EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, March 31, 2013

IRENE MWAMFUPE JAMII Blog inawatakia Heri Ya Pasaka


Maneno manne yenye uwezo wa kumteka mwanamke kimapenzi

Maneno haya manne yenye nguvu ya kumdatisha mwanamke, ambayo ni NAKUPENDA, NAKUHITAJI, SAMAHANI na ASANTE.
Ni wazi kwamba kuna wanaume wengi ambao huanza na gia kubwa ya maneno hao wamebainika kupoteza mvuto wa kimapenzi waliokuwa nao mwanzo kwa wapenzi wao. Binafsi nathibitisha hili kwa kuwa nimeshafanya uchunguzi kupitia wanaume wanaonijia kutaka majibu ya kwa nini wapenzi wao wamewageuka na kutokuwapenda kama awali.

Kabla ya kuwashauri nimekuwa nawadodosa na hatimaye kutambua kuwa waliacha kutumia maneno hayo mara tu walipoona wamefanikiwa walichokuwa wanakitafuta.
 
Kama nilivyosema neno la kwanza lenye nguvu ya kumteka kimapenzi mwanamke ni NAKUPENDA. Neno hili ni tiba inayoponya hofu na kumfanya mwanamke ajiamini.

MLEMAVU AMWANGUKIA WEMA SEPETU

Na. Mwandishi Wetu
MPIGAPICHA wa kujitegemea  ambaye ni mlemavu wa miguu wa mjini hapa, Elias Ngole Ngoswe amemwangukia msanii wa filamu Bongo, Wema Sepetu kwa kumuomba msaada ili aweze kutibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ya jijini Dar es Salaam.
 
Akizungumza na mwandishi wetu Jumanne iliyopita, Ngoswe ambaye ulemavu wake ulitokana na kugongwa na gari kwenye mahafali ya wanafunzi wa kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe, Februari 2, mwaka jana na akavunjika miguu na mfupa wa nyonga, alisema uamuzi wake wa kumuomba msaada Wema unatokana na kuvutiwa kwake na msaada aliompa  msanii mwenzake, Kajala Masanja ambaye alimuokoa kufungwa jela kwa kumtolea faini.
 
“Nimegundua kuwa Wema ana huruma sana nami nikaamua nimuombe msaada kupitia gazeti hili kwani nina matatizo mazito. Nilipovunjika miguu na nyonga nilikimbizwa Hospitali ya Wilaya Magunga, Korogwe baadaye nikahamishiwa Hospitali ya Tumbi Kibaha, nikalazwa miezi mitatu baadaye nilihamishiwa Muhimbili ambako bei niliyoandikiwa nilipe imenishinda,” alisema Ngoswe.

Idadi ya wagombea urais Iran yaongezeka.

 Waziri wa Barabara na Ustawi wa Miji Iran Ali Nikzad
Waziri wa Barabara na Ustawi wa Miji Iran Ali Nikzad ametangaza rasmi uamuzi wake wa kugombea kiti cha urais katika uchaguzi ujao nchini na hivyo kufanya idadi ya waliotangaza azma ya kugombea kiti hicho kuwa tisa.
Nikzad alitangaza uamuzi wake huo Jumamosi alipotembelea mji wa Ardebil ulio kaskazini magharibi mwa Tehran.

Uchaguzi wa 11 wa rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran utafanyika mwezi Juni na wagombea wote wanatakiwa kujiandikisha kati ya Mei 7 na 11. Rais Mahmoud Ahmadinejad anamaliza muhula wake wa pili na hivyo kikatiba hawezi kugombea. 

Kati ya waliotangaza kuwa tayari kugombea kiti cha urais Iran ni pamoja na waziri wa zamani wa mambo ya nje Manouchehr Mottaki, manaibu spika wawili wa bunge Sheikh Mohammad Hassan Aboutorabi-Fard na Mohammad Reza Bahonar.

Katuni yetu..

Maaskofu waijia juu Serikali

Dodoma. 
Wakristo wamesema Serikali ya Rais Jakaya Kikwete imeshindwa kuwasaidia ili waishi kwa amani na utulivu katika nchi yao.
 
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma, Amon Kinyunyu 
Kauli hiyo ilitolewa jana na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma, Amon Kinyunyu, wakati akisoma tamko la Maaskofu wa madhehebu ya Kikristo Tanzania katika ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika Kanisa lililopo eneo la Jamatini.
Katika tamko hilo alilolisoma kwa niaba ya Maaskofu wote, Kinyunyu alisema kuwa umefika wakati ambao Wakristo wamechoka na vitendo wanavyofanyiwa na baadhi ya waumini wa dini zingine.

“Tatizo ni kuwa Serikali inashindwa kuchukua hatua mapema, makanisa yanachomwa, migogoro inazidi, lakini hakuna hatua zozote ambazo Serikali inachukua katika kunusuru hali hiyo, tumechoka,” alisema.

“ Serikali imeshindwa kuchukua hatua kwa muda mwafaka kwa kila jambo ambalo linatokea kwa Wakristo na hata inapoonyesha kuwa imechukua hatua haionyeshi sana kujali juu ya yale wanayofanyiwa Wakristo. Askofu huyo alisema kuwa matokeo yanayotokea Zanzibar mathalan, Wakristo wanaoishi huko yamewasababishia hofu hivyo wengi kuanza kuvikimbia visiwa hivyo na kukimbilia Tanzania Bara.

Mahakama ya Juu ya Kenya imemthibitisha Uhuru Kenyetta kuwa Rais halali Kenya.

Nairobi.
Mahakama ya Juu ya Kenya imemthibitisha Uhuru Kenyetta kuwa Rais halali mteule wa nchi hiyo pamoja na mgombea mwenza wake, William Ruto.
Mahakama hiyo iliwathibitisha Kenyatta na Ruto jana katika uamuzi wa kesi ya kupinga matokeo uliowapa ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika Machi 4, 2013, iliyofunguliwa na mpinzani wao mkuu katika kinyang’anyiro hicho, Waziri Mkuu, Raila Odinga.

Odinga katika kesi hiyo aliituhumu Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya nchi hiyo kuwa ilihujumu matokeo ya uchaguzi ili kumpa ushindi, Kenyatta.Hata hivyo, katika uamuzi wake jana Mahakama hiyo ilisema kwamba Kenyatta na Ruto walichaguliwa kihalali katika uchaguzi huo mkuu.

Vilevile, Jaji Mkuu wa Mahakama hiyo, Dk Willy Mutunga alisema kwamba uchaguzi ulikuwa wa haki na huru, kwa sababu katiba na sheria zilifuatwa, hivyo Mahakama imempitisha Rais huyo Mteule kuwa Rais wa Kenya.

Saturday, March 30, 2013

NI AIBU... NDANI YA BESENI MBAGALA CHARAMBE DAR.

Ilikuwa sherehe ya aina yake wenyewe wanaita beseni.
Beseni ni zawadi ambayo hupelekewa mzazi aliyejifungua nguo,mafuta na sabuni za mtoto ni Mbagala Charambe kwa mdada huyo aliyejifungua siku chache zilizopita.Wazazi wa mwana dada huyo walijipanga na kumnunulia besen!!!!!!!
                                                           Matukio katika picha.
Waliandaa ngoma,muziki kwa ajili ya sherehe hiyo,pia waliandaa chakula na pombe.Baada ya kukabidhi beseni walianza kusherekea kwa kucheza muziki. 

Cha ajabu  muda ulivyozidi kwenda  WALICHEZA HUKU WAKIVUA NGUO   kama wanavyoonekana katika picha.

Ni aibu sana mbele ya watoto wanacheza na kuvua ngua,watoto wamejifunza nini!!!!!!!! Kuna umuhimu wa Serikali kuziangalia sherehe hizi za mitaaani kwa kuwa zina mafundisho mabaya kwa jamii yetu.
IRENE MWAMFUPE JAMII Blog tumeshangazwa na aibu hii!!!!!!!!!!!!

Afukua kaburi la mwanamke, atundika mtini nguo za marehemu

MKAZI wa Kijiji cha Itunge wilayani Kyela, Asanga Mwandepu (67) amefukua kaburi la mwanamke katika kijiji cha Kingila, akachukua nguo za marehemu na kuzitundika juu ya mti na kulima tuta la viazi kwenye kaburi hilo. Inadaiwa katika kaburi hilo alizikwa mwanamke Basikaja Nkemwa miaka mitatu iliyopita.

Akielezea tukio hilo mtoto mkubwa wa marehemu, Semu Mwakalebela alisema wazazi wake wote wamekwisha kufariki dunia.

Semu alisema alishangazwa na kitendo alichokumbana nacho cha kukuta kaburi la mama yake likifukuliwa na mfukuaji akitoa nguo za marehemu na kuzitundika juu ya mti.

Alisema alipiga mayowe kuomba msaada kwa majirani ambao walifika na kujionea kitendo hicho wakamkamata mtu huyo na kumfikisha kwenye ofisi ya serikali ya kijiji kabla ya kumfikisha polisi.

“Nashangazwa na kitendo hiki kwa maana mtu huyu analifahamu fika kaburi la mama yangu na hata yeye alishiriki katika mazishi hayo… sijui ni kipi kilichomsibu hadi kufikia uamuzi hao mgumu,’’ alisema Mwakalebela.

Bashe wa New Habari (2006) Ltd anusurika kutekwa


Ofisa Mtendaji Mkuu wa New Habari (2006) Ltd
WIMBI la viongozi wakuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, kuendelea kuwindwa na watu wasiofahamika, limeendelea kushika kasi, baada ya usiku wa kumkia jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Hussein Bashe, kunusurika kutekwa. Tukio hilo, lilitokea juzi usiku wakati Bashe alipokuwa akitoka ofisini kwake Sinza Kijiweni, akielekea nyumbani kwake Mbezi.

Akizungumzia tukio hilo, Bashe alisema wakati anaondoka ofisini kwake kwa gari lake, alianza kufuatiliwa kwa nyuma na magari mawili, likiwamo aina ya NOA ambalo hata hivyo hakufanikiwa kujua lilikuwa na watu wangapi.

“Kama kawaida nilishinda ofisini kwa ajili ya majukumu yangu ya kazi na muda wa kutoka ulipowadia, niliondoka kurudi nyumbani.

“Awali wakati navuka geti la pale ofisini, sikuwa na shaka yoyote, lakini kadri nilivyozidi kuendelea na safari yangu, niliona nyuma nafuatiliwa na magari mawili ambayo yalikuwa yakiendeshwa kwa tahadhari.

“Nilipofika Mwenge ile NOA ilikuwa bado iko nyuma yangu, sasa nikaanza kupatwa na wasiwasi, nikajua hapa kuna jambo.

“Moyoni niliendelea kumuomba Mungu, huku nikijiuliza maswali mengi hawa jamaa ni akina nani, kwa kweli sikupata jibu zuri.

“Nilipofika Mbezi, niliona yale magari yanazidi kunisogelea, kwa hiyo, nikaamua kuongeza kasi na wao wakazidi kuja tu.

Anayedaiwa kumuua Padri mbaroni


Omar Mussa Makame, mkazi wa Mwanakwerekwe Zanzibar
MTU mmoja, Omar Mussa Makame (35), mkazi wa Mwanakwerekwe Zanzibar, amekamatwa na Jeshi la Polisi Zanzibar, kwa tuhuma za mauaji ya aliyekuwa Padri wa Kanisa Katoliki Zanzibar, Evaristus Mushi. Taarifa hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Kamishna wa Jeshi hilo Zanzibar, Mussa Ali Mussa, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Kwa mujibu wa Kamishna Mussa, mtuhumiwa huyo alikamatwa Machi 13, mwaka huu, katika Mtaa wa Kariakoo, Zanzibar na atafikishwa mahakamani baada ya taratibu zote kukamilika.

“Huu ni mwanzo tu, kwani Jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi wa kitaalamu ili kuhakikisha watu wote wanaohusika na matukio ya uhalifu hapa Zanzibar, wanakamatwa na kufikishwa katika mkondo wa sheria.

“Jalada la mtuhumiwa huyu tayari limeshapelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka kwa hatua za kisheria kwa sababu yeye ndiye atakayetupa mwongozo juu ya suala hili.

“Kabla mtuhumiwa hajakamatwa, tulifanya upelelezi kwa kutumia michoro na alipokamatwa, watu waliokuwa eneo la tukio siku ambayo padri aliuawa, walimtambua kwamba ndiye aliyekuwapo.

Mastaa wa Tanzania waibua mjadala Mombasa

ABDULRAHMAN SHERIFF, MOMBASA
WATANZANIA wanaofanya biashara mjini hapa wameeleza masikitiko yao kwa wanasoka wanaochezea timu ya Bandari kutoitwa timu ya taifa ya nchi yao, Taifa Stars.

 
Mohamed Mbwana kutoka Tanga alisema kwamba anashangaa ni kwa nini wanaochagua wachezaji wa timu ya taifa hawafiki Mombasa kuwashuhudia wanasoka wanaoichezea Bandari kutoka Bongo.

Mbwana aliliambia Mwanaspoti mara baada ya Bandari kuishinda Sony Sugar mabao 3-0 kwamba beki Meshack Abel na viraka David Naftali na Thomas Maurice wote wanacheza vizuri na wanastahili kuitwa Taifa Stars.

"Dar es Salaam na Mombasa ni karibu, benchi la ufundi lifike kuwashuhudia hawa wachezaji wanavyocheza kwa masilahi ya timu ya Taifa," alisema Mbwana.

Yanga: Niyonzima amesaini miaka miwili

MPAMBANAJI, mfanyabishara na kiongozi mwenye ushawishi mkubwa ndani ya Yanga hususani kwenye usajili, Seif Ahmed 'Seif Magari' amesisitiza kuwa kiungo Mnyarwanda Haruna Niyonzima ameshasaini Yanga na kama Simba na Malkia wao wa Nyuki walikuwa na mipango naye wamechemka.

Haruna mwenyewe ambaye yupo jijini Dar es Salaam amekataa kukiri kama amesaini Yanga na ameendelea kusisitiza kuwa itajulikana msimu ukimalizika Mei 18 kwani atakuwa ameshaamua.

Seif, ambaye ni mmoja wa wajumbe wa Baraza la Udhamini la Yanga, amekuwa akifanya usajili wa Yanga kwa kushirikiana na Abdallah Bin Kleb na benchi la ufundi kwa takribani misimu mitatu mfululizo sasa.

Kiongozi huyo amewahakikisha mashabiki wa Yanga kuwa wasiwe na wasiwasi wala wasitishwe na maneno ya Simba au Azam kwavile tayari amemsainisha Niyonzima mkataba wa miaka miwili muda mfupi kabla ya kwenda kwao wikiendi iliyopita kucheza mechi ya taifa lake la Rwanda dhidi ya Mali. Mali ilishinda 2-1.

Lakini, Haruna wikiendi hiyo hiyo alizungumza na Mwanaspoti jijini Kigali baada ya mechi na Mali, akatamka kwamba hajasaini Yanga kwavile anasubiri msimu umalizike na wakala wake aliyeko Ulaya anamtafutia timu na kwamba endapo mambo hayataenda sawa atasaini mkataba mfupi na klabu moja kubwa ya Tanzania.

Evander wa Marekani kuzipiga na Mbongo

IMANI MAKONGORO
BONDIA wa Tanzania, Alphonce Mchumiatumbo ametangaziwa zali la kucheza na Evander Holyfield wa Marekani, lakini mwenyewe anabainisha tangu alipoambiwa anajifua usiku na mchana kumkabili mkali huyo wa dunia.

Mchumiatumbo bondia namba moja kwenye uzani wa juu hapa nchini ameeleza kuwa siku ya bambino hilo ataonyesha uwezo wake wote hadi ule wa ziada kwani hiyo ndiyo nafasi ya yeye kutoka.

"Nimepewa taarifa kuwa Evander anakuja Tanzania Julai mwaka huu kama kutalii lakini pia atacheza pambano moja, na mimi ndiyo nitacheza naye, ni pambano la kuhamasisha ngumi hapa nchini," alisema Mchumiatumbo katika mahojiano na Mwanaspoti.

Mchumiatumbo anabainisha kuwa kuna promota kutoka Marekani aliyemtaja kwa jina la Jorge alimfuata baada ya pambano lake na Joseph Marwa na kumwambia ajiandae atacheza na Evander.

"Kwa maelezo ya promota huyo Evandar ameshuka kiuchumi siyo yule wa enzi hizo wakati anampiga Mike 'Iron' Tyson' na sasa ameamua kuja Tanzania kutalii," alibainisha bondia huyo.

DIAMOND PLATINUM AFUNIKA GEITA USIKU WA KUAMKIA LEO

....usipime....

Taratibu ikaanza nyimbo...

Watu 40 wahofiwa kufukiwa baada ya jengo la ghorofa 15 kuporomoka Dar

Dar es Salaam. 
Watu zaidi ya 40 wanahofiwa kufukiwa na kifusi baada ya jengo la ghorofa 16 lililokuwa linajengwa kuporomoka katikati ya Jiji la Dar es Salaam jana asubuhi.

Kuporomoka kwa ghorofa hilo lililokuwa katika Mtaa wa Indira Gandhi, kulizua huzuni, taharuki na simanzi kwa ndugu na jamaa waliofika kwenye eneo la tukio kutaka kufahamu nini kimetokea.

Shughuli mbalimbali katikati ya jiji hilo zilisimama kwa siku nzima baada ya jengo hilo kuanguka na kusababisha vifo vya watu watano, 13 kuokolewa huku zaidi ya watu 40 wakisadikiwa kufukiwa na kifusi cha udongo wa jengo hilo.

Jengo lililoporomoka

Jengo hilo lililokuwa likijengwa mkabala na Msikiti wa Shia Ithnasheri ulioko Barabara ya 
Indira Gandhi na Kampuni ya ‘Lucky Construction Limited’ lilianguka majira ya saa 2.30 asubuhi wakati ujenzi ukiendelea juu huku chini watoto wakicheza mpira na mama lishe wakiendelea na biashara zao kama kawaida.
Pamoja na vifo na wengine kujeruhiwa, magari takribani manne yalifunikwa na kifusi cha jengo hilo na kupondwa pondwa na kuwa kama chapati.

Katibu wa Msikiti wa huo wa Shia Ithnasheri, Mushtaq Damji alisema: “Leo tulikuwa na kitu kama jumuiya kwa jamii ya wahindu, tulipanga kusherehekea lakini yote yakafutika.
“Baada ya swala ya alfajiri, watu walikuwa wanazungumza hapa na pale na baada ya kupambazuka, watoto walikuwa wanacheza mpira, walikuwa 9. Sasa, bahati nzuri watoto saba wakakimbia na watoto wawili wakawa wamekwama,” alisema Damji.

HUYU NDO BINTI ALIYECHEZEA KICHAPO KUTOKA KWA MPENZI WAKE BAADA YA KUBUSU KIFUA CHA DIAMOND

Binti uzalendo ulimshinda, akaenda kumnyonya kifua DiamondBinti uzalendo ulimshinda, akaenda kumnyonya matiti Diamond
Binti huyo akilia baada ya kuvutwa na kuchezea kichapo kutoka kwa bwana wake

Binti huyo akilia baada ya kuvutwa na kuchezea kichapo kutoka kwa bwana wake
Binti alipokua kwenye show ya Diamond, uzalendo ulimshinda, akaenda kunyonya chuchu za diamond kama inavyoonekana pichani  Kitendo hicho kilimuudhi bwana wake, ambapo alimvuta binti huyo na kumchapa makofi. Katika picha ya pili, binti huyo anaonekana akilia baada ya kuchezea kichapo, huku akiwa amewekwa “chemba” na boyfriend wake.

Friday, March 29, 2013

RAIS KIKWETE AFIKA ENEO LA TUKIO NA KUSHUHUDIA HALI HALISI YA KUANGUKA KWA JENGO LA GHOROFA 16

IRENE JAMII Blog Tunakupongeza Rais wetu kwa hili jambo unajiruma sana Rais Jakaya Kikwete.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mbunge,Mh Mbatia muda mfupi mara baada ya kufika na kujionea hali halisi ya jengo la Ghorofa lililoporomoka mapema leo asubuhi na kupelekea watu wawili kupoteza maisha na wengine 17 kujeruhiwa vibaya.,aidha shughuli za ukoaji zinaendelea kwani inadaiwa kuna watu wengi zaidi wamefunikwa na jengo hilo.
Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar Es Salaam,Mh Said cMeck Sadick shoto akiwa ameambatana na Rais Jakaya Kikwete muda mfupi mara baada ya kufika na kujionea hali halisi ya jengo la Ghorofa lililoporomoka mapema leo asubuhi na kupelekea watu wawili kupoteza maisha na wengine 17 kujeruhiwa vibaya,kulia ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar Es Salaam,Mh Said Meck Sadcik akifafanua jambo kwa Rais Jakaya Kikwete muda mfupi mara baada ya kufika na kujionea hali halisi ya jengo la Ghorofa lililoporomoka mapema leo asubuhi na kupelekea watu wawili kupoteza maisha na wengine 17 kujeruhiwa vibaya,kulia ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Rais Kikwete akiondoka eneo la tukio mara baada ya kujionea hali halisi ya tukio zima la kuanguka kwa ghorofa linalodaiwa kuwa na idadi ya ghorofa 16.

Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar Es Salaam,Mh Said Meck Sadick akipewa pole na Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.Dkt.ASha-Rose Migiro kuhusiana na tukio zima la kuanguka kwa jengo la Ghorofa mapema leo asubuhi,jijini Dar.

PICHA ZA KINACHOENDELEA KATIKA ENEO LILIPOANGUKA GOROFA DAR

Imetokea leo hii Morogoro Road na Indira Gandhi,inasemekana Watu wapatao 60 walikuwepo ndani yake.. watoto wa Madrassa walikuwemo katika jengo hili na pia mpaka sasa maiti zilizoopolewa ni zaidi 60 na majeruhi zaidi ya 30 wamekimbizwa hospitali, Bado pia kuna baadhi ya watu hai ndani yake.
Jitihada za uokoaji zimeanza kufanyika, Waziri Nchimbi tayari amekwishafika eneo la tukio mpaka sasa japo kuna uhaba wa vyombo vinavyostahili kushughulikia hali hii.




Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa, jengo lenye ghorofa zaidi ya 12  jijini Dar es Salaam limeanguka na kusababisha vifo vya makumi ya watu.

Inasadikika watoto waliokuwa wanacheza kwenye uwanja wa michezo na wafanyakazi wa ujenzi wamefukiwa. Kwa sasa tunaendelea na jitihada za uokozi na tutatoa taarifa baadae.”
Picha ya jengo hilo baada ya kuanguka
IMG-20130329-WA001
BBC Swahili: Kulingana na walioshuhudia ajali hiyo, watu walisikika wakipiga mayowe kutaka msaada.

BREAKING NEWS ! INDIRA GANDHI NA MOROGORO RD JENGO LA GOROFA ZAIDI 16 LIMESHUKA LOTE

Jengo lililokua bado linaendelea kujengwa katika makutano ya barabara ya Indra Gadhi na morogoro lenye ghorofa zaidi ya 16 limedondoka wakati likendelea na ujenzi na kuangukia msikiti ambao unasadikiwa kuwa na madrassa ambayo kulikua na wanafunzi ndani wakati wa tukio
                     Jengo hili lililopo mjini katika mtaa wa Indra Gjandi limeanguka asubuhi.
Mpaka sasa watu watu 12 wameshapoteza maisha,limedondokea msikiti wa SHIA.
Mpaka sasa eneo la tukio kuna mkuu wa mkoa wa Dar es salaam na meya,Mmiliki wa jengo hilo bado hajajulikana.Ndani ya jengo hilo kulikuwa na watu wasio pungua 60 wakiendelea na ujenzi.Watu zaidi ya 14mpaka sasa wameshakimbizwa hospitali.Tutaendelea kuwajulisha zaidi.

BREAKING NEWS:Jengo la ghorofa Limeanguka Morogoro road muda si mrefu.

Chanzo bado hakijajulikana waokoaji wako wanaendelea na shughuli za uhokoaji zinaendelea..
Limeangukia msikiti na ndani kulikuwa na watoto,mpaka sasa watu 10 wameshakimbizwa hospital.Jengo hilo lilikuwa linaendelewa kujengwa lina golofa 16.
                PICHA ZOTE NA IRENE JAMII Blog Habari kamili kuwajia baadae...
Picha kutoka K/KOO eneo la tukio.

PICHA AMBAZO HUJAONA ZA TUZO YA MWANAMAKUKA

Unity of Women Friends katika picha ya pamoja!
Mwenyekiti wa UWF Bi Mariam Shamo.
Mc wa siku hiyo Babie Kabaye.
Mkurugenzi mtendaji wa clouds media Joseph Kusaga na Sheba Kusaga.
 Q Chief akitoa burudani
Ommy Dimpoz kazini.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA MACHI 29,2013

.
.
.

Mwanafunzi akamatwa na meno ya tembo.

MWANAFUNZI wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Kibaha, Christopher Julius (18), amekamatwa na vipande 13 vya meno ya tembo. Akizungumza Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleimani Kova, alisema mwanafunzi huyo alikamatwa Machi 22, mwaka huu eneo la Kimara Wilayani Kinondoni.
Alisema mwanafunzi huyo alikamatwa baada ya askari kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema ambapo walifika eneo husika na kufanikiwa kumkamata pamoja na vipande 13 vya meno ya tembo.

Alisema thamani ya vipande hivyo bado haijafahamika na wanaendelea na upelelezi kubaini kama mtuhumiwa huyo alikuwa peke yake au alikuwa na wenzake.

Katika tukio jingine, alisema wamefanikiwa kukamata watuhumiwa wanne wakiwa na bunduki mbili aina ya Short gun yenye namba za usajili AB44736 na ya pili ni Greener yenye namba za usajili 10883 pamoja na risasi 17.

Kesi ya Lwakatare yaanza Mahakama Kuu


Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare
MAOMBI yaliyowasilishwa na jopo la mawakili wanaomtetea Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare kupinga uamuzi wa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini kufuta na kumfungulia kesi nyingine mteja wao yatasikilizwa na Jaji Laurence Kaduri.

Jaji Kaduri wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam alipangwa kusikiliza maombi hayo jana. Majalada mawili ya kesi ya kujihusisha na ugaidi inayomkabili Lwakatare na Ludovick Joseph yalifikishwa mahakamani hapo Jumanne.

Majalada hayo yalipelekwa Mahakama Kuu kutokana na maombi yaliyowasilishwa na jopo la mawakili wa Lwakatare ambao wanaiomba mahakama hiyo kuyafanyia marejeo au kuchunguza ili kujiridhisha usahihi na uhalali wa mwenendo wa kesi katika jalada namba 37 na namba 6 ya mwaka huu.

Wanaomba mahakama hiyo kutengua hati ya DPP iliyofuta mashtaka dhidi ya washtakiwa hao kabla ya kuwafungulia mashtaka mengine kama hayo.

Jopo hilo linaomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa uamuzi wa maombi ya dhamana uliokuwa umepangwa kutolewa na Hakimu Mkazi Emilius Mchauru Machi 20 mwaka huu katika kesi namba 37 iliyofutwa.

“Tunaomba mahakama ifanye marejeo na kutengua mwenendo wa kesi mpya namba 6/2013 iliyofunguliwa baada ya kesi namba 37 kufutwa badala yake tunaomba jalada lililofutwa liendelee.

Mzazi aeleza chanzo cha wanafunzi kufeli kidato cha nne mwaka jana.

MWENYEKITI wa Wazazi Wilaya ya Babati Vijijini, Willy Bayo, amesema matokeo mabaya kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha nne mwaka jana yametokana na mitaala mibovu ya kufundishia pamoja na kuzibwa kwa mianya ya uvujaji wa mitihani iliyokuwa ikifanywa na baadhi ya walimu nchini.

Bayo alitoa kauli hiyo juzi wakati akichangia mada kwenye kikao cha wadau wa elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Manyara, kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo.

Alisema pamoja na matokeo hayo kuwa ni janga la kitaifa inapaswa serikali ielewe kwamba tatizo hilo limechangiwa na kuzibwa na kudhibitiwa kwa uvujaji wa mitihani uliokuwa ukifanywa na baadhi ya walimu kwenda kwa watahiniwa nchini.
Alibainisha kwamba tegemeo la kuvuja kwa mitihani kuliwafanya pia walimu kutokuwa na ari ya kufanya kazi kwa kutegemea kuwa mwisho wa masomo mwanafunzi atafaulu kwa kununua mitihani.

Mtoto Debora Riziki (3) auawa, azikwa sebuleni katika nyumba yao.

MTOTO Debora Riziki (3), mkazi wa Kijiji cha Isange wilayani Rungwe, ameuawa na mwili wake kuzikwa sebuleni katika nyumba yao.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya 7:40 mchana na anayetuhumiwa kuhusika na mauaji hayo ni baba mzazi wa mtoto huyo, Riziki Mwangoka (27).

Alisema sababu ya kufanya ukatili huo ni kutokana na mgogoro wa kindoa kati ya baba huyo na mama wa mtoto huyo, Esther Msafiri Mwambenja (23), mkazi wa Kijiji cha Kimbukwe.
Kamanda Diwani alisema kutokana na mgogoro wa muda mrefu wanandoa hao walitengana na kwamba siku ya tukio baba huyo alifika nyumbani kwa mzazi mwenzake na kumchukua mtoto huyo kwa nguvu na kwenda kumuua.

Alisema mwili wa marehemu umeshafanyiwa uchunguzi na umekabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi. Polisi wanaendeea na utaratibu kwa ajili ya kumfikisha mtuhumiwa mahakamani.
Kamanda Diwani alitoa wito kwa jamii kuacha kujichukulia sheria mkononi ili kuepusha matatizo yanayoweza kuepukika.

MASHUJAA BAND WASEMA: CHONDE CHONDE TWANGA, MSTITUCHOKOZE TUTANYOFOA NUSU YA BENDI YENU

KUFUATIA tetesi za baadhi ya wanamuziki wa Mashujaa kutaka kurejea Twanga Pepeta, bendi hiyo ya Mashujaa imepiga mkwara mzito juu ya jambo hilo.

Meneja wa Mashujaa Band, Martin Sospeter ameiambia Saluti5 kuwa anajua Twanga ingependa kurejesha wanamuziki wao wote waliojiunga na Mashujaa lakini amewataka kufanya hivyo kwa umakini mkubwa.
Martin (pichani kushoto) amesema Twanga wahakikishe kuwa wana mikataba na wanamuziki wao kabla gharika halijawaangukia.

“Wao wachukue wanamuziki wetu lakini wajue kuwa kuna siku kisu kitagusa mfupa, hatutavumilia tutazoa wanamuziki wao wote ambao hawana mikataba, tutanyofoa zaidi ya nusu ya bendi kuanzia mstari wa nyuma kwa wapiga vyombo hadi mbele kwa waimbaji.

Mtoto mgonjwa atelekezwa Kivukoni

MWANAMKE asiyefahamika juzi alimtelekeza mtoto mdogo wa kike anayekadiriwa kuwa na miaka mitano ambaye ni mgonjwa katika eneo la Kivuko cha Kisorya, wilayani Bunda, Mara.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kisorya, Mashaka Mahulilo, alisema mtoto huyo ambaye pia amepooza mguu mmoja alitelekezwa juzi, majira ya saa 9:30 mchana katika eneo la kijiji cha 

Kisoya, baada ya Kivuko cha MV Ujenzi kinachofanya safari kati ya ng’ambo ya Kisorya, wilayani Bunda, na Ngoma Lugezi wilayani Ukerewe kutia nanga katika eneo hilo.

Alisema mwanamke huyo alikuwa ni kati ya abiria waliokuwa ndani ya kivuko hicho wakitokea wilayani Ukerewe na kwamba baada ya kufika eneo hilo alimtelekeza mtoto huyo.
Mahulilo alisema mtoto huyo ambaye ni kiziwi aliachwa na mama yake eneo hilo, akiwa na mifuko miwili midogo ya nailoni iliyokuwa na nguo zake.

Alisema mtoto huyo aliokotwa na wasamaria wema akiwa ukingoni mwa daraja la kivuko hicho na kwamba alichukuliwa na mwananchi mmoja mkazi wa kijiji hicho aliyekabidhiwa mbele ya viongozi wa serikali ambaye sasa ndiye anayeishi naye.
Kutokana na tukio hilo, baadhi ya wananchi wamelaani kitendo kilichofanywa na mwanamke huyo.

Watanzania 235 wakamatwa na ‘unga’

WATANZANIA 235 wanaojihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya nje ya nchi wamekamatwa.

Kamishna wa Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya Nchini, Christopher Shekiondo, alibainisha hayo jijini Dar es Salaam jana alipozungumza na waandishi wa habari.
Shekiondo alisema Watanzania hao wamekamatwa kuanzia mwaka 2008 hadi mwaka jana katika nchi za Brazil, Kenya, China, Pakistan, Falme za Kiarabu na Mauritius.

Kwa mujibu wa kamishna huyo, baadhi ya Watanzania wamehukumiwa adhabu ya kifungo cha maisha na wengine adhabu ya kifo.
Aidha alisema jumla ya kilo 728.3 za heroin zilikamatwa katika kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2008 hadi 2012 na kwamba kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu kilo 12 za dawa hizo zilikamatwa.

“Pia kilo 352.3 za cocaine zilikamatwa kati ya 2008 hadi 2012, kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu kilo tatu za cocaine zilikamatwa,” alisema.
Aliongeza katika kipindi hicho watuhumiwa 149 walikamatwa na kufikishwa mahakamani kati ya mwaka 2010 na 2012 kwa makosa mbalimbali ya kujihusisha na biashara hiyo.
Kwa mujibu wa kamishna huyo, kati ya mwaka 2010 hadi 2012, kilo 96.88 za heroin ziliteketezwa katika mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Mtwara na Lindi.

NSSF yalidai Kanisa Anglikana Sh36 milioni

Tanga. Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanga, limefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kutokulipa michango ya wafanyakazi 25 wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Pia, linadaiwa kulipa hundi hewa ya Sh4,434,716.06
Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwanasheria wa NSSF, Samson Maira mbele ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Tanga, Ramla Shehangilo kuwa kanisa hilo halikuwasilisha michango ya watumishi wake kuanzia Januari 2006 hadi Juni 2012, ikiwa na thamani ya Sh35,950,573.63.

Aliendelea kudai kuwa, kati ya 35,950,5673.63 ni deni halisi la michango ya wafanyakazi wa kanisa hilo, ambao ni wanachama wa NSSF ambalo baada ya makubaliano lilitakiwa kulipwa kwa awamu hadi Aprili 2008.

Pia, Maira alidai katika kipindi hicho, Kanisa hilo lilitoa hundi ya Sh4,434,716.06, ikiwa ni malipo ya wanachama wa NSSF, lakini ilipofikishwa benki ikabainika ni hewa.

Hata hivyo, hakuna mwakilishi yeyote wa kanisa hilo aliyehudhuria mahakamani na Hakimu Shehagilo alitoa hati ya kukamatwa kwa kiongozi wa kanisa hilo, kwa kukaidi wito wa mahakama.

Moshi, Arusha kuingia dijitali

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema, inatarajia kuzima mitambo ya kurusha matangazo ya televisheni ya mfumo wa analojia katika Mji wa Moshi na Jiji la Arusha Machi 31 mwaka huu.

Kuzimwa kwa maeneo hayo kunafikisha jumla ya mikoa sita ambayo ni Dar es Salaam, 

Tanga, Dodoma na Mwanza  ambayo tayari inapokea matangazo ya televisheni kwa njia ya dijitali na kubaki Mkoa wa Mbeya utakaozimwa Aprili 30, mwaka huu.

Meneja  Mawasiliano wa Mamlaka hiyo, Inocent Mungi akizungumza katika kipindi cha Jambo Tanzania cha Shirika la Utangazaji TBC1  juzi, aliwataka wadau kushirikiana na TCRA ili kuondoa changamoto zilizopo zinazotokana na mfumo huo.


Bei ya vyakula Dar yashika kasi kipindi cha Pasaka

Dar es Salaam
Wakati Wakristo nchini wakijiandaa kuungana na wenzao duniani kusherehekea Sikukuu ya Pasaka, bei ya  vyakula jijini imezidi kupanda kutokana na  sababu mbalimbali.

Akizungumza sababu ya kupanda kwa bei hizo mfanyabiashara wa Soko la Kisutu, Japheti Kibiriti alisema moja ya sababu ni baadhi ya magari yanayosafirisha bidhaa kukwama njiani kitokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Alisema bidhaa zilizopanda kwenye masoko mbalimbali jijini Dar es Salaam ni mchele, nyanya, viazi karoti na unga wa sembe.
Kibiriti alisema bei ya nyanya imepanda ambapo tenga la ndoo mbili za plastiki  sasa linauzwa kwa Sh50,000 kutoka Sh30,000.

Mchele unauzwa Sh2,400 hadi Sh2,600, karoti Sh2,000, viazi vinauzwa kwa Sh2,000, unga wa sembe kilo moja huuzwa Sh1700 huku pilipili hoho zikiuzwa kwa kilo moja  Sh3,000.
Mfanyabiashara wa  Soko la Buguruni, Bakari Mponda alisema mkungu mmoja wa ndizi huuzwa kuanzia Sh22,000 hadi  Sh30,000 awali mkungu huo ulikuwa unauzwa kwa Sh15,000.

Huzuni yatawala kifo cha mbunge wa CUF

Mbunge wa Chambani (CUF), Salim Hemed Khamis (60) amefariki dunia jana katika hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa amelazwa baada ya kuanguka ghafla juzi kwenye Ofisi za Bunge, Dar es Salaam.
               Mbunge wa Chambani (CUF),marehemu Salim Hemed Khamis.
Kifo cha mbunge huyo kimewagusa wengi akiwamo Rais Jakaya Kikwete ambaye ametoa ndege yake ili kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Pemba. Ofisi ya Bunge imethibitisha kutokea kwa kifo hicho cha mbunge huyo na kueleza kuwa, alipatwa na ugonjwa wa kiharusi uliosababishwa na ugonjwa wa moyo (Hypertension).

Khamis anatarajiwa kusafirishwa kisha kuzikwa leo kijijini kwao Chambani, Pemba baada ya jitihada za kumsafirisha jana kushindikana na wabunge wengi kuomba kushiriki kumuaga.
Mbunge huyo atasafirishwa leo saa tatu asubuhi baada ya shughuli ya kuaga itakayofanyika kwenye Viwanja vya Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. Spika wa Bunge, Anne Makinda ametangaza kusitishwa kwa shughuli zote za Kamati za Bunge hadi Jumanne Aprili 2, kutokana na msiba huo.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Makinda alisema: “Ninatoa pole kwa familia ya marehemu, wananchi wa Chambani, Wajumbe wa Kamati ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, wabunge wote na Watanzania wote kwa jumla”.

Thursday, March 28, 2013

DIDA AMPA MAKAVU LIVE SINTAH


WADAU KWELI MIMI NI MTU MZIMA WALA SI KIPANDE NA SIJAFIKIA UTU UZIMA UOOOO SABABU SICHAMBII PANGA WALA SIPIGI DANADANA KWA MAKALIO,ILA NAPENDA NIWATOE HOFU NYIE MNAOJIFANYA MNANIJUA SANA KULIKO MAMA YANGU MZAZI NI HIVI NAMTAJA LIVE SABABU ANAJUA SIMUHOFII WALA SIMUOGOPI NA SINA SHARI NAE ILA AKIITAKA KWANGU ATAINUNUA KWA BEI RAHISI BILA YA VAT,SINTA NAKUTAJA NA NAJUA HUWEZI CHAMBANA NA MIMI HATA ROBO MAANA NITAKUPA UMAARUFU WA MUDA MCHACHE MAANA HATA WA KUTATIZA KATIKATI YA MSAFARA WA RAISI UTACHUKUA MUDA,NYIE MNAOSEMA NAMUOGOPA SINTA ANALIJUA ILO KUWA SIMUOGOPI HATA KIDOGO NA NIKITAKA KUCHAMBANA NAE SI HUMU NAMTAFUTA KWA GHARAMA ZANGU TUCHAMBANE FACE TO FACE KWA HIYO SINTA FANYA YAKO ANDIKA YAKO UMO KWENYE BLOG YAKO KWELI MIMI MTOTO WA KISWAHILI SINA UZUNGU HATA ROBO ILA UKINICHOKONOA UTAJUA KAMA MIMI MZUNGU AU MZARAMU NYIE WAZUNGU ENDELEENI NA UZUNGU WENU KWANGU NDIO KWANZA MKOKO UMEALIKA MAUA,KUMBUKENI MATUSI YENU HAYANITOI KOPE NDIO KWANZA ZIMENISIMAMA KAMA KIBANDA CHA SIMU.

Breaking News:Mbunge wa Chambani Salim Hemed Khamis,amefariki dunia muda mfupi uliopita.

 
Katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili .Taratibu za kuusafirisha mwili kuelekea Pemba kwa mazishi zinafanyika.

BREAKING NEWS. ALIEKUA MBUNGE WA JIMBO LA CHAMBANI AFARIKI DUNIA LEO

ALIEKUA MBUNGE WA JIMBO LA CHAMBANI AMEFARIKI DUNIA LEO BAADA YA KUZIDIWA ALIPOANGUKA KATIKA VIKAO VYA BUNGGE,HABARI KAMILI ZITAFUATE BADO UONGOZI WA CHOMBO HICHI UNAFATILIA KUJUA ZAIDI KUHUSU KIFO HICHO.

SIKU YA JANA..
MBUNGE wa Chambani, Salim Hemed Khamis (CUF), jana alianguka ghafla katika mkutano wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Salim alianguka saa tano asubuhi wakati akihudhuria mkutano wa kamati hiyo, uliokuwa ukifanyika katika ofisi ndogo za Bunge, jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo lilizua hofu kwa wabunge wengine waliokuwamo, ambapo mkutano huo ulisitishwa kwa muda na juhudi za kumshughulikia zilianza, kwani alitolewa nje ya ukumbi na kuanza kupepewa.

Hata hivyo mbunge huyo alikimbizwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuingizwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU) kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Edward Lowassa, alilazimika kutoka nje ya ukumbi ambapo aliungana na wenzake katika kuchanga mawazo kuhusu namna ya kumpeleka hospitali mbunge huyo.

Wakati majadiliano hayo yakiendelea, hali ya mbunge huyo anayedaiwa kuwa anasumbuliwa na shinikizo la damu iliendelea kubadilika, huku akitokwa na jasho jingi.

Habari kuwajia baadae..

Kikwete asimulia alivyoiba wali JKT


Rais Jakaya Kikwete
RAIS Jakaya Kikwete amesimulia maisha yake ya jeshini, huku akikumbuka namna alivyokamatwa na mkuu wa jiko (afande ubwabwa) akiiba wali. Rais Kikwete alitoa ushuhuda huo wakati akifunga mafunzo maalumu ya uongozi kwa wabunge na kuzindua mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria.

Hafla hiyo ilifanyika juzi katika Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kikosi cha 832 KJ, kilichopo Ruvu, Kibaha mkoani Pwani, ambapo viongozi mbalimbali walihudhuria.

Rais Kikwete aliwakumbusha vijana hao kwamba yeye ni miongoni mwa watu waliochukua mafunzo ya JKT kambini hapo akiwa katika Operesheni Tumaini mwaka 1972.

Rais Kikwete alisema katika mafunzo hayo alijengwa vizuri, ingawa hadi leo bado anakumbuka matukio mawili ya kufurahisha na kusikitisha akiwa kambini hapo.

Alisema tukio la kwanza ambalo hawezi kusahau ni pale alipokamatwa akiiba wali na tukio jingine ni kuhusu kifo cha askari mwenzao aliyefariki dunia baada ya kukanyagwa na trekta.

“Nawashukuru kwa kunialika katika shughuli hii, nimetembelea na kujionea miradi mbalimbali inayoendelea kufanywa hapa kambini.

Mbunge aanguka kikaoni ni Salim Hemed Khamis (CUF).

MBUNGE wa Chambani, Salim Hemed Khamis (CUF), jana alianguka ghafla katika mkutano wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Salim alianguka saa tano asubuhi wakati akihudhuria mkutano wa kamati hiyo, uliokuwa ukifanyika katika ofisi ndogo za Bunge, jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo lilizua hofu kwa wabunge wengine waliokuwamo, ambapo mkutano huo ulisitishwa kwa muda na juhudi za kumshughulikia zilianza, kwani alitolewa nje ya ukumbi na kuanza kupepewa.

Hata hivyo mbunge huyo alikimbizwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuingizwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU) kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Edward Lowassa, alilazimika kutoka nje ya ukumbi ambapo aliungana na wenzake katika kuchanga mawazo kuhusu namna ya kumpeleka hospitali mbunge huyo.

Wakati majadiliano hayo yakiendelea, hali ya mbunge huyo anayedaiwa kuwa anasumbuliwa na shinikizo la damu iliendelea kubadilika, huku akitokwa na jasho jingi.

Kutokana na hali hiyo, mwishowe mbunge huyo alipoteza fahamu katika majengo ya Ofisi za Bunge, kitendo ambacho kiliwafanya wabunge wenzake kushindwa la kufanya.

Wabunge wanne walijaribu kumbeba mbunge huyo ili waweze kushuka naye chini, lakini walishindwa kutokana na uzito wake na hivyo wakalazimika kuomba msaada kwa waandishi wa habari.

Siri nzito za kumpagawisha mpenzi wako

Ili uweze kuwa na furaha maishani, lazima uwe katika uhusiano imara usiotetereka. Kama unaishi na mke au mume ambaye moyo wako umemchagua lazima furaha itatawala katika nyumba yenu. Lakini rafiki zangu, huwezi kuwa katika ndoa yenye furaha kama hukuwa na mchumba bora. Kwa maneno mengine, lazima uanze kuboresha uchumba wako kwanza, uwe na uhakika kwamba mwenzi uliyenaye ni sahihi ili ukiingia kwenye ndoa usijute.

Mapenzi ni sawa na bustani nzuri ya maua rafiki zangu, wakati mwingine inahitaji mbolea, kumwagiliwa maji na hata kupaliliwa.

Kwa kufanya hivyo utazidisha ladha ya mapenzi na kuyafanya yazidi kuwa na nguvu zaidi ya awali. Lakini kama hutamwagilia, hutaweka mbolea, hutapalilia, hesabu kwamba mapenzi yako yanaweza kuanza kupoteza nguvu taratibu na hatimaye kufa kabisa.

Kikubwa ambacho nimepanga kuzungumza nanyi leo ni jinsi ya kumpagawisha mwenzi wako ili awe wako peke yako. Umeshawahi kufikiria kwamba, kama ukishindwa kutimiza mambo fulani katika penzi au ndoa yako, mwenzi wako anaweza kuwa wa kushea?

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate