EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, November 30, 2013

SNURA KUYASHUSHA MAJANGA EBSS LEO


Snura Mushi akifanya yake stejini.
MAMA wa Majanga, Snura Mushi leo anadondoka katika Ukumbi wa Escape One,  Mikocheni jijini Dar katika fainali za Shindano la Epic Bongo Star Search.
Kwenye fainali hizo ambazo mshindi anatarajiwa kuondoka na kitita cha Sh. Mil. 50, wasanii mbalimbali wanatarajia kutumbuiza akiwemo Barnaba, Young Killer, Shaah, Msechu na Walter Chilambo.

TID ALALA MAHABUSU

Khaleed Mohamed 'TID'.
Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya, Khaleed Mohamed 'TID' yupo mahabusu katika Kituo cha Polisi Oysterbay tangu jana usiku baada ya kukamatwa na polisi kwa tuhuma za kumpiga na kumjeruhi msichana anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake,  Mariam Nnauye.CREDIT:GPL

WALIMBWENDE WA MISS TANZANIA USA PAGEANT WAJINOA KWA MARA YA MWISHO

 Joy Kalemera kutoka New Jersey
 Faith Kashaa kutoka Alabama
 Julia Nyerere kutoka Maryland.
 Hellena Nyerere kutoka Maryland.

TOVUTI KUU YA SERIKALI YAZINDULIWA RASMI, TAARIFA NA HUDUMA MBALIMBALI SASA KUPATIKANA KWA NJIA YA MTANDAO.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda (katikati) akiwa ameambatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma Celina Kombani wakiwasili katika Ofisi za Wakala ya Serikali Mtandao kupata maelezo ya Tovuti Kuu ya Serikali kabla ya kuizindua tovuti hiyo leo jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa Tovuti Kuu ya Serikali www.tanzania.go.tz itakayowawezesha wananchi kupata taarifa na huduma mbalimbali za serikali kwa urahisi, haraka na kwa wakati. Wanaoshuhudia kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma Celina Kombani na Dkt. Jabiri Bakari ,Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao ambao ni wasimamizi wa Tovuti hiyo.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akifurahia jambo mara baada ya kuzindua Tovuti Kuu ya Serikali na kuwataka wananchi kuitumia katika kupata taarifa mbalimbali za serikali.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipata maelezo kuhusu uundwaji wa Tovuti Kuu ya Serikali na namna inavyoendeshwa kutoka kwa Mkurugenzi wa Msaidizi wa Mifumo Shirikishi ya Umma Bw. Fratern Hassani (kulia) katika Ofisi za Wakala ya Serikali Mtandao wasimamizi wa Tovuti Kuu ya Serikali. Wengine wanaosikiliza kutoka kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala hiyo Dkt. Jabiri Bakari, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma Celina Kombani,Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa, Makatibu wakuu na watendaji wengine wa serikali.

MTIKISIKO BIAFRA KESHO

 
Linah Sanga.
Wasanii wakubwa Bongo, watafanya shoo kali itakayoambatana na ujumbe mahsusi kuhusu gonjwa hatari la Ukimwi, wakati wa kilele cha Siku ya Ukimwi Duniani, Desemba Mosi 2013.
Linah, Barnaba, Amin, Linex, Recho, Snura, Ally Nipishe, Mataluma, Kundi la Makomando na wengine wengi, wataangusha shoo kali siku hiyo katika Viwanja vya Biafra, Kinondoni, Dar es Salaam.
Rachel Haule ‘Recho’
Mratibu wa tamasha hilo, Paul Makonda, amesema kuwa shoo hiyo imeandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) kwa lengo la kufikisha ujumbe kwa jamii kuhusu hatari ambayo imeendelea kutanda dhidi ya janga hilo.

Friday, November 29, 2013

RAY, CHUCHU HANS LAIVU


AMA kweli penzi ni kikohozi kulificha huwezi! Hatimaye uliokuwa uhusiano wa chini kwa chini wa nyota wawili wa sinema za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Chuchu Hans, siyo siri tena baada ya wahusika hao wakuu kujiachia ‘live’, Ijumaa limeshiba.
Ray na Chuchu Hans wakiwa katika pozi la kimahaba.
KIMAHABA ZAIDI
Ishu hiyo ilitokea mapema wiki hii ambapo Chuchu alitundika picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa na Ray chumbani kimahaba.
Kufuatia tukio hilo kuliibuka gumzo kubwa na kulifanya jambo hilo kuwa ndiyo habari ya mjini katika ulimwengu wa mastaa wa filamu za Kibongo.
Katika picha hiyo, Chuchu anayetumia jina la Chukichuku kwenye Instagram aliambatanisha na maneno yaliyosomeka ‘Me n U’ akimaanisha yeye na Ray hivyo kutoa fursa kwa mashabiki wao kusema chochote.
Kwa mujibu wa mashabiki hao, Ray na Chuchu kwa sasa ndiyo love bird au ‘maua’ yanayopendezesha tasnia hiyo.
“Mmependezaaa…mapenzi waziwazi,” ilisomeka komenti ya mmoja wa mashabiki hao.
“Nilikuwa simuelewi Ray lakini hapa nimemsoma. Wamependeza sana,” ilisomeka komenti nyingine iliyoungwa mkono na mashabiki wengi kwa kupata ‘likes’ nyingi.
Mwingine aliandika: “Sasa walichokuwa wanagombea Mainda (Ruth Suka) na Johari (Blandina Chagula) kipo wapi? Ona sasa wamekosa wote… hahahaaa… wawaache miaka isiyohesabika.”
HAKUNA KIFICHO TENA
Katika kunogesha mambo, baadaye Chuchu aliweka picha ya Ray akimsifia jambo lililodhihirisha kuwa kwa sasa hawafanyi tena kificho kama miezi kadhaa iliyopita.
Habari za chini ya kapeti kutoka kwa wasanii wenzao wanaokuwa nao lokesheni zilieleza kuwa wawili hao wamekuwa wakionesha waziwazi kuwa wao ni item (kitu kimoja).
“Kuna siku tulikuwa tuna-shoot maeneo ya Sinza-Mori (Dar), yaani ungewaona wala usingeuliza maana kama hujui kusoma, ungeangalia hata picha. Yaani mapenzi kama njiwa!
“Sasa hivi ndiyo uhusiano ambao upo ‘hoti’ kwenye tasnia yetu, sema ndiyo hivyo wenyewe walikuwa hawapendi ijulikane lakini naona wameshindwa kuendelea kujificha,” alisema mwigizaji huyo kwa sharti la kutotajwa gazetini.
CHUCHU ATAKA WASIINGILIWE
Baada ya kujikusanyia data, Ijumaa lilimtafuta Chuchu akiwa mmoja wa wahusika wakuu ambapo alipopatikana alikuwa na haya ya kusema: “Hayo ni mambo yetu binafsi, naomba tusiingiliwe katika mambo yetu.”
Ijumaa: Chuchu wewe ni kioo cha jamii na mashabiki wako wanataka kujua ukweli juu ya uhusiano wako na Ray. Unalizungumziaje hilo?
Chuchu: Weweee…sikia! Nimeshasema sitaki mtu aniingilie mambo yangu. Kwani mnataka nini nyiye?
Ijumaa: Je, hiyo picha mliyopiga chumbani ni hotelini au nyumbani?
Chuchu: Siwezi kukuelezea tumepiga wapi, iwe hotelini au nyumbani haiwahusu, naomba mniache jamani mbona hivyo? Kwani vipi? (kisha akakata simu).
KAKA MKUBWA VIPI?
Jitihada za kumpata Ray ‘Kaka Mkubwa’ katika tasnia ya filamu za Kibongo ili kupata neno lake juu ya ishu hiyo ziligonga mwamba baada ya simu yake ya kiganjani kuita bila kupokelewa na hata alipofuatwa ofisini kwake, RJ Productions pale Sinza-Mori, Dar hakupatikana.
KABLA YA PICHA
Kwa muda mrefu kumekuwa na madai mazito kuwa Ray na Chuchu wanatoka lakini habari hizo zilikosa mashiko kwa kuwa hakukuwa na ushahidi wowote.
Ilidaiwa kuwa hata ile vita ya hivi karibuni ambapo Johari na Chuchu walizichapa kavukavu ilitokana na kugombea penzi la Ray.
JOHARI ASARENDA

Thursday, November 28, 2013

USAFI WA MITARO ENEO LA MAKUMBUSHO IMEKUWA TATIZO KUBWA,MAGONJWA YA MLIPUKO YANAWEZA KUTOKEA‏

Huu ni mtaro ambao umeziba na maji hayaendi,na watu kutupa uchafu ndani yake kama unavyoonekana.
Juu ya huo mtaro kuna mgahawa wa chakula,ambao watu wanautumia kwa mahitaji ya chakula.

VIDEO:JACK WOLPER AKIFUNGUKA KUHUSU SIRI ZAKE TANO

JK AKAGUA NA KUZINDUA MIRADI MKOA MPYA WA SIMIYU

 Msanii wa kundi la sanaa kutoka Bariadi akicheza na nyoka aina ya Chatu wakati wa uzinduzi wa Ujenzi wa Barabara ya Bariadi –Lamadi.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wananchi waliohudhuria ufunguzi wa Barabara ya Bariadi Lamadi.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli(watatu kushoto),Mbunge wa Bariadi  Mhe. Andrew Chenge(kushoto)pamoja na viongozi wengine w akifunua kitambaa kuashiria kuweka jiwe la msingi na kuzindua ujenzi wa Barabara ya Bariadi-Lamadi yenye urefu wa kilometa 71.8 huko enelo la Old Maswa mkoa mpya wa Simiyu.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Old Maswa muda mfupi baada ya kuzindua ujenzi wa barabara ya kilometa ya Bariadi-Lamadi 71.8 huko eneo la old Maswa, Mkoani Simiyu.

RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA MAOMBOLEZO KUFAUTIA MSIBA WA MZOBORA

Marehemu  Dunia Mzobora enzi za uhai wake.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara kufuatia kifo cha Mwandishi wa Habari na Msanifu wa Habari Msaidizi Mkuu wa Gazeti la Uhuru, Bwana Dunia Mzobora, kilichotokea tarehe 27 Novemba, 2013 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alikokuwa amepelekwa kwa matibabu ya shinikizo la damu.
Marehemu aliajiriwa katika Magazeti ya Uhuru na Mzalendo mwaka 1989 kama Mwandishi wa Habari Mwanafunzi, kisha akaendelea kupanda ngazi hadi kufikia cheo cha Msanifu wa Habari na hatimaye kuwa Msanifu Mkuu Msaidizi, cheo alichokuwa akikishikilia hadi mauti yalipomkuta.

Waziri Mkuu wa Latvia ajiuzulu

Waziri Mkuu wa wa Latvia, Valdis Dombrovskis, amejiuzulu kufuatia kuporomoka kwa jengo moja nchini humo, Alhamisi iliyopita na kusababisha watu wapatao hamsini kuuawa.
Bwana Dombrovskis amesema amekubali kuwajibika kisiasa kutokana na mkasa huo ambapo paa ya duka moja kubwa la bidhaa katika mji mkuu, Riga, lilipinda na kuporomoka. 
Valdis Dombrovskis,waziri mkuu wa Latvia
Polisi wameanzisha uchunguzi wa kihalifu kubaini kama taratibu za ujenzi wa jengo hilo zilizingatiwa au la; bustani ilikuwa ikijengwa juu ya paa la jengo hilo la maduka wakati ajali hiyo ikitokea.

Berlusconi atimuliwa bungeni Italia


Bunge la seneti nchini Italia limepitisha hoja ya kumtimua Waziri Mkuu mstaafu wa Italia Silvio Berlusconi katika bunge kutokana na kupatikana na hatia ya kukwepa kulipa kodi.
Kufuatia hatua hiyo sasa Berlusconi anaweza kushtakiwa kutokana na kukosa kinga ya bunge.
Silvio Berlusconi
Kwa upande Berlusconi amewaambia wafuasi wake kuwa leo ni siku ya maombolezo katika demokrasia na kwamba kura hiyo ya bunge la seneti inaonyesha chuki binafsi ya wale wa upande wa kushoto.

EXCLUSIVE: SIRI 5 ZA WOLPER ZAVUJA

MOYO huhifadhi mengi mazito hasa ya kuumiza! Staa mkubwa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe amejikuta akimwaga machozi wakati akianika siri tano nzito kuhusu mapenzi katika mahojiano (exclusive interview) na Amani kwa takriban saa mbili.
Wolper akifunguka ndani ya Ofisi za Global Publishers, Bamaga-Mwenge jijini Dar.
Akizungumza kwa masikitiko, uchungu na majuto, Wolper alisema hawezi kumsahau mwanaume huyo ambaye ni Abdallah Mtoro ‘Dallas’ kwa namna alivyomwingia kijanja na kutaka kumvunjia heshima aliyoijenga karibia miaka kumi nyuma.

Wednesday, November 27, 2013

DAVINA: NDOA IMENIFUNZA MENGI

MSANII wa filamu za Kibongo, Halima Yahya ‘Davina’ amekiri kujifunza mambo mengi ya maisha baada ya kuingia kwenye ndoa.
Halima Yahya ‘Davina’.
Akizungumza na mwandishi wetu, Davina alisema kwamba anaichukulia ndoa yake kama chuo cha mafunzo kwa jinsi alivyobadilika na kuwa tofauti na Davina aliyekuwa nje ya ndoa.

“Nimekuwa tofauti kabisa na Davina wa kabla ya ndoa, sasa hivi kila kitu nakifanya kwa ustaarabu kwa kuwa najiona nimekuwa mwenye majukumu mengi,” alisema.

Akifafanua zaidi, Davina alisema zamani alikuwa ni mtu wa kurandaranda hovyo tofauti kabisa na hivi sasa.
“Zamani nilikuwa napenda safari zisizokuwa na faida tofauti na sasa hivi, kweli nimeamini ndoa ni chuo cha mafunzo,” alisema huku akiwaombea wasanii wenzake walio nje ya ndoa wafunge ndoa na kuwa na familia zao kwani watajifunza mengi.

KINA KAKA WAPENI RAHA WAPENZI WENU SI KARAHA

 
AMANI hamjambo? Kama ada tumekutana kwenye kona yangu Naa miye, nina imani msemaji ni mmoja siku zote, mshereheshaji  akizungumza wote mnakuwa wasikilizaji mpaka atakapotoa ruhusa. Hapo ndipo nilipokuwa napataka, baada ya kuwa kimya sasa nisikilizeni nataka kuzungumza nini.

Leo sitakuwa mzungumzaji bali kumkaribisha mzee mwenzangu Babu Poa, ambaye mlimmisi muda mrefu. Mzee mwenzangu alikuwa katika honeymoon, mwenzenu na utu uzima wake kaongeza mke wa nne, safari hii kaoa mtoto mbichiii utamwambia nini?

Nina imani amerudi na mambo mapya hasa baada ya kusoma mada yangu ya wiki jana niliyozungumzia kumpa mgonjwa dozi kamili na wala usizidishe kwa vile inaweza kuwa sumu itakayomdhuru.
Baada ya kuisoma mada yangu ya wiki jana, naye aliomba wiki hii akandamizie juu yake ili kuwapa wanaume elimu bure. Sikutaka kuwa mzungumzaji saana bali kumkaribisha mwenyewe, Babu Poa karibu.

“Asante Bi Nasra, sitaki kuzunguka sana bali kwenda kwenye kusudio la mimi kuwa hapa. Jamani leo nataka kugandamizia juu ya mada ya wiki jana, nina imani kila mmoja aliisoma na kuona jinsi wanaume wengi tunavyotumia  nguvu nyingi  katika tendo la ndoa bila akili na kulifanya kuwa mateso badala ya starehe.
 
 Siku zote mapenzi ni raha na mkimaliza mpeane asante na mabusu, siyo mwenzio kageukia ukutani huku kakunja uso na ugonjwa wa tumbo juu.

Tuesday, November 26, 2013

DK KAWAMBWA AJIBU MAKOMBORA YA NAPE

Bagamoyo. 
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa amejibu madai yaliyotolewa hivi karibuni na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye kwamba ni mmoja wa mawaziri walioshindwa kazi, hivyo kustahili kung’olewa.
 
Katika madai yake, Nape alisema Dk Kawambwa ameshindwa kusimamia vyema madai ya walimu na kwamba akiwa Waziri wa Miundombinu, aliingia mkataba na Kampuni ya ujenzi ya Progressive iliyopewa zabuni ya kujenga Barabara ya Namtumbo hadi Tunduru wakati mkandarasi huyo hana uwezo wa kuijenga.

Nape alikaririwa akisema kwamba umefika wakati kwa waziri huyo na wenzake wa Fedha, Dk William Mgimwa; Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza; na Naibu wake, Adam Malima kuhojiwa na Kamati Kuu (CC) ya chama hicho.

KINANA ASHIRIKI NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA RUNGWE MASHARIKI


 Ndugu Kinana na Ujumbe wake wakipita kukagua jengo la Maabara katika shule ya  sekondari ya Mwakaleli,katika halmashauri ya Busokelo,Wilayani Rungwe mkoani Mbeya.Mradi huo wa ujenzi wa madarasa na maabara ni  mpango serikali  wa kuboresha shule za sekondari zilizopo kwenye kata na Taifa kwa ujumla kwa kushirikiana na benki ya Dunia.
 Pichani chini, Ndugu Kinana akiwa amebeba tofali ikiwa ni sehemu ya ushiriki wa ujenzi wa madarasa katika  shule ya  sekondari ya Mwakaleli,katika Halmashauri ya Busokelo,wilayani Rungwe.

ATEMBEZWA UCHI MTAANI BAADA YA KUFUMANIWA NA MKE WA MTU CHUMBANI

WANASEMA za mwizi arobaini, ikiongezeka moja mshukuru Mungu! Novemba 16, mwaka huu ilikuwa siku ya aibu kwa bosi Hussein Shaban (35) kufuatia kudaiwa kufumaniwa katika nyumba ya kiongozi mmoja wa Chama cha Mapinduzi (CCM) huko Tegeta jijini Dar es Salaam.
Hussein Shaban akiwa amevuliwa nguo na kupewa kichapo baada ya fumanizi.
Sakata hilo la aina yake lilitokea katika kitongoji cha Nyeishozi, Tegeta kwa kumuhusisha Hussein ambaye ni mfanyabiashara  na mke wa kigogo huyo ambaye jina lake tunalihifadhi kwa sasa.
CHANZO CHA FUMANIZI, KUTOWEKA AMANI
Akisimulia tukio zima mwanzo hadi mwisho, kiongozi huyo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini, alisema miezi miwili iliyopita alianza kuhisi ndani ya ndoa yake kuna jambo lanaloendelea kwa siri baada ya nyumba yake kupoteza amani, mke alibadilika tabia ghafla.

MCHUMBA ALIYEUA NA KUJIUA ILALA, CHANZO PICHA ZA UTUPU

Stori: Waandishi Wetu, Dar es Salaam na Mwanza
MAPENZI ni sanaa tata sana, inawaumiza wengi, inavunja mioyo ya watu, inakatisha tamaa ya maisha, inaleta umaskini, inasababisha mauaji lakini siyo rahisi kuachana nayo na kwa mantiki hiyo, matukio mengi yataendelea kujiri.

Christina Newa.
Tukio la Gabriel Munisi kuua watu wawili kisha naye kujiua kwa kisa cha mapenzi, ni mwendelezo wa ‘sinema machafuko’ za mapenzi.
Nyuma ya tukio hilo kuna mengi yanazungumzwa, ila gazeti hili limenasa habari kuwa picha za utupu na SMS za mapenzi ni chanzo cha kila kitu.
Alpha Alfred Newa enzi za uhai wkae.
NINI HASA CHANZO?
Gazeti hili limebaini kuwa tukio hilo la mauaji, lililochukua nafasi alfajiri ya Jumanne iliyopita, chanzo chake ni Gabriel ‘Gaby’, kunasa picha zinazomuonesha mchumba wake, Christina Newa akiwa na mwanaume mwingine.

Monday, November 25, 2013

KAMPUNI YA USAMBAZAJI WA FILAMU YA DJ MARKETING AND PROMOSHEN YATOA MSAADA




Msemaji wa Kampuni ya usambazaji wa Filamu ya DJ Marketing and Promoshen, Seraphine Baraka kulia akigawa sabuni za Twiga Soup ambayo nayo inasambazwa na kampuni hiyo kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko Dar es salaam mwishoni mwa wiki ilyopita kampuni hiyo imetoa sabuni na baadhi ya nguo kwa watoto hawo
Msemaji wa Kampuni ya usambazaji wa Filamu ya DJ Marketing and Promoshen, Seraphine Baraka kushoto akimkabidhi sabuni aina ya Twiga  inayosambazwa na kampuni hiyo kwa Aisha Omari anaelelewa katika kituo cha Shule ya Uhuru Mchanganyiko Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita

ZITO KABWE:SITOKI CHADEMA

MKUTANO WA RAGE NA WANAHABARI

PICHA ZA KIMAHABA ZA WASTARA ZAZUA UTATA

PICHA za aliyekuwa mke wa marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ Wastara Juma akiwa na mwigizaji Bondi bin Salim ‘Bond’ zimezua utata ambao unakazia ukweli wa taarifa ya kuwa wawili hao ni wapenzi.
Kikizungumza na Ijumaa Wikienda chanzo chetu kilicho makini, kilisema kinawashangaa sana Wastara na mwenzi wake huyo kuukana upenzi wao kila kukicha wakati picha zinajieleza.

MAGARI YA WEMA YAGEUZWA GESTI

TAARIFA ikufikie kuwa chanzo cha Mkurugenzi wa Endless Fame Productions, Wema Isaac Sepetu kutimua baadhi ya wafanyakazi wake akiwemo dairekta wake ni ufuska uliokubuhu huku magari yake yakigeuzwa gesti au danguro.
Wema Sepetu.
‘NI TOO MUCH’
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Wema alifikia hatua hiyo hivi karibuni ili kuficha skendo hiyo kubwa kwa sababu ilikuwa ‘too much’.
Ilifahamika kuwa pamoja na Wema kumpenda dairekta huyo kiasi cha kumwachia magari yake kutokana na ubunifu wake na uchapaji kazi lakini ilifika mahali akamshindwa.
“Alimpa uhuru wa kufanya kila kitu ikiwemo kutumia magari yote kama kiongozi wa kampuni,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Kweli jamaa alikuwa anatanua kila mahali. Mara Uhuru Peak, mara Coco Beach akiwa na totozi.
COCO BEACH, KINONDONI
“Kuna siku, moja kati ya magari ya Wema lilinaswa pale ufukweni Coco Beach likinesanesa na baada ya muda alishuka mwanamke akijitengenezatengeneza nguo zake.
“Ukiacha hiyo kuna siku nyingine lile jeusi lilinaswa maeneo ya Kinondoni ambapo mabinti walikuwa wakipishana kuingia na kutoka.”

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AWASILI WILAYANI RUNGWE‏

1 
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto akipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Ndugu Bw. Crispin Meela katika mji wa Ushirika wilayani Rungwe mara baada ya kuwasili wilayani huo, akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Mbeya ambayo aliianza jana wilayani Kyela akitokea Mbamba Bay wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma , Kinana ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi Ndugu Nape Nnauye na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa , Kinana ameanza kazi katika wilaya ya Rungwe kwa kufanya mkutano wa ndani ambapo atapokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi na uhai wa chama wilayani huo.PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-RUNGWE 2 
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Rungwe Mashariki Mh. David Mwakyusa mara baada ya kuwasili katika mji wa Ushirika Wilayani Rungwe ambapo ndipo alipopokelewa leo 3 
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia jambo na Richard Kasesela mmoja wa wana CCM waliofika kwenye mapokezi hayo. 5 
Katibu wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akisalimiana na Richard Kasesela katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Nd. Crispin Meela. 6 
Baadhi ya viongozi wa CCM wilayani Rungwe wakiwa katika mkutano wa ndani ambao Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana atapokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM unaofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri mjini Tukuyu. 7 
Baadhi ya wajumbe wakimpokea Ndugu Abdulrahman Kinana tayari kwa kikao hicho cha ndani. 8 
Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya na Mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki Mh Godfrey Zambi ,Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi wakisaini vitabu vya wageni mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa mkutano mjini Tukuyu.

Sunday, November 24, 2013

‘Nilikuwa naomba Mungu kila siku ili afukuzwe Chadema’ - Mama Zitto

Dar es Salaam. 
Siku moja baada ya Kamati Kuu ya Chadema kumvua uongozi aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Taifa wa chama hicho, Zitto Kabwe, mama yake mzazi, Shida Salum ametoa ya moyoni akieleza kuwa kilichomkuta mwanaye kimefunika mabaya mengi yaliyopangwa afanyiwe.


 Baada ya Kamati Kuu ya Chadema kumvua uongozi aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Taifa Zitto Kabwe, mama yake mzazi Shida Salum (pichani) aibuka kueleza jinsi zahama hiyo ilivyokuwa ‘ushindi’ kwa mwanae. PICHA | MAKTABA 

“Kwa upande wangu naona kama ni ushindi kwa Zitto kutokana na jinsi ninavyojua hali ilivyo, mambo yalikuwa ni mengi mno na nikwambie tu, Zitto kuvuliwa uongozi kumefunika hayo yaliyokuwa yamekusudiwa kufanywa dhidi yake. Nilikuwa naomba Mungu  kila siku ili afukuzwe Chadema,” alisema mama huyo wakati akizungumza na gazeti hili nyumbani kwake Tabata, Dar es Salaam.

Shida Salum alisema kuwa Mungu amemnusuru mwanaye na kusisitiza, “Watu walikaa na kutengeneza ripoti ya siri kuhusu Zitto na kuiweka kwenye mtandao kisha kuituma kwa wanachama wa Chadema wanaowafahamu. Mpaka wanafikia hatua hiyo maana yake ni kwamba wamejaribu njia zote za kummaliza, lakini wameshindwa.”

SOMA ALICHOKIANDIKA MWANA FA KWENYE FACEBOOK KUHUSIANA NA MUHESHIMIWA ZITTO KABWE

Kwa jinsi ninavyoziamini akili za Zitto,naamini kabisa patakuwa na 'shule ya bure' kwy reaction yake juu ya hili suala...NIMEPANIA kujifunza kitu..NASUBIRI...

Tazama picha 10 mpya za msanii wa filamu za kibongo Amanda Poshy akiwa kwenye mapozi tofauti tofauti

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate