EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, December 31, 2014

MAHABUSU AUAWA AKIJARIBU KUTOROKA MAHAKAMANI KISUTU‏, DAR

Muonekano wa mahabusu aliyekuwa anatuhumiwa kubeba madawa ya kulevya, Abdul Koroma raia wa Sierra Leone baada ya kupigwa risasi.

TUNAKUTAKIA MWAKA MPYA MWEMA


RAYUU AMUANIKA MWANDANI WAKE

Msanii wa filamu Bongo, Alice Bagenzi ‘Rayuu’.
Stori: Mayasa Mariwata
MSANII wa filamu Bongo, Alice Bagenzi ‘Rayuu’ amezua gumzo baada ya picha zake zinazomuonesha akiwa chumbani na mwanaume kuenea mtandaoni, huku kijana huyo akionekana kujichora tatoo yenye jina la mwanadada huyo.

Kijana huyo aliyefahamika kwa jina moja la Brown hakuweza kupatikana ili kuthibitisha uhusiano wake na mrembo huyo, lakini Rayuu alikiri kuwa ingawa picha iliyowekwa mtandaoni ilionyesha wakiwa kikazi zaidi, huyo ni mpenzi wake wa siku nyingi.

WELLU ANASA MIMBA TENA!


Msanii wa filamu Bongo, Wellu Sengo, ‘Matilda’.
Stori: Waandishi Wetu
IMEVUJA! Msanii wa filamu Bongo, Wellu Sengo, ‘Matilda’, licha ya kuwa na mtoto mdogo ambaye hajafikisha hata mwaka, inadaiwa tayari amenasa ujauzito mwingine.Chanzo makini kinaeleza kuwa ujauzito huo ni wa mmoja wa wasanii wenye majina maarufu hapa nchini, ambao wamekuwa katika uhusiano kwa muda mrefu sasa.

DOKTA AONYA MIMBA YA AUNT!

TABIA za mitoko ya usiku matembezini, uvaaji viatu virefu na unywaji pombe unaofanywa na wamama wajawazito, kama alivyo sasa muigizaji Aunt Ezekiel, zimeelezewa kuwa si nzuri na zina uwezekano mkubwa wa kusababisha madhara kwa mtoto anayetarajiwa kuzaliwa.
Mkali katika tasnia ya filamu Bongo, Aunt Ezekiel.
Akizungumza baada ya kuulizwa na gazeti hili juu ya mwenendo wa muigizaji Aunt Ezekiel ambaye mara kadhaa huonekana akiwa ‘viwanja’  usiku, daktari mtaalamu wa magonjwa ya kina mama na watoto,  aliyejitambulisha kwa jina moja la Dokta Chale, alisema utokaji wa usiku na uvaaji wa viatu virefu unaweza kusababisha matatizo ya nyonga, shida wakati wa kujifungua, miguu kuuma na uvimbe kwenye vifundo vya miguu ‘enka’.

Tuesday, December 30, 2014

DIAMOND PLATNUMZ ATUA RWANDA KWA SHANGWE


 
Staa wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz' akiwa na mfanyabiashara mrembo na muimbaji wa Uganda, Zarinah Hassan 'Zari'  au 'The Boss Lady' baada ya kuwasili Rwanda jana.
Diamond Platnumz (katikati) akiwa kamshika mkono mpenzi wake wa sasa Zarinah Hassan 'Zari'  au 'The Boss Lady baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Rwanda.
Diamond na The Boss Lady wakifanya yao.

VIDEO MPYA YA NAY WA MITEGO - AKADUMBA

WAIMBA INJILI WANA NINI?


 
CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS
MENGI yameibuka kufuatia waimba Injili Bongo kukumbwa na kashfa mbalimbali zikiwemo ndoa zao kuvunjika, madai ya kuchepuka, kupata ujauzito nje ya ndoa na matumizi ya madawa ya kulevya, Uwazi limechimba na kuchimbua.
Janet Mreme akiwa na mume wake Jonas Mrema.
BADO JINAMIZI LA KUVUNJA NDOA LAWAANDAMA
Mpaka sasa, waimba Injili wanawake wameshakumbwa na mikasa mbalimbali lakini mpya kabisa ni madai ya hivi karibuni kwamba, ndoa ya mwimbaji mwingine, Kabula George imesambaratika.
Kabula George mwaka 2012 alitamba na Albamu ya Nitang’ara Tu! Inadaiwa hayuko kwa mumewe baada ya ndoa yao kudumu kwa miaka nane!

JANET MREMA ANAUMWA
Huyu aliwahi kuripotiwa na Gazeti la Amani miezi miwili iliyopita kwamba, ndoa yake na mumewe, Jonas Mrema imesambaratika madai makubwa ni mume kutomwamini mkewe huyo na kudai alitoroshwa nyumbani na mchungaji mmoja kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) aliyejulikana kwa jina moja la Emmanuel.
Bahati Bukuku.
Habari mpya ni kwamba kwa sasa hali yake ni tete, anaumwa lakini wengi wanaamini ugonjwa wake unatokana na mawazo ya kuchanika kwa ndoa yake.Tayari mwanaume huyo ameshafungua kesi Mahakama ya Kinondoni, Dar akimlalamikia Mchungaji Emmanuel kumtoroshea mkewe. Anataka fidia ya pesa ambazo mahakama itaamua kama itaona ni sahihi.
BAHATI BUKUKU
Huyu ni mwimba Injili mkongwe Bongo. Ndoa yake na Daniel Basila ilivunjika mwaka 2005, mume alimtuhumu Bahati kutoroshwa nyumbani na mzungu mmoja ambaye hakumtaja jina.
Baadaye Bahati alikanusha, akasema aliamua kuondoka nyumbani kwa Daniel kutokana na manyanyaso mengi. Alishindwa kuvumilia. Mpaka sasa, Bahati hayuko kwenye ndoa.
Rose Mhando.
NEEMA MWAIPOPO
Alipovuma sana na wimbo wa Sipati Picha alikuwa akijulikana kwa jina la Neema Mushi. Mumewe ndiye Mushi. Baadaye, ndoa yake ilivunjika, akarudia jina la ukoo wake, Mwaipopo. Akatoa albamu inaitwa Raha Jipe Mwenyewe.

BONDI, WASTARA PENZI LAO KIZUNGU-MKUTI

BAADA ya wiki iliyopita msanii wa filamu Bongo, Wastara Juma kuripotiwa kwenye moja ya magazeti pendwa kuwa hana uhusiano na mtu yeyote ndani ya Bongo Muvi na yupo mbioni kumuanika mrithi wa Sajuki mengi yameendelea kuibuka.
Msanii wa filamu Bongo, Wastara Juma akiwa kwenye pozi la kimahaba na Bondi Bin Salim.
Akizungumza na Uwazi, mpenzi wa Wastara anayetambulika kwa jina la Bondi Bin Salim alidai kuwa yupo kwenye mchakato wa mwisho wa kutoa mahari kwa ndugu wa msanii huyo kiasi cha shilingi milioni 5 pamoja na pete za dhahabu ili aweze kuwa na Wastara.
Alisema kuwa maamuzi ya kutoa posa yamekuja baada ya kuona kila mmoja anaweza kuishi na mwingine kwani wameshasomana kwa muda mrefu.
“Najua si jambo la watu kuhoji sana kwa sababu ndoa ipo na kila mtu atafanya hivyo, nina hela ya mahari tayari na siku ikipangwa ya kutoa tutafanya hivyo lakini ninachowaza sasa ni kuona nafanya vipi ili harusi yangu iwe ya kipekee na zoezi hili tutalifanya mwakani,” alisema.

MWANAMKE ADAIWA KUTEKA WATOTO

Mama anayefahamika kwa jina la Sara Zoya akiwa na watoto wake, Imani (14) na Leila (5).
Stori: Shani Ramadhani
Mama mmoja, Sara Zoya mkazi wa Mabibo Makuburi, jijini Dar es Salaam amekimbilia polisi na kudai kuwa watoto wake walitekwa na ndugu yake  kisha kupelekwa kusikojulikana baada ya kufukuzwa kwenye nyumba yao ya familia.

Monday, December 29, 2014

The Carters walivyo sheherekea Birthday Ya Jay Z

Ni kweli Beyonce anajua kumfanya Jay Z awe mtu mwenye raha sasa kama inavyonyesha kwenye baadhi ya picha walizopiga kwenye siku ya kuzaliwa ya Jay Z ‘Dec 4′ . Wawili hawa walikwenda  Iceland kujiachia kwa muda huku wakisherehekea miaka 45 ya maisha ya Jay Z
Beyonce-and-Jay-Z-in-Iceland-23 beyonce-jay-z-iceland-christmas-2014-5 beyonce-jay-z-iceland-christmas-2014-6

JACK PATRICK ATWANGWA TALAKA AKIWA JELA

Masikini! Wakati akiendelea kutumikia kifungo cha miaka saba jela huko Macau nchini China, mwanamitindo mwenye mvuto wa kipekee Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick, ametwangwa talaka na aliyekuwa mumewe, Abdullatif Fundikira ‘Tiff’ na tayari amemuoa Miss Tanzania 2011, Salha Israel.
Wakati mwanamitindo Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick akiwa na mumewe, Abdullatif Fundikira ‘Tiff’.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda wikiendi iliyopita baada ya gazeti ndugu na hili, Amani kutoa habari ya Miss Tanzania kuolewa na mume wa Jack, Tiff alisema kuwa mke wake wa sasa (Salha) amemuoa kihalali na kwamba yeye siyo mume wa mtu kwa sababu ameshampa talaka Jack aliyemuoa mwaka 2011.

ROSE MUHANDO KWA UTAPELI TOO MUCH!

LILE jinamizi la kupokea fedha kwa ajili ya kushiriki tamasha la kuimba nyimbo za Injili kisha kutotokea siku ya tukio linazidi kumwandama nyota wa muziki huo nchini, Rose Athuman Muhando, safari hii akidaiwa kumliza tena mtu, Ijumaa Wikienda lina kesi hiyo mkononi.
Nyota wa muziki huo nchini, Rose Athuman Muhando.
Kwa mujibu wa chanzo makini cha ndani, safari hii ameendelea kupokea fedha kutoka kwa mshirika wake kwenye mambo ya Injili, Alex Msama kwa makubaliano ya kushiriki Tamasha la Krismasi kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa lakini siku ya tukio, Ijumaa iliyopita, mwanadada huyo hakutokea!

BATULI: NAYACHUKIA MAPENZI YALIYOPITA


Stori: Imelda Mtema
STAA mkali wa filamu za hapa Bongo, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ amefunguka kuwa hakuna kitu ambacho kinamuuza na kukichukia kama mapenzi yaliyopita.
Staa mkali wa filamu za hapa Bongo, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni, Batuli alisema kuwa  anachukia na kudharau mno uhusiano uliopita kwani haukuwa ni sahii kwake hivyo hataki hata kuukumbuka.
“Nayachukia sana mapenzi yaliyopita kwa kweli na kuna wakati sipendi kabisa kuifanya akili yangu ikumbuke uhusiano wa nyuma, maana hauna kumbukumbu nzuri kwangu,” alisema Batuli ambaye alishawahi kubanjuka penzini na mwigizaji Mohamed Mtonesia ‘Mtunis’ na Mr. Kelvin walifunga naye ndoa na kumwagana.

CHECK MFALME WA BONGO FLEVA, DIAMOND PLATNUMZ ALIVYOWEKA HISTORIA DAR LIVE SIKUKUU YA KRISMASI

DUDE: MWAKA 2014 NI GUNDU KWANGU

Stori: Gladness Mallya
TUKIWA tunaelekea ukingoni mwa mwaka, msanii wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ amefunguka kuwa mwaka 2014 ulikuwa hauna bahati (gundu) hivyo anamuomba Mungu huo ujao uwe wa baraka kwake.
Msanii wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’.
Akipiga stori na gazeti hili, Dude alisema ndani ya mwaka huu hakuweza kufanikisha lengo lolote kati ya yale aliyojiwekea ikiwa ni pamoja na kufunga ndoa jambo ambalo linamuumiza kwani alitegemea kufanya mambo mengi lakini hakufanikisha.
“Nilitegemea kufunga ndoa lakini imeshindikana kwa sababu upande wa kazi mambo hayakuwa mazuri pia nilipanga kwamba kipindi changu cha Bongo Dar es Salaam kitarudi hewani lakini ikashindikana, ukweli mwaka huu haukuwa mzuri kabisa kwangu namuomba Mungu ujao akanifanikishe malengo yangu,” alisema Dude.

Saturday, December 27, 2014

BABY MADAHA MAPENZI NI HOBI YANGU

 
Mwanadada asiyeishiwa matukio Bongo, Baby Madaha.
Stori: Gladness Mallya MWANADADA asiyeishiwa matukio Bongo, Baby Madaha ameibuka na kutoa kali ya mwaka kwamba anapenda mapenzi kuliko kitu kingine chochote duniani.

DIAMOND HANA UWEZO WA KUMPA MWANAMKE UJAUZOTO!

 
 
Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na Penny.
BAADA ya kudaiwa na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuwa alichoropoa mimba zake mbili, mtangazaji wa Radio E-FM, Penniel Mungilwa ‘Penny’ ameibuka na kujibu mapigo kwamba mwanamuziki huyo hana uwezo wa kumpa mwanamke mimba, Risasi Jumamosi linakupa mchapo kamili.
 
Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na Wema Sepetu.
CHANZO CHA YOTE
Akizungumza na GlobalTV Online kwenye ofisi za gazeti hili Bamaga-Mwenge jijini Dar, hivi karibuni, Diamond alifunguka: “Nilimpa (Penny) mimba ya kwanza, sikuamini ikabidi twende naye hospitalini tukapime, akaambiwa anayo…nikafurahi nikampiga na ndinga (gari) mpya siku hiyohiyo, nikamwambia mama tulia unizalie mwanangu.

WASTARA KUMUANIKA MRITHI WA SAJUKI

 
Staa wa filamu Bongo, Wastara Juma.
Stori: Imelda Mtema STAA wa filamu Bongo, Wastara Juma, ametamka hadharani kuwa hana uhusiano wa kimapenzi na msanii yeyote ndani ya Kundi la Bongo Movie.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni, Wastara alisema kuna maneno mengi yanasemwa kuwa ana uhusiano na mtu ndani ya kundi hilo kitu ambacho si sahihi, atamuanika mrithi wa marehemu Sajuki siku si nyingi.
“Unajua muda utafika tu lakini kwa hivi sasa sina bwana wala sihitaji mtu yeyote ndani ya Kundi la Bongo Movie na mtu ambaye ataishi na mimi muda ukifika nitawatambulisha na kila mmoja atamjua na siyo mtu kunitabiria au kubuni nitamuweka wazi muda si mrefu,” alisema Wastara.

MTOTO ASOMBWA NA MAJI, AFARIKI

 
CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS
MTOTO wa miaka sita, Bernard Benjamin ambaye alikuwa mwanafunzi wa Shule ya Msingi Nyamunge, wilayani Ilemela jijini Mwanza, amesombwa na mafuriko na mwili wake kukaa siku kumi na tano bila kuharibika.
Mafuriko yaliyosababisha kifo cha marehemu mtoto Bernard Benjamin.
Tukio hilo lilijiri Desemba 2, mwaka huu kwenye Mto Kenge jijini hapa, maeneo ya Mabatini, Wilaya ya Nyamagana baada ya kujaa maji ambapo marehemu alisombwa na mafuriko hadi pembezoni mwa Ziwa Victoria.

Friday, December 26, 2014

SAFARI YA MABALOZI KUPANDA MLIMA KILIMANJARO KATIKA SIKU YA KWANZA


Desemba 16 mwaka huu Waziri wa Mambo ya nje ya Nchi ,Mh Benard Membe alikabidhi bendera kwa Balozi Adadi Rajabu kwa niaba ya Mabalozi ,ikiwa ni ishara ya kuanzisha safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro na safari hiyo ilianza kwa muda wa siku sita.
Baada ya kupumzika katika eneo la Kisambioni na kupata chakula ,safari iliendelea ya kwenda kituo cha Mandara.
Kila mmoja alikuwa na Morali ya juu wakati wote wa kupanda Mlima Kilimanjaro.

TAMASHA LA WAFALME: MZEE YUSUF AFANYA KWELI, NYOMI YAPAGAWA DAR LIVE


Mfalme wa Taarab, Mzee Yusuf akilishambulia jukwaaa la Dar Live na kuwaacha hoi mashabiki waliofurika vilivyo.
Mzee Yusuf akifanya yake stejini.

VIDEO: SHOO YA DIAMOND PLATNUMZ YAACHA GUMZO DAR LIVE

SHOO YA DIAMOND DAR LIVE YAACHA HISTORIA


Mwanamuziki Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' akipozi katika picha na mashabiki baada ya shoo ya nguvu Dar Live.
Diamond akiwa na tuzo pamoja na cheti baada ya kuibuka mshindi wa shindano la Ijumaa Sexiest Bachelor.

R.I.P WASANII WETU! KINACHOWAUA KWA KASI CHAJULIKANA


MWAKA 2014 unakatika, matukio ya kukumbukwa ni pamoja na wasanii Bongo kupoteza maisha katika mazingira yasiyotarajiwa, Ijumaa linakupa hatua kwa hatua.Kumbukumbu za haraka zinabainisha kuwa, tangu mwaka 2011 mpaka 2014, wasanii  wenye majina makubwa na madogo wasiopungua 32 wamefariki dunia kwa sababu mbalimbali.
Recho Haule enzi za uhai wake.
Inauma sana! Katika kipindi cha miaka mitatu kuwapoteza wasanii kwa kiasi hicho ni pigo kubwa kwa tasnia, hasa filamu na muziki, ukiwemo wa muziki wa Injili.
Leo katika toleo hili maalum, Ijumaa linawakumbusha wasanii hao walioaga dunia na namna vifo vyao vilivyotokea.
ALBERT MANGWEHA ‘NGEA’
Alikuwa msanii wa Bongo Fleva. Akiwa na miaka 31 alifariki dunia Mei 28, 2013 nchini Afrika Kusini. Chanzo cha kifo chake inadaiwa ni matumizi yaliyopitiliza  ya madawa ya kulevya. Alizikwa Morogoro, Tanzania, Juni 6, 2013.
LANGA KILEO ‘RAIS WA GHETO’
Alikuwa msanii wa Bongo Fleva. Alifariki dunia Juni 13, 2013 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar akiwa na miaka 28. Kifo chake kilithibitishwa kuwa, kilitokana na kuzidiwa na Ugonjwa wa Malaria. Alizikwa  Juni 17, kwenye Makaburi ya Kinondoni, Dar.

Thursday, December 25, 2014

Tunawatakia Christmas 'Noeli' njema na maandalizi mema ya mwaka mpya 2015

Nicki Minaj Kwenye Kurasa Ya Mbele Ya Jarida La Rolling Stone

nicki-minaj_1500x640
Imekuwa ni wiki ya rappa Nicki Minaj ambaye ameweza kushika vichwa vya habari akitangaza album yake mpya ‘The Pink Print’ .Wiki hii Minaj ameng’ara kwenye kurasa ya mbele ya jarida la Rolling Stone toleo la  January 2015  na wanasema mpaka sasa hili ndio cover lenye mvuto zaidi alilowahi kutokea Nicki Minaj.
Kwenye chati kubwa za dunia za album, Nicki Minaj amefanikiwa kushika na 2 kwenye wiki ya kwanza ya kutoka kwa album yake ya Pink Print ikikadiriwa kuuza kopi 150,000 na mpaka sasa imeuza kopi 244,000 .
Nicki-Minaj-x-Rolling-Stone

MADAI MAZITO ROSE NDAUKA, RICHIE WARUDIANA

Staa  wa sinema Bongo, Rose Ndauka akifurahia jambo.
Na Waandishi Wetu
MASTAA  wa sinema waliowahi kuwa wapenzi enzi hizo, Rose Ndauka na Single Mtambalike ‘Richie’ wanadaiwa kurudiana na hivi sasa ni mapenzi motomoto!Kwa mujibu wa chanzo, Rose na Richie wamedaiwa kurudiana baada ya mwanadada huyo kumwagana na mzazi mwenzake, Malick Bandawe miezi ya hivi karibuni.

MARTIN KADINDA KUOA SOON!


Mbunifu wa mavazi Bongo, Martin Kadinda.
Na Laurent Samatta
MBUNIFU wa mavazi Bongo, Martin Kadinda, amesema kuwa baada ya kuishi bachela kwa miaka mingi amepanga kuoa ‘ soon’ mwanamke ambaye ni mpenzi wake wa siku nyingi ili kumaliza maneno ya watu kuwa hajiwezi.
Akizungumza na Amani, Kadinda alisema kuwa mwanamke anayemuoa si aliyezaa naye mtoto bali ni mwanamke aliyekuwa naye kwenye uhusiano kwa muda mrefu na tayari anatambua tabia zake hivyo hana shaka juu ya kuishi kwao pamoja.
“Wazazi wako tayari juu ya hilo nadhani na sitaki kumweka hadharani sasa hivi maana watu hawakawii kuharibu kwa maneno yao machafu, lakini wale ambao walidhani sitaweza kufanya hivyo watambue kuwa mwakani naoa,” alisema Kadinda.

ESCROW BADO MOTO

WAKATI Rais Jakaya Kikwete akiwa amemuwajibisha Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Anna Tibaijuka kufuatia kumegewa mgawo wa fedha za Tegeta Escrow, binti anayedaiwa kuwa mwanaye, amejikuta akipata wakati mgumu baada ya kumtetea mama yake kupitia mitandao ya kijamii.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Anna Tibaijuka.
Katika Mtandao wa Twitter, binti huyo aliyejitambulisha kwa jina la Kagem Tibaijuka, alimtetea mama yake akisema fedha zilizowekwa kwenye akaunti yake zilikuwa ni safi na halali na kwamba ziliwekwa kwa nia njema ya kuwasaidia kielimu watoto wa kike.
“My mum did nothing wrong except wanting to help young girls get an education. A school built with my late father. Accepted a donation,” (Mama yangu hakufanya kosa lolote isipokuwa alitaka kuwasaidia wasichana kupata elimu. Shule ilijengwa na marehemu baba yangu. Mchango ukakubaliwa)yalikuwa  ni moja ya maneno yake katika mtandao huo wa Twitter.
Aidha, aliwashambulia wanawake walioonekana kushangilia wakati Rais Kikwete alipotangaza kumuwajibisha mama yake, akiwaambia kuwa anawashangaa kushangilia anguko la mwanamke mwenzao na kwamba hata wao iko siku yatawakuta ya kuwakuta.
Rais Jakaya Kikwete.
Lakini katika mitandao mingine ya kijamii, ikiwemo Facebook na Jamii Forum inayotembelewa na watanzania wengi, walimshambulia binti huyo kwa kumwelezea kama mtu aliyelewa fedha na kwamba mama yake alistahili kuondolewa kwenye nafasi yake, ikiwa ni pamoja na kushtakiwa.

HUKU MKEWE AKISOTA GEREZANI MISS TZ AOLEWA NA MUME WA JACK PATRICK

Stori: Imelda Mtema DUNIA ina mambo! Wakati mkewe mwanamitindo Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’ akiwa nyuma ya nondo kwa msala wa madawa ya kulevya ‘unga’ nchini China, mumewe, Abdulatif Fundikira ‘Tif’ amefunga ndoa ya siri na Miss Tanzania 2011, Salha Israel, Amani linakupa mchapo kamili.
Mume wa ‘Jack Patrick’, Abdulatif Fundikira ‘Tif’ akifunga ndoa ya siri na Miss Tanzania 2011, Salha Israel(liyeshika karatasi).
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, uhusiano wa Salha na Tif uliibuka na kushamiri mwaka jana baada ya Jack kukamatwa na unga huo.“Penzi lao liliibuka ghafla tu, jamaa naona ana ‘aleji’ na warembo wenye majina yao maana penzi lake na Jack lilipoyumba na kisha mrembo huyo kukamatwa na madawa ya kulevya nchini China, fasta akaanzisha uhusiano na Salha,” kilisema chanzo hicho.
UMAARUFU WA JACK UPOJE?
Jack ni mshiriki wa Miss Tanzania mwaka 2006 akitokea Miss Ilala lakini umaarufu wake ulizidi kukua baada ya kushiriki kama ‘video queen’ katika video mbalimbali za wasanii wa muziki wa Bongo Fleva ikiwemo video ya She Got Gwan ya marehemu Albert Mangwea.

Miss Tanzania 2011, Salha Israel akipozi.
VYANZO VINGINE
Hata hivyo, vyanzo vingine vimeeleza kuwa, Jack na mumewe walikuwa na mgogoro mzito kabla modo huyo hajakamatwa na madawa ya kulevya.“Walikuwa na mgogoro, ilifika wakati Jack alikuwa akidai talaka mahakamani lakini bahati mbaya kabla hajafanikiwa kupewa akaswekwa nyuma ya ndondo,” kilieleza chanzo hicho.

Wednesday, December 24, 2014

ODAMA, NISHA WAIPA UJIKO STEPS

Staa wa filamu Bongo, Jenipha Kyaka 'Odama'.
Stori: Mwandishi wetu
MASTAA wa filamu Bongo, Nisha, Odama na Aunt Ezekiel wameipongeza kampuni ya Steps Entertainments kwa kitendo chake cha kuagiza mtambo wa kurekodia filamu kitu ambacho kitawasaidia wasanii kufaidika.

DIAMOND APELEKA TUZO ZA CHANNEL O KWA JK


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete akiwa na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul  'Diamond Platnumz' baada ya kumtembelea jana Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa msanii Naseeb Abdul “Diamond” wakati akimuonesha moja ya tuzo kati ya tuzo tano za muziki za kimataifa alizoshinda mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumanne Desemba 23, 2014. kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Hermas Mwansoko.

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na msanii Naseeb Abdul “Diamond” baada ya kumkaribisha na kumpongeza kwa kushinda tuzo tano za muziki za kimataifa mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Desemba 23, 2014. Kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Hermas Mwansoko, na kushoto ni katibu wa Bodi ya filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo.

MAAJABU MWANAUME APATA SIKU KAMA WANAWAKE

Stori: Chande Abdallah na Deogratius Mongela MAAJABU! Ndivyo unavyoweza kusema unapokutana na mwanaume mmoja aliyejitambulisha kwa jina  la Frank Kalamu (53) mkazi wa Ilala Jijini Dar es Salaam, aliyetoa ushuhuda wa kufunga mwaka kwamba kwa zaidi ya miaka miwili, alikuwa akipata siku zake kama ilivyo kwa wanawake, ingawa yeye ni kupitia njia ya haja kubwa.
Frank Kalamu akiombewa kanisani.
Akitoa ushuhuda huo ndani ya Kanisa la The Revelation lililopo Buza-Kipera Desemba 21 mwaka huu, Frank alidai amepata mateso hayo kwa muda mrefu huku akizunguka kwa waganga na madaktari wengi bila mafanikio, mbaya zaidi, kwa kipindi chote hicho ameshindwa kushiriki tendo la ndoa na mkewe.

PETE YA SHILOLE YAIBUA MAZITO!


Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Naftari Mlawa ‘Nuhu Mziwanda’ akiwa na bebi wake Zuwena Mohammed ‘Shilole’.
Stori: Waandishi Wetu
JAMBO limezua jambo, saa chache baada ya mwanadada mtafutaji kunako tasnia ya muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, kuvalishwa pete ya uchumba na mchumba wake, Naftari Mlawa ‘Nuhu Mziwanda’ tayari watu wameanza kuisengenya.

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate