EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, July 31, 2012

‘Dawa ya Babu wa Loliondo ni feki’

Utafiti umebaini kwamba dawa iliyokuwa ikitolewa na mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila maarufu kama babu wa Loliondo ni feki na kwamba haina uwezo wa kutibu Ukimwi wala kisukari.

Hayo yalielezwa bungeni jana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi, alipokuwa akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka 2012/13.

Alisema utafiti wa kulinganisha wagonjwa wa ukimwi na kisukari waliokunywa dawa hiyo na wale ambao hawakunywa umebaini kwamba hakuna utofauti wa afya ya mgonjwa.

Alisema utafiti huo unafanywa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMRI), ulianza Machi mwaka huu na kwamba unahusisha wagonjwa 200 wanaofuatiliwa kwa kupimwa damu, kinga ya mwili (CD4) na uzito wa mgonjwa, ambao ulifanyika tangu mgonjwa alipokunywa kikombe cha babu.

“Matokeo ya awali ya utafiti yameonyesha kuwa hakuna utofauti katika vipimo vya kimaabara pamoja na damu, CD4, uzito na ubora wa afya ya wagonjwa kati ya waliokunywa na wale ambao hawakunywa dawa ya mchungaji,” alisema Dk. Mwinyi.

Alisema lengo la utafiti huo ni kubaini uwezo wa dawa hiyo katika kutibu magonjwa aliyosema dawa yake inayatibu ili kuona kama kuna utofauti wowote baada ya mgonjwa kutumia dawa.


 CHANZO: NIPASHE

Tamko la Wanamuziki: Zuio la matumizi ya nyimbo kwa Kampuni za Simu kwenye ringtone



YAH: KUFUTA MIKATABA NA KUSIMAMISHA KUUZA MUZIKI WA BONGO FLEVA, GOSPEL, DANSI NA TAARABU KWENYE MITANDAO YA SIMU.

Husika na kichwa cha habari hapo juu,

Kwa ujumla wetu sisi Wasanii toka Tanzania tunaofanya muziki wa Gospel, Rhumba , Taarabu pamoja na Bongo fleva tumeamua kutoa agizo kwenu la kusimamisha mauzo ya kazi zetu za muziki katika mtindo wa Ringtone na Callertunes katika mitandao ya simu ya VodaCom, Zantel, Tigo na Airtel na kufuta mkataba tuliosaini kati yetu sisi Wasanii na Kampuni yako mpaka hapo tutakapokaa sisi kama wasanii, nyinyi kama wasambazaji wa muziki wetu, pamoja na Mitandao ya simu ili kuzungumzia namna mpya ya sisi na nyinyi tutakavyofanya kazi.

Sababu ya sisi Wasanii kusimamisha na kufuta mikataba kati yetu na wanaofanya biashara ya kuuza maudhui yetu ni pamoja kampuni husika kushindwa kuweka wazi taarifa za mauzo ya nyimbo pamoja na kutolipa katika muda husika kama ilivyoanishwa katika mikataba husika.

Sababu ya pili ni mitandao ya simu kuchukua kiasi kikubwa cha fedha ambacho ni asilimia themanini ya mauzo yote ya maudhui yetu, jambo hili linatuumiza na limetufanya tuendelee kuishi kwa kutegemea aina moja ya pato toka kwenye shoo.

Hivyo tumeziagiza kampuni zote zinazofanya kazi ya kuuza maudhui yetu kutoa maelekezo kwenye mtandao husika kuwaelekeza kusimamisha mauzo ya kazi zetu za sanaa ndani ya siku saba kuanzia leo tarehe 30/07/12 ikiwa pamoja na kusimamisha matangazo yote yanayotangaza mauzo ya kazi zetu kwa njia ya Television, Radio, blogs, website, Magazeti na Ujumbe Mfupi wa maneno mpaka hapo tutakapofikia muafaka.

Jumla ya wasanii 153 wameshasaini barua hizo na wengine wanaendelea kusaini.

Mwisho tunawashukuru kwa ushirikianao wenu, na tunaambatanisha sahihi zetu ili kuonyesha uthibitisho wa umoja wetu katika jambo hili.
Asante.

Tamko la CHADEMA kuhusu kufungiwa kwa gazeti la MwanaHalisi

TAMKO LA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

 KUHUSU KUFUNGIWA KWA MWANAHALISI 


Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinalaani uamuzi wa Serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kulifungia kwa muda usiojulikana gazeti la MwanaHalisi kwa kutumia mwanya wa sheria mbovu ya magazeti inayokwenda kinyume na haki za binadamu na utawala bora.

CHADEMA kinaitaka Serikali kulifungulia gazeti hilo haraka iwekanavyo na kimewasiliana na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA kuchukua hatua za kibunge kuisimamia Serikali  kurekebisha udhaifu huo ikiwa inaheshimu uhuru wa habari na inazingatia maslahi ya taifa.

CHADEMA kinatafsiri hatua hiyo ya Serikali ya kufungia gazeti la MwanaHalisi kuwa ni sawa na kufungia uhuru wa kusambaza habari, uhuru wa kupokea habari na uhuru wa kutoa maoni, hivyo tunatoa mwito kwa wananchi na wadau wote wa habari kuungana pamoja kupinga hatua hiyo, na CHADEMA kitaeleza hatua za ziada za kuchukuliwa iwapo Serikali haitasikiliza kauli za wadau wa habari juu ya suala hili.

CHADEMA kinatambua kuwa uamuzi wa Serikali kufungia gazeti hilo kwa mara nyingine tena ni kwenda kinyume na haki za binadamu, kinyume na utawala bora na ni kikwazo kwa demokrasia na maendeleo nchini.

CHADEMA kinapinga hatua ya Serikali ambayo viongozi na watendaji wake wakiwa wametajwa kama watuhumiwa katika habari zilizoandikwa na gazeti hilo imetumia mamlaka haramu ya Waziri mwenye dhamana ya sekta ya habari kugeuka mlalamikaji, mwendesha mashtaka na mfungaji huku ikipuuza taasisi za kusimamia uwajibikaji na haki.

CHADEMA ilitarajia badala ya kulifungia gazeti la MwanaHalisi ingewezesha kufanyika kwa uchunguzi huru kufuatia habari za kiuchunguzi zilizoandikwa na gazeti hilo juu ya watendaji na watumishi wa Serikali kuhusishwa na jaribio la mauji ya Dr Ulimboka Steven, kupanga njama za mauji ya viongozi wa CHADEMA na matukio mengine ambayo yenyewe ndiyo yenye mwelekeo wa kufanya wananchi wapoteze imani na vyombo vya dola hali ambayo inaweza kuhatarisha amani na mshikamano uliopo nchini.

CHADEMA kinalinganisha uamuzi huo wa Serikali uliotangazwa tarehe 30 Julai 2012 na Msajili wa Magazeti chini ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo  kuwa ni sawa  kujichukulia sheria mikononi kwa kuwa Serikali yenye kuheshimu misingi ya asili ya haki ingezingatia kwamba ikiwa chombo chochote cha habari kimedaiwa kuvunja sheria ama kukiuka maadili dhidi ya Serikali, viongozi wake ama watu binafsi mashtaka au malalamiko yangepelekwa kwa taasisi zinazohusika mathalani Baraza la Habari (MCT) au mahakama.

CHADEMA kinafahamu kuwa Serikali imeamua kulifungia kutochapishwa kwa muda usiojulikana gazeti la MwanaHalisi, kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976, kifungu Na. (25) (i); hata hivyo uamuzi huo ni kinyume cha misingi ya asili ya utawala wa sheria.

CHADEMA kinaelewa kwamba zipo sheria nyingine katika nchi yetu ambazo Serikali ingeweza kuzitumia kushughulikia madai iliyoyatoa kuwa Gazeti la Mwanahalisi limeandika habari na makala za uchochezi, uhasama na uzushi kupitia mahakama lakini imeamua kwa makusudi kuendelea kutumia sheria mbaya isiyokuwa na uhalali wa kihaki (illegitimate).

CHADEMA kinakumbusha kuwa kwamba Sheria hiyo ni kati ya Sheria zilizotajwa na Tume ya kukusanya maoni juu ya mfumo wa vyama vingi (Tume ya Nyalali) kuwa ni sheria mbaya miaka 20 iliyopita kuwa na Sheria mbaya na Serikali imekuwa ikikwepa kutunga sheria mpya pamoja na wadau wa habari kuandaa miswada ya sheria ya huduma za vyombo vya habari na uhuru wa taarifa kwa nyakati mbalimbali.

CHADEMA kinatoa mwito kwa wananchi na taasisi zote za kitaifa na kimataifa kufuatilia kwa karibu tukio hili la kufungiwa kwa gazeti la MwanaHalisi na matukio mengine ya hivi karibuni kuhusu asasi za kiraia, makundi mbalimbali katika jamii ikiwemo madaktari na vyama vya siasa hususan CHADEMA yenye kuashiria kwamba Serikali inayoongozwa na CCM imeanza mkakati wa kuficha ukweli na kudhibiti mabadiliko kwa kutumia sheria kandamizi, vyombo vya dola na njia nyingine haramu.

Hivyo, ieleweke kwamba hatua hii dhidi ya Gazeti la MwanaHalisi ni mwanzo tu wa hatua zingine zaidi dhidi ya magazeti mengine na taasisi nyingine hali ambayo inahitaji wananchi na wadau wote kuunganisha nguvu za pamoja katika kuchukua hatua za haraka kuinusuru nchi na mwelekeo huo.

Imetolewa tarehe 30 Julai 2012 na:

John Mnyika (Mb)
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi

PICHA 13 ZA MAANDALIZI MAONYESHO YA NANE NANE ARUSHA YATAANZA SIKU YA KESHO 1/8/2012

                        PICHA ZOTE NA NICOLAUS TRAC -ARUSHA
                                   PICHA ZOTE NA NICOLAUS TRAC -ARUSHA
                                 PICHA ZOTE NA NICOLAUS TRAC -ARUSHA
PICHA ZOTE NA NICOLAUS TRAC -ARUSHA

Watu 13 (majina yametajwa) wakiwamo Walimu, Viongozi wa CWT wamekamatwa na Polisi

Picture
POLISI Mkoani Mbeya, inawashikilia watu 13  wakiwemo viongozi wa Chama cha Walimu na Walimu wenyewe kwa tuhuma za kuhusika na vurugu zilizosababisha hasara zaidi ya shilingi milioni 100 wakati wa mgomo wa walimu ulioanza juzi.

Kitendo cha walimu hao kugoma kuingia darasani kilisababisha baadhi ya maeneo, wanafunzi  kufanya maandamano ya amani ya kudai haki ya kufundishwa  jambo ambalo linadaiwa kutumiwa vibaya na wahalifu kwani walitumia nafasi hiyo kufanya uhalifu kwa kuiba mali za watu.

Wahalifu hao walichoma ofisi za Halmashauri ya Mbozi ndani ya Mji mdogo wa Tunduma  na kuiba mali zilizokuwemo kama  kompyuta 5 za ofisi, pikipiki yenye namba STK 6264, kumbukumbu na nyaraka mbalimbali.

Wahalifu hao  walivunja milango ya ofisi zote, kuvunja vioo vya magari ya kubebea taka aina FAW  SM 8726, na kuiba betri mbili za gari hilo  na gari dogo aina ya Nissan lenye namba SM 2858 mali ya mamlaka hiyo.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani, aliwataja watuhumiwa hao wanaodaiwa kuhusika na uhalifu  na kusababisha hasara ya shilingi  milioni 117, 515,000  kuwa ni Mexon Mbilinyi, Akida Kondo, Chalres Rupia, Athumani Mgala, Stela Garbert, Atiliyo Benard, Nikodemus Exavely, Mashaka Amoni na James Kabuje.

Diwani, alisema kuwa watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kuhusika na uhalibifu wa ofisi ya halmashauri ya mji mdogo wa tunduma ikiwa na kuiba mali yenye thamani zaidi ya milioni 100 na kwamba wote kwa pamoja wamefikishwa mahakamani leo.
Akizungumzia suala la kukamatwa kwa viongozi wa Chama cha walimu pamoja na walimu  alisema watuhumiwa hao wamekamatwa kutokana na tuhuma za kuhamasisha wezao kugoma jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Aliwataja wahusika hao kuwa ni Mwalimu wa Patro Mangula na ni Katibu wa chama cha walimu wilaya ya Kyela ambapo inadaiwa kuwa kiongozi huyo alikuwa akishirikiana na watu wengine kupita mashuleni kuhamasisha walimu waliokuwa wanaendelea na kazi ya kufundisha wajiunge na mgomo.

Wengine ni Mwalimu Emanuel Kyejo wa shule ya msingi Mbebe Wilaya ya Ileje na mjumbe wa chama cha walimu wilaya ya Ileje, Anyakingwe Lwinga na mjumbe wa chama cha walimu ambapo wote kwa pamoja wanatuhumiwa kuhamasisha walimu kugoma.

Aidha, katika uhalifu wa Tunduma, Kamanada Diwani alisema kuwa polisi Mkoani Mbeya kwa kushirikiana na wananchi walifanikiwa kuokoa Mabati 168, Printa moja na mita mbili za maji, Bendera moja ya Taifa na photocopy mashine.

Pia, Kamanda Diwani alitumia nafasi hiyo kutoa ufafanuzi kwa nini askari wake walitumia  Bomu  na risasi katika vurugu hizo ambapo alisema kuwa Bomu hilo lilitumiwa kulitawanyisha kundi kubwa la watu lililokuwa linazidi kuelekea kwenye ofisi za serikali pamoja na Taasisi za kibenki  na kwamba hakuna madhara yaliyojitokeza.

“Baadhi ya watu wamekuwa wakiipotosha jamii kuwa askari walitumia bomu kuwatawanya wanafunzi na ndio sababu za wananchi kuanzisha vurugu jambo hilo si kweli kwani bomu lilitumiwa baada ya kundi la wahuni lililokuwa likivamia ofisi na kuiba mali zilizomo ndani,”alisema.

Alisema,  wakati kundi hilo linafanya vurugu tayari wanafunzi walikuwa wamerejea kwenye makao yao lakini kundi hilo la wahuni ndio lilikuwa likizidi kujikusanya na kuendelea kufanya uhalifu huo huku baadhi wakiwa wanaelekea kwenye eneo la Benki.

“Baada ya walinzi wa Benki kuona kundi hilo linaikaribia benki askari walipiga risasi mbili juu ili kuwatawanya na kwamba zoezi hilo lilisaidia kuwarudisha watu hao waliokuwa na lengo la kufanya uhalifu katika benki hiyo ,”alisema

Aidha,  Diwani aliitaka jamii kuondoa mawazo potofu kwamba huenda vurugu hizo zimechangiwa na baadhi ya wanasiasa jambo ambalo si kweli kwani jeshi la polisi linaamini kuwa kundi hilo la uhalifu halina itikadi yoyote ya siasa.

“Polisi inawashikilia watu hao kwa tuhuma za uhalifu na ninaamini watu hawa ni wahalifu hivyo watafikishwa mahakani kwa makosa ya uhalifu tu na wala hakuna siasa,”alisema

Hata hivyo aliwataka walimu pamoja na viongozi wa chama cha walimu kuacha kuwahamasisha wezao kufanya mgomo kwani wao tayari walitangaza kugoma na wamegoma hivyo kupita mashuleni na kuwakuta wezao wanafundisha na kuwalazimisha kugoma ni uvunjifu wa amani hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa zidi yao.

via Mbeya Yetu

Mtikisiko


Wanafunzi wa shule za Msingi za Temeke wakiingia kwenye ofisi za Manispaa ya Temeke kufuatia mgomo wa walimu ulioanza rasmi jana na kuwasababishia kukosa masomo.Picha na Elizabeth Edward
WALIMU WAGOMA KILA KONA, WANAFUNZI NAO WACHACHAMAA, SERIKALI YAONYA, YATISHIA KUWAFUTIA MISHAHARA
Waandishi Wetu
NCHI imetikiswa. Mgomo wa walimu ulioanza jana katika sehemu mbalimbali nchini, umeathiri kwa kiasi kikubwa sekta ya elimu huku kukiwa na taarifa za matukio yasiyokuwa ya kawaida yaliyoambatana na mgomo huo usio na ukomo.

Katika sehemu mbalimbali nchini, walimu waliripotiwa kugoma kwa kutoingia madarasani na wengine walifika kazini na kusaini vitabu vya mahudhurio kisha kuondoka hali iliyosababisha wanafunzi kurandaranda ovyo katika sehemu za miji iliyo karibu na shule hizo.

Mjini Dodoma ,wabunge jana walimbana Naibu Spika, Job Ndugai wakitaka shughuli za Bunge zisitishwe ili kujadili mgomo wa walimu ambao umeanza rasmi jana nchi nzima, na kuziacha shule nyingi zikiwa na walimu wakuu na wakuu wa shule pekee.

Hata hivyo, Ndugai alisema Bunge lisingeweza kujadili suala hilo kwani tayari Serikali ilikuwa imelifikisha mahakamani baada ya kushindwa kuafikiana na walimu katika ngazi ya usuluhishi.Wakati hayo yakiendelea, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa amesema Serikali itafuta mishahara kwa walimu walioitikia mwito Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wa kushiriki mgomo ambao alisema siyo halali.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Dk Kawambwa pia aliwaonya walimu ambao alisema wamekuwa wakiwabughudhi wenzao ambao waliamua kwenda kazini.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo akiwa Mjini Morogoro aliwaagiza wakuu wa shule za msingi na sekondari mkoani humo kuandaa orodha ya majina ya walimu wasiofika kazini Julai 30 na waifikishe kwa maofisa elimu wa wilaya kabla ya saa 2:00 asubuhi ya Julai 31.

Waandishi wetu katika sehemu mbalimbali nchini pia waliripoti kwamba katika baadhi ya shule, wanafunzi waliruhusiwa kurejea nyumbani mapema kwa maelezo kwamba hakukuwa na masomo.Hali hiyo ilizua kizaazaa kwani katika baadhi ya mikoa wanafunzi walicharuka na kuitisha maandamano hadi katika ofisi za maofisa elimu wa wilaya, wakitaka Serikali iingilie kati mgomo huo ili waendelee kusoma.

Kadhalika, baadhi ya viongozi na watendaji wa Serikali walinukuliwa wakitoa matamko ya kuwasihi au kuwaamuru walimu warejee madarasani, kauli ambazo hata hivyo, hazikubadili uamuzi wa walimu hao.

Wanafunzi waandamana
Maandamano ya wanafunzi yaliripotiwa katika Mji wa Tunduma, Mbeya ambako polisi walitumia mabomu ya machozi kuwadhibiti wanafunzi.

Wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi katika Wilaya ya Mbozi mkoani humo waliandamana wakidai haki ya kufundishwa. Hata hivyo, maandamano hayo yaliingiliwa na vibaka ambao baadaye walivunja ofisi za Halmashauri ya Mji wa Tunduma na kuiba mali kadhaa kisha kuchoma nyaraka zilizokuwemo.
Tukio hilo lilitokea asubuhi wakati wanafunzi wa shule 14 za msingi zilizopo katika halmashauri ya Tunduma walipojikusanya na kufanya maandamano hadi nyumbani kwa diwani na baada ya kumkosa walielekea kituo cha polisi na baadaye ofisi katika hizo.

Katika manispaa ya Temeke, Dar es Salaam zaidi ya wanafunzi 400 wa shule nne za msingi wameandamana hadi katika Ofisi ya Ofisa Elimu wa Manispaa hiyo kupinga mgomo huo.
Wanafunzi wao ambao waliandamana walitoka  katika Shule za Msingi Bwawani, Mbagala Kuu, Mtoni Kijichi na Maendeleo.

Wilayani Tarime, Mara wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi jana waliandamana hadi Ofisi ya Ofisa Elimu wa Wilaya hiyo na zile za CWT, wakidai haki yao za kupata elimu baada ya walimu kugoma kuingia madarasani na kisha kuwataka wanafunzi kurejea nyumbani.

Wanafunzi hao walisikika wakiimba na baadaye kuzungumza mbele ya Ofisa elimu wa Wilaya, Emmanuel Johnson kwamba kitendo cha walimu kugoma kufundisha kinawaathiri wao, hivyo waliitaka Serikali kuwalipa walimu madai yao ili waendelee na kuwafundisha.

“Watoto tunataka haki zetu, Watoto tunataka  kupata elimu,  watoto tunataka kusoma tunaomba walimu walipwe madai yao tuingie madarasani, watoto tusinyimwe haki yetu ya kupata elimu walimu wanapogoma waathirika ni sisi wanafunzi Serikali tatueni mgomo wa walimu,” walisema wanafunzi hao.
Johnson aliwatuliza wanafunzi hao na kuwaahidi kwamba atatatua tatizo hilo, hivyo kuwataka kurejea shuleni leo kuendelea na masomo.

Mkoani Pwani mgomo wa walimu ulisababisha maandamano yaliyowahusisha wanafunzi wa shule za msingi kadhaa katika Wilaya za Kisarawe, Mkuranga, Bagamoyo na Kibaha waliokuwa wakiishinikiza Serikali kusikiliza madai ya walimu ili wao waweze kupata haki yao ya kufundishwa.

CWT wanena
Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Ezekiel Olouch alisema mgomo wa walimu umefanikiwa kwa asilimia 90 nchi nzima na kwamba walimu katika mikoa mbalimbali hawakwenda kazini ikiwa ni hatua ya kushinikiza kupewa haki yao.

“Tunawashukuru walimu kwa kuunga mkono azimio lao ambalo walilipigia kura la kufanyika kwa mgomo na kubaki nyumbani bila ya kwenda kazi hadi pale Serikali itakaposikiliza matatizo yao” alisema Oluoch na kuongeza:

“Mgomo huu ambao umeanza leo (jana) hautahusiana na Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika usiku wa kuamkia Agosti 26, mwaka huu.”
Oluoch alisema kikomo cha mgomo huo ni pale itakapotolewa taarifa na Rais wa CWT, Gratian Mukoba na si mtu mwingine yeyote wala Serikali.

“Walimu wanatakiwa kutambua kuwa mgomo huu utaendelea hadi pale Rais Mukoba atakapowatangazia kinachoendelea hivyo kwa hivi sasa waendelee na mgomo huu,” alisema Oluoch.

Serikali yang’aka
Akizungumzia mgomo huo Dk Kawambwa alisema: “Tutatumia sheria kwa kushikilia malipo ya mishahara kwa walimu wanaogoma na tutatumia pia sheria kuwaadhibu walimu wanaowabughudhi wenzao kwa kuwalazimisha wagome.”

Alisema kwa mujibu wa Sheria ya Kazi ya mwaka 2004 ambayo vyama vya wafanyakazi vinaitumia kufanikisha migomo, Kifungu cha 83(4) kinaeleza kwamba mfanyakazi hatapaswa kulipwa mshahara katika kipindi chote ambacho itatokea amegomea utoaji huduma kwa umma.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, Dk Kawambwa alisema Kuwa Serikali itahakikisha kwamba inawalinda walimu wote ambao hawaungi mkono mgomo huo aliodai ni haramu kwa kuwa suala hilo kwa sasa linashughulikiwa mahakamani.

Katika hatua nyingine, Dk Kawambwa aliwaonya wazazi kuhakikisha kwamba watoto wao hawatumiwi na wagomaji kwa kuhimizwa kufanya maandamano  na vurugu.

DK. ULIMBOKA SI WA LEO WALA KESHO



Dk. Steven Ulimboka.
Na Mwandishi Wetu
Hali ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka, inaendelea vizuri lakini si wa kupona leo wala kesho, imeelezwa na vyanzo vyetu.
Dk.Ulimboka anayetibiwa Afrika Kusini, yupo chini ya uangalizi mkali wa madaktari katika hospitali aliyolazwa na wanafanya kazi kubwa kuhakikisha anapona.
Chanzo chetu kimetoa taarifa kuwa, Dk. Ulimboka anapata matibabu sahihi kwa sababu hospitali aliyolazwa ni ya uhakika.
Awali, kabla ya mazungumzo ya moja kwa moja kwenye simu, ripota wetu alimtumia SMS mtoa habari wetu kumuulizia maendeleo ya daktari huyo naye akajibu: “He’s recovering slowly.” (Anapona taratibu).
Alipomuuliza Watanzania wamtegemee lini daktari huyo kurudi nchini, alijibu: “Itachukua muda kupona. Muhimu kwa sasa ni Watanzania na wote wanaompenda, wamuombee kwa Mungu ili matibabu yaende sawa.”

VIPI USALAMA WAKE?
Chanzo chetu kilibainisha kuwa usalama wa Dk. Ulimboka ni wa uhakika, kwani watu wanaomlinda hospitalini hapo wapo makini.
“Nani asiyejua mazingira ya hatari aliyonayo Steven (Dk. Ulimboka)? Hii inasababisha maisha yake hospitalini yawe chini ya ulinzi mkali.
 
“Kwanza si kila mtu anaruhusiwa kwenda kumuona. Hospitali yenyewe aliyolazwa hatutaki itangazwe. Maisha ya Steven ni siri,” alisema mtoa habari wetu na kutoa siri hii:
“Wiki iliyopita pale hospitali alipolazwa, alitokea mtu fulani hivi Mwafrika. Muonekano wake ukawafanya watu wahisi ni Mtanzania. Watu wanaohusika na usalama wa Steven walikuwa makini sana.
 
“Kilichosababisha yule mtu aonekane ni Mtanzania ni fulana aliyovaa, kifuani ina ramani ya Tanzania. Watu wanaomlinda Steven wakaogopa sana, wakamfuatilia hatua kwa hatua bila mwenyewe kujua. Bahati nzuri naye alikuwa amekwenda kwa shughuli zake na akaondoka salama.
“Kwa kifupi, hali ilivyo pale hospitali ni kwamba ulinzi ni mkali, tena afadhali mtu awe wa taifa lingine, Watanzania ndiyo wanaogopwa zaidi, kwani huwezi kujua nani mzuri wa Steven na adui yake ni yupi.”

TATIZO LILIPOANZIA
Dk. Ulimboka, akiwa kwenye harakati za kuendeleza mgomo wa madaktari ili kuishiniza serikali iridhie madai yao, alitekwa kisha akavunjwa mbavu, miguu yote, kung’olewa meno yote ya mbele na kuumizwa vibaya katika sehemu mbalimbali za mwili.
Tukio hilo, linadaiwa kufanywa na watu wasiojulikana ambapo kabla ya kufanyiwa unyama huo walidaiwa kumteka na kumpiga kisha kumtelekeza katika eneo la Msitu wa Mabwepande, nje ya Jiji la Dar es Salaam.

ALIYETAKA KUMUUA MANDELA JELA MAISHA



Mike du Toit.

Elvan Stambuli na Mitandao
MHUSIKA mkuu wa mpango wa kumuua Nelson Mandela, wiki iliyopita katika Mahakama Kuu ya nchi hiyo alipatikana na hatia ya uhaini kwenye kesi moja iliyodumu kwa takriban miaka 10 na atahukumiwa jela maisha.
Mike du Toit alikuwa mhadhiri wa chuo kikuu na kiongozi wa kundi la kibaguzi la Jeshi la Kaburu la Chama cha Boeremeg, baada ya kupatikana na hatia na mahakama kusema atahukumiwa siku zijazo kuhusiana na jaribio lililoshindwa la kumpindua Mandela mwaka 2002 nchini Afrika Kusini, wanasheria akiwemo Steve Mhokholo, wamefunguka na kusema hukumu yake itakuwa kifungo cha maisha jela.
Mashahidi waliieleza mahakama kuwa du Toit na wenzake walipanga kumuua Mandela ambaye mwaka 1994 alikuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini pia walikusudia kuwapiga risasi weupe wenzao ambao wangepinga mtazamo wao wa kuwa taifa kamili la kibaguzi la Makaburu.
Du Toit alitaka kukiondoa madarakani kwa nia ya mapinduzi chama tawala cha African National Congress (ANC) na mahakama kuu nchini humo imesema atahukumiwa katika tarehe itakayotangazwa baadaye.
Ilidaiwa kuwa du Toit angefanikiwa kumpindua Mandela angewafukuza Waafrika wapatao milioni 40 kwa kuwalazimisha kwenda kuishi Zimbabwe tena basi wakiwa na vifurushi tu vya chakula na Wahindi wangepakiwa katika boti na kupelekwa kwao India.

Manispaa ya Kinondoni itaanzisha wodi za matibabu ya kulipia

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, imejipanga kuazisha wodi za kisasa za kulipia 'Fast track', katika Hospitali ya Mwananyamala ambazo zitatoa huduma bora kwa wananchi.

Naibu Meya wa Manispaa hiyo, Bw. Songoro Mnyonge, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akitoa ufafanuzi juu ya hatua walizo zichukuwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za matibabu katika hospitali hiyo, “Tunaamini mwaka huu wa fedha, tutaanzisha huduma hii katika Hospitali ya Mwananyamala, ingawa watalipia lakini mgonjwa atajisikia faraja zaidi kupata huduma bora kwa gharama ndogo, hadi sasa tuna wataalamu wa kutosha,” alisema.

Alisema kwa kuanzia, watakuwa na wodi ya wanawake, wanaume na wataanza kuchukua wagonjwa ambao ni wanachama wa Bima za Afya na baadae wanatarajia kuwa na wodi ya watoto, “Tumeamua kuanzisha huduma ya matibabu ya kulipia kwa sababu baadhi ya Watanzania hawana utamaduni wa kwenda kutibiwa katika hospitali za umma,” alisema.

Alitoa wito kwa wananchi kuwa na tabia ya kwenda kuhudumiwa katika hospitali za umma ambazo zina usalama mkubwa kwa afya zao na wataalamu wazuri.

Darlin Said
MAJIRA

Mchango wa John Mnyika (Mb) kwenye hotuba ya bajeti ya Wizara ya Afya

Jana tarehe 30 Julai 2012 baada ya Hotuba ya Waziri wa Afya ya Ustawi wa Jamii kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2011/2012 na makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2012/2013; Taarifa ya Kamati ya Huduma za Jamii kuhusu Wizara husika na Maoni ya Kambi ya Upinzani nilitaka mjadala usiendelee mpaka kwanza wabunge tupewe nakala ya ripoti ya Kamati ya Huduma za Jamii iliyoshughulikia mgogoro kati ya Serikali na madaktari na kuandaa mapendekezo ya kuboresha Sekta ya Afya nchini.

Nilifanya hivyo kwa kunukuu Taarifa ya Kamati ya Huduma za Jamii ambayo pamoja na kuwa mwezi Februari 2012 bunge lilikataliwa kujadili masuala husika mpaka kwanza kamati hiyo ikapate ukweli wa pande zote mbili na kuwasilisha mapendekezo kwa bunge, taarifa ya Kamati hiyo kuhusu bajeti iliyowasilishwa jana haikueleza chochote nini kamati ilibaini baada ya kukutana na wadau mbalimbali wa sekta ya afya wala haikueleza ni ushauri gani iliutoa kwa serikali kuupatia ufumbuzi mgogoro uliokuwepo wala haikuwasilisha bungeni mapendekezo yoyote yaliyotokana na kazi waliyopewa na bunge. Aidha, Nilinukuu pia maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani ambayo yalieleza bayana kuwa mwezi Juni yalitolewa majibu yasiyokuwa ya kweli bungeni kuwa Taarifa ya Kamati hiyo iliwasilishwa bungeni.

MAGAZETI YA LEO JULY 31 2012, UDAKU, MICHEZO


Walimu waliogoma kutolipwa mishahara

Mgomo waanza, watikisa kila kona ya nchi
WAKATI walimu wakianza mgomo wa kutoingia madarasani jana, serikali imesema kuwa walimu watakaobainika kujihusisha na mgomo huo hawatalipwa mishahara.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, alisema hayo jana wakati akitoa tamko la serikali kuhusu mgomo huo kwa waandishi wa habari.

Kwa mujibu wa Dk. Kawambwa, licha ya mwajiri kutowalipa mshahara walimu wote waliogoma watachukuliwa hatua kali huku wale wanaowatisha wenzao na kuwashirikisha wanafunzi kwenye mgomo, watawajibishwa.

Serikali pia imevitaka vyombo vya habari kuacha kuchochea mgomo huo kwa aina ya habari inazopeleka kwa umma, huku akisema kwamba si kazi ya vyombo hivyo kulibomoa taifa.
“Kwa mujibu wa sheria namba sita ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004 ambayo mchakato wake ni mfupi, kifungu cha 83(4)g cha sheria hiyo, mwajiri hatalazimika kulipa mshahara kwa mtumishi aliyeshiriki katika mgomo kwa kipindi chote cha mgomo huo.

“Sheria ipo wazi, tutafanya hivyo kwa kipindi chote watakachokuwa kwenye mgomo… lakini pia kesi ipo mahakamani tayari na kesho mchana itatolewa hukumu,” alisema Dk. Kawambwa na kuongeza kwamba Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kimefuata taratibu zote za mgomo huo.
Awali waziri huyo alisema serikali inaithamini elimu na walimu pia, haina sababu ya kushindwa kutatua kero zao ikiwemo ya kuwaongezea mishahara kwa asilimia 100; posho ya kufundishia kwa asilimia 55 ya mshahara walimu wa sayansi na asilimua 50 walimu wa sanaa.

“Walimu wanadai pia posho ya mazingira magumu ya kazi kwa asilimia 30 ya mshahara wao,” tunayo nia ya kufanya hayo lakini uwezo wa serikali ni mdogo ndiyo maana Juni 30 mwaka huu tuliweza kulipa sh bilioni 56 madai yao kwenye malimbikizo ya likizo na madai mengine ya walimu.
Dk. Kawambwa aliyepata kuwa waziri kwenye wizara nne tofauti katika utawala wa Awamu ya Nne, alisema juhudi za usuluhishi wa mgogoro huo zimekwama baada ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) kushindwa kufanya hivyo, hali iliyoilazimu serikali kukimbilia Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi.

“Baada ya CMA kushindwa pale walimu walipokataa nyongeza ya asilimia 14 ya mishahara yao tofauti na watumishi wengine wa serikali, ikasema itatoa cheti cha kushindwa kuleta suluhu kwenye mgogoro ule (Certificate of Deadlock).

“Julai 26 serikali iliwasilisha ombi la kuzuia mgomo uliotangazwa na CWT nchi nzima, Julai 27 serikali na CWT tulitakiwa kupeleka maelezo yetu kwa maandishi ambapo serikali iliamriwa kupeleka maelezo yake leo (Julai 30) na wenzetu wapeleke maelezo yao kesho (Julai 31) kabla ya kuanza kwa mgomo huo,” alisema Dk. Kawambwa ambaye ni Mbunge wa Bagamoyo.
Bila kueleza iwapo mahakama hiyo ilitoa amri ya kuzuia mgomo ama la, waziri huyo aliwataka waandishi wa habari kusubiri uamuzi wa mahakama utakaotolewa leo mchana.

Hali ya mgomo nchini
Licha ya serikali kutangaza kuwa mgomo wa walimu ni batili, walimu wa mikoa mbalimbali nchini wameanza rasmi mgomo huo.
Jijini Dar es Salaam, mwitiko wa mgomo huo ulikuwa mkubwa wakati katika mikoa ya Mbeya na Arusha Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) walilazimika kupiga mabomu ya machozi kuwatawanya wanafunzi waliokuwa wakiandamana kupinga mgomo wa walimu wao.
Jijini Dar es Salaam, wanafunzi wa shule mbalimbali walikuwa nje wakicheza wakati walimu wao walijikusanya kwenye vikundi kujadili mgomo huo bila kuingia madarasani.

Miongoni mwa shule hizo ni Shule ya Msingi Nzasa na Charambe wilayani Temeke, ambapo katika Shule ya Nzasa walifika walimu wawili licha ya shule hiyo kuwa na walimu 63 na katika Shule ya Msingi Charambe mwalimu aliyefika ni mmoja kati ya walimu 48.
Shule nyingine ambazo walimu wake waliingia kwenye mgomo kuanzia jana ni Shule ya Msingi na Sekondari ya Makumbusho Wilaya ya Kinondoni, ambapo mkuu wa Shule ya Sekondari Makumbusho alikataa kuzungumzia hali hiyo na kutaka atafutwe ofisa elimu ili atolee maelezo mgomo huo.

Wakizungumza na gazeti hili jana, baadhi ya wanafunzi katika shule hizo walisema mgomo huo una waathiri kwani baadhi yao wapo katika maandalizi ya mitihani ya taifa.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili, umebaini kuwa baadhi ya shule kulikuwa na walimu wachache.
Hali ilikuwa tofauti kwenye shule za Msingi Mnazi Mmoja, Buruguni, Bunge na nyingine zilizopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam, ambapo walimu walikuwa wakiendelea kufundisha.

“Hatuoni sababu ya sisi kugoma ikizingatiwa kuwa madai ya mgomo huu hatuyajui, pia hatujashirikishwa,” walisema baadhi ya walimu hao walipozungumza na gazeti hili.
Shule nyingine zilizoguswa na mgomo huo ni Shule ya Msingi Malamba Mawili Mbezi, ambapo mwalimu mkuu wa shule hiyo, Leah Sanga, alieleza kushangazwa na baadhi ya walimu wake kutofika kabisa eneo lao la kazi.

“Shule ina wanafunzi zaidi ya 3,000 lakini nimefika peke yangu, kutokana na hali hiyo imenilazimu nikae nao kwa maelewano hadi saa 5 asubuhi ndipo nilipowaruhusu kurudi nyumbani,” alisema Mwalimu Sanga.
Shule za msingi Mbagala Kuu, Bwawani na Kijichi walimu wake pia hawakuingia madarasani.
Kutoka Mbeya, Mwandishi Gordon Kalulunga, anaripoti kuwa mgomo wa walimu jana ulitikisa baadhi ya shule za mjini humo.
Kwa mujibu wa habari hizo, wanafunzi wa shule nyingi mjini hapa walionekana wakicheza muda wote wa masomo, huku walimu wao wakiwa nje wakibadilishana mawazo.

Katika baadhi ya mitaa ya katikati ya Jiji la Mbeya, FFU walilazimika kutumia nguvu kuwatawanya wanafunzi waliokuwa wakiandamana kupinga mgomo huo.
Kutoka mjini Arusha, inaripotiwa kuwa baadhi ya shule zimeingia katika mgomo huo kwa walimu wao kugoma kuingia darasani.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili katika mikoa ya Iringa, Mwanza, Shinyanga na mikoa mingine, walimu wengi walifika mashuleni na kusaini kitabu cha mahudhurio, lakini hakuna aliyeingia darasani kufundisha. 

Wafanyakazi watangaza maandamano yatakayofanyika Dar es Salaam

Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), limetangaza maandamano ya amani yatakayofanyika Dar es Salaam wiki hii ili kupeleka malalamiko yake kwa Serikali ya kutokubaliana na sheria mpya ya mafao ya Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi za Jamii (SSRA).

Sheria inayolalamikiwa na wafanyakazi inazuia wanachama wa mifuko hiyo kujitoa uanachama na kuchukua mafao yao mpaka wafikishe umri wa kustaafu kwa hiari wa kati ya miaka 55 na 59 na kwa lazima miaka 60 au wanapopata ulemavu wa kudumu.

Mratibu wa Kamati ya TUCTA ya Mkoa wa Dar es Salaam, Musa Mwakalinga jana alisema maandamano hayo yatafanyika Agosti 4 na yataanza saa 1.30 asubuhi katika ofisi za TUCTA makao makuu Mnazi Mmoja hadi ofisi za SSRA eneo la Makochi, Kinondoni barabara ya Ali Hassan Mwinyi.

Mwakalinga alisema maandamano hayo yatashirikisha wafanyakazi, wafanyabiashara na wakulima na kueleza kuwa wameshatoa taarifa Polisi kupata ulinzi ili kufikisha kilio chao, kwa kuwa mabadiliko hayo yataongeza umasikini kwa wafanyakazi pindi watakapoachishwa au kuacha kazi, “Sisi tunachofanya ni maandamano ya amani, hivyo hatuna haja ya kuomba kibali, ila tulichofanya ni kuwapa taarifa tu ili watupe ulinzi,” alisema Mwakalinga.

Katibu Mkuu wa TUCTA, Nicholaus Mgaya alisema wanabariki maandamano hayo na wanataka mabadiliko ya haraka yafanyike kwenye sheria hiyo ya hifadhi ya jamii, ili fao la kujitoa lirejeshwe.

Alisema wadau na TUCTA hawakuona kifungu hicho cha sheria kwa kuwa hakikujitokeza kwa uwazi kwenye muswada au kama ilivyoelezwa na SSRA, baada ya sheria kupita na kifungu pekee cha muswada kilichotaja suala la mafao ya kujitoa ni cha 107 kilichotoa mapendekezo ya kufuta fao la kujitoa kwa mfuko wa PPF.

Hivyo alisema wadau na vyama vya wafanyakazi walielewa kuwa kifungu hicho kinalenga kufuta fao la kujitoa kwa mfuko wa PPF tu, ambao ndio pekee uliokuwa na fao hilo na kwamba malipo ya kujitoa yangeendelea kutolewa kama ilivyokuwa ikifanyika kwa mifuko mingine.

Kutokana na hilo, alisema TUCTA inataka uandaliwe utaratibu mwafaka utakaohakikisha mwanachama anayeshindwa kuendelea na uanachama wa Mfuko anarejeshewa michango yake na ya mwajiri pamoja na riba mara tu anapokoma uanachama wa mifuko hiyo.

lisema TUCTA haitasita kuchukua hatua za kisheria, endapo mamlaka itaendelea kushikilia msimamo wake wa kubakiza kifungu hicho kinachomtaka mwanachama wa mfuko afikishe miaka 55 ndipo alipwe mafao.

Aidha, alisikitishwa na kushangazwa kuwahishwa kutangazwa kwa mabadiliko ya sheria ya hifadhi ya jamii, huku mchakato wake ukiwa haujakamilika baada ya kuridhiwa na Rais, kama vile kupita kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali, akisema huo ni ukiukwaji mkubwa wa taratibu, “Hali hii inatupa shaka kuwa huenda sheria hiyo ikawa na mabadiliko ambayo wadau hatukuyaridhia, jambo ambalo TUCTA kamwe hatutalikubali,” alisema.

Alisema TUCTA inataka SSRA kuchukua jukumu la kutoa elimu kwa wanachama kuhusu sheria hiyo mpya ili kupunguza malalamiko yasiyo ya lazima.

via HabariLeo

HAWA NDIO MAPACHA WALIOTENGANISHWA.


       Waziri wa Afya wa Malaysia Liow Tiong Lai akiwa hospitalini kuwaona watoto hao baada ya kufanikiwa kutenganishwa.                            
Mara kadhaa watoto mapacha wanapozaliwa wakiwa wameungana huwa inakua kazi nzito kuwatenganisha na wakati mwingine huwa wanafariki wakiwa kwenye zoezi la kutenganishwa na wengine wanapoteza maisha kutokana na pesa ya hayo matibabu ya gharama kukosekana lakini kwa Malaysia wamepata bahati wakati huu.

Kuna watoto walizaliwa April 2011 wakiwa mapacha walioungana mguuni ambapo baada ya juhudi za Madaktari mabingwa kufanya upasuaji, wamefanikiwa kuwatenganisha hawa malaika Muaiman na Muaimin na wakabaki kuwa hai.
Idadi kubwa ya wananchi wakiwemo wazazi waliokua wanaifatilia habari ya watoto hawa wamejawa na furaha baada ya kusikia hilo zoezi limefanikiwa.

Pamoja na kwamba upasuaji umefanikiwa, ugumu ulikuwepo kwenye sehemu ya kuhifadhia mkojo mwilini ambayo pia ilikua imeungana toka wamezaliwa, sasa hivi wapo chini ya uangalizi wa kitaalam mpaka hali yao itakapo ruhusu kuruhusiwa kwenda nyumbani kwa mujibu wa Star news paper.

Bahanunzi: Namsubiri Poulsena aniite Stars

MFUNGAJI bora wa michuano ya Kombe la Kagame, Said Bahanunzi wa Yanga amesema kwa sasa anafikiri ni wakati wake kuitwa kikosi cha timu ya Taifa Stars.Mshambuliaji huyo aliyejiunga na Yanga akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro, aliliambia Mwananchi jana jijini Dar es Salaam:
 
                                                       Said Bahanunzi wa Yanga
"Nafikiri kwa sasa tuna tatizo la ufungaji timu ya taifa, naamini nitakapopewa nafasi nitaendeleza haya niliyofanya Kagame na timu kupata ushindi."Aliongeza: "Siri yangu kubwa kuibuka mfungaji bora ni kwa sababu nilimtanguliza Mungu mbele kwa kila jambo na kujituma."
"Nimezaliwa na kulelewa katika mazingira ya dini, ninamwamini zaidi mwenyezi Mungu kuliko chochote."
"Sidhani kama kweli kuna uchawi kwenye soka, ni imani potofu za watu wachache, nimejipanga kufanya vizuri zaidi na siyo kuishia hapa."

"Kila jambo nalofanya namtangulia Mungu, nafikiri ndiyo siri kubwa yangu kufanya vizuri kwenye mashindano ya Kagame.
Aliongeza kusema ushirikiano kati yake na wachezaji ulimsaidia kujiona yuko nyumbani na kujituma zaidi.
Bahanunzi alishawahi kuichezea Ocean View ya Zanzibar na Mtibwa Sugar ya Morogoro kabla ya kutua Yanga msimu huu.

Lissu ayataja majina ya Wabunge watuhumiwa wa hongo; Baadhi yao wazungumza

Mnadhimu Mkuu wa kambi hiyo, Tundu Lissu amewataja wabunge wa CCM ambao wanatuhumiwa kujihusisha na hongo kuwa ni Nasir Abdallah (Korogwe Mjini), Mariam Kisangi (Viti Maalumu), Vicky Kamata (Viti Maalumu) na Charles Mwijage (Muleba Kaskazini) ambao hata hivyo, wote wamekanusha madai hayo.

Wabunge wengine watatu gazeti la MWANANCHI limeshindwa kuwataja kwa kuwa hawakupatikana kuzungumzia tuhuma dhidi yao.

Katika orodha hiyo wamo wawili wa Viti Maalumu na mmoja wa jimbo na Lissu alidai kwamba wamekuwa wakishiriki vikao vya Kamati ya Nishati na Madini huku wakijua kuwa wana maslahi binafsi na wengine kutumia fursa hiyo kujinufaisha, “Kwa takriban juma moja sasa kumekuwa na mjadala mzito wa ufisadi hapa bungeni, sasa Kambi Rasmi ya Upinzani imejitathmini na kuona kwamba wabunge wake hasa walioko kwenye Kamati ya Nishati na Madini iliyovunjwa, John Mnyika, David Silinde na Mwanamrisho Abama hawahusiki,” alisema Lissu na kuendelea: “Ila uchunguzi wetu umefanikiwa kupata majina ya wabunge wanaohusika moja kwa moja na mgongano wa kimaslahi ambao tunaona tuwataje kwa maslahi ya umma.”

Lissu alikwenda mbali zaidi na kutaja tuhuma zinazowahusu wabunge hao akisema wawili ambao gazeti hili halikuwaja, wamejihusisha kufanya biashara na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) hivyo wana mgongano wa kimaslahi.

Alisema Mwijage ana mgongano wa kimaslahi katika mchakato mzima wa kuipa zabuni ya kusambaza mafuta kampuni ya Puma Energy kwa kuwa yeye ni mtalaamu mwelekezi wa kampuni hiyo inayomilikiwa na Serikali kwa asilimia 50, “Nasir Abdalah na Mariam Kisangi; Hawa wanamiliki vituo vya mafuta. Sasa kwa namna yeyote ile kuwa wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini hawawezi kutenda haki katika mchakato wowote unaohusu suala la mafuta,” alisema na kuendelea; "....(jina limehifadhiwa) hana mgongano wa moja kwa moja wa maslahi, lakini kwa kadri tunavyofahamu, yeye ndiye aliyekuwa akiyafanyia kampeni ya kupata zabuni makampuni ya mafuta ya Oryx na Camel na ....(jina limehifadhiwa), suala lake ni complicated kidogo. Maslahi aliyonayo katika suala hilo ni kuwa ana uhusiano wa Kimapenzi na kigogo mmoja katika Wizara ya Nishati na Madini.”

“Hawa ndiyo wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini ambao sisi Kambi ya Upinzani tunawafahamu kuwa ndiyo waliojihusisha na mgongano wa kimaslahi. Tumewaangalia wabunge wetu wote watatu hawamo ila kama kuna mtu ana taarifa zinazowahusu, aseme na tutazifanyia kazi.”

Lissu alisema kitendo cha wabunge kujihusisha na mgongano wa kimaslahi na taasisi za umma ni kinyume na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995 na ni kinyume na maadili ya kibunge.

Katika hatua nyingine Lissu amemshauri Spika wa Bunge Anne Makinda kuzivunja pia kamati za Bunge za Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Mashirika ya Umma (POAC) akisema nazo zina madudu mengi, “Hili lisiishie tu kwa kuvunja Kamati ya Nishati na Madini, tunataka pia kamati za POAC na LAAC zivunjwe, uchunguzi ufanyike na wahusika waitwe kujitetea na hatimaye wenye hatia watajwe hadharani bungeni na majina yao yachapishwe kwenye magazeti ili haki itendeke,” alisema.

Alipoulizwa CHADEMA imefanya nini dhidi ya Mbunge wake, Zitto Kabwe kutajwa katika orodha hiyo, alijibu: “Nikiri kwamba sisi taarifa tunazo ila hatujamwita kumwuliza. Naomba ieleweke kwamba kama chama au Kambi Rasmi ya Upinzani hatuna maslahi na mbunge yeyote anayeonekana kujihusisha na masuala hayo.”
“Katika hili tunaomba uchunguzi ufanyike na matokeo yake yatangazwe ili tupate msingi wa tuhuma hizo na ninaahidi kwamba tutazifanyia kazi ipasavyo.”

MAJIBU YA WATUHUMIWA

Alipotakiwa kuzungumzia tuhuma hizo, Kisangi alikiri kumiliki kituo cha mafuta lakini akasema sheria haimzuii mtu kama mambo yake anayafanya kwa uwazi, “Nimekuja bungeni nikitokea kwenye ualimu, nilikuwa nafundisha Shule ya Msingi ya Mianzini na biashara hii ni ya familia. Inaendeshwa kwa uwazi na mwanangu wa kwanza ndiye anayeisimamia. Kutokana na uwazi katika shughuli zangu, mwaka jana Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma ilinipongeza. Mimi ni msafi na siko huko wanakofikiri wao (CHADEMA).”

Kwa upande wake, Mwijage alikanusha kuwa mtaalamu mwelekezi wa Kampuni ya Puma, badala yake akasema ni mtaalamu wa petroli anayefanya kazi ya kuishauri Serikali kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu nishati hiyo, "Siyo kweli, hawa wanadandia hoja. Mimi ni mtaalamu wa petroli ambaye mchango wangu kimsingi una faida kubwa bungeni na hata kwa jamii kwa ujumla. Sijafanya maamuzi yeyote ya kulihujumu taifa hili na hata kwenye Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini pekee, nilitoa mchango wa kurasa 10 kuhusu masuala hayo ya petroli,” alisema

Aliishauri kambi hiyo ya upinzani kuvuta subira, akieleza kuwa jambo lililoko bungeni linahusu ufisadi na uhujumu uchumi hivyo kauli zinazotolewa bila utafiti zinaweza kuvuruga mchakato mzima uliokwishaanzwa na Kamati ya Maadili ya Bunge.

Awali, Abdallah alipoulizwa kuhusu tuhuma za kumiliki vituo vya mafuta hivyo kuwa na maslahi binafsi, alicheka na kuahidi kwamba angepiga simu baadaye, lakini hakufanya hivyo na alipopigiwa baadaye alikata simu. Hata hivyo, alizungumza na waandishi wa habari na kukanusha kumiliki vituo vya mafuta.

Kamata kwa upande wake alisema: “Kuna kamati maalumu imepewa kazi ya kuchunguza mambo hayo, hivyo yote yanayoulizwa yatakuwa wazi na ukweli utajulikana tu. Nina maslahi au sina ukweli mtaujua, haraka ya nini?.

via gazeti la MWANANCHI

ZITTO; NIMEJIELEZA KWA MASAA MATATU MBELE YA SEKRETARIETI YA CHAMA

Kwa masaa 3 nimejieleza mbele ya sekretariat ya chama kuhusu tuhuma za rushwa dhidi yangu. Niliomba kutaka kutoa maelezo kwa katibu Mkuu
Nimetaka chama changu kufanya uchunguzi dhidi ya tuhuma hizi.
Kesho Nitazungumza na waandishi wa Habari ofisi za Bunge Dar Es Salaam kuanzia saa tano asubuhi. Kuendelea kukaa kimya ni silaha kwa adui.

Mshindi wa TUSKER PROJECT FAME 2012 ni RUTH kutoka NAIROBI-KENYA


Pichani: Ruth mshindi wa kwanza
Age: 26 Years Old
Country: Kenya
I am a 26 year old lady born in the Western part of Kenya.
I love music and I believe that I will die doing music because that is my passion. Aside from being a passion, I know it is a gift I got from God. It keeps me going through life’s issues.
Through music, I get to express myself easier and better. However, I want to use my music as a tool to speak to the voiceless out there. People who cannot speak for themselves yet they have a lot that they would want to share with the rest of the world.
I am currently participating in the Tusker Project fame music competition and I am enjoying every bit of it despite the few surprises that come with it. I love God and I thank Him for the gift.
 Pichani: Doreen mshindi wa pili
Age: 21 Years Old
Country: Kenya
Purple Diva is what they call me. Doreen Naira is the name my parents gave me… I am a lover of art, a student of nature, a poet and a girl that is crazy about the color purple…but above all these, I am a music fanatic. I come from Kenya, the closest place I know to the mythical land of milk and honey. I am no scientist; in fact, I believe music makes the earth go round. I am a spirited singer (music is bigger than me, than you and its greater than us all) music is not what I do it is who I am, it is through music, I believe, that I can tap into my reservoir, and give to human kind the best of me.
It’s a unifying factor that makes us come together and bring out the best in us… Try as we may, we cannot live without music (at least I can’t)
I want them to remember me, and when I am gone… I don’t want them to say much… Just that I was here,” and boy, did she sing her heart out!” I will feel that I lived my life, and lived it well.
Much love
Doreen xoxox
Pichani: Jackson mshindi wa tatu
Age: 25 Years Old
Country: Rwanda
Hi I am Jackson, I am a performing artist from a beautiful country; they call it the land of a thousand hills. I am the fourth of six children and I love my mother. She always told me that if I loved something, I should do it wholeheartedly. Since my childhood ,I have loved music….it is my greatest passion. I believe that music has power, it inspires me. To all my fans, my music is like the spirit…it unites the body to the soul. It is good for us to know our fellow men while on earth, since the heart has a lot of secrets it hides….God gave man the ability to compose and perform music…so that we can share what is in our hearts.
Jackson
Pichani: Joe mshindi wa nne
Age: 24 Years Old
Country: Burundi
hellowz
Its Joe Irankunda aka Kiki in the Tusker Project Fame Academy…..
I am from Burundi with the current help of the best East African faculty of Tusker Project Fame I’m on my way too being a singer by career! I have been singing since I was 5 years old and i would like to thank God for giving me this amazing talent that I’m learning to use skillfully every day. I’m enjoying my time here and loving it. I’m a caring gentleman with a natural trait of a considerate person, I care about people and I’m always compelled to make you feel better by singing to you.
To my homies, my mom, and my beloved brother thank you for believing me. I want to be with you all, but until then, I enjoy singing for you!
Yours always Joe.

Monday, July 30, 2012

Wanafunzi wamlabua Mwalimu ambaye hakushiriki mgomo

Na Gideon  Mwakanosya, Songea.
MWALIMU  mmoja  wa jinsia ya kike aliyefahamika kwa jina moja  la Kahimba  wa shule ya msingi  ya Kambarage  iliyopo    Kata ya Msamala katika Halmashauri ya  Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma  amajeruhiwa vibaya  kwa kupigwa  sehemu mbalimbali za mwili  na kundi  linalodaijwa kuwa ni la wanafunzi wa shule hiyo ambao  wanadaiwa kuwa na hasira  baada  ya walimu wengi wa shule hiyo kutoonekana  eneo la shule kufuatia mgomo wa chama cha Walimu  (CWT).

Akizungumuza na waandishi wa habari hizi Mjini Songea  mwalimu mkuu wa shule ya msingi  Kambarage  Adolfina Ndunguru alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo alidai kuwa  ni udhalilishaji  mkubwa kwa mwalimu kupigwa na wanafunzi.

Ndunguru alisema kuwa  yeye pamoja na walimu wenzake hawakuweza kufika  kwenye eneo la shule kwa kuwa wao ni walimu ambao wamekubaliana kugoma  kutokana na Serikali  kushindwa kutimiza  ahadi yao wanayodai.

Alifafanunua kuwa  inadaiwa kundi la wanafunzi lilipomuona mwalimu Kahimba kwenye  eneo la shule hiyo lilimvamia na kuanza kumpiga mawe sehemu  mbalimbali za mwili na baadaye  alifanikiwa kukimbia.

Kwa upande wa baadhi ya walimu  wa shule za msingi, Sekondari na Chuo cha Ualimu cha Songea kilichopo Manispaa ya Songea ambao wameomba majina yao yahifadhiwe walisema kuwa  mgomo utaendelea mpaka Serikali itakapo ridhia kuwalipa madai yao hasa ikizingatiwa kuwa  wao wanafanyakazi katika mazingira magumu.

Waandishi wa habari walifanikiwa kutembelea baadhi ya shule  za Msingi na sekondari ambazo zilikuwa hazina walimu kabisa na kwamba wanafunzi wa shule hizo  wakiwa wamezagaa mitaani huku wakiinung`unikia Serikali kwa kuto watendea haki walimu wao ambao alikuwa wakiwaandaa wanafunzi katika Mitihani  ya kumaliza Elimu ya Msingi na sekondari.

Shule zilizotembelewa na waandishi wa habari ambazo hazikuwa na walimu kabisa  ni Shule  za Msingi za Matarawe, Mwembechai, Sabasaba, Mkombozi, Kawawa, Mfaranyaki, Majengo, Songea, Kambarage, Msamala na Majimaji na shule za sekondari za matarawe, Mfaranyaki, Shule ya wavulana Songea na Shule ya wasichana  songea.

Kwa upande wake mmoja  wa wanafunzi  wa shule ya msingi Majimaji Tamimu Ajali anayesoma darasa la tano ameiomba Serikali kuharakisha kutekeleza madai ya walimu  wanayodai kwani bila kufanya hivyo kunauwezekano mkubwa  wa kushuka kwa kiwango cha Elimu hasa  ikizingatiwa kuwa  wanafunzi wapo kwenye maandalizi ya kufanya mitihani.

Tamimu alisema kuwa  ni vyema serikali ikatambua umuhimu  wa mwalimu kwa kumuuongezea mshahara  sawa na taaluma  zingine muhimu kwa mfano. Wanajeshi, Madaktari,Wauguzi na wahudumu wa afya.

Afisa Elimu wa halmashauri ya Manispaa ya Songea  Fulgensi Mponji amethibitisha kuwepo kwa mgomo huo wa walimu  amabapo alisema Manispaa hiyo ina shule  72, Sekondari za Serikari 23, Shule za seskondari za binafsi 13 ambazo  idadi kubwa ya walimu hawakuwepo kwenye maeneo yao ya kazi.

Alisema kuwa tayari ameshawaagiza walimu wakuu  wa shule za msingi na waratibu Elimu  kata wote kukutananao katika shule ya msingi Mfaranyaki  kwa lengo kuwakutanisha walimu ili kuzungumzia namna ya kutatua tatizo hilo.

Naye  Katibu wa chama cha walimu mkoa wa Ruvuma  Luya Ng`onyani alisema kuwa mgomo  huo ni halali na umezingatia sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 kifungu cha  80 (1) ambapo hatua ya kwanza CWT kwa niaba  ya wanachama tayari imetekeleza  kutangaza mgogoro wa siku 30 kwa kujaza fomu  CMA No: 1.
habari via dj-sek.blogspot.com
Wanafunzi wa shule za msingi Bwawani na Kijichi Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, wakiandamana jana Jumatatu Julai 30, 2012, kupinga haki yao ya msingi ya kupata elimu kuvurugwa kufuatia mgomo wa walimu ulioanza rasmi jana. Wanafunzi hao waliandamana umbali wa kilomite 10 hadi ofisi za Afisa elimu wa manispaa hiyo na kueleza "kesi" yao ambapo wameitaka serikali kumalizana na walimu ili wao wasome.
Wanafunzi wa shule za Makuburi na Mabibo, wakiwa chini ya mwembe, jana asubuhi Jumatatu Julai 30. Walimu wengi hawakuingia madarasani kufundisha jana wakiitikia mwitoi kutoka chama cha walkimu nchini kilichowataka kutofanya kazi leo Jumatatu na kuendelea hadi madai yao kuhusu maslahi yatakaposhughulikiwa na serikali.
Baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Makuburi, wakijisomea baada ya walimu shuleni hapo kugoma kufundisha jana Julai 30, 2012. Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, ambaye hata hivyo alikataa kutaja jina lake, alisema walimu walifika lakini hawakufanya kazi wakiunga mkono agizo la rais wa chama cha walimu Gratian Mukoba, aliyewataka walimu wote kushiriki mgomo usio na kikomo kuanzai leo Jumatatu.
Afisa Elimu Taaluma wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, Juliana Mlay (Kushoto) akitafakari nini cha kuwaambia "Wageni" wake, wanafunzi wa shule za msingi Kijichi na Bwawani za jijini walioandamana umbali wa kilomita 10 hadi ofisini hapo wakilaani kutosoma jana, kufuatia mgomo wa walimu ulioanza nchi nzima jana Julai 30, 2012.
Kiongozi wa wanafunzi walioandamana jana jijini Dar es Salaam, Christofa Msifuni Msuya wa darasa la saba, shule ya msingi Bwawani, akizungumza kwa niaba ya wenzake kwenye ofisi za Afisa Elimu wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam Jumatatu Julai 30, 2012.
Wanafunzi wa shule za msingi Bwawani na Kijichi, zajijini Dar es Salaam, wakiamnadmana jana kupinga kile walichokiita kuvurfughwa kwa haki ya mtoto ya kupata elimu, na hii ni kufuatia mgomno wa walimu ulioanza jana nchi nzima. Wanafunzi hao waliandamana hadi urefu wa kilomita 10 kutoka shuleni kwao hadi ofisi ya Afisa Elimu wa Manispaa ya Temeke, ziliko shule hizo, jirani na uwanja wa taifa ili kufikisha kilio chao.

                                         PICHA: Bashir Nkoromo blog
                      Wanafunzi wakiwa wanaelekea ofisi ya Mkuu wa wilaya
Wanafunzi wa shule za msingi Vwawa wakiwa wanapiga vidumu huku wakielekea ofisi ya mkuu wa wilaya ni Baada ya walimu kugoma.
Moja ya wanafunzi wa shule ya msingi Meta baada ya kuona walimu hawajaingia darasani yeye alichukua jukumu la kuwafudnisha wenzake
Wanafanzi wa darasa la saba shule ya msingi Meta wakiendelea kupeana mazoezi ya masomo mbalimbali baada ya waalimu wao kugoma kuingia madarasani
Wanafuzi wapo makini kumsikiliza mwanafunzi mwenzao
Mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi muungano akiwa nje ya shule akichezea mchanga maana walimu wamegoma
Picha na Arithy via Mbeya Yetu blog
Mwalimu wa Shule ya Msingi Mmoja, Salma Mtili akisahihisha daftari la mwanafunzi wa darasa la nne wa shule hiyo licha ya rais awa Chama cha Walimu Tanzaniza (CWT) kutangaza mgomo wa walimu nchi nzima.
                                            Picha na Habari Mseto Blog 
Wanafunzi wa shule ya msingi Ipembe, Nyerere, Unyankindi na Singidani katika Manispaa Singida (picha na Nathaniel Limu)



HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate