EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, October 31, 2013

ROSE NDAUKA: SIJABEBA MIMBA HOVYOHOVYO.

STAA wa sinema za Bongo, Rose Ndauka amesema suala la kubeba mimba ya mpenzi wake, Malick Bandawe kabla ya ndoa halikutokea bila mpangilio, walishauriana kabla.
 
Rose Ndauka akiwa na mpenzi wake, Malick Bandawe.
Akipiga stori na paparazi wetu, Rose alisema hajutii kubeba mimba hiyo ambayo ameitangaza kwa vile alishauriana na mwandani wake huyo na anamuamini.

“Sijajibebea tu mimba hovyohovyo hata Malick alipogundua hali hii alifurahi sana, ndiyo maana sina presha hata kidogo kwa kuwa sisi ni wapenzi wa muda mrefu na tunaaminiana,” alisema Rose.

VIONGOZI MBALIMBALI WA KISERIKALI WAMZIKA MAREHEMU BALOZI SEPETU HAPO JANA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Padri wa Kanisa Katoliki la Minara miwili Mjini Zanzibar Cosmas Amani Shayo, alipowasili katika eneo la Mazishi ya Marehemu Balozi Issac Abraham Sepetu,yaliyofanyika kijijini kwao Mbuzini Wilaya ya  Magharibi Unguja jana.
Jeneza la Marehemu Balozi Issac Abraham Sepetu,likiwa limebebwa na Askari Polisi na kulifikisha katika kaburi lake yalipofanyika mazishi kijijini kwao Mbuzini Wilaya ya  Magharibi Unguja jana.
Padri wa Kanisa Katoliki la  Minara miwili Mjini Zanzibar Cosmas Amani Shayo, akiuombea mwili wa marehemu Balozi Issac Abraham Sepetu,wakati wa mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwao Mbuzini Wilaya ya  Magharibi Unguja jana.
Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Balozi Issac Abraham Sepetu,ukitemshwa katika kaburi wakati wa mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwao Mbuzini Wilaya ya  Magharibi Unguja jana.
( PICHA RAMADHAN OTHMAN IKULU )

‘KUTEMBEA’ NA BOSI WAKE KWAMLETEA BALAA BABY MADAHA

Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’.
Mwanamuziki na mwigizaji Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’, amemshukia mwanamuziki memba mwenzake wa Candy n’ Candy, Top C na kumtaka asimuingilie katika maisha yake.

DIAMOND LUPANGO MIEZI MIWILI, KISA MAPENZI


Nasibu Abdul ‘Diamond’.
STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amewahi kusota lupango ya Keko, Temeke jijini Dar es Salaam kwa miezi miwili kisa kikiwa ni kugombea demu wa mtu.

Akizungumza na Amani juzi jijini Dar, Diamond alisema tukio hilo lilimtokea mwaka 2007 akiwa ‘andagraundi’ wa muziki wa kizazi kipya.

Diamond aliyasema hayo kufuatia kuulizwa swali na paparazi wetu kwamba, amerudiana na Miss Tanzania 2006 ambaye pi ni staa wa filamu za Bongo, Wema Sepetu. Je, haogopi kufanyiwa kitu mbaya na jamaa wake ambaye ndiye anayemuweka mjini?

TAARIFA YA CHADEMA KWA UMMA.

Kutokana na hatua ya Samson Mwigamba, aliyesimamishwa uenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha, kukiri mbele ya waandishi wa habari kuwa amevunja katiba, kanuni, maadili, miongozo, taratibu na itifaki za chama kwamba yeye ndiye aliyeandika (kwa kutumia jina bandia);

Kwenye mitandao ya kijamii, waraka uliojaa uongo, upotoshaji na uchonganishi kwa wanachama na viongozi, Idara ya Habari ya CHADEMA (kupitia Ofisa Habari, ambaye alikuwepo kwenye kikao hicho) imechukua hatua ya kuanza kutoa na kuandaa utolewaji wa taarifa rasmi zinazojibu uongo, upotoshaji na uchonganishi ulioandikwa na Mwigamba, ili kuweka kumbumbu sawa, wanachama na Watanzania wote waelewe.

Kwa kuanzia, leo tunatoa ufafanuzi juu ya suala la kikatiba la ukomo wa uongozi ndani ya chama.

Kupitia taarifa hii ya Idara ya Habari, kwanza tunapenda kushangazwa na hatua ya Mwigamba kuendelea kuvunja katiba, kanuni, maadili, miongozo, taratibu na itifaki ya chama, ambapo kupitia vyombo vya habari ameendelea kutunga mambo yasiyokuwepo badala ya kuwasilisha hoja zake (kama anazo) kupitia vikao halali vya chama ambavyo yeye anao uwezo wa kuitisha au kuhudhuria.

Tungependa umma ufahamu masuala kadhaa, kwamba katika kikao cha Baraza la Uongozi wa Kanda ya Kaskazini (Tanga, Manyara, Kilimnajaro a Arusha), muda mfupi kabla Mwigamba hajatuhumiwa kwa usaliti na hujuma, alikuwa ametoka kuwasilisha taarifa ya hali ya chama katika mkoa wa Arusha.

SOSPETER MUHONGO ATEMBELEA KITUO CHA KUFUA UMEME CHA SUMBAWANGA.

 Waziri wa Nishati  na Madini Profesa Sospeter Muhongo akipata  maelezo kutoka kwa mhandisi wa usafirishaji wa njia kuu za umeme Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi Stanslaus Deogratias mara alipotembelea kituo kidogo cha kuzalisha  umeme cha Sumbawanga chenye uwezo wa kuzalisha megawati  5.
 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akitoa maelekezo kwa watendaji wa kituo cha kuzalisha umeme cha Sumbawanga mara alipotembelea kituo hicho.

Wednesday, October 30, 2013

TAZAMA PICHA ZA MAZISHI YA BABA YAKE NA WEMA SEPETU YALIVYOKUWA HUKO ZANZIBAR LEO.

VIJANA WAPINGA KODI YA SIMU

Katibu Mkuu wa UVCCM, Sixtus Mapunda.
BARAZA Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) limeitaka Serikali kurejesha bungeni kwa hati ya dharura Muswada wa Marekebisho ya Tozo ya Sh 1,000 kwa laini za simu kwa mwezi.

UVCCM imesema ikiwa tozo hiyo itatekelezwa, itanyima Watanzania zaidi ya milioni nane haki ya msingi ya mawasiliano na huduma za kupokea na kutuma fedha kwa mtandao, jambo ambalo pamoja na kwamba lililenga kuongeza mapato, ni dhahiri litayashusha.
Sambamba na hilo, Baraza limempa Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza siku 21 kutoa kwa umma hatua anazochukua ili kuokoa wakulima wa korosho nchini dhidi ya unyonyaji, unaofanywa na walanguzi wa zao hilo.

Katibu Mkuu wa UVCCM, Sixtus Mapunda aliwaambia waandishi wa habari jana katika ofisi za Makao Makuu ya CCM mjini hapa kuwa maazimio hayo yalifikiwa na Baraza Kuu la Umoja huo katika kikao chake cha siku moja jana, chini ya Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Sadifa Juma Hamis.
Kwa mujibu wa Mapunda, katika kikao hicho walijadili migogoro ya wafugaji na hifadhi, taarifa ya utekelezaji wa tozo ya Sh 1,000 kwa laini za simu na masuala ya wakulima wa korosho.

JENEZA LA DIAMOND LAIBUA MAZITO

Stori: Shakoor Jongo na Musa Mateja
STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambaye hakaukiwi na stori, safari hii amekuja na mpya baada ya kuibuka na jeneza lenye msalaba ambalo limeibua maswali mazito, Risasi Mchanganyiko linakupasha.
Jeneza aliloingia nalo Diamond katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar.
Diamond ambaye wimbo wake mpya wa ‘Number One’ upo katika chati ya juu katika muziki huo, usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita aliingia na jeneza hilo katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar na kusababisha maswali mengi tata kutoka kwa mashabiki waliojazana kwenye onesho la Serengeti Fiesta 2013.
ILIKUWA SAPRAIZI
Mapaparazi wa Risasi Mchanganyiko waliokuwa wamejaa katika viwanja hivyo wakihakikisha wananasa matukio muhimu hasa yale ‘exclusive’, walipenyezewa mapema kuhusu Diamond kuingia na jeneza.
Diamond akipozi na madansa wake siku alipoingia na jeneza katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar.
Mtoa habari alisema Diamond aliingiza jeneza viwanjani humo kwa lengo la kupanda nalo jukwaani wakati akiimba wimbo wake uitwao Nikifa Kesho ambao mashabiki wake wengi wanasema amejichulia kifo.
Kwa sharti la kutoandikwa jina lake gazetini, mtoa habari huyo ambaye ni mtu wa karibu na Diamond alisema:
“Diamond amekuja na jeneza, limefichwa kule nyuma wanakobadilishia nguo wasanii, atapanda nalo jukwaani. Anataka kuwafanyia sapraizi mashabiki wake.”
Jeneza la Diamond Platnumz.
SAPRAIZI YAKWAMA
Hata hivyo, baada ya matatizo ya kiufundi yaliyojitokeza, Diamond hakuweza kupanda jukwaani Jumamosi usiku huo na badala yake akatakiwa kupanda kesho yake Jumapili ambapo pia hakulitumia jeneza hilo kama mawazo yake ya awali yalivyokuwa.
Mapaparazi wetu walisaka sehemu lilipohifadhiwa jeneza hilo na kufanikiwa ambapo pia walikuta baadhi ya watu wakilishangaa na kuulizana maswali.

Arsenal nje ya kombe la Capital One.

Katika mashindano ya Capital one huko uingereza Arsenal ambao wako kileleni mwa ligi kuu ya uingereza waligaragazwa bila huruma na Chelsea kwa mabao mawili kwa bila. Lakini Chlesea walipokuwa wakiwatesa the Arsenal nyumbani kwao Manchester United waliwachapa Norwich kwa mabao manne kwa bila.

Juan Mata wa Chelsea akisherekea bao dhidi ya Arsenal.
Hii inafanya Man u Kushinda mara sita mfulululizo, bila shaka na kumpa Moyes matumaini ya kufanya vizuri katika ligii ya Uingereza halikadhalika kombe hilo la Capital one.

Na katika kile kinachonekana kuwa wanasoka wa afrika wameshuka katika chati ni kiungo wa kati Yaya Toure pekee kutoka Ivory Coast ambaye yumo katika orodha ya wachezaji 23 walioteuliwa kuwaniwa tuzo ya mchezaji bora wa Fifa mwaka huo.

Kwa sasa wachezaji nyota wa zamani kama Didier Drogba, Samuel Eto'o na Michael Essien wanaonekana kufifia.

Na Yaya Toure yuko nchini Kenya katika juhudi za kupiga vita biashara haramu ya pembe za ndovu.
Toure saa ni balozi wa shirika la mazingira duniani UNEP. Mchezaji huyo mshidi mara mbili barani Afrika alifurahi katika hotuba yake kukubali wadhifa huo mpya.

8 wauawa kwenye ajali ya treni Nairobi

Watu wanane wamethibitishwa kufariki katika ajali iliyohusisha treni na basi iliyokuwa imewabeba watu wakielekea kazini katika mtaa wa Umoja viungani mwa mji wa Nairobi.

Basi hiyo inayoaminika kuwa na watu 33 iligongwa na treni kwenye njia ya reli kuelekea mjini.
Walioshuhudia ajali hiyo wanasema kuwa basi hilo lilisukumwa umbali wa mita hamsini baada ya kugongwa.
Inaarifiwa watu sita walifariki papo hapo na wengine wawili kufariki baadaye kutokana na majeraha waliyoyapata.Wengine wengi wamejeruhiwa kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu.

WANAFUNZI WA KIKE IKUWO SEKONDARI WANALALA CHINI


 Wanafunzi wa kike wa Ikuwo sekondari kwa sasa wanalala hapa kama ilivyoshuhudiwa na mtandao huu.
 kama kawaida wamepanga magodoro yao chini kwa raha zao
 Mkuu wa shule ya Ikuwo Sekondari akifafanua jambo kwa mwandishi wetu.
=====

Na Edwin Moshi, Makete
Kutokana na idadi ya wanafunzi wengi wa kike wilayani Makete mkoani Njombe kukatisha masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo kupata mimba, shule ya sekondari Ikuwo imeonesha kukerwa na tatizo hilo na kuamua kuchukua hatua za awali za kupambana nalo

Mwandishi wa mtandao huu alifika shuleni hapo na kukuta wanafunzi wa kike wote wakiwa wanalala shuleni hapo licha ya mabweni hayo kukumbwa na changamoto ya ukosefu wa vitanda

Mkuu wa shule hiyo akizungumza na mwandishi wetu amesema kutokana na tatizo hilo kuzidi kuwa kubwa, uongozi wa shule na wilaya kwa ujumla walikubaliana wanafunzi hao watandike magodoro sakafuni waendelee kulala mabwenini humo, wakati serikali ikiendelea kutafuta vitanda kwa ajili ya mabweni hayo

"Kwa wakati huu ambao tunasubiri kuletewa vitanda na serikali, tumeona ni bora wanafunzi hawa wa kike waendelee kulala chini kwa kutandika matandiko yao ili kupunguza ukubwa wa kupata mimba pamoja na kufeli" alisema mwalimu mkuu huyo

Mtandao huu ulipenya kwenye mambweni hayo na kushuhudia magodoro yaliyotandikwa kwa unadhifu wa hali ya juu, ambapo wanafunzi hao wanalala kwa muda wakisubiria vitanda

Hivi karibuni katika mahafali ya kidato cha nne Iwawa sekondari afisa elimu sekondari wilaya ya Makete Jacob Meena alikaririwa akisisitiza wanafunzi wa kike wa shule hiyo waanze kulala shuleni kuanzia mwakani hata kama mabweni hayana vitanda kama wanavyofanya Ikuwo sekondari.

WEMA AELEZEA MSIBA WA BABA YAKE BALOZI ISAAC SEPETU

Tuesday, October 29, 2013

RAIS KIKWETE NA MAMA SALMA KIKWETE WATOA POLE KWA MJANE NA FAMILIA YA BALOZI ISAAC SEPETU.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa pole mjane wa Balozi Isaac Sepetu, Mama Miriam Sepetu, alipokwenda na Mama Salma nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es Salaam jana, kutoa pole kwa mjane huyo na familia ya Marehemu Sepetu aliyefariki juzi jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pole kwa wanafamilia wa Balozi Isaac Sepetu alipokwenda na Mama Salma nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es Salaam jana, kutoa pole kufuatia msiba Marehemu Sepetu aliyefariki juzi jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mjane wa Balozi Isaac Sepetu alipokwenda  nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es Salaam, kutoa pole kufuatia msiba Marehemu Sepetu aliyefariki juzi jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa Balozi Isaac Sepetu  alipokwenda  nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es Salaam jana, kutoa pole.

YANGA, MGAMBO KUUMANA UWANJA WA TAIFA VPL LEO


Baadhi ya wachezaji wa Yanga SC.
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inakamilisha raundi ya kumi na moja leo (Oktoba 29 mwaka huu) kwa mechi tatu huku Yanga ikiwa mwenyeji wa Mgambo Shooting kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Mbeya City na Tanzania Prisons. Rhino Rangers na JKT Ruvu zitacheza katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Raundi ya 12 ya ligi hiyo itaanza Oktoba 31 mwaka huu kwa mechi kati ya Simba na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Novemba Mosi mwaka huu kutakuwa na mechi kati ya Yanga na JKT Ruvu kwenye uwanja huo huo.

Novemba 2 mwaka huu kutakuwa na mechi nne; Mgambo Shooting na Coastal Union (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Tanzania Prisons na Oljoro JKT (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro).

GWAJIMA TAJIRI NO. 1 NDIYE NDIYE ANAYEONGOZA KWA UTAJIRI WA VIONGOZI WA IMANI YA KIKRISTO.

UCHUNGUZI  wa kina uliofanywa na Gazeti la Uwazi kwa muda wa siku 30 umebaini kuwa Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima la jijini Dar, Josephat Gwajima ndiye anayeongoza kwa utajiri wa viongozi wa imani ya Kikristo, hususan wa njia ya kilokole.
Gari la kifahari aina ya Hummer 2 analomiliki Mchungaji Gwajima.
Utafiti huo umefanywa kwa kutembelea makanisa makubwa ya kiroho ya jijini Dar es Salaam na kuomba kuzungumza na viongozi wake ambapo Gwajima alitoa ushirikiano kwa asilimia mia moja kuliko wengine.

MAKANISA YALIYOTEMBELEWA
Makanisa yaliyotembelewa na majina ya viongozi wake kwenye mabano ni pamoja na Full Gospel Bible Fellowship (Askofu Zachary Kakobe), Living Water Center ‘Makuti Kawe’ (Mtume Onesmo Ndegi), Kanisa la Maombezi ‘GRC’ (Lusekelo Anthony ‘Mzee wa Upako’), Mikocheni B Assemblies of God (Mama Rwakatare) na Kanisa la Efatha (Nabii na Mtume Josephat Mwingira).
Mabasi aliyonunua Gwajima kwa ajili ya waumini wake.
KWA NINI GWAJIMA NI NAMBA MOJA?
Anakuwa namba moja kwa sababu alianika mali zake na kipato chake kingine bila kushikwa na kigugumizi. Gwajima alisema anamiliki gari la kifahari aina ya Hummer 2 ambalo gharama ya manunuzi mpaka kufika Tanzania ni wastani wa shilingi milioni 250.
AWANUNULIA WACHUNGAJI MAGARI
Akizungumza na Uwazi hivi karibuni kwenye ofisi za kanisa lake, Kawe, Dar, Mchungaji Gwajima alisema hivi karibuni aliwanunulia wachungaji wake 30 magari ya kutembelea. Alisema fedha hizo alizitoa mfukoni mwake.
Baadhi ya magari aliyonunua Mchungaji Gwajima kwa ajili ya wachungaji wake.
Baadhi ya magari aliyoyakumbuka ni Subaru Forester (sokoni linauzwa shilingi milioni 17), Mitsubishi Pajero (shilingi milioni 16), Toyota Spacio new model (milioni 20) na Toyota Harrier Lexus (milioni 35).

PROF. SOSPETER MUHONGO AZINDUA RASMI MRADI WA UMEME WA SUMBAWANGA.


Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo katikati akishirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kulia kwake, Mbunge wa Nkasi Kusini Ally Kessy kushoto kwake na wazee wawili kulia na kushoto wakiwawakilisha wananchi wa Namanyere (Wilaya ya Nkasi) katika uzinduzi rami wa mradi wa umeme kutoka Sumbawanga hadi Namanyere Wilayani Nkasi leo tarehe 28, Oktoba 2013. Mradi huo uliogharamiwa na Serikali ya Tanzania na kukamilika hivi karibuni una gharama ya Tsh. Bilioni 4.3 na umepitia jumla ya vijiji kumi na mbili vya njiani kabla ya kutua katika Mji huo wa Namanyere uliopo Wialayani Nkasi Mkoani Rukwa. Tangu Tanzania ipate Uhuru mwaka 1961 na tangu kuundwa kwa Mkoa wa Rukwa mwaka 1974 Wilaya hiyo haikuwa na umeme jambo ambalo limepokelewa kwa shangwe na wananchi wa Wilaya hiyo.  
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo na washirika wake katika uzinduzi huo wakibofya kitufe maalum kama ishara ya kuwasha umeme katika Mji wa Namanyere leo tarehe 28, Oktoba 2013 baada ya Wilaya hiyo kukosa huduma hiyo katika kipindi chote cha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania. Katika uzinduzi huo Prof. Muhongo amesema Mkoa wa Rukwa umetengewa zaidi ya Tsh. bilioni 30 kwa ajili ya umeme vijijini kupitia REA, Wakala wa Umeme Vijijini ambapo jumla ya vijiji 66 katika kipindi cha miezi 20 ijayo kuanzia Novemba mwaka huu 2013 vitanufaika na mradi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimkaribisha Katibu Tawala Mkoa huo Alhaj Salum Mohammed Chima kuwasalimia wananchi wa Kirando katika ziara ya kikazi ya siku mbili ya Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo Mkoani Rukwa. Katika ziara yake hiyo anatembelea miradi mbalimbali ya umeme pamoja na kuzungumza na wananchi. 
Meneja Mahusiano wa Shirika la Umeme nchini TANESCO Bi. Badra Masoud akisherehesha baadhi ya mambo katika hafla fupi ya uzinduzi wa mradi huo uliofanyika Namanyere Wilayani Nkasi leo tarehe 28, Oktoba 2013.

BABA MZAZI ATUMIA SILAHA ZA ULINZI KUMWADHIBU MTOTO WAKE WA MIAKA 10 KWA KOSA LA KUTOKWENDA SHULE JIJINI MBEYA

 Victoria Mukama (10) akiwa hospitali ya rufaa mbeya baada ya kupigwa na baba yake mzazi  sehemu mbali mbali za mwili wake akitumia vifaa  vya ulinzi likiwemo Lungu.
Mwalimu wa zamu wa Shule ya Msingi Airport, Damali Obadia alisema tukio hilo la ajabu lilitokea  majira ya saa mbili na nusu asubuhi ambapo akiwa ofisini alimuona mzazi huyo akiwa na mtoto huku akiendelea kumpiga wakielekea ofisini.

Mahojiano na Waziri Fenella Mukangara alipozindua RASMI Jamii Production.

Monday, October 28, 2013

Watu 20 wa familia moja hoi kwa kula chakula cha sumu.

Watu  20 wa familia moja akiwamo Ofisa Mtendaji wa kata katika kitongoji cha Igogo A kata ya Nyampurukano wilayani Sengerema, wamelazwa katika Hospitali Teule ya wilaya hiyo baada ya kula chakula kinachohofiwa kuwa na sumu.
Mbunge wa Sengerema (CCM), William Ngeleja.

Watu hao wanadaiwa kula chakula hicho cha usiku Oktoba 23, mwaka huu.

Imeelezwa kwamba mara baada ya kula chakula hicho, walianza kusikia maumivu makali ya tumbo na kulazimika kukimbizwa hospitalini kwa uchunguzi na matibabu.
Aidha, baba wa familia hiyo amelazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) kutokana na hali yake kuwa mbaya zaidi.

Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Mary Jose, alithibitisha kulazwa hospitalini hapo kwa watu hao tangu Alhamisi iliyopita kwa hofu ya kula chakula chenye sumu.
Hata hivyo, Dk. Jose alisema aina ya sumu iyohofiwa kuliwa na watu hao, bado haijafahamika.

''Ni kweli wagonjwa hao wapo lakini haijafahamika  chanzo halisi cha matatizo yao na uchunguzi ulikuwa bado unafanywa kubaini hasa chanzo chake," alisema Dk. Jose.

MALINZI ALIVYOIBUKA KIDEDEA UCHAGUZI MKUU TFF

Jamal Malinzi akishangilia na usinga aliokabidhiwa baada ya ushindi.
Rais wa TFF aliyemaliza muda wake Leodgar Tenga (kushoto) akimkabidhi Malinzi mpira kama ishara ya kumkabidhi ofisi.
Kura zikihesabiwa.

ALICHOKIFANYA DIAMOND NA NEY WA MITEGO JANA KWENYE JUKWAA LA FIESTA 2013.


Mashabiki wakiwa ndani ya Full SHANGWE.

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate