema ulimi umeteleza. Alipoulizwa kuhusu mkutano huo, Mwenyekiti wa NLD, Dk Emmanuel Makaidi alikiri kuwa leo kulikuwa na mpango wa kumtangaza mgombea wa Ukawa, lakini alidhani ingekuwa Dar es Salaam, hivyo kwa kuwa wameamua iwe Mwanza angefanya utaratibu wa ndege ili aweze kuwahi. Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi, James Mbatia hakupatikana kuzungumzia mkutano huo, lakini Katibu Mkuu wa chama hicho, Mosena Nyambabe alisema hakuwa na taarifa hizo, hasa kwa kuwa vikao vya mwisho vilivyofanyika Jumapili na Jumatatu vilihusisha wenyeviti wa vyama pekee. Hata hivyo, alisema ilibidi mgombea huyo atangazwe ama jana au leo. Chama cha CUF kimekwishatangaza kuwa kinasubiri uamuzi wa kikao cha Baraza Kuu la Uongozi litakaloketi Julai 25 kuamua juu ya hatima yake ndani ya Ukawa. Alipotakiwa kudokeza ni nani atasimama kuwakilisha Ukawa, Njugu alisema jukumu hilo ni la viongozi wa juu na kwamba yeye akiwa kiongozi wa Kanda anatambua mgombea urais wa Ukawa atatangaziwa Mwanza leo. Mkutano huo utakaorushwa moja kwa moja katika televisheni, pia unatarajia kumpokea Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Ester Bulaya aliyetangaza kukihama chama hicho juzi bila kuweka wazi anakohamia. Hata hivyo, mbunge huyo ambaye tayari ameweka wazi kupitia ukurasa wake wa Facebook kuwa atawania ubunge katika Jimbo la Bunda Mjini, amekaririwa akisema hatima yake itakuwa hadharani leo.


Baada ya vuta vikuvute ya muda mrefu, hatimaye leo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinatarajia kumtangaza mgombea wake wa urais katika mkutano maalumu utakaofanyika jijini Mwanza.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na viongozi wa chama hicho Kanda ya Ziwa Magharibi na makao makuu zilisema kuwa leo mgombea huyo atatangazwa mkoani hapa huku zikibainisha kuwa anayepewa nafasi kubwa ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa.

Taarifa hizo zimekuja wakati kukiwa na tetesi kuwa chama hicho kilikuwa kinafanya mazungumzo na waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa aliyekuwa anawania urais kupitia CCM na kutemwa katika hatua za awali, huku vyanzo mbalimbali vikisema mazungumzo hayo yanachukua muda mrefu na kuna uwezekano mkubwa wa kutozaa matunda.

Diamond: Aibu yao!

MSHTUKO! Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amefunguka siri nzito kwa mashabiki waliokuwa wakimpigia kampeni katika mitandao mbalimbali ili ashindwe kwenye Tuzo za MTV Africa Music (Mama) 2015, zilizofanyika usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita huko Durban, Afrika Kusini  baada ya kushinda tuzo moja na kudai kuwa ni aibu kwa waliokuwa wakifanya kampeni asishinde.
Diamond-MTVBase-Red-Carpet-03Diamond akiwa katika red carpet ya tuzo hizo.
DIAMOND MTUMBUIZAJI BORA AFRIKA
Diamond alitwaa Tuzo ya Best Live Act (Mtumbuizaji Bora Afrika) ambapo alijikuta akifurahi kupindukia huku akiwakejeli wale waliokuwa wakimpigia kampeni ashindwe kwamba bado ataendelea kuwakalisha vibaya.
WAMEBAKI NA AIBU
“Nina furaha sana kupata tuzo tena, wale waliokuwa wakipiga kampeni kwenye mitandao kwamba nisipigiwe kura naona wamebaki na aibu yaani nimewaumbua, hapa bado ninaongeza nguvu zaidi na nina mpango wa kufanya kazi na mastaa wakubwa wa Marekani, ila ninawashukuru wale walionipigia kura,” alisema Diamond.

Aunt na Wema wamezidi ‘kusherehesha’ bifu lao baada ya kupigana vikumbo kwenye mgahaw

shostMafahari wawili Bongo Movies, Aunt Ezekiel na Wema Sepetu ‘Madam’.
Imelda Mtema
MAFAHARI wawili Bongo Movies, Aunt Ezekiel na Wema Sepetu ‘Madam’ wamezidi ‘kusherehesha’ bifu lao baada ya kupigana vikumbo kwenye mgahawa unaojulikana kama Snow Cream na kuchuniana kama vile hawajuani.
wemasepetuWema Sepetu.
Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho kiliusoma ‘mchezo’ mwanzo mwisho, Wema ndiye aliyekuwa wa kwanza kuingia kwenye mgahawa huo na wapambe wake kisha baada ya muda kidogo kupita, Aunt pamoja na watu wengine nao walifika na kukaa meza nyingine.
auntezekiel1Aunt Ezekiel.
Habari zinazidi kudai kuwa baada ya Aunt kukaa, walitupiana macho na Wema bila kupeana salamu ingawa Wema hakuwahi kumuona mtoto wa Aunt tangu ajifungue.

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate