EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, May 31, 2013

HARAKATI ZA MSANII WA BONGO MOVIE JENNIFER KYAKA (ODAMA) KUWEKA MWILI SAWA.

MSANII M TO THE P AKIWA HOSPITALINI

Msanii M To The P aliyekuwa na marehemu Albert Mangwea, M To The P anaendelea vizuri na matibabu kama anavyoonekana kwenye picha hospitalini Helen Joseph huko Afrika ya Kusini.
Habari na CloudsFm.

FAMILIA YA ALBERT MANGWEA YATOA TAARIFA KUHUSU MABADILIKO YA RATIBA YA MAZISHI.

 
Habari zilizotufikia hivi punde kutoka kwa
msemaji wa Familia,ambae ni
Kenneth Mangwair,Kuwa mwili autowasili tena
 Tarehe 1 mwezi wa sita alasiri
kutoka nchini South Afrca......
kama ilivyotegemewa bali,utawasili siku ya Jumapili
tarehe 2 ya mwezi wa Sita
2013 alasiri.......
Hii imetokana na Watanzania waishio Nchini South
 Africa kuomba kwa Familia
nao kupewa nafasi kutoa Heshima za mwisho kwa Super
 Star huyo wa Muziki wa
Bongo......kwa mara ya mwisho katika safari ya mwisho
ya Ndugu yetu Albert Mangwair....

Endelea kutembelea Blog yetu ya IRENE MWAMFUPE JAMII official
updates zote za msiba
huu kwenye tasnia ya muziki wa Bongo,Albert Mangwair.....!!

JOKATE NISAMEHE NI MANENO YA DIAMOND NDANI YA TAKE ONE.

MKALI wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, ameibuka na kuelezea kuhusu uhusiano wake na mpenzi wake zilipendwa, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ ambaye ni mwigizaji na modo moto wa kuotea mbali Tanzania.
Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa na Jokate Mwegelo ‘Kidoti’.
Akizungumza kwa uhakika kabisa, Diamond alisema inampasa amuombe radhi Jokate kwa sababu katika uhusiano wao, Jokate hakuwahi kumkosea ila yeye ndiye tatizo na chanzo cha kuachana kwao.
 
Diamond alisema hayo kwenye mahojiano na Mtangazaji Zamaradi Mketema katika Runinga ya Clouds kwenye Kipindi cha Take One, kilichorushwa juzi Jumanne usiku kituoni hapo.

DIAMOND ANAFAFANUA
“Inanipasa nimuombe radhi Jokate. Ni kweli nilimtenda vibaya wakati wa mapenzi yetu. Hakukosea sana maana hakuwahi kufanya jambo lolote kinyume. Sijui niseme nini lakini nataka kueleza wazi kuwa mimi ndiyo sababu ya kuachana kwetu na ilitokea tu.
...Diamond na Jokate wakicheza.

“Naamini hilo jambo lilimuuma sana, maana nakumbuka wakati ule, baada ya mimi kurudi kwa Wema (Sepetu), watu walimwandama sana kwa maneno na alionekana msaliti lakini ukweli ni kwamba nilimpenda sana lakini ndiyo hivyo, siwezi kufafanua zaidi.
“Kutoka moyoni mwangu, namuomba msamaha Jokate, kama hatanisamehe nitaendelea kumuomba mpaka naingia kaburini. Sina raha kabisa kutokana na jambo hilo. Lazima niwe mkweli.”

JACQUELINE WOLPER
Diamond alikwenda mbali zaidi na kuwazungumzia baadhi ya wasichana aliowahi kutoka nao kimapenzi akiwemo mwigizaji Jacqueline  Wolper ambaye alisema ni mwanamke aliyempenda sana, ndiyo maana alimtungia wimbo wa Mawazo.

PENNY SASA
Kwa upande wa mpenzi aliye naye sasa, Mtangazaji wa Runinga ya DTV, Penieli Mungilwa ‘Penny’ alisema ni mwanamke mtulivu na sahihi kwake kwa sababu anatambua majukumu yake kwake, pia anamheshimu.
“Huyu kwa kweli ana karibu sifa zote alizonazo Wema ila uzuri wa Penny ananiheshimu sana. Hafanyi mambo yake hadharani. Unajua wakati nikiwa na Wema hata kama akifanya mambo yake siku mbili au tatu baadaye nayaona kwenye magazeti, tofauti na Penny ambaye kwangu mimi naona ananiheshimu, hata kama anafanya mambo yake ni kwa siri.”
CHANZO CHA HABARI NI GLOBAL PUBLISHERS.

YAH: MICHANGO YA MAANDALIZI YA MAZISHI YA ALBERT MANGWEHA

Kamati ya maandalizi ya msiba / mazishi ya msanii ndugu yetu Albert Kenneth Mangweha inapenda kutoa taarifa ya mchakati unaoendelea wa maandalizi ya mazishi, Kamati inahitaji michango yenu kwa ajili ya kufanikisha mazishi pale mwili wa marehemu utakapofika nchini Tanzani,kuanzia kuagwa kwa marehemu shughuli itakayofanyika jijini Dar es Salaam na kusafirishwa mjini Morogoro eneo la Kihonda kwa ajili ya Maziko.

Mpaka sasa ushirikiano tulioupata ni kampuni ya Clouds Media Group ambayo imebeba jukumu la kusafirisha mwili wa marehemu kutoka South Africa mpaka Tanzani, Bongo Records wameshachangia shilling milion 5 na Push Mobile wametoa million 5. Kamati inaomba wizara husika, mashirika, makampuni pamoja na watu binafsi kutoa michango yao katika kukamilisha jukumu la kumhifadhi katika nyumb yake ya milele ndugu yetu Albert Kenneth Mangweha.
Kwa wale wanaoweza kuchangia kupitia mitandao ya simu tuma kwa kaka wa marehemu Kenneth Mangweha namba zifuatazo:
Tigopesa - +255 717 553905
MPESA - +255 754 967738
Jina la akaunti: Kenneth B Mangweha
Namba ya akaunti: 2012505840
Benki: NMB
Tukitegemea ushirikiano wenu tunatanganguli shukrani za dhati

NECTA yatangaza Matokeo Kidacho cha SITA LEO.


Hoja ya ushoga bungeni

Dodoma. Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai ameahirisha mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, baada ya msemaji wa kambi ya upinzani kwa wizara hiyo kukataa kuomba radhi kulingana na maagizo ya kiti cha Spika.

Ndugai alikuwa amemwamuru msemaji huyo wa Upinzani, Ezekiah Wenje aombe radhi kwa kile alichoeleza ni kukashifu chama cha CUF na afute maneno ya kashfa hizo kwenye hotuba yake.

Wenje alikubali kutosoma maneno hayo yaliyokuwa kwenye hotuba hiyo lakini akakataa kuomba radhi kwa maelezo kuwa yaliyoandikwa ni ya ukweli na ana ushahidi.
Mbunge wa Nyamagana(Chadema), ambaye ni Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Ezekia Wenje, akitolewa nje ya Ukumbi wa Bunge na askari wa Bunge huku akionyesha alama ya ‘V’, baada ya wabunge wa CUF kutaka kumpiga, kutokana na hotuba yake waliyodai kuwaudhi wabunge hao. Picha na Emmanuel Herman.  

Awali wakati wa asubuhi pia Ndugai alilazimika kuahirisha kikao cha Bunge, baada ya kuzuka vurugu kubwa kati ya wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Chama cha Wananchi (CUF).

Vurugu hizo zilizuka baada ya Mbunge wa CUF (Mtambile) Masoud Salim, kutoa hoja ya kutaka Msemaji wa Kambi rasmi ya Upinzani bungeni katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ezekiel Wenje, kusitisha hotuba yake kwa kile alichoeleza kuwa “imejaa uzushi, uhuni, uzandiki, uongo na ushenzi.”
Salim alitoa hoja hiyo saa 6:15 mchana, wakati Wenje akiwa anasoma hotuba hiyo katika ukurasa wa tatu.

Taarifa ya uchunguzi juu ya kuteswa Kibanda

Kibanda, ambaye ni Mwenyekiti wa TEF, alitekwa na watu wasiojulikana Machi 5, 2013 mwaka huu na kukumbana na mateso karibu na maeneo ya nyumbani kwake, Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam.
Kutokana na hali hiyo, TEF iliamua kuunda timu ya watu watano kwa ajili ya kuchunguza tukio hilo na viashiria vya kutishia usalama wa wanahabari nchini.
Taarifa hiyo, ambayo pia ilisomwa na Mwenyekiti wa Kamati iliyofanya uchunguzi huo, Deodatus Balile kwenye mkutano wa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari uliofanyika mjini Tanga, imebainisha viashiria mbalimbali vilivyofanya Kibanda kukutana na zahama hiyo.
Pia imevitaka vyombo vya dola kufanyia kazi ripoti hiyo, ili kufuatilia viashiria vilivyoainishwa na wahusika wakamatwe.
Ifuatayo ni ripoti kamili ya uchunguzi:
Utangulizi:
Usiku wa Jumanne ya Machi 5 kuamkia Machi 6, 2013, Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari (2006) Ltd, ambaye pia Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda alivamiwa na kujeruhiwa vibaya akiwa nje ya lango la kuingilia nyumbani kwake Mbezi Juu, Dar es Salaam.

Tukio hilo lilishtua na kutikisa taifa kwa kiwango kikubwa si tu katika tasnia ya habari nchini, bali pia jamii kwa jumla hasa baada ya aina ya utekaji, utesaji na usiri uliotumika katika kufanikisha uhalifu huu kufanana kwa karibu na tukio lililomkuta Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tanzania, Dk. Stephen Ulimboka lililotokea karibu miezi tisa kabla ya tukio la Kibanda yaani, usiku wa Juni 26, 2012.

Ukiacha matukio hayo, miezi sita kabla ya Kibanda kutekwa na kuteswa Mwandishi Daudi Mwangosi, aliuawa akiwa mikononi mwa vyombo vya dola Septemba 2, 2012 huko Nyololo, Iringa akiwa kazini.
Tukio la Kibanda limekuwa na sura ya mwendelezo wa mauaji au utesaji wa wanahabari, hasa ikitiliwa maanani kuwa Mwandishi Issa Ngumba (45) wa Radio Kwizera aliyekuwa anafanyia kazi zake katika Wilaya ya Kakonko, Kigoma, Januari mwaka huu, alipigwa risasi na kuuawa katika mazingira ya kutatanisha.

Yanga yaongezewa mamilioni na Kilimanjaro Premium Lager, imewazadia sh milioni 25.

KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro Premium Lager, imewazadia sh milioni 25 mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, kwa kutwaa taji hilo.
Mbali na zawadi hiyo ya TBL, Yanga ilijihakikishia kitita cha sh milioni 70 kutoka kwa wadhamini wakuu wa ligi hiyo, kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom, kwa kuibuka mabingwa.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi hundi hiyo, Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe, alisema kwamba zawadi hiyo ni sehemu ya ahadi ya udhamini wao kwa timu itakayoshinda au kushika nafasi za juu.

“Kama wadhamini wa klabu kongwe za Yanga na Simba, tuliahidi kutoa sh milioni 25 kwa timu itakayotwaa ubingwa wa Ligi Kuu na sh milioni 15 kwa timu itakayoshika nafasi ya pili, hivyo kutokana na Yanga kutwaa ubingwa ndio tunaikabidhi fedha hizi,” alisema.
Kavishe aliongeza kuwa zawadi hiyo ni sehemu ya sh bilioni 1.5 za udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager kwa Yanga na imetolewa kwa lengo la kuhamasisha klabu kujitahidi kwa kushinda zaidi na kusaidia katika maandalizi yake kwa ajili ya mashindano ya kimataifa.

Sofapaka yazihofia Simba, Yanga.

UBORA wa klabu kongwe za Simba na Yanga, umeifanya timu ya Sofapaka kutoka Kenya kuleta kikosi chake chote ili kukabiliana nazo katika michezo ya kirafiki itakayopigwa hapa nchini.
                                                       Sofapaka kutoka Kenya.
Sofapaka inatarajiwa kutua nchini Juni 10 kwa ziara ya kimichezo, ikiwa na lengo la kuzipima klabu hizo kongwe zitakazokuwa katika maandalizi ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati maarufu kama Kombe la Kagame, itakayoanza kutimua vumbi Juni 18 hadi Julai 2, huko Sudan Kusini.

Akizungumza kwa simu kutoka Kenya, Meneja wa Sofapaka, Ngalambe Roberto, alisema kwamba hawana budi kuleta kikosi kamili ili kushinda michezo yake.

“Sisi tumejiandaa vizuri, tunazifahamu na kusoma kwenye mitandao kuhusu timu hizi, hivyo tutakuja na majeshi yote ili tushinde mechi zote mbili,” alisema Ngalambe.
Alisema Tanzania kuna timu nyingi nzuri zenye ushindani, lakini kwa Simba na Yanga ni zaidi, hasa kutokana na upinzani mkubwa uliopo kwa timu hizo mbili.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya Smartsports, iliyoandaa ziara hiyo, George Wakuganda, alisema Sofapaka itacheza mechi yake ya kwanza Juni 12 dhidi ya Simba, kabla ya Juni 13 kukwaana na Yanga. Mechi zote zitapigwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Madaktari wa mifupa warejea nchini

MADAKTARI Bingwa wanne kati ya 20 waliopelekwa nje ya nchi kwa nyakati tofauti kujifunza zaidi kuhusu upasuaji na utaalam wa mifupa wamerejea.

Kurejea kwa madaktari hao kulibainishwa jijini Dar es Salaam jana na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Seif Rashid wakati akifungua mafunzo ya upasuaji kwa madaktari bingwa 80 kutoka nchi mbalimbali Afrika.

Mafunzo hayo yanafanyika kwenye Kitengo cha Mifupa cha Hospitali ya Taifa Muhimbili (MOI) chini ya udhamini wa taasisi za Sign Fructure Care International, Chuo Kikuu cha Saint Francisco, 
AO Foundation zote za Marekani wakishirikiana na uongozi wa MOI.
“Serikali inalielewa tatizo la ukosefu wa wataalamu bingwa wa upasuaji na mifupa ndiyo maana tuliwapeleka 20 nje ya nchi kujiendeleza sasa wanne kati yao wamesharudi.

“…Lakini mchakato wa kuwaandaa wataalamu hawa ni mrefu kidogo, kwa sababu lazima wamalize masomo yao ya kawaida ya udaktari kabla ya kuwa wataalamu mabingwa,” alisema.
Hata hivyo, Naibu Waziri huyo alielezea juhudi za serikali kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazoikabili MOI na hospitali nyingine ikiwemo msongamano wa wagonjwa kutokana na ongezeko la ajali nchini.

MATOKEO MAPYA: Kidato cha nne majanga tena.

MATOKEO ya kidato cha nne ambayo serikali iliagiza yapitiwe upya na kufanyiwa uhakiki kwa vigezo vya miaka ya nyuma, yametolewa jana huku kukiwa na mabadiliko kidogo.
Matokeo hayo mapya yalionyesha hali bado ni mbaya kwani ni watahiniwa 30,000 tu kati ya 240,909 waliopata daraja sifuri ndiyo walionufaika na ‘mbeleko’ ya serikali.
Mabadiliko hayo yanaonyesha waliopata daraja sifuri wamepungua kidogo na sasa wamefikia 210,846.
               Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa.
Matokeo yanaonyesha kiwango cha ufaulu kimeongezeka kwa asilimia 9 ambapo mara ya kwanza ilikuwa asilimia 34.5 wakati hivi sasa ni asilimia 43.08.
Matokeo hayo mapya yanaonyesha kuwa takriban asilimia 61 ya watahiniwa walipata daraja sifuri awali sasa yamepungua na kuwa asilimia 56.9.

Akitangaza matokeo hayo kwa waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam, Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, alisema hali bado ni mbaya.
Kawambwa alisema kuwa jumla ya watahiniwa 480,029 walisajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana wakiwemo wasichana 217,587 sawa na asilimia 45 .33 na wavulana 262,442 sawa na asilimia 54.67.

Alisema watahiniwa waliofanya mtihani ni 458,139 sawa na asilimia 95.44 ambapo watahiniwa 21,890 sawa na asilimia 4.56 ya watahiniwa wote waliosajiliwa hawakufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali.

Majambazi yateka kijiji, yapora.

WATU sita wanaosadikiwa kuwa majambazi wakiwa na silaha wamevamia kijiji cha Mwamkulu, kilichoko wilaya ya Mpanda na kupora vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya sh milioni tisa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi, majira ya saa 2:00 usiku.

Alivitaja vitu vilivyoporwa kwenye tukio hilo kuwa ni pikipiki tatu zenye namba T964 BUZ aina ya SUNLG, T792 BWT aina ya Kiboko na T 452 BNZ aina ya Shanray zikiwa na thamani ya sh milioni 5.6.

Vitu vingine vilivyoporwa ni simu 16 za mikononi zenye thamani ya sh 720,000 , pesa taslimu sh milioni mbili za wafanyabiashara, katoni mbili za sigara zenye thamani ya sh 420,000 na vocha za simu zenye thamani ya sh 820,000.

Alisema polisi baada ya kupata taarifa ya tukio hilo walifika na kufanya msako mkali na kufanikiwa kukamata pikipiki tatu ambazo zilitelekezwa na majambazi hao baada ya kugundua wanafuatwa na polisi, simu moja ya Nokia yenye thamani ya sh 45,000 mali ya Shadrack Abel.
Alisema katika tukio hio maganda matano ya risasi aina ya SMG/SAR yaliokotwa, kwani majambazi hayo yalipiga risasi sita hewani kwa lengo la kuwatisha wanakijiji hao.

Thursday, May 30, 2013

Pata Matokeo ya Kidato cha Nne 2012

Baraza la mitihani Tanzania NECTA limetangaza rasmi matokeo ya Kidato cha Nne 2012. Idadi ya watahiniwa waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka jana imeongezeka kwa kati ya asilimia 20 na 23 baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), kufanya marekebisho alama za viwango vya ufaulu.

Matokeo hayo mapya yanaonyesha kuwa, ufaulu wa kuanzia daraja la kwanza hadi la nne umeongezeka kutoka asilimia 34.5 kwa matokeo yaliyotangazwa awali na huenda yakafikia asilimia 57.
 Hii inamaanisha kwamba watahiniwa wapatao 82,000 ambao awali walikuwa wamepata sifuri katika matokeo ya awali sasa wamepanda na kupata madaraja ya ufaulu katika matokeo mapya.
Kwa matokeo hayo, watahiniwa wa mwaka 2012 watakuwa wamefanya vizuri kuliko wa mwaka 2011, ambao watahiniwa 225,126 sawa na asilimia 53.37 ya 349,390 waliofanya mtihani huo walifaulu.

Matokeo ya awali yaliyotangazwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa yalionyesha kuwa kati ya watahiniwa 367,756 waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana, waliokuwa wamefaulu kwa daraja la kwanza mpaka la tatu walikuwa 126,847 sawa na asilimia 6.4. Waliopata daraja la nne walikuwa ni 103,327 sawa na asilimia 28.1.
Katika matokeo hayo, watahiniwa 240,909 sawa na asilimia 65.5 walipata sifuri, hesabu ambayo imebadilika katika matokeo mapya ambayo yanaonyesha kuwa sasa waliopata daraja hilo ni 158,100 ambayo ni asilimia 43.
Ili kupata matokeo hayo kwa urahisi na haraka zaidi tafadhali bofya link inayo onekana hapo chini.
Pata Matokeo ya Kidato cha Nne 2012 Fasta Hapa

Matokeo ya Kidato cha Nne 2012

Matokeo kidato cha nne yazidi kuibua mapya.

Dar es Salaam. 
Matokeo ya kidato cha nne yanayotarajiwa kutangazwa leo, yamezidi kuzua mapya baada ya Baraza la Mitihani nchini (Necta) kulazimika kutumia kanuni iliyofanya ufaulu upande kwa asilimia tisa kutoka 34 wa awali, lengo likiwa ni kuepusha watahiniwa waliokuwa wamefaulu mwanzo kufeli.

Kanuni iliyokuwa imetumika mwanzo, ilifanya matokeo hayo yapande kwa asilimia kati ya 20 na 23, kiwango ambacho Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete aliwaeleza wabunge wa chama chake Mei 19, mwaka huu mjini Dodoma.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kutoka ndani ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, wiki iliyopita maofisa wa wizara na taasisi zake wakiongozwa na Waziri Dk Shukuru Kawambwa, walijadili matokeo hayo.


                       Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk Shukuru Kawambwa.
“Wakati yakijadili, ufaulu bado ulikuwa kulekule kwenye zaidi ya asilimia 54, kutokana na kanuni hiyo wanafunzi kama 2,500 waliokuwa wamefaulu kwa madaraja ya juu walikuwa washuke,” kilisema.

Kutokana na hali hiyo, kwa sasa ufaulu ni asilimia 43 jambo linalofanya matokeo hayo yawe chini ikilinganishwa na mwaka 2011.

Sofapaka kuwapima wapya wa Yanga, Simba

Na Mwandishi Wetu

TIMU ya Sofapaka ya Kenya, inatarajia kuwasili nchini Juni 10, kwa ajili ya kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Yanga na Simba.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Kampuni ya Smartsports, George Wakuganda, amesema kuwa, mechi hizo zitakuwa nzuri kwa timu zote kuwajaribu wachezaji wapya.

“Hii itakuwa nafasi nzuri kwa timu zote kuwajaribu wachezaji wao wapya watakao wasajili kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara,” amesema.

Wakuganda amesema baada ya Sofapaka kuwasili jijini Dar es Salaam, itacheza mechi yake ya kwanza Juni 12 dhidi ya Simba, itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
“Sofapaka wataanza kucheza na Simba Juni 12, mwaka huu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, tunaamini Wekundu wa Msimbazi watatumia nafasi hii kuwaonesha mashabiki wao vifaa vyao vipya,” amesema.

Mkurugenzi huyo wa Smartsports, alisema Juni 13, kikosi hicho kutoka Kenya kitashuka tena uwanjani kuumana na mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Afrika Mashariki (Kombe la Kagame), Yanga.

Serikali kuchimba visima 1,300 nchini mwakani

Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Christopher Sayi amesema, zaidi ya vijiji 1,300 nchini vitajengewa visima vya maji safi na salama ifikapo mwaka 2014.
Sayi alisema hayo juzi usiku wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa kujadili jinsi ya kupunguza hatari ya upatikanaji wa maji na uendelevu wa huduma hiyo.

“Upatikanaji wa maji mijini unaongezeka na unaridhisha lakini kwa vijijini bado ni tatizo ambapo wizara inahakikisha ifikapo mwaka 2014 zaidi ya vijiji 1,300 katika kila vijiji 10 vitakuwa na visima vya maji,” alisema Mhandisi Sayi.

“Wadau wa sekta binafsi kwa kushirikiana nao uzoefu na mbinu mbalimbali tunaweza kufukia malengo ya huduma ya maji kupatikana kwa wingi na kwa ufanisi,” alisema Sayi.
Naye Balozi wa Ujerumani Nchini, Klaus-Peter Brandes ambaye nchi yake kupitia Shirika la
Maendeleo la (GIZ) ndio waandaaji wa mkutano huo alisema, wataendelea kujitolea kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya maji kwa nchi za Ukanda wa Jangwa la Sahara unaimarika.
Alisema katika ukanda huo,Tanzania imekuwa ikionyesha jitihada za kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma hiyo hivyo kuwa mfano kwa nchi za Jangwa hilo.

CUF wahojiwa kwa ghasia za Mtwara

Dar es Salaam.
Viongozi kadhaa wa CUF, wamehojiwa na Polisi kutokana na kile kinachodaiwa kuwa chama hicho kinashiriki kuchochea vurugu za Mtwara.

Taarifa za kuhojiwa kwa viongozi hao zilithibitishwa Dar es Salaam jana na Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro, wakati akizungumza na wandishi wa habari. Alisema hata hivyo hakuna kiongozi aliyekamatwa, akihusishwa na tuhuma hizo.
Alisema viongozi hao walihojiwa wiki iliyopita katika Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam na Mtwara.

“Waliohojiwa ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana ya CUF Katani Katani na Katibu wa Wilaya ya Mtwara mjini, Said Kulaga,” alisema.
Alisema chama hicho kilikuwa na taarifa za kina kuhusu mpango wa kuwakamata viongozi wa ngazi za juu kwa madai ya kuchochea vurugu hizo.

Full Interview P-Funk Akizungumzia Kifo Cha Marehemu Albert Mangwair

Waziri Nchimbi awahakikishia Tanzania ni salama

Dar es Salaam.
Serikali ya Tanzania imesema itahakikisha inaendelea kuimarisha hali ya ulinzi na usalama kwa Watanzania na raia wa kigeni waliopo na wanaoendelea kutembelea hapa nchini kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za binafsi na kimaendeleo ili watu wote waweze kutekeleza majukumu yao na kuishi kwa amani na usalama nchini.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi alisema hayo jana wakati akizungumza katika kikao baina yake na Ujumbe wa Wawakilishi wa nchi za Umoja wa Ulaya na mabalozi wa nchi hizo hapa nchini kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa wizara hiyo.

Taarifa ya wizara ilisema Nchimbi alisema kwa sasa Serikali kupitia polisi imejiwekea mikakati mbalimbali ya kukabiliana na vitendo vya uhalifu katika Jiji la Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.
‘‘ Polisi tayari imeanzisha dawati maalumu litakalowahudumia raia wa kigeni ili kuwawezesha kufungua kesi zao kwa urahisi, kuwapo kwa wepesi wa majadiliano na ziweze kushughulikiwa kwa haraka na hatimaye kupatiwa ufumbuzi”, alifafanua Waziri Nchimbi.

Waziri Nchimbi alisema pia katika kusimamia suala la ulinzi na usalama wa raia na mali zao kwa sasa wizara yake itafanya ukaguzi wa kampuni binafsi za ulinzi ili kuangalia na kujiridhisha kama zinakidhi viwango vya ubora vinavyotakiwa.

HOTEL NO. 1 KWA UBORA DUNIANI IPO TANZANIA- Singita Grumeti Reserves.

Singita Grumeti Reserves, Sasakwa Lodge
Ni nzuri kiukweli watembelee zaidi kujionea hapa Singita Grumeti Reserves
CHANZO CHA HABARI NI 2JIACHIE --www.2jiachie.com

Wednesday, May 29, 2013

Mrembo Zari Kutoka Uganda Ndio Huyu Aliyedai Hawezi Kushindana Big Brother Kwa $300,000.

Do you think $300,000 is a lot of money? Well, for many of us, that’s a fortune and we might even leave this terrible world without having ‘money we call our own’ half of that spondulicks (mouth-watering money). But as many Tanzanians say ‘Usiseme hatuna hela, sema mimi sina hela’ $300,000 is merely a peanut to the boss lady herself, Zari Hussein.
BCvgVIwCIAAYh5o
BD9-UvJCEAAxE8a
The beautiful Ugandan enterprenuer and singer, thinks three hundred thousand US dollars which is a grand price that Big Brother Africa contestants compete for, is a small amount of money you can spend in hours. As matter of fact, Zari owns a 389,500 car!! Did we forget to tell you that Zari drives a Lamborghini among other expensive toys?

Maajabu Agness Jerald ‘Masogange’ anasumbuliwa na tatizo la kuota ndoto mbaya usiku na kuamka kisha kutoka nje na kutimua mbio.

VIDEO Queen wa Bongo Fleva, Agness Jerald ‘Masogange’ anasumbuliwa na tatizo la kuota ndoto mbaya usiku na kuamka kisha kutoka nje na kutimua mbio, jambo ambalo kwa wengi linaweza kuonekana kuwa ni maajabu.
 
                                                        Agness Jerald ‘Masogange’.
Habari kutoka kwa sosi wetu, zinasema kuwa katikati ya wiki iliyopita, Masogange akiwa ndotoni, aliamka na kufungua milango na geti la nje kisha kutimua mbio umbali mrefu akiwa na nguo za kulalia na miguuni hana  viatu.

“Bahati nzuri ni kwamba, wakati anahangaika kufungua geti, rafiki yake aliyekuwa amelala naye alishtuka na kushangaa kukuta milango iko wazi. Alipotoka nje, akakuta Masogange ndiyo anamalizia kufungua geti kubwa na kuanza kukimbia hivyo akamkimbiza,” kilieleza chanzo chetu.
Akaongeza: “Lakini pia aliwapigia simu marafiki zake wengine na kuwajulisha juu ya tukio hilo, maana mwenyewe ilikuwa mara ya kwanza kumuona katika hali hiyo.”

MASOGANGE ANASEMAJE?
Risasi Mchanganyiko kama ilivyo kawaida yake ya kutokukurupuka, lilimsaka Masogange kwa simu na kufanikiwa ambapo alithibitisha tukio hilo na kufafanua kwamba liliwahi kumtesa kwa muda mrefu huko nyuma, likaisha.

“Ilikuwa hatari sana lakini namshukuru rafiki yangu kwa kunisaidia. Unajua hili tatizo liliwahi kunitesa sana wakati nikiwa mdogo lakini nilikwenda Mbeya nikapewa dawa tatizo likapotea kabisa hadi juzi liliporudi tena,” alisema.
Habari na Global Publishers.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO TAREHE 29/05/2013

13 215fe10 842369 c540e8 9eef57 02703

Ilala yatoa siku saba ghorofa litoke

Dar es Salaam.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imetoa notisi ya siku saba kwa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) pamoja na mmiliki wa jengo la ghorofa 16 lililopo Mtaa wa Indira Gandhi mkabala na Msikiti wa Shia Ithnasheri kulibomoa ndani ya kipindi hicho.

Ghorofa hilo linalomikiwa na mfanyabiashara maarufu nchini Ally Raza linabomolewa baada ya kuanguka kwa jengo pacha la aina hiyo Machi 29 mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 36, kujeruhi 18 na uharibifu wa mali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini jana, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa alisema kuwa, notisi hiyo imeanza Mei 27 hadi Juni 3 mwaka huu.

“Tayari tumewakabidhi NHC na Ally Raza mmiliki wa jengo la ghorofa 16 notisi ya siku saba ya kumtaka kubomoa jengo hilo ndani ya siku saba na asipotekeleza hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa,” alisema Silaa.

‘‘Kwa mujibu wa sheria ya mipango miji, mmiliki halali wa kiwanja hicho ni NHC, na wao ndiyo waliomuuzia Raza eneo hilo ili aweze kujenga ghorofa’’ alisema.
Kwa mujibu wa Silaa, kutokana na ramani iliyotolewa na mipango miji, maeneo yote ya Kisutu yanatakiwa kujengwa ghorofa 10 na si vinginevyo, lakini cha kushangaza, Mhandisi kutoka Bodi ya Wahandisi, msanifu majengo na makandarasi wameweza kusimamia ujenzi wa ghorofa 16 kinyume na taratibu.

Tiketi za mabasi kukatwa kwa njia ya simu.

KAMPUNI ya ACG-E-Bus Ticketing ya jijini Dar es Salaam imekuja na huduma ya kukata tiketi za mabasi yaendayo mikoani kwa njia ya mtandao wa simu za mkononi.

Huduma hiyo ambayo tayari imeshaanza, itakuwa dawa ya kuwaondoa wapiga debe ambao mara nyingi wamekuwa wakilalamikiwa na abiria kwa usumbufu.

Akizungumza jana, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Martin Kaswahili, alisema huduma itafanywa kupitia mitandao yote ya simu za mkononi na itaondoa usumbufu wa abiria kulazimika kufika Kituo cha Mabasi Ubungo kukata tiketi.

Kwa mujibu wa Kaswahili, kuanzishwa kwa huduma hiyo ni matokeo ya utafiti wa muda mrefu katika vituo vya mabasi vya miji mikubwa ya Ubungo, Dar es Salaam, Mwanza na Mbeya ambao umebaini kuwapo kwa urasimu na usumbufu wa abiria kupata tiketi za mabasi wanayotaka kusafiri nayo.

“Tulifanya utafiti katika sekta ya usafirishaji wa nchi kavu hasa mabasi, tuliongea na wenye mabasi, baadhi ya mawakala, abiria wenyewe na tukagundua tatizo kubwa la abiria waendao mikoani hasa katika vituo vya miji mikubwa kama vile Mwanza, Dar es Salaam, Mbeya na mikoa mingine ni urasimu wa kupata tiketi na abiria kusumbuliwa hivyo njia ya mtandao ni suluhisho kwao,” alisema Kaswahili.

JK aomba walimu toka Jamaica.

 
RAIS Jakaya Kikwete ameomba msaada wa walimu wa Hisabati na Sayansi kutoka nchini Jamaica ili kukabiliana na upungufu wa wataalam hao nchini.

Rais Kikwete alitoa ombi hilo juzi kwenye Hotel ya Sheraton mjini Addis Ababa, Ethiopia wakati wa mkutano wake na Waziri Mkuu wa Jamaica, Mama Portia Simpson Miller.

Ikulu ilisema kuwa Rais Kikwete alikuwa Addis Ababa kuhudhuria sherehe za miaka 50 tokea kuanzishwa kwa Umoja wa Afrika, Juni 25, 1963 na Mkutano wa 21 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa AU wakati Mama Simpson Miller alipokuwa mmoja wa viongozi mashuhuri wa nchi mbali mbali duniani walioalikwa kuhudhuria sherehe hizo.
Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu iliyosambazwa jana kwa vyombo vya habari, ilisema kuwa katika mazungumzo ya viongozi hao wawili, Mama Portia Simpson Miller ambaye aliapishwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamaica Januari 5, 2012 baada ya chama chake cha Peoples National Party (PNP) kushinda uchaguzi mkuu nchini humo, alimwuliza Rais Kikwete jinsi gani Jamaica inavyoweza kuisaidia Tanzania.

Kutokana na swali hilo, Rais Kikwete aliomba mambo mawili, mosi kupatiwa walimu wa masomo ya hisabati na sayansi pamoja na kocha wa riadha.

WIMBO KWA AJILI YA MAOMBOLEZO YA NDUGU YETU MANGWEA...


R.I.P Mangwea: SOMA CHANZO CHA KIFO CHA MSANII ALBERT MANGWEA.

 
Ngwea akiwa na msanii M to the P juzi south africa. Kuna taarifa za tetesi kuwa chanzo cha kifo cha ghafla cha rapper Mangweir ni kuzidisha madawa ya kulevya aliyotumia usiku wa kuamkia leo.  Hussein Original ambaye yupo Pretoria amesema Ngwear na M to the P ambaye walikuwa room moja wamekutwa wamezima baada ya kuzidhisha madawa ya kulevya... 
IRENE MWAMFUPE JAMII BLOG Bado tunafuatilia kwa karibu kujua sababu ya kifo chake.

Kibadeni sasa rasmi Simba

Dar es Salaam. 
Kocha Abdallah ‘King’ Kibadeni anaanza kazi rasmi Simba kesho ya kuinoa Simba kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na mashindano yajayo ya Kombe la Kagame.


Akizungumzia kuhusu kutua kwa Kibadeni katika klabu ya Simba, Kaimu Makamu wa klabu hiyo, Joseph Itang’ale alisema mkataba rasmi bado hawajasaini na Kibadeni ila wanatarajia kumpa mkataba wa miaka miwili au wa mwaka mmoja.


Kuhusu wana malengo gani na Kibadeni, Makamu huyo alisema Kibadeni ndiye kocha pekee ambaye ameshawapa ubingwa Simba mara tatu na alijenga timu ya vijana ya Simba ambayo mpaka sasa inafanya vizuri.


Akizungumzia kwa nini wameamua kuachana na kocha Patrick Liewig raia wa Ufaransa, Makamu huyo wa Simba alisema kocha Liewig alikuwa akibagua watu ndani ya klabu ya Simba na kujiona yeye ndiye yeye jambo ambalo lilikuwa likiwakera wachezaji, pia hajafanya kazi yake vizuri katika kukinoa kikosi cha Simba.

ILO yawataka waajiri wa ‘Housegirl’ kuwalipa Sh65,000

Dar es Salaam.
Shirika la Kazi Dunia (ILO), limewataka waajiri wa wafanyakazi wa nyumbani kuwalipa mshahara wa Sh65,000 kama ilivyopitishwa na Serikali.

Mkurugenzi wa ILO Tanzania, Alexio Musindo alisema licha ya wafanyakazi wa nyumbani kuwa na haki kama wengine kulipwa mshahara unaokidhi mahitaji, uzoefu unaonyesha wengi wao hubaguliwa na kunyanyaswa na waajiri.
Musindo alisema hatua hiyo inatokana na utii na ufuatiliaji mdogo wa sheria za kazi zilizopo.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa semina ya wadau wa ajira jana, Musindo alisema kuna haja sasa
 Serikali kuharakisha kuridhia mkataba wa kimataifa wa kazi namba 189. Mkurugenzi wa Jinsia ,Watoto na Vijana wa Chama cha Wafanyakazi wa Hifadhi, Hoteli, Nyumbani na Huduma za Jamii (Chodawu), Deograsia Vuluwa alisema wafanyakazi wa nyumbani wamekuwa wakinyimwa haki zao za msingi kwa muda mrefu.

Vuluwa alisema hiyo inatokana na sheria za kazi zilizopo kutoweka bayana masuala muhimu kama kima cha mshahara, mapumziko, likizo na likizo za uzazi.
Naye Mkurugenzi wa Ajira Wizara ya Kazi na Ajira, Ally Msaki alisema kuna changamoto nyingi zinazokabili sekta ya ajira kwa wafanyakazi wa nyumbani.

Tuesday, May 28, 2013

BREAKING NEWS: ALBERT MANGWAIR AAGA DUNIA

Taarifa zilizotufikia hivi punde ambazo bado hazijathibitishwa zinasema kuwa msanii Albert Mangwair amefariki dunia akiwa nchini Afrika Kusini alipokuwa amelazwa katika hospitali ya St Hellen.
 

Beauty of the day: Elizabeth Michael Lulu.

elizabeth-michael-lulu-15 elizabeth-michael-lulu-16 elizabeth-michael-lulu-00 elizabeth-michael-lulu-11

MAMA ALIYEJIFUNGUA WATOTO WATANO ARUHUSIWA KURUDI NYUMBANI KUTOKA HOSPITALI

Bi Jane Mlelwa aliyekaa kitandani akiwa amebeba mmoja wa  wawatoto watano aliowazaa kabla ya watototo hao kufa wote(Picha na maktaba)
Hawa ndio watoto aliojifungua katika hospital ya Mkoa wa Ruvuma na kesho wakafaliki dunia (Picha na maktaba)
Na Nathan Mtega,Songea

 MWALIMU Sophia Mgaya(28) mkazi wa Ruhuwiko mjini Songea mkoani Ruvuma aliyejifungua watoto watano kwa wakati mmoja kwa njia ya upasuaji mnamo Mei 25 mwaka huu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma iliyopo mjini Songea na watoto hao kuishi kwa muda wa masaa kumi kabla hawajafariki dunia ameruhusiwa kutoka hospitalini hapo.

Akizungumza na Demashonews kwa njia ya simu Sophia Mgaya akiwa nyumbani kwake Ruhuwiko mjini Songea alisema alilazimika kuomba kutoka wodini kwa sababu alikuwa akijisikia uchungu anapowaona wanawake wenzake wodini humo wakiwakumbatia watoto wao baada ya kujifungua huku wa kwake wote wakiwa wamefariki dunia baada ya kuzaliwa.

MAGAZETI YA LEO HII MEI 28.5.2013

NAMBA YA FREEMASON YAZUA HOFU KATIKA JAMII.

 
Na Makongoro Oging'
HOFU imezuka nchini baada ya namba ya simu inayotajwa kuwa ni ya jamii ya watu wasiomwamini Mungu, Freemason kuhusishwa na umwagaji damu na kafara kutumika kuwapigia watu mbalimbali, Uwazi lina taarifa hii kwa ukamilifu.

Taarifa ambazo Uwazi limezipata, zinaeleza kwamba namba hiyo ni ya Freemason na kwamba, mpigiwaji akijaribu kupokea na kuzungumza, atakuwa ameunganishwa kwenye kafara hiyo.
Baada ya namba hiyo ya kutatanisha kuzuka na kuwapigia watu mbalimbali, inaelezwa kwamba iligundulika kuwa ni ya jamii hiyo na hivyo kusambazwa meseji ya kuwaonya watu wasipokee simu hiyo.
 
NI NAMBA GANI?
Namba hiyo ni 0800226655 ambayo Uwazi limejiridhisha kuwa si namba ya mtandao wowote wa simu nchini wala nje ya mipaka ya Tanzania, maana hakuna namba kama hiyo.
Ukiachilia mbali kujichanganya kwake, kwa kawaida namba za nje ya nchi huja na alama ya jumlisha, ikifuatiwa na namba za utangulizi za nchi husika, tofauti na namba hiyo.

Raia 25 wauliwa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Watu wasiopungua 25 wameuawa baada ya wanamgambo wa Muungano wa Seleka wa Jamhuri ya Afrika ya Kati kushambulia vijiji kadhaa katika mji wa Bossangoa ulioko magharibi mwa nchi hiyo. 

Taarifa zilizotolewa na Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu zinasema kuwa, miongoni mwa waliouawa ni wanawake na watoto wadogo. 

Wanamgambo wa Seleka ambao hivi sasa wanashikilia  uongozi wa nchi hiyo, wanatuhumiwa kutenda vitendo kadhaa za jinai ikiwa ni pamoja na uporaji wa mali, mauaji, ubakaji na unyanyasaji wa raia. 

Mashirika ya Kutetea Haki za Binadamu yanasema kuwa, mara baada ya wanamgambo wa Seleka kumuondoa madarakani Rais Francois Bozize tarehe 24 Machi mwaka huu, hali ya amani na utulivu imetoweka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Li Keqiang azuru Ujerumani kuimarisha ushirikiano.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameahidi kutumia ushawishi wa kiuchumi wa nchi yake, kuuzuia Umoja wa Ulaya usiziwekee vikwazo vya ushuru baadhi ya bidhaa zinazoagizwa kutoka China, ili kuepusha vita vya kibiashara.
Kansela Merkel aliyasema hayo katika mkutano wa waandishi wa habari mjini Berlin jana jioni, akiwa na waziri mkuu wa China, Li Keqiang, ambaye yuko ziarani nchini Ujerumani.

''Ujerumani itapigia debe mazungumzo ya kina kati ya Umoja wa Ulaya na China, kutafuta suluhisho katika tofauti zao za kibiashara haraka iwezekanavyo.'' ameyasema Kansela Merkel, ambaye nchi yake ndiyo yenye uchumi imara zaidi barani Ulaya, akiwa na mgeni wake, waziri mkuu wa China, Li Keqiang, mjini Berlin.

ICC yatuhumiwa kwa ubaguzi wa rangi.

AU inapinga hatua ya ICC kusisitiza kusikiliza kesi za washukiwa wa ghasia za baada ya uchaguzi Kenya mwaka 2007, Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya binadamu.

Uhuru Kenyatta alichaguliwa kama rais wa nne wa Kenya mwezi Machi
Muungano wa Afrika umeituhumu mahakama ya kimataifa ya ICC kwa kuwaandama wafrika kwa sababu ya rangi yao.
Waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn aliyasema hayo akiongeza kuwa italalamika mbele ya Umoja wa Mataifa kuhusu hilo.

Rais Kenyatta anatarajiwa kufika mbele ya mahakama hiyo mwezi Julai kusikiliza mashtaka dhidi yake kuhusu uhalifu dhidi ya binadamu.

Aidha Kenyatta amekanusha tuhuma hiuzo ambazo zinatokana na madai ya kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi Kenya mwaka 2007 ambapo maelfu walipoteza maisha yao na wengine kuachwa bila makao.

Alichaguliwa kama Rais katika uchaguzi uliofanyika mwezi Machi na kumshinda mpinzani wake mkubwa Raila Odinga katika uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali.

Akihutubia kikao cha marais wa Afrika kwenye mkutano wa AU mjini Addis Ababa , bwana Hailemariam alisema kuwa viongozi wa Afrika wameelezea wasiwasi kuwa asilimia 99 ya wale wanaotakikana na mahakama ya ICC kwa makosa yoyote yale ni waafrika.

"hii ni dalili ya kuwa mambo sio sawa, mfumo wa ICC una hujuma,'' alisema bwana Hailemariam
Mahakama ya ICC ilibuniwa ili kuangamiza kile kilichoonekana kuwa viongozi wanaofanya uhalifu bila kujali, lakini sasa ''mfumo huo umegeuka na kuwa mfumo wa kuwaandamana watu kwa misingi ya rangi,'' alisema bwana Hailemariam.

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate