IMG_9492
Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar. Kushoto ni Mtaalamu wa Ofa kutoka Tigo, Bi. Jacqueline Nnunduma.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga, alisema kwamba waliona umuhimu wakuanzisha kodi hii mpya ili kuwarahisishia wateja wake kuweza kupata bidhaa na huduma mbali mbali kutoka Tigo kupitia menyu moja tofauti na kutumia nambari tofauti tofauti kama ilivyozoeleka hapo awali.

“Kama mnavyofahamu, kampuni ya simu ya Tigo ina huduma mbali mbali, kwahiyo kitu tulichokifanya ni kumrahisishia mteja kutokupoteza muda na kuondokana na usumbufu wa kukariri nambari tofauti tofauti za huduma zetu kwa kuyakusanya huduma zote na kuziweka katika menyu moja,” alisema Mpinga.

“Kitendo cha kupiga *148*00# wateja wetu watakuwa na uwezo wakupata huduma na bidhaa za Tigo kwenda Tigo, pamoja na za Tigo kwenda mitandao mengine kama vifurushi vyetu vya Xtreme na Mini Kabaang. Huduma zingine ambazo zitapatikana katika hii kodi mpya ni vifurushi vya Intaneti, Burudani na Nunua pitia Tigo Pesa,” aliongeza.