Muendelezo wa Makala 02,03 Soma chini yake Muda wote hapa
PADRI
MLA NYAMA ZA WATU-01
Mkasa
huu unasimuliwa na Padri Moses au kwa kifupi Faza Moze lakini si jina lake
halisi , akiweka bayana mambo aliyoyafanya mpaka kujutia. Padri Moses hakutaka
kuweka wazi ni wa kanisa gani kwani Mapdri hutumiwa na makanisa ya Anglikani na
Romani. Anasema:
“Ilikuwa
mwaka 1999, mwezi Desemba wakati wakristo wanajiandaa kwa sherehe ya Krismasi,
kanisani walikuja wazee wawili ambao ni wageni machoni pangu miongoni mwa waumini
wa kanisa langu hilo .
Walikaa
fomu moja na waumini wengine, lakini katika kukaa walitenganishwa na mzee
mmoja. Nikiwa naendelea na ibada, kila wakati niliwaona wale wazee wageni
wakiangaliana kwa kupitia mgongoni kwa yule mzee aliyewatenganisha.
Kwa
sababu moyo wangu ulikosa amani na wao, nikawa nawakazia macho hatua kwa hatua
ili nione kila walichokuwa wakikifanya.
Kuna
wakati nilishtuka sana kuona mmoja wao akibadilika sura na kuwa kama ya bundi,
lakini nilipojiweka sawa kushangaa, akarudi katika sura ya kawaida, na mwenzake
akacheka kama vile alijua mwenzake amegeuka sura na mimi nimeogopa.
Ndipo
nilipoanza kukumbuka ujaji wao kama ulifanana na mazingira ya kuwa waumini
wangu.
Nikakumbuka
kuwa, wakati wanaingia, walipitia njia zote za uumini, na pia walionekana ni
wanyenyekevu kupita hata waumini wangu wa kila siku.
Wakati
nikiwaza hayo, ghafla mmoja wa wale wazee alisimama mbele yangu bila kumwona
akitoka kwenye fomu kuja mbele, nikashituka, lakini kumbe waumini wengine
waliniona nilivyoshituka, wakakaza macho kiwangu wakishangaa.
Nilikatisha
maneno ya ibada na kuinua mikono juu kisha nikafanya ishara ya msalaba, kwa
jina la baba, la mwana na la roho…
Akapotea
mbele ya macho yangu na kuonekana amekaa na mwezake kama mwanzoni, wakacheka
sana lakini si kwa kutoa sauti.
“Nilishtuka
sana , nikafikicha macho kuyaweka sawasawa kwani yalionekana kama yana ukungu
wa moshi.
Yalipokaa
sawasawa, nikaendelea na ibada lakini mwili wangu ukiwa umechoka sana, hauna
nguvu tena mwilini kama kuna vitu vunatembeatembea.
Baadhi
ya waumini walipata picha hiyo, kwamba sikuwa sawasawa, lakini walikuwa hawajui
kama nilikuwa naona watu wa ajabu.
Nilipofika
eneo la kuongea maneno ambayo ikawalazimu waumini wasimame, wale wazee wawili
wakawa wa kwanza kusimama kabla sijamaliza maneno na wakawa warefu kuliko
waumini wangine.
Kurefuka
kwao kama kuliambatana na moshi mkubwa wa moto wa kuni.
Nilipowaangalia
waumini wengine walionekana hakuna wanalolijua kuhusu maono yangu kwani
walisimama, wakafunga mikono kwa unyenyekevu mkubwa wakinisikiliza.
Kama
wangekuwa wamegundua kitu, basi hata wale waumini waliokaa jirani wangejua,
kwani wao walikuwa wakinitazama tu wakati jirani yao kuna mambo ya ajabu!
Nilikata
maneno ya ibada na kuwaamuru waumini wakae, wakatii lakini mshangao:
“Humu
ndani kuna watu wawili naona kama si wa imani yetu,” nilisema.
Waumini
wote wakawa wanageukageuka na kutazamana wakiwatafuta wao watu wawili.
Walichokifanya
wale wazee sasa, muumini aliyekaa katikati yao alipogeuka kumwangalia mmoja
wao, wakaonekana wote wamekaa pamoja na yule muumini akawa amekaa pembeni yao,
kwa hiyo alipogeuka akawa anamwangalia muumini ambaye anamfahamu.
“Naamini
hakuna atakayeweza kuwaona, maana wanatumika sana na ibilisi,” nilisema.
Ninawapa
muda wa wao kujisema ni akina nani?” Nilisema huku nikiwaangalia kwa kuwakazia
macho huku waumini nao wakinikazia macho mimi na kuyafuatilia
ninakoangalia.
Walichokifanya
wale wazee sasa, muumini aliyekaa katikati yao alipogeuka kumwangalia mmoja
wao, wakaonekana wote wamekaa pamoja na yule muumini akawa amekaa pembeni yao ,
kwa hiyo alipogeuka akawa anamwangalia muumini ambaye anamfahamu.
“Naamini
hakuna atakayeweza kuwaona, maana wanatumika sana na ibilisi,” nilisema.
Ninawapa
muda wa wao kujisema ni akina nani?” Nilisema huku nikiwaangalia kwa kuwakazia
macho huku waumini nao wakinikazia macho mimi na kuyafuatilia
ninakoangalia.
Mara
walipotea machoni pangu. Niliwaambia waumini kuwa, wametoweka na nikaonesha
mahali walipokuwa wamekaa.
Yule
mzee aliyewekwa kati akasema, anachojua yeye ni kwamba, waumini waliokwenda
kukaa kulia na kushoto kwake ni wanawake na alitaka kuwauliza kisa cha kukaa
upande ule wa wanaume.
Basi,
niliendelea na ibada huku kila muumini akionekana hana amani moyoni. Hata pale
alipoingia mtu na kuliza mlio wa viatu sakafuni, waumini wote waligeuka
kuangalia mpaka ikabidi mimi nisitishe kuendelea na ibada ili waumini wamalize
kuangalia.
Ibada
ilipokwisha, niliingia kwenye chumba nikavua mavazi ya utumishi, nikabaki na
mavazi yangu ya kawaida. Nikiwa natoka nje ya chumba, ghafla nikaona giza nene
mbele.
Nikawahi
kushika flemu ya mlango huku nikiwa nahakikisha sianguki au kukanyaga sehemu
ambayo siyo ardhi. Mpaka hapo nilikuwa siunganishi tatizo la kuona giza na
uwepo wa wale waumini wawili wa ajabu ajabu.
“Mtumishi
wa Mungu kwema?” Nilisikia sauti ikiniuliza.
“Siyo
kwema kabisa.”
“Unaona
nini mbele?”
“Naona
giza .”
“Fumba
macho.”
Nilifumba.
“Haya
fumbua sasa.”
Nilifumbua.
Nikaendelea
kuona kama kawaida, lakini hakukuwepo na mtu yeyote aliyesimama mbele, nyuma,
kulia wala kushoto kwangu.
Lakini
pamoja na hali hiyo, niliisaka ile sauti akilini mwangu na kuigundua kuwa,
ilikuwa ya yule mzee aliyekaa jirani na wale watu wa ajabu.
“Khaa!”
Nilijikuta nikishangaa sasa.
Nilitembea
kwa mwendo wa haraka hadi kwa waumini waliokuwa wamesimama nje ya kanisa
wakiongea, wengine wakisalimiana na kuulizana maisha, kwani waumini wengi
huitumia Jumapili kuonana na kuongea mambo yao mbalimbali ya maisha.
Nilizungusha
macho kumwangalia yule mzee, nikamwona katikati ya watu akicheka na kupiga soga
na wazee wenzake, nikamfuata, lakini huku waumini ninaowapita wakinisalimia,
wengine wakionekana kutaka kujua kile kisa cha ndani ya kanisa.
Wakati
nakaribia kumfikia, nilijiuliza mwenyew, je, kweli kwa sauti ile kama angekuwa
ni yeye angeshafika katikati ya watu?
“
Kama ni hivyo, mbona sasa wakati nafumbua macho sikumwona mbele yangu?”
“Faza
pole na majukumu bwana,” yule mzee niliyekuwa namfuata alinisalimia na kuwawahi
wenzake wote aliyosimama nao. Sauti yake niliikumbuka vizuri sana, ndiyo ile
iliyonielekeza mpaka nikafumbua macho.
“Nimeshapoa
mzee wangu.”
Wazee
wengine nao pia wakanisalimia huku wakinipa mikono.
“Eti
mzee ulikuwa unasemaje?” Nilimuuliza yule mzee.
“Wapi?”
Na yeye aliniuliza.
“Hukusimama
na mimi pale mlangoni?”
“Mlangoni!
Wapi?”
“Kule
kwenye chumba?”
“Hata,
hapana.”
Wazee
wengine nao wakaonesha kunishangaa mimi, nikajisikia soni kwa nafasi yangu ya
u-Padri.
“Oke,
sawa basi.”
Nilitembea
kwenda kwenye ofisi yangu, lakini nyuma nikamsikia mzee mmoja akisema.
“Kwani
mzee Makwaya imekuwaje?”
“Sijui
chochote,” mzee Makwaya alijibu, hali ya mshangao na minong’ono ya chini kwa
chini iliendelea hadi ilipofika mahali nikawa siwasikii.
Kule
ofisini nilikuwa peke yangu, nikainamia mezani na kuwaza ile hali mwanzo hadi
pale ilipofikia nikaona giza nene mbele yangu.
“Hivi,
wale ni akina nani?”
“Ni
kwanini walinijia kanisani?”
“Wametumwa
au?”
Nikiwa
naendelea kuwaza hivyo, mara nikasikia sauti ndani ya ofisi.
“Unaendeleaje
mtumishi wa Mungu?”
Ilikuwa
ni sauti ya yule yule mzee Makwaya.
Nilishtuka
sana , nikaangalia kila kona ya ofisi.
“Hakuwepo
popote pale jambo lililonifanya nizidi kuogopa.
Nikiwa
natafakari huku kijasho chembamba kikinichuruzika, mara nikasikia kishindo
kikuu kwa nje kama vile kuna kitu kizito kinatua toka juu kwenda ardhini.
“Wewe
ni nani?” Niliuliza lakini sauti yangu ikitoka kwa woga.
Sikusikia
jibu wala sauti yoyote, ulipita ukimya, nikaendelea kutafakari huku kama
nashikwa na usingizi mzito na macho yangu hayaoni.
Ghafla
nilihisi kiumbe kusimama mbele yangu, nikajitahidi kufumbua macho.
Niliona
binadamu mwenye mguu mmoja, sikio moja, mkono mmoja, tundu moja la pua, jicho
moja amesimama mbele yangu akiachia tabasamu la kutisha.
“Kwa
jina la baba na la mwana na la…”
Kabla
sijamaliza kusema, alipotea mbele yangu, lakini bado macho yangu yakawa yana
kivuli chake kwani alikuwa wa kutisha sana sijapata kuona mfanowe.
Nilitamani
waumini wangu, hata mmoja tu aje, lakini ajabu ni kwamba hakukuwa na dalili na
si haikuwa kawaida yao, kwani mara zote, kila baada ya ibada waumini walikuja
ofisini kwangu na kueleza matatizo yao.
Ilifika
mahali nikahisi labda siko mahali salama, labda mimi niliona nipo ofisini
lakini kumbe sikuwa ofisini, ingawa nilipojaribu kutupa macho huku na kule,
akili yangu iliamini niko ofisini kwangu.
“Ngo
ngo ngo.”
Mlango
uligongwa.
“Karibu,
ingia,” niliitikia haraka.
Waliingia
wanawake wawili, wakiwa wamejitanda vitenge hadi kichwani na kubakiza uso tu.
Walikuwa wageni machoni pangu, nikiwa na maana sijawahi kuwaona hata siku moja
katika maisha yangu ya utumishi.
“Karibuni
sana akina mama.”
Hakuna
aliyejibu hata kwa kutingisha kichwa.
Waliangalia
wenyewe sehemu ya kuketi, wakaketi na kunikazia macho mimi.
Na
mimi niliwaangalia kwa uso wa kuwauliza shida yao . Lakini hakuna aliyesema
mpaka mimi nilipotoa sauti yangu.
“Niwasaidieni
nini akina mama zangu?”
Ajabu
iliyotokea hapo sijapata kuona wala kuisikia siku yoyote ile.
“Tuna
shida na wewe Padri,” alisema mmoja, lakini kwa sauti nene na nzito, ya
kiume.
Kwanza
nilishtuka sana kusikia sauti ya kiume ikitoka kwenye mwili ule mwembamba.
“Shida
gani mama zanguni?” Niliwauliza kwa sauti yenye woga woga kwani sasa nilianza
kuyaona maisha yangu kama yanajaribiwa.
“Tunataka
kuwa na wewe kazini kwetu,” alisema yule wa pili ambaye naye sauti yake ilikuwa
nene zaidi kupita ya wa kwanza hadi nikajikuta nikitetemeka.
“Mna…mnanitaka
kwe…kwenye kazi gani?” Niliuliza huku sauti yangu ikitetemeka kwa wasiwasi
mkubwa moyoni, jasho jembamba lilizidi kuchuruzika licha ya kwamba nilipoingia
niliwasha pangaboi.
“Ina
maana hutujui?” Wote walisema kwa wakati mmoja huku wakisimama na kujivua
vitenge. Nilishangaa sana kuwaona wamebaki na suruali na mashati, ina
maana kumbe ni wanaume kama mimi na walivaa vile kike ili kinipoteza
mawazo ya awali, niliwaza kwa wasiwasi huku nikiwakodolea macho pima.
“Mtumishi
wa Mungu aliye hai, tunakutaka kwenye kazi yetu bwana, eee?”
Mmoja
wao alisema akinisogelea nilipokuwa nimekaa mimi. Sasa niliibaini sauti yake,
ndiyo ile ya yule mzee muumini wangu.
“Nyinyi
si mliingia kanisani kwangu loe mkawa mnafanya maajabu?”
“Eee,
ni sisi,” walinijibu huku yule wa pili naye akisimama, akanisogelea na kusimama
sambamba na mwenzake.
“Sasa
mnataka nikafanye kazi gani na nyinyi, ya maajabu kama nyinyi?”
“Eee,
ndiyo,” walijibu wote.
“Mnatoka
wapi?”
Mmoja
wao akajibu:
“Tunatoka
kwa Mungu.”
“Yupi?”
Niliwauliza huku nikiwa nataka kusema ‘kwa jina la baba na la mwana…lakini
wakaniwahi wao kwa kusema:
“Mungu
kama wako, ametutuma kwako, amesema unatakiwa kupata nguvu ambayo na sisi
tunayo, kwa hiyo na sisi tunakupa nguvu hii, POKEA!”
Waliposema
‘pokea’ walinigusa kwa pamoja kwenye paji la uso, nikaanguka chini na kupoteza
fahamu.
Nilipokuja
kuzinduka, nilikuwa katikati ya pori lenye miti minene, mirefu na matawi yakiwa
juu sana .
Nililala
kwenye nyasi, pembeni yangu nilizungukwa na watu wengi ambao niliwaona miguu
tu. Kwa haraka haraka nilihesabu miguu ile na kupata idadi ya ishirini na sita,
ina maana watu waliosimama walikuwa kumi na watatu.
Niliinuka
ili kukaa, lakini mmoja wa wale watu alinizuia nisikae, niendelee kulala,
nikatii kwa vitendo na kurudi kujilaza majanini.
Ghafla
nikasikia sauti nzito, yenye tetemeko.
“Umetakiwa
kupokea nguvu ya kwetu,” ilisema ile sauti.
Yakapigwa
makofi pale, halafu ukafuatia ukimya wa muda mrefu kama vile nililala peke
yangu bila kuwepo mtu mwingine.
“Simama,”
ile sauti ilisema kwa haraka na kwa amri.
Nilijikuta
nasimama lakini nikiwa ndani ya ofisi yangu. Nilijiangalia na kujiona niko kama
nilivyovaa awali, kila kitu ndani ya ofisi kilikuwa sawasawa, hakuna hata kitu
kimoja kilichoharibika au kutokuwepo.
Hofu
ikaniingia kuhusu waumini wangu nje, kwamba kama walikuja wakakuta mazingira yenye
utata wataelewaje?
Niliusogelea
mlango na kushika kitasa, nikaufungua polepole na kuangalia nje. Hakukuwa na
muumini hata mmoja, hata mtoto.
“Khaaa!”
Nilishangaa.
“Ina
maana nimetumia muda mwingi sana ?” Nilijiuliza.
Niliangalia
saa ya ukutani na kugundua kuwa, wakati namaliza ibada ilikuwa saa nne na nusu,
muda ule naangalia saa ilikuwa saa saba mchana, ina maana kuingia kwa wale
watu, kupoteza fahamu hadi kuzinduka ilipita saa tatu?!
Mlango
uligongwa, akaingia mtu mmoja, simfahamu. Nilimkaribisha, akakaa kwenye fomu.
“Nikusaidie?”
“Ee
baba, mimi nimekuja uniombee,” alisema akijiweka sawasawa.
“Nikuombee
nini?”
“Uniombee
naumwa.”
“Unaumwa
nini?”
“Huwa
nikilala usiku naona watu wanakuja kunikaba.”
“Unaona
au unaota?”
“Naona,
wakati mwingine huwa napiga kelele kwa kuwaogopa.”
“Wewe
ni muumini wangu?”
“Hapana,
nasali mjini.”
“Sasa
kwanini usiende kwa mtumishi wa Mungu wa kanisa lako?”
“Ameshaniombea
sana lakini hakuna mafanikio.”
“Sasa
unaamini nini kuja kwangu, kuna mafanikio?”
“Naamini
yapo mtumishi.”
Nilihisi
ni miongoni mwa wale watu walionijia na kunifanyia maajabu yao, lakini sijui ni
nini, kwani ghafla nilijawa na ujasiri wa kutoogopa lolote na kuamua kumwombea
kweli.
Nilisimama,
nikamtaka yeye apige magoti kisha nikamwekea mkono wangu wa kulia kichwani
kwake na kuomba sana mpaka akaanguka chini.
Alipokuja
kusimama, akasema anajisikia mwepesi, ana imani amepona kabisa.
“Usijali,
nenda kwa amani lakini jilinde na dhambi.”
“Sawa
Padri.”
Alipoondoka
tu, mzee mmoja, aliyevaa shuka jeusi kuzunguka kiuno, chini akiwa hana kiatu
wala sendoz, pekupeku, ju mabega wazi, mkononi alishika mkia wa mnyama,
alisimama mbele yangu bila kujua aliingiaje?
“Karibu
mzee wangu,” nilimkaribisha kwa ujasiri mkubwa sana, moyoni sikuwa na hofu wala
wasiwasi. Pamoja na kuvaa kiajabu kama vile, lakini nilimwona kama mtu wa
kawaida sana kwangu.
“Fumba
kiganja cha mkononi,” aliniambia kwa amri.
Nikajikuta
nafumba bila kuhoji yeye ni nani na ametoka wapi na kaja kwangu kufanya nini.
“Fumbua.”
Nilipofumbua,
unga mweusi ulikijaza kiganja changu.
“Jipake
kidogo usoni.”
Nilijipaka
kidogo huku nikiwa nimeinama kuangalia chini.
“Unaona
nini?”
“Sioni
kitu.”
“Haya,
hiyo dawa ndiyo tunayotumia kufanyia kazi, tunapotoka usiku kwenda kazini kila
mmoja anakuwa na dawa hiyo, ndiyo inayosaidia watu wasituone…
“Fumba
kiganja.”
Nikafumba.
“Fumbua.”
Nilipofumbua,
sikuona ile dawa, kiganja kilikuwa cheupe kama mwanzo.
“Fumba
tena kiganja.”
Nikafumba…
“Fumbua.”
Nilipofumbua
mkononi, nusu kulikuwa na unga unga wa kijani nusu unga unga mweusi.
“Chota
huo unga kisha changanya.”
Nilitii,
kisha akaniambia nijipake kidogo usoni, nikafanya hivyo na kujikuta nakuwa
mwepesi kuliko kawaida ya siku zote.
“Unaona
nini?”
“Najiona
mwepesi sana .”
“Unaweza
kujaribu kupaa?”
“Nijaribu?”
“Jaribu
basi.”
Niliinua
mikono kama vile ndege anavyoinua mabawa, taratibu nilijiona napaa juu huku
miguu ikiiacha ardhi taratibu bila ridhaa yangu.
“Unaonaje?”
“Napaa
sasa.”
“Shusha
mikono.”
Niliishusha,
taratibu miguu ikakanyaga ardhi na kusimama kama mwanzo.
Baada
ya hapo yule mtu akapotea machoni pangu na kuniacha nikiwa na maswali kibao.
Nilijiweka
sawa, nikafunga madirisha ili kutoka, nikafunga mlango na kuondoka kabisa
katika eneo la ofisi.
Nilikwenda
kwenye makazi yangu, lakini kwa wakati huo nilijihisi mnyonge sana, mwili
ulikuwa hauna nguvu, macho hayaoni vizuri mbele na miguu mizito.
*
* *
Saa
saba za usiku, nilishtuka kutoka usingizini baada ya kushikwa na kuvutwa kidole
cha mguu wa kulia na mtu. Kulikuwa na giza kwa hiyo sikujua nani alifanya zoezi
lile.
Swichi
ya kuwashia taa haikuwa mbali na nilipolala, nikaiwasha chapchap, chumba
kilipojaa mwanga sikuona kitu, nikaendelea kulala.
Baada
ya muda nikawa katika ndoto.
“Wewe
Padri, unadhani utafanya kazi mpaka lini?”
“Mungu
apende,” nilijibu.
“Je,
asipopenda?”
“Atapenda
tu.”
“Kwanini
unafanya kazi lakini huna nguvu.”
“Nguvu
gani?”
“Ya
kiroho.”
“Kwa
sababu bado.”
“Bado
nini?”
“Wakati
wa kuwa na nguvu.”
“Ni
sasa.”
“Kwa
maana ipi?”
“Njoo.”
Nilimfuata
huyo mtu, akanishika na kunivuta hadi mahali, akasimama na kuniambia.
“Nenda
kaingie kwenye kanisa lile.”
Mbele
yangu kulikuwa na kanisa, nikaenda kuingia.
Lilikuwa
kanisa langu, waumini wangu, wake kwa waume wengine wamekaa wengine wamesimama.
Walikuwa wengi sana.
Mimi
nikapita hadi mbele kwenye madhabahu na kusimama pale.
“Wale
wenye matatizo waje niwaombee.”
Karibu
kanisa zima walipita mbele kuombewa.
Ule
wingi wao, nikaanza kuogopa kwamba nitaweza kweli?
Wa
kwanza nikamwekea mikono juu kichwani na kumwombea, pale pale aliposimama
akaanza kupiga kelele na kuanguka chini kisha akasimama akiwa amepona na
kurukaruka huku akimtukuza Mungu wake.
“Hee,
hee nimekuwa mzima sasa.”
“Nenda
usitende dhambi tena, sawa?”
“Sawa.”
Niliombea
karibu kanisa zima, nilipomaliza nikawa natoka huku napigiwa makofi na waumini
waliokuwa wamesimama kulia na kushoto kwangu.
“Padiri
Padiri Padiri,” walisema wakipiga makofi, pwa pwa pwa.
Kufika
nje, nikakutana na yule mtu aliyenichukua nyumbani.
“Umefanikiwa?”
“
Sana ,” nilimjibu.
“Umekubali?”
“Nini?”
“Kwamba
wakati wa kuwa na nguvu ya kiroho ni sasa?”
“Nimekubali.”
“Haya,
sasa twende kwa aliyekupa nguvu.”
“Kwa
Mungu?”
“Wetu
sisi.”
Tuliongozana
hadi kwenye mti mmoja mkubwa, mrefu sana kwenda juu.
Chini
walikaa watu wengi wakiwa kama wapo kwenye maongezi.
Kilichonishangaza
miongoni mwa hao watu walikuwepo waumini wangu wa kanisani.
“Afadhali
umekuja faza.”
“Faza
nimefurahi sana kukuona.”
“Faza
karibu sana .”
Wale
waumini wangu wote walinikaribisha kwa furaha, amani na upendo wa hali ya juu.
Nilikaa
sehemu ambayo kulikuwa na nafasi ya mtu mmoja, yule mtu niliyekwenda naye
sikumwona tena alikopotelea.
“Bwaba
umekuja huku, uko tayari kwa lolote?” Aliniuliza mzee wa kanisani ambaye sikuwa
na mazoea naye.
“Kwani
hapa ni wapi?” Nilihoji.
“Hapa
ni kwa wachawi.”
“Wachawi!”
“Eee,
umekuja kwa wachawi, kazini kwetu, karibu.”
Alipomaliza
kusema, alikaa chini, akasimama sasa yule mzee ambaye siku ile kanisani
walipoingia wale watu wawili wa ajabu, yeye alikaa katikati yao.
“Eee,
nina kila sababu ya kujisifu kwa kupewa heshima hii ya kumkuza kazini mtu
mkubwa kama huyu,” alisema yule mzee.
Yakapigwa
makofi kwa muda wa dakika tano nzima huku yule mzee akiwa amesimama tu
akisubiri yaishe ili aendelee kuongea.
Lakini
kwa jinsi nilivyokuwa namwangalia mimi, alikuwa anaongea kwa kujiamini sana na
hakuonekana kujali kama mimi ni kiongozi wake wa kiroho.
“Kwa
hiyo kuanzia leo mtumishi utakuwa chini yangu ukizitii na kuzifuata amri zangu,
sawa bwana mdogo?”
Nilimjibu
kwa sauti ya unyonge sana :
“Sawa.”
Pale
pale alitembea kuelekea nilikokuwa mimi, akaniwekea mkono kichwani.
***
Wiki
moja ilikatika toka hayo yatokee, lakini hakukuwa na jipya jingine, sikuwahi
kumwona mtu mwingine akinijia nyumbani wala kanisani ninapokuwa nafanya kazi za
Mungu.
Lakini
siku hiyo, nikiwa nimelala majira ya saa saba usiku, nilishtuka ghafla.
Nikatupa macho mlangoni. Kwa sababu ya giza sikuona vizuri, ila dalili ya kama
kitasa cha mlango kikifunguliwa.
Nilinyoosha
mkono hadi kwenye taa ya kitandani (bed switch) nikawasha kwa umakini sana ili
mlio wa swichi usisikike.
Kitasa
kikawa kinakaribia chini, lakini kikanata kwa muda. Nadhaani ni baada ya mimi
kuwasha taa.
Hali
hiyo ilinifanya nitoke kitandani na kusimama katikati ya chumba huku macho yote
yakiwa kwenye kile kitasa mlangoni.
Huku
taa ikiwa bado inawaka, kitasa kiliendelea kwenda chini, yaani kufunguka,
lakini ilionekana aliyekuwa anakifungua yupo makini sana kwani kwa kukitazama
haraka tu ilikuwa vigumu kujua kitasa kinafunguka kwa kwenda chini.
Mara
mlango ukaanza kusukumwa polepole na mimi nilisimama nikaza macho kujua
nani aliyekuwa akifanya kazi ile. Wazo kwamba ni mwizi sikuwa nalo kwani
nawajua wezi, wao ni papara au kushtukiza.
Mlango
uliendelea kusukumwa mpaka ukawa wazi wote, yaani kama kuna mtu alisimama
kwenye korido angeona chumbani, lakini cha kushangaza hakukuwa na binadamu wala
kiumbe chochote nyuma ya mlango.
Nilipotaka
kuuliza nani mwenzangu, nikasikia sauti ya mtu kukohoa kwa kujibana. Halafu
nikasikia mlio wa viatu, ko! Ko! Ko! Ko! Ukisikika kuingia ndani ya chumba,
nikarukia kusimama pembeni kwani niliamini aliyekuwa akiingia angeweza
kunikumba.
Mlio
wa viatu kutembea uliposimama ukafuata mlio wa kufunguliwa kwa dirisha la chumba,
na kweli likawa linafunguka hadi mwisho, halafu pazia ikawa inakunjwa na
kufungwa katikati kama vile mkunjaji alitaka upepo uingie kwa vizuri.
Baada
ya hapo, nikiwa nimesimama pembeni, mlio wa viatu ukatembea kwa mwendo ule ule
wa ko! Ko! Ko hadi ukutani kwenye swichi, ghafla nikasikia tap na giza
likatanda. Ina maana huyo mtu alizima taa.
Halafu
mlio wa viatu ukaendelea tena hadi usawa wa kitanda, ukakwamba pale. Giza
likiwa limetanda, nikasikia hali ya mtu anayepanda kitandani kwani kitanda
kilitoa mlio Fulani na baadaye, kama baada ya dakika moja ikasikika sauti ya
mtu kukoroma.
“Khooooo!
Khoooo!”
Niliamini
ni uonevu usiokuwa na maana kwangu kwani sikuwa na kosa la kunifanya nishindwe
kulala na kulala mtu mwingine, nilikasirika sana . Nikatembea kijeuri
hadi ukutani na kuwasha taa.
Ile
inawaka tu, ile swichi ya kitandani ikasikika ikizimika, tap! Kukawa giza tena.
Niliifuata
kwa fujo ile swichi ya kitandani, nikaiwasha na macho yangu yakakimbilia moja
kwa moja kitandani. Mtu mnene, mrefu alikuwa amejifunika shuka huku akiwa
amenyoosha miguu na anaangalia juu, yaani amelala chali.
“Wewe
ni nani?” Nilimuuliza bila woga.
“Msafiri,”
sauti nzito ilijibu kwa mkato.
“Ndiyo
jina lako au msafiri unakwenda mahali?”
“Siendi
popote.”
“Khaa!
Sasa hapa kwako?”
“Hapana.”
“Sasa
kwanini umefungua mlango bila hodi na umepanda kitandani kulala bila ridhaa
yangu?”
“Nisamehe
sana .”
“Basi
ondoka.”
Kauli
yangu hiyo haikupata jibu zaidi ya mlio wa kukoroma kusikika kama mwanzo.
Nilimsogelea
yule mtu pale kitandani kwa lengo la kumfunua shuka na kumwona vizuri.
Niliishika shuka kwenye ncha moja, nikaifunua kwa
nguvu…
“Ha
ha ha ha ha ha!” Alicheka sana yule mtu huku akitoka kitandani na kuficha uso
kwa mkono mmoja.
Nilijitahidi
sana kuhakikisha namwona uso yule mtu, lakini na yeye alikuwa akawa anaangalia
ukutani huku akiendeelea na kicheko chake.
“Wewe
ni nani?” Nilimuuliza kwa ukali kidogo.
“Ha
ha ha ha! Msafiri bwana, si nilikwambia!”
“Umetumwa?”
“Hapana.”
“Umekuja
tu mwenyewe?”
“Ha
ha ha ha! Eee!”
Kusema
ule ukweli nilichanganyikiwa, kwani sasa nikawa sijui ukweli upo wapi, kila
ninachomuuliza ananijibu kinyume na matarajio yangu.
“Basi
mimi naomba uondoke humu chumbani kwangu,” nilimwamuru.
“Ha
ha ha ha ha! Sawa,” alisema akielekea mlangoni na kutoka kweli lakini nikiwa
sijafanikiwa kuona sura.
Kwa hiyo mpaka hapo nikawa sijui ni nani yule.
Alipovuka
tu ukuta wa chumba changu, nikajikuta napata wasiwasi na woga tofauti na mwanzo
alipoingia.
Nilifunga
mlango ili nipande kitandani kulala, lakini kabla sijapanda, nikasikia vishindo
ti ti titi! Watu kama sita walisimama katikati ya chumba changu.
“Mtumishi
wa Mungu vipi? Habari za kulala?”
“Salama.”
“Aaa,
tumetumwa kwako.”
“Na
nani?”
“Aaa,
vaa miwani yako kwanza kisha utuangalie vizuri.”
Nilipeleka
mkono kwenye stuli ndogo iliyokuwa pembeni ya kitanda na kuchukua miwani,
nikaivaa na kuwaangalia.
Walikuwa
tofauti na nilivyowaona wakati wanatua. Walikuwa wamevaa viguo vyeusi (kaniki)
kukatisha kiunoni kwenda chini ya mapaja, kila mmoja alionekana amekasirika na
hana utani na usoni walipaka vitu vyeupe, kama si unga, basi chokaa.
“Unatuona
vizuri sasa?”
“Ndiyo.”
“Basi
ndivyo tulivyo, toa miwani.”
Nilipotoa
tu, walirejea na kuwa kama walivyotua, wamevaa kawaida.
“Unatakiwa
kuhudhuria mateso ya waumini wako usiku wa sasa,” mmoja wao aliniambia, wengine
wakatingisha vichwa kama ishara ya kukubaliana na maneno ya mwenzao.
“Wapi?”
“Katika
kila nyumba yenye muumini au waumini wako.”
“Ni
mateso ya aina gani?”
“Utajua
huko huko na huna hiyari katika hili, kwani ulishapata baraka zote za uchawi.”
Nilijikuta
nasimama, naanza kutembea kuwafuata kutoka nje mpaka uwanjani mbele ya nyumba,
wakaanza kutengeneza duara na mimi nikawa mmoja wa wanaduara.
Mmoja
akapeleka mikono na kuwashika wa kulia na kushoto kwake, wengine wakafanya
hivyo mpaka mimi. Tukawa tumekamatana mikono. Yule aliyeanza kushika, akainama
kama dalili ya kusujudia, wengine wakafuatia na mimi pia, kufumba na kufumbua,
tukajikuta tukipaa juu na kutua chini ya mti mkubwa wa Mvule. Sikumbuki
tulitumia dakika ngapi kuwa angani na kushuka.
Milio
ya ngoma iliyotawala pale ilinifanya niamini kuwa, kweli nilikuwa katikati ya
maskani ya kichawi.
“Bila
kupoteza muda sasa tunaingia mitaani, hasa kwenye nyumba za waumini wa kanisa
ambalo padri wao tunaye kwenye kundi letu na kufanya kazi ya kuwatesa, sawa?”
Sauti nzito, iliyokuwa ikisikika na kitetemeshi ilisema.
Nilipomwangalia
msemaji huyo, ni mzee mmoja aliyekuwa amevaa kanzu ndefu nyeusi, juu, yaani
kichwani alivaa pembe za mnyama, mkononi alishika mkia, pia wa mnyama.
“Sawa,”
wenzangu waliitikia kwa sauti ya juu.
Kifupi
mimi nilikuwa sijui kitu chochote. Nilikuwa sijui watafanyaje huko kwenye
kutesa watu, sijui nani atakayeteswa, kama ni waumini wote pia sikujua. Ila,
mzee mmoja alinifuata na kuniambia:
“Tuondoke
mimi na wewe.”
Nikawa
namfuata hadi kando kando ya ule mti mkubwa, akasimama ghafla hadi nikamkumba.
Kufumba
na kufumbua, tulitua nje ya nyumba ya muumini wangu mmoja ambaye anamiliki
mashine ya kusaga na trekta moja.
“Haa!
Hapa si kwa..?”
Kabla
sijamaliza kusema, yule mzee akaniambia kwa kunikatisha:
“Ulisikia
tulivyoambiwa kule?”
“Kwamba?”
“Tunawatesa
akina nani?”
“Waumini
wangu.”
“Sasa
unauliza nini?” Alinijibu huku akitembea kwa kurukaruka kwa mguu mmoja.
Alipoona
mimi nimezubaa akanifuata:
“Jipige
kifuani kwa mkono.”
Nikafanye
hivyo.
“Hapo
sawa sasa, nifuate mimi kwa kila hatua mpaka ndani na kuanza kazi, sawa?”
Aliniuliza.
Inaendelea!!!!!!!!!!!!!!!! Usikae mbali na Irene Mwamfupe Ndauka pande hizi.
PADRI
MLA NYAMA ZA WATU-2
Tulikwenda
hadi kwenye mlango mkubwa, nikadhani atagonga ili tufunguliwe, kumbe sivyo
bwana.
“Kila
ninachofanya mimi na wewe unaniiga, sawa?” Aliniambia akinigeukia, kwani
nilikuwa nimesimama nyuma yake.
“Sawa.”
“Haya
tunaanza sasa.”
Alijipiga
tena kifua na mimi nikajipiga. Kufumba na kufumbua tukawa ndani, sebuleni.
“Sasa
niigize kwa kila kitu.”
“Sawa,”
nilimjibu kwa sauti ya chini kama ile aliyoitumia yeye kuniambia.
Alitembea
kwa kurukaruka kwa mguu mmoja, huku mguu wa pili ukiwa unaning’inia tu. Kwa
mimi nilivyoona, hakukuwa na sababu yoyote ya kutembea vile, ila kwa kichawi
nadhani ni sawa na ni kawaida kwao.
Na
mimi niliruka ruka kwa mguu mmoja huku mwingine ukining’inia hadi kwenye mlango
wa kuingia kwenye vyumba, yule mzee akasimama, lakini kwa mguu mmoja.
Tulisimama
vile mpaka mimi nikabadili msimamo, nikatumia mguu mwingine maana nilichoka
sana .
Ghafla
akaweka mguu mwingine chini huku akigeukageuka kuniangalia.
“Sasa
tunaingia chumbani kwa baba mwenye nyumba, sawa?”
“Sawa.”
“Una
swali lolote kabla hatujaingia?” Aliniuliza.
“Ndiyo.”
“Enhe,
lipi hilo ?”
“Haaa…”
“Uliza
haraka.”
“Sawa,
hatutaonekana?”
“Wapi?”
“Tunakokwenda.”
“Kwani
si nimekwambia kila kitu unaigiza kwangu?”
“Kabla
sijaigiza je?”
“Hatutaonekana.”
“Basi,
swali langu ni hilo tu.”
“Kwa
hiyo huna swali jingine?”
“Sina
na wala sitakuwa nalo.”
“Oke
nifuate.”
“Niko
nyuma yako.”
Aliinua
mikono juu, akapiga makofi na mimi nikafanya hivyo hivyo. Kufumba na kufumbua
tukawa tumesimama katikati ya chumba.
Yule
mzee akanigeukia, akaniangalia lakini hakusema kitu. Mdomo akauangalizia juu na
kufanya tendo kama anapuliza moto, na mimi nikafanya hivyo hivyo. Akamsogelea
mzee mwenye nyumba aliyekuwa amelala usingizi mzito wa chali, akamkalia tumboni
huku akijisotesha kuanzia kiunoni kwenda kifuani na kurudi.
Mimi
nikawa mtazamaji tu, lakini yule mzee akaniangalia na kunipa ishara kwamba na
mimi nimpandie mke wa yule mwenye nyumba ambaye alikuwa amelala kitanda kingine
na mtoto mdogo kama wa mwaka mmoja.
Nilipanda
bila kujiuliza maswali kwanini napanda, nikajisotesha kama alivyokuwa akifanya
yule mzee, lakini nilipotua macho usoni kwa yule mama ambaye naye alilala
chali, nikamjua kuwa ni muumini wangu mzuri pale kanisani.
Kusema
ule ukweli niliumia sana moyoni, nikajihisi ni mtenda dhambi nisiyestahili
msamaha wa aina yoyote ile.
Lakini
ilinibidi niendelee tu na kazi niliyokuwa naifanya kwani ni jukumu ambalo
nilishalivalia njuga sikuwa na budi kulimaliza sawasawa na safari yetu ya
kuingia ndani ya nyumba ile.
Mara
yule mzee alishuka kutoka kwenye tumbo la yule mzee mwenye nyumba huku
akinifanyia ishara ya mimi pia kushuka.
Tulishuka
wote, tukasimama tukiangaliana. Mara mwenzangu akaufuata ukuta sehemu ya
kichwani ya yule mzee, akasimama na kumwinamia kisha akapeleka mkono hadi
jirani na shingo yake na kuukunja kama vile ameshika shingo na kumkaba.
Yule
mwenye nyumba akawa anarusharusha miguu kama anayeitafuta pumzi baada ya kuziba
kwa pua na kinywa, huku akisema maneno yasiyojulikana:
“Mmmh!
Mmmmmm! Mmm!”
Alivyokuwa
akiendelea kubana mkono ndivyo na yule mtu alivyokuwa akizidi kulalamika, sasa
akapeleka mikono kwenye koo lake na kujishika huku akizidi kulalamika.
Alichofanya
yule mchawi, akawa anambana huku mkono mmoja anafanya kama anamtisha kwa ngumi
ya uso yule mzee. Alipokuja kumwachia, akasimama pembeni yake kisha yule mtu
mwenye nyumba akashituka kutoka usingizini na kukaa huku akikohoa sana.
“Mungu
wangu, Mungu weee! Ooo! Mama,” alisema akiendelea kushika koo lake.
Akamwita
mkewe kwa sauti ya juu, naye akashituka na kumuuliza kulikoni:
“Kuna
nini mume wangu?”
“Nimekabwa
vibaya sana .”
“Na
nani?”
“Najua
ni wachawi tu hao.”
“Umejuaje?”
“Wamenishika
koo kwa kunikaba kisha wakanipiga ngumi za uso. Kwani huoni kama umevimba?”
“Nini?”
“Uso
wangu?”
“Hata,
ila macho kama mekundu.”
“Ni
hao hao lakini mmoja kama nimemwona.”
“Unamjua?”
“
Kama namjua.”
“Ni
nani?”
“
Kama ..!”
“Vipi
tena mume wangu?”
“Tumbo
nalo kama limejaa, ooo linauma sasa, wachawi hao mke wangu.”
Mara
mkewe naye akaanza kulia huku akishika tumbo lake na kulalamikia.
Moyoni
nilitamani sana yule mzee atokee ili akabiliane na zile tuhuma zile ambazo mimi
zilinifika shingoni na niliingiwa na kinyongo na kazi ile ya kichawi ambapo
awali niliambiwa hakuna ambaye angeweza kutuona wakati tukiwa kwenye matukio
yetu.
“Eee
Bwana niepushe na aibu hii, sirudii tena mimi, nimeshajirekebisha,” nilisali
kimoyomoyo peke yangu pale mbele ya madhabahu. Nikajikuta nakohoa pia bila
sababu.
Ghafla
mzee mwingine akanyoosha kidole, wakawa wawili sasa. Lakini pia wakati yule
akiendelea kuongea na vile vidole viwili vikiwa juu, mke wa yule mzee aliyekuwa
akiongea naye akanyoosha kidole.
“Mbaya
zaidi, watu waliotuingilia kutufanyia hivyo huwezi kuamini ukiambiwa, hii ni
aibu kwa kanisa na pia ni kufa kiroho. Mungu hawezi kuuvumilia ubaya huu.”
Wakati
anazidi kubomoa, mimi haja ndogo ilinibana, nikawa navumilia tu.
Nilitamani
ardhi ipasuke, mimi niingie ndani mwake na nisionekane tena maishani mwangu.
Mwili ulinitetemeka, akili ikanipotea, nikawa sijui niamue nini.
“Hali
ikiwa hivi kuna siku humu huku kanisani watu watashikania mapanga kutoana damu,
hakiyanani vile.”
Yule
mzee alipomaliza kusema hayo, akaa ghafla kama vile alishikwa na kukalishwa kwa
nguvu.
Nikataka
kusema muda umekwisha, lakini mzee mmoja kati ya wale walionyoosha vidole
alisimama hata bila kuruhisiwa, alipoona mwenzake amekaa tu.
“Nashukuru
sana na mimi kwa kupata muda huu. Zamani uchawi hapa kanisani ulikuwa ni msemo
tu, si kitu ambacho kinatingisha, lakini mimi nina habari kwamba, sasa uchawi
umo ndani kabisa ya hili kanisa, tena washiriki ukitajiwa majina unaweza
kubisha hadi unaanguka chini.
“Mimi
kama nitapata baraka za waumini wenzangu niko tayari nitaje majina, lakini
nilindwe.”
Nilimwangalia
vizuri yule mzee nikamwona kama ametumwa, kwani wakati anaongea, hakuwa
ananiangalia mimi, wala mtu mwingine, alaiinama tu huku akibwabwaja.
“Sema.”
“Wataje.”
“Waweke
wazi bwana.”
“Tutajie.”
“Tuambie.”
Hayo
yalikuwa maneno ya waumini wa kanisa lile ambayo yalinichanganya kabisa. Baadhi
ya waumini wakawa wanainama kunong’onezana huku wakiniangalia kwa kuniibiaibia.
“Niwataje?”
Yule mzee aliuliza tena kwa sauti ya juu.
“Watajeeee.”
Wakati
huo, yule mzee mwingie na yule mke wa yule wa kwanza, vidole vyao vilikuwa bado
juu wakiomba nafasi ya wao kuongea.
“Eti
niwataje?”
Inaonekana
aliniuliza mimi kwani aliniangalia. Na hapo ndipo nilipojua kuwa, hata mimi
niko ndani ya tuhuma za kutajwa kwani kama nisingekuwemo, yule muumini
angeniuliza hivi, ‘eti mtumishi wa Mungu niwataje?’ sasa hakusema mtumishi kwa
sababu alishajua sina cha utumishi wala uchungaji.
“Nalinda
heshima ya kanisa, siwataji, ila nawataka waache mara moja tabia hiyo,”
alimaliza yule mzee na kukaa.
Ghafla
tena akasimama mzee mwingine hiku akiendelea kunyoosha kile kidole chake.
Jamani
muda naona umetuishia, siwezi kuruhusu mambo hayo, ila nitaunda kamati ya
kushughulikia, matokeo yatatangazwa humu humu kanisani.
“Lini?”
Waumini walihoji kwa pamoja.
“Eee,
Jumapili ijayo.”
“Tuhakikishie.”
“Ha!
Niwahakikishie kwani mimi ndiye mchawi?” Nilijibu kwa jabza sasa.
“Mh!”
“Mh!”
“Mh!”
Waumini
waligunia chini kwa chini. Sasa sikujua waliguna kwa sababu ya majibu yangu au
kwa sababu walishajua mimi ni mchawi. Hiyo iliniuma sana , lakini sikuwa na
jinsi zaidi ya kusema hivyo.
Kilichonishangaza
zaidi hata wale wazee wenye hekima zao katika kanisa hakuna aliyetoa sauti
kuongea kitu kwa kunitetea wala kutengeneza amani.
Nilimaliza
ibada, watu wakatoka nje mmoja baada ya mwingine. Lakini kule nje wakasimama
katika makundi makundi isivyo kawaida.
Halafu
wakawa wanaonekana wakiongea kwa tahadhari sana, kwani kila mara walionekana
kuangalia mlango wa kuingilia kanisani na wa ofisini kwangu.
Na
mimi nilitoka nje na kuiacha ofisi tupu, nikasimama ili kuangalia nini
kinaendelea kwa waumini wangu, lakini nao wakaanza kutimka mmoja mmoja.
Hoja
kwamba walinigundua mimi ilipata nguvu baada ya baadhi ya waumini kunipita tu
wakati wanaondoka wakati su jambo la kawaida kwao.
“Mama,”
nilimwita muumini mmoja, akasimama. Mimi ndiyo nikamfuata aliposimamia.
“Mama
kwani kuna nini leo?” Nilimuuliza.
“Hujui?”
“Sijui
kitu.”
“He
he! Uchawi kanisani,” alisema.
“Sasa
mbona watu wananitenga?” Nilimuuliza, lakini badala ya kunijibu akaondoka zake
haraka.
Ghafla
nikasikia mlango wa ofisini kwangu ukigongwa kwa nguvu kama kuna mtu ndani,
nikaenda haraka.
Kufika
nikamkuta yule mzee tuliyekwenda kuwanga naye usiku nyumbani kwa wale waumini.
“Umefanya
nini sasa? Ona yaliyokupata.” Aliniuliza kwa hasira sana .
“Kwani
kosa langu ni nini?” Nilimuuliza na mimi nikiamini sikuwa na hatia, bali yeye
ndiye aliniingiza mkenge.
“Wewe
umekwensa kanisani bila kumwomba mkuu kwa sala.”
“Mkuu
gani?”
“Kwani
mkuu wako kwa sasa ni nani?”
“SI
Mungu!”
“Ha
ha ha ha! Siyo Mungu, Mungu yupi kwanza, yule wako wa zamani?”
“Hata
sasa.”
“Amekwambia
nani, hujui kama umeshasajiliwa kwa mkuu wa giza ? Kuanzia siku ile pale wewe
ni wa mkuu wa giza kama sisi.”
“Oke,
turudi kwenye msingi wa maongezi, kosa langu ni lipi?”
“Kosa
nimeshakwambia, leo kanisani kila mtu amekushangaa wewe kwa jinsi ulivyokuwa
umevaa nguo za kulalia madhabahuni, lakini wewe mwenyewe ulidhani uemvaa joho.”
Moyo
ulinilipuka lip. Nikashangaa sana huku nikijiuliza maswali mengi na kuvuta
picha ya jinsi nilivyoonekana.
Lakini
mpaka hapo, nilipojiangalia mwenyewe nilikuwa nimevaa joho la utumishi, sasa
hizo nguo za kulalia ni zipi!
“Mbona
nimevaa inavyotakiwa?” Nilimuuliza.
“Ndivyo
unavyojidanganya?”
“Kh!
Si hivi, kwani we hunioni?”
Yule
mzee alicheka, akaangalia chini kisha akatembeza mkono wake chini kama anafuta,
ukawa na vumbi kisha akanipaka lile vumbi usoni kwangu.
Pale
pale nilipojiangalia, kweli nilionekana nimevaa pajama ya kulalia, ya chini na
ya juu.
Nilishtuka
zaidi, mwili ukaingiwa na ganzi na kuanza kuhisi mshangao niliousababisha kwa
waumini wangu, nikaanza kupitia maongezi ya wale waumini waliosimama kuongea
wakisema hivi:
“Mbaya
zaidi, watu waliotuingilia kutufanyia hivyo huwezi kuamini ukiambiwa, hii ni
aibu kwa kanisa na pia ni kufa kiroho. Mungu hawezi kuuvumilia ubaya huu.”
“Hali
ikiwa hivi kuna siku humu humu kanisani watu watashika mapanga kutoana damu,
hakiyanani vile.”
(Mzee
mwingiune anasimama).
“Nashukuru
sana na mimi kwa kupata muda huu. Zamani uchawi hapa kanisani ulikuwa ni msemo
tu, si kitu ambacho kinatingisha, lakini mimi nina habari kwamba, sasa uchawi
umo ndani kabisa ya hili kanisa, tena washiriki ukitajiwa majina unaweza
kubisha hadi unaanguka chini.
“Mimi
kama nitapata baraka za waumini wenzangu niko tayari nitaje majina, lakini
nilindwe.”
“Sema.”
“Wataje.”
“Waweke
wazi bwana.”
“Tutajie.”
“Tuambie.”
“Niwataje?”
“Watajeeee.”
“Eti
niwataje?”
“Nalinda
heshima ya kanisa, siwataji, ila nawataka waache mara moja tabia hiyo.”
“Niachieni
mimi, nitalifanyia kazi na matokeo yatatangazwa humu kanisani.”
“Lini?”
“Eee,
Jumapili ijayo.”
“Tuhakikishie.”
“Ha!
Niwahakikishie kwani mimi ndiye mchawi?” (Waumini wanaguna).
“Mh!”
“Mh!”
“Mh!”
(Anamwita
muumini mmoja nje).
“Mama
kwani kuna nini leo?”
“Hujui?”
“Sijui
kitu.”
“He
he! Uchawi kanisani.”
“Sasa
mbona watu wananitenga?”
(Yule
mama anaondoka haraka).
“Oooph!
Kweli nitakuwa nimeumbuka sana , sasa?” Nilimuuliza yule mzee baada ya kuwaza
hayo yote yalivyokuwa kwenye ibada.
“Hakuna
cha sasa, hapa kampeni moja tu, kuhakikisha wale wote waliosimama kuuliza
maswali wanakufa.”
“Mh!
Kwa njia gani. Halafu na wewe una makosa, kwanini usije kunishtua pale
madhabahuni kuwa nimevaa pajama?” Nilimwambia na kumuuliza yule mzee.
“Nilijitahidi
lakini kukufikia pale mbele ikawa kazi. Unajua makanisa karibu yote yana nguvu
ya Mungu mbele, huwezi kufika kirahisi. Mimi nilisimama kushoto kwako nikawa
nakuangalia.”
Tukiwa
tunaongea hayo, mara mama mmoja akasimama mbele yetu, ni muumini wa kanisani
lakini sikujua kama ni mchawi.
“Leo
padri umechemsha sana.”
Mwili wote
ulikufa ganzi tena, nikahisi roho inataka kumrudia aliyeiumba, mwili kwenda
mavumbini.
“Kwani unadhani
mimi sijui kitu kuhusu wewe kujiunga na Mungu wa giza , najua.”
Niliendelea
kumkodolea macho ya mshangao.
Yule mzee
alimwangalia sana , akamuuliza.
“Wewe upo
kwenye kambi ya mzee Masomo?”
“Ndiyo,”
alijibu yule mwanamke lakini akionekana kama hana habari sana na yule mzee
kuliko mimi. Akaniuliza.
“Ni kwanini
umeamua kumtumikia Mungu wa upepo?”
“Sijamtumikia
mimi,” nilimjibu kwa hasira.
Wote, yaani
yule mwanamke na yule mzee wakacheka.
“Umechelewa
sana, kama unataka kufa endeelea kusema hivyo,” yule mzee aliniambia kwa sauti
ya kukazia, nikaogopa mwenyewe.
Yule mwanamke
akasimama sawasawa kisha akainama kidogo aliponyanyua shingo, akasema:
“Padri mimi
nimekuja na ujumbe wako, naamini utaupokea na utaufanyia kazi haraka sana,
naomba uupokee.”
“Ujumbe gani na umetoka kwa nani?” Nilimuuliza
nikimwangalia kuuona huo ujumbe wenyewe, kama ni barua au maneno tu.
“Ni
maneno tu Padri,” alisema huku yule mzee akimkazia macho.
“Una
maanisha nini?”
“Kwani
hujui?”
“Ningejua
nisingekuuliza.”
“Ulikujaje
kanisani vile?”
“
Hilo ndilo tunalolizungumza hapa.”
“Hapa
hatuzungumzi, ni kuachana na huyu, sisi tukutane usiku kwa ajili ya kupanga
mikakati mizito mizito ya kuua wale wote walijidai ni vinara kwa kusimama na
kusema sema ovyo,” alisema yule mzee.
Tulikubaliana
kuwa hivyo, wote tukatoweka, kwa ahadi ya kukutana usiku ili kupanga hiyo
mikakati mizito ya kuua.
***
Ilikuwa
ni usiku wa saa sita, nikiwa nimemaliza kusali kwa Mungu wangu, sasa nausaka
usingizi mwingine wa awamu ya pili.
Nilipokuwa
naanza kusinziasinzia tu, nikasikia kishindo tii!
Nikashtuka
na kuangalia mle chumbani, nikaona miguu ya watu karibia kumi, lakini
niliona kuanzia miguuni hadi kwenye magoti, lakini kwa upande wa nyuma.
Hii
miguu ilikuwa minene, na ilitembea kwa mwendo wa pole kutoka pale iliposimama
kuelekea ukutani.
Halafu
ghafla nikawa naona ile miguu inaongezeka katika kuonekana kwake, yaani
inaonekana zaidi ya magotini na kuelekea juu hadi kwenye mapaja.
Nikasikia
sauti nzito:
“Sisi
ni wenzako, tumekuja, amka.”
Niliamka
polepole kitandani mpaka nikakaa, nikaangalia kulia na kushoto, wote wakajionesha
moja kwa moja. Wengine niliwafahamu, wengine sikuwafahamu.
“Simama,”
yule mzee wangu alisema akiniangalia na tena akawa ananyoosha mkono kuelekea
kwangu kama vile alikuwa akitaka na mimi nimpe mkono wangu ili anishike.
Nilinyoosha
mkono, nikamshika, naye akanishika, nikasimama lakini mwili ukiwa mzito sana.
Nilipoweza
kusimama vizuri mwenyewe, mwanamke mmoja akanirushia nguo nyeusi, ikanivaa
mwilini, watu wakapiga makofi chumbani kwangu, nikashangaa sana kwani sikuona
ni jambo la kawaida watu wengi kuwemo ndani ya chumba changu na kupiga makofi
na kelele za vifijo kwa wingi.
Yule
mzee akasema wote tushikane, yaani kila mmoja aliposimama amshike mwenzake
mkono, wote tukafanya hivyo, tukashikana mikono.
Kufumba
na kufumbua tukawa kwenye mti mmoja mkubwa sana , chini palikuwa na moto mkubwa
uliokuwa unawaka kwa kasi huku waliouzunguka moto ule wakiwa wanacheza ngoma ya
kienyeji.
Kufika
kwetu kukasababisha wasitishe ngoma na kuungana na sisi, wote tukasimama mstari
mmoja.
Tukiwa
mstarini, mzee mmoja akasimama mbele na kusema kuwa, mkutano ule ulikuwa ni
maalum kwa ajili ya kunisimika mimi kuwa kiongozi wa kundi mojawapo la wachawi
akidai naweza.
Nilinyoosha
mkono ili kupinga, lakini wachawi wote walikataa wakisema aliyoyaongea bosi wao
ni ya kweli kabisa.
Basi,
nilipitishwa mbele huku nikiwa sijui itakuwaje na wachawi wengine
walinisindikiza huku wakipiga makofi kwa furaha ya mimi kusimikwa.
“Haya,
piga magoti hapa,” yule mzee aliniamuru.
Nilipiga
magoti kwa unyenyekevu wa hali ya juu huku nikishikanisha mikono kama
ninavyokuwaga mbele za Mungu wangu.
Yule
mzee alinishika kichwa, pale pale mwili wote ukabadilika, nikajiona shujaa,
jasiri, sina woga na wala siogopi kitu cha kufikiria au kuonekana.
Kisha
akaanza kusema maneno ya kilugha na sijui alikuwa akitumia lugha gani.
Alitumia
muda wa kama dakika tano kusema kilugha alipokuja kubadilisha, akasema
Kiswahili na pale pale nikahisi nipo usingizini, nikaota ndoto.
Nilikuwa
nikipita kwenye kundi la watu nikiwa uchi wa mnyama, lakini watu walikuwa
hawanioni kama napita na nikaelekea kwenye ukingo wa barabara huku nikiwa
nawashika vichwa watu niliokuwa nawapita.
Hakuna
aliyejua hata kwa dalili kama kuna mchawi anapita katikati yao, hivyo nikajiona
ni jasiri na mjanja kuliko wajanja wengine wote wa dunia hii ya mambo na
vituko.
Niliposhtuka
kutoka katika ndoto hii, nilijiona nipo bado chini na wachawi wenzangu
wakiniangalia kwa macho ya ushindi.
Nilisimama
haraka, nikasema:
“Si
muda wa kupoteza huu, wako wanaojifanya wanajua, lazima wakatoke uhai.”
“Ndiyo,”
wachawi wakaitikia.
“Na
sasa kila wote mjipange vikundi vitano, vya watu wanne wanne na kwenda
kukabiliana na uovu huu, mume makini sana,” nilisema.
“Sawa,
tutakuwa makini,” walisema kwa pamoja.
Nilipomaliza
kusema, niliwachagua wachawi watatu na mimi wa nne, wengine wakachaguana hivyo
hivyo, safari ya kwenda kuvamia nyumba za wale watu waliojifanya wana maswali
mengi kanisani ilianza pale pale huku mimi nikiwa jasiri kabisa, siogopi mtu
wala sihofii maisha yangu ya baadaye.
“Mtakuwa
mnanifuata mimi ninavyofanya, sawa jamani?” Niliwaambia watu wangu huku
tukisonga mbele.
“Sawa
mkuu.”
“Nilitembea
kukanyaga ardhi huku wachawi wakinifuata kwa nyuma, kila nilipotoa mguu, nyuma
yangu alikanyaga mtu.
Tuliingia
kwenye nyumba moja ya miongoni mwa wale watu waliosimama kuuliza kule kanisani.
Wote
tulifikia sebuleni, nikasimama na kuinua mikono huku nikisema kila jicho la mtu
aliye ndani ya nyumba hii lisituone, hata kama lina nguvu.
Nilipomaliza,
nilitangulia mbele, nikasimama kwenye mlango wa chumba, lakini hatukujua ni cha
nani.
Nilichofanya,
niliufanya mkono kwa ishara kama nafungua pazia la dirisha ili mwange upite,
pale pale tukaona ndani ya chumba, walilala watu watatu kwenye kitanda
kimoja kidogo, lakini tukajua ni watoto.
Mimi
nikageukia mlango mwingine ambao nao ulikuwa umefungwa, nikafanya vile vile
kama mwanzo, mlango na ukuta vikayeyuka, chumba kikawa wazi.
Kitandani
walilala watu wawili, tukajua ni mke na mume. Nikiwa kama kiongozi wa msafara,
sikutaka tuingie ndani, nilinyoosha mkono, nikafanya ishara kama ya kuwaita
waje pale mlangoni tuliposimama sisi wachawi.
Nilikuwa
nachezesha kiganja kwa staili ya kuita, nachezesha, nachezesha, mpaka wakainuka
kitandani na kukakaa. Walifanya hivyo kwa pamoja, yaani mke na mume.
Walitutumbulia
macho, nikajua wanatuangalia sisi, wakakaza macho sana kwetu, lakini hakuna
aliyeonekana kututambua. Nikazidi kuwaita kwa kutumia ile ishara ya mikono.
Taratibu
walianza kutoka pale kitandani huku wakiziacha shuka zao mpaka waliposimama
wima wakasita kutembea. Ilibidi nitumie tena njia ile ile ya kuwaita kwa ishara
ya kiganja cha mkono, wakaanza kutembea kuja mpaka mlangoni.
Mambo
hayo yalikuwa yakifanyika kwa mwendo wa pole pole sana mpaka wakatufikia, na
mimi nikagueka, wachawi wenzangu nao waligeuka, wote tukaanza kutembea kwenda
nje ya nyumba hiyo.
Ulikuwa
uwazi mkubwa nje, ni eneo ambalo unaweza kujenga nyumba hata mbili. Nilisimama
na kuwaambia wenzangu watengeneze mduara, wakatii.
Mduara
ule uliwaweka kati wale watu wa familia tuliowatia ndani kwao. Wakiwa kati,
niliinama na kuchota mchanga, nikawarushia, ukawamwagikia, wale watu wakawa
wadogo kama mpira, nilikuwa wa kwanza kuwafuata na kuwapiga teke kama mpira,
wachawi nao wakaja na kuanza kuwacheza kama mpira. Ikawa vurugu ndogo pale nje,
huyu anapiga, yule anadaka, yule anaurusha.
Tulifanya
hivyo mpaka kunakaribia kucha, kama kwenye saa tisa na nusu usiku, nikasitisha.
Nilichota mchanga na kuwamwagia tena, wakarudi katika hali zao za kawaida.
Nilitangulia
ndani, wakafuata wale wana familia, baadaye wakaja na wachawi wenzangu.
Tuliwaingiza
hadi chumbani kwao, sisi tukasimama pale mlangoni, wao wakaenda mpaka
kitandani, wakapanda na kulala tena kwa kujifunika gubi gubi.
***
Asubuhi,
kwenye saa tatu nilitoka kwenda mjini, njiani nilisimamishwa na mwanamke mmoja,
akanisalimia vizuri sana.
“Padri,
umesikia uchawi unavyoshika kasi kwenye eneo lako?” Yule mwanamke aliniambia,
nikajifanya kushangaa, lakini nilishangaa kweli, maana sikujua alikuwa na maana
gani.
“Imekuwaje
tena?” Nilimuuliza nikimkazia macho.
Aliniuliza
kama namfahamu mzee…(jina).
“Ndiyo
namfahamu, kafanyaje?”
“Basi,
wachawi wamewaingilia usiku wamewachukua na kwenda kuwalimisha usiku kucha,
wameamka asubuhi wakiwa wamechoka sana, wamechafuka pia.”
Nilijifanya
kushtuka na kwamba siyajui hayo huku ukweli ni kwamba, kila kitu alichokiaongea
mimi ndiye nilikuwa kinara ingawa si kweli kwamba tuliwalimisha.
“Sasa
waliwatambua?”
“Hapana,
mchawi unaweza kumtambua?”
“Kweli
huwezi.”
“Eee,
mchawi hata akiwa baba yako au mama yako, anaweza kukuingilia na usimjue, labda
kama una malaika wakali,” alisema.
Tuliagana,
akaendelea na safari yake na mimi na safari yangu. Mbele nikasimamishwa na mzee
mmoja, huyu mzee tunaelewana sana kupita wote wanaoabudu katika kanisa lile.
“Bwana
nilikuwa nataka kuja kwako,” alisema.
“Sasa?”
“Sasa
basi, labda niongee hapa hapa.”
“Ongea
mzee wangu.”
Alianza
kwa kuniambia kuwa, kuna watu wanajiandaa kwenda kwa Askofu kutoa malalamiko
kuhusu siku ambayo mimi nilipanda madhabahuni na pajama badala ya mavazi ya
kitumishi.
Nilishtuka
sana kusikia hivyo, nikamuuliza majina ya hao wazee, miongoni mwao ni wale wote
waliosimama siku hiyo na kujifanya wanajua zaidi, akiwemo yule tuliyemcheza
mpira yeye na mkewe usiku.
“Aaa,
sasa kwani kuvaa pajama jamani si bahati mbaya tu, wao walichukuliaje?”
“Wao
walichukulia ulikuwa unatuwangia. Na hivi sasa kanisa limegawanyika, wengine
wanasema wewe ni mwanga, wengine wanakataa, Padri hawezi kuwa mwanga.”
“Wewe
unanichukulia mimi ni nani?” Nilimuuliza yule mzee.
“Ni
mtumishi wa Mungu aliye hai.”
“Sawa,
usimwambie mtu maneno hayo, waache wafikirie hivyo hivyo.”
Tuliagana, akaondoka zake lakini mbele kidogo,
nikasimamishwa na mwanamke mmoja, mzee sana, yaani bibi kizee, sijawahi kumwona
hata siku moja. Lakini kwa rika langu angeweza kuwa mama yangu mzazi.
“Shikamoo mama.”
“Marhaba, hujambo mwanangu?”
“Sijambo mama, haya unasemaje?”
“Ah! Nina usemi basi, njaa tu.”
“Hujala mama?”
“Nimekula, tena nimeshiba sana ,” alinijibu.
“Sasa njaa ya nini?”
“Nyama.”
“Nyama! Nyama gani mama, ya ng’ombe?”
Badala ya kunijibu, alinisogelea hadi mlangoni kabisa kwenye
gari, akanyoosha shingo ili kunifikia sikioni.
“Nyama nzito.”
“Mh! Mama, mbona sijakuelewa, nyama nzito ni ipi?”
Inaendelea!!!!!!!!!!!!!!!! Usikae mbali na Irene Mwamfupe Ndauka pande hizi.
--------------------------------------------------------------
PADRI MLA NYAMA ZA WATU-03
PADRI MLA NYAMA ZA WATU-03
“Ile yenye minofu
minene.”
“Mbona siijui, ya nguruwe?”
“Hapana, ya mtu! Najua unaweza kufanya nikapata.”
Damu zilinisisimka mwili mzima, nikahisi kupoteza fahamu
huku nikiwa nawaza yule mama alinifikiriaje au alisikia nini kuhusu mimi mpaka
kusema maneno yale.
“Sasa mama, mimi nyama ya mtu nitaipata wapi?”
“Popote pale.”
“ Kama wapi?” Nilimuuliza.
“Utanipa hunipi?” Aliuliza kwa sauti ya juu sasa.
Nilitaka kufunga kioo cha gari niondoke, lakini kwa vile
sikuwa nimemjua kiundani sana, niliamua kuacha.
“Nataka uniletee nyumbani kwangu usiku wa leo.”
“Wapi?”
“N’takuonesha,” alisema huku akianza kutembea kwenda upande
mwingine.
Sikujua atanionesha kwa mimi kumnyima nyama ya mtu au wapi
atapatikana ili nimpe hiyo nyama. Niliamua kumpuuza na kuendelea na safari yangu.
Nilifika njia panda moja ambapo nilitakiwa kwenda kulia,
lakini nikaona kuna mlima upande huo ambapo kawaida huwa hakuna mlima kama
nilivyoona pale.
Nilisimama kwa muda wa kama nusu dakika nikiuangalia ule
mlima. Ulianza kurefuka, ukaendelea kidogo kidogo huku ukiota majani ya kijani
pembeni. Urefu wake ulizidi hata mlima Kilimanjaro, lakini kufumba na kufumbua
ukafutika na kusindikizwa na sauti nzito.
“Huo urefu wa mlima ndiyo utakuwa wako katika ulimwengu wa
kichawi.”
Ile sauti ikakata, barabara ikaonekana kama kawaida,
nikaelekea upande huo.
***
Usiku wa siku hiyo, nikiwa nyumbani, nilianza kumfikiria
yule mama aliyesema anataka nyama ya mtu na alivyoondoka. Pia nilifikiria ni
kwanini baada ya kuondoka tu, mbele ya safari yangu ndiyo mlima mkubwa ukachipuka
kimaajabu?
Nikiwa bado nawaza, nikachukuliwa na usingizi mzito sana,
kuja kushtuka nikasikia filimbi ya kuitwa kwenye makutano yetu wachawi.
Nilisimama, nikageuka kuangalia kitandani, nikanyoosha mkono
pembeni na kuchukua shuka jeupe, nikalivaa kama taulo, kufumba na kufumbua
nilikuwa kwenye makutano yetu. Waliokwishafika walikuwa wakipiga ngoma na
kucheza huku wote waliokuwa wakicheza wakitumia mguu mmoja kutembelea eneo lile
lote.
Baada ya wachawi wengi kufika, nilisimama katikati yao na
kunyoosha mikono yangu juu, wakatulia, nikapiga makofi, wote wakaunga kwa
makofi.
“Pa pa pa pa pa!”
Kabla sijasema, mwanamke mmoja wa kanisani ambaye pia ni
mchawi alipita mbele akasimama jirani yangu, huku akiinamisha kichwa akasema:
“Unanikumbuka mkuu?”
Nilimwangalia kwa umakini sana, nikawaza kwanini anasema
vile wakati wachawi wote wa kanisani tunajuana na ni siri yetu.
“Nakufahamu vizuri sana ,” nilimjibu nikimkazia macho.
“Uliniona wapi?”
“Khaa! Wewe si tuko pamoja hapa na pia kule kanisani?”
Nilimhoji.
“Ndiyo najua, lakini je hukumbuki leo tumeonana mahali?”
“Sikumbuki, labda unikumbushe wewe.”
Alinikazia macho huku taratibu akianza kuzeeka na nguo
alizovaa zikianza kubadilika. Ilifika mahali akawa ni yule bibi kizee
aliyeniomba nimpatie nyama ya mtu na akasema atanionesha.
Mpaka hapo nilikuwa siunganishi tatizo la kuona giza na uwepo wa wale waumini
wawili wa ajabu ajabu.
“Mtumishi
wa Mungu kwema?” Nilisikia sauti ikiniuliza.
“Siyo
kwema kabisa.”
“Unaona
nini mbele?”
“Naona
giza .”
“Fumba
macho.”
Nilifumba.
“Haya
fumbua sasa.”
Nilifumbua.
Nikaendelea
kuona kama kawaida, lakini hakukuwepo na mtu yeyote aliyesimama mbele, nyuma,
kulia wala kushoto kwangu.
Lakini
pamoja na hali hiyo, niliisaka ile sauti akilini mwangu na kuigundua kuwa,
ilikuwa ya yule mzee aliyekaa jirani na wale watu wa ajabu.
“Khaa!”
Nilijikuta nikishangaa sasa.
Nilitembea
kwa mwendo wa haraka hadi kwa waumini waliokuwa wamesimama nje ya kanisa
wakiongea, wengine wakisalimiana na kuulizana maisha, kwani waumini wengi
huitumia Jumapili kuonana na kuongea mambo yao mbalimbali ya maisha.
Nilizungusha
macho kumwangalia yule mzee, nikamwona katikati ya watu akicheka na kupiga soga
na wazee wenzake, nikamfuata, lakini huku waumini ninaowapita wakinisalimia,
wengine wakionekana kutaka kujua kile kisa cha ndani ya kanisa.
Wakati
nakaribia kumfikia, nilijiuliza mwenyew, je, kweli kwa sauti ile kama angekuwa
ni yeye angeshafika katikati ya watu?
“
Kama ni hivyo, mbona sasa wakati nafumbua macho sikumwona mbele yangu?”
“Faza
pole na majukumu bwana,” yule mzee niliyekuwa namfuata alinisalimia na kuwawahi
wenzake wote aliyosimama nao. Sauti yake niliikumbuka vizuri sana , ndiyo ile
iliyonielekeza mpaka nikafumbua macho.
“Nimeshapoa
mzee wangu.”
Wazee
wengine nao pia wakanisalimia huku wakinipa mikono.
“Eti
mzee ulikuwa unasemaje?” Nilimuuliza yule mzee.
“Wapi?”
Na yeye aliniuliza.
“Hukusimama
na mimi pale mlangoni?”
“Mlangoni!
Wapi?”
“Kule
kwenye chumba?”
“Hata,
hapana.”
Wazee
wengine nao wakaonesha kunishangaa mimi, nikajisikia soni kwa nafasi yangu ya
u-Padri.
“Oke,
sawa basi.”
Nilitembea
kwenda kwenye ofisi yangu, lakini nyuma nikamsikia mzee mmoja akisema.
“Kwani
mzee Makwaya imekuwaje?”
“Sijui
chochote,” mzee Makwaya alijibu, hali ya mshangao na minong’ono ya chini kwa
chini iliendelea hadi ilipofika mahali nikawa siwasikii.
Kule
ofisini nilikuwa peke yangu, nikainamia mezani na kuwaza ile hali mwanzo hadi
pale ilipofikia nikaona giza nene mbele yangu.
“Hivi,
wale ni akina nani?”
“Ni
kwanini walinijia kanisani?”
“Wametumwa
au?”
Nikiwa
naendelea kuwaza hivyo, mara nikasikia sauti ndani ya ofisi.
“Unaendeleaje
mtumishi wa Mungu?”
Ilikuwa
ni sauti ya yule yule mzee Makwaya.
Nilishtuka
sana , nikaangalia kila kona ya ofisi.
“Hakuwepo
popote pale jambo lililonifanya nizidi kuogopa.
Nikiwa
natafakari huku kijasho chembamba kikinichuruzika, mara nikasikia kishindo
kikuu kwa nje kama vile kuna kitu kizito kinatua toka juu kwenda ardhini.
“Wewe
ni nani?” Niliuliza lakini sauti yangu ikitoka kwa woga.
Sikusikia
jibu wala sauti yoyote, ulipita ukimya, nikaendelea kutafakari huku kama
nashikwa na usingizi mzito na macho yangu hayaoni.
Ghafla
nilihisi kiumbe kusimama mbele yangu, nikajitahidi kufumbua macho.
Niliona
binadamu mwenye mguu mmoja, sikio moja, mkono mmoja, tundu moja la pua, jicho
moja amesimama mbele yangu akiachia tabasamu la kutisha.
“Kwa
jina la baba na la mwana na la…”
Kabla
sijamaliza kusema, alipotea mbele yangu, lakini bado macho yangu yakawa yana
kivuli chake kwani alikuwa wa kutisha sana sijapata kuona mfanowe.
Nilitamani
waumini wangu, hata mmoja tu aje, lakini ajabu ni kwamba hakukuwa na dalili na
si haikuwa kawaida yao, kwani mara zote, kila baada ya ibada waumini walikuja
ofisini kwangu na kueleza matatizo yao.
Ilifika
mahali nikahisi labda siko mahali salama, labda mimi niliona nipo ofisini
lakini kumbe sikuwa ofisini, ingawa nilipojaribu kutupa macho huku na kule,
akili yangu iliamini niko ofisini kwangu.
“Ngo
ngo ngo.”
Mlango
uligongwa.
“Karibu,
ingia,” niliitikia haraka.
Waliingia
wanawake wawili, wakiwa wamejitanda vitenge hadi kichwani na kubakiza uso tu.
Walikuwa wageni machoni pangu, nikiwa na maana sijawahi kuwaona hata siku moja
katika maisha yangu ya utumishi.
“Karibuni
sana akina mama.”
Hakuna
aliyejibu hata kwa kutingisha kichwa.
Waliangalia
wenyewe sehemu ya kuketi, wakaketi na kunikazia macho mimi.
Na
mimi niliwaangalia kwa uso wa kuwauliza shida yao . Lakini hakuna aliyesema
mpaka mimi nilipotoa sauti yangu.
“Niwasaidieni
nini akina mama zangu?”
Ajabu
iliyotokea hapo sijapata kuona wala kuisikia siku yoyote ile.
“Tuna
shida na wewe Padri,” alisema mmoja, lakini kwa sauti nene na nzito, ya
kiume.
Kwanza
nilishtuka sana kusikia sauti ya kiume ikitoka kwenye mwili ule mwembamba.
“Shida
gani mama zanguni?” Niliwauliza kwa sauti yenye woga woga kwani sasa nilianza
kuyaona maisha yangu kama yanajaribiwa.
“Tunataka
kuwa na wewe kazini kwetu,” alisema yule wa pili ambaye naye sauti yake ilikuwa
nene zaidi kupita ya wa kwanza hadi nikajikuta nikitetemeka.
“Mna…mnanitaka
kwe…kwenye kazi gani?” Niliuliza huku sauti yangu ikitetemeka kwa wasiwasi
mkubwa moyoni, jasho jembamba lilizidi kuchuruzika licha ya kwamba nilipoingia
niliwasha pangaboi.
“Ina
maana hutujui?” Wote walisema kwa wakati mmoja huku wakisimama na kujivua
vitenge. Nilishangaa sana kuwaona wamebaki na suruali na mashati, ina
maana kumbe ni wanaume kama mimi na walivaa vile kike ili kinipoteza
mawazo ya awali, niliwaza kwa wasiwasi huku nikiwakodolea macho pima.
“Mtumishi
wa Mungu aliye hai, tunakutaka kwenye kazi yetu bwana, eee?”
Mmoja
wao alisema akinisogelea nilipokuwa nimekaa mimi. Sasa niliibaini sauti yake,
ndiyo ile ya yule mzee muumini wangu.
“Nyinyi
si mliingia kanisani kwangu loe mkawa mnafanya maajabu?”
“Eee,
ni sisi,” walinijibu huku yule wa pili naye akisimama, akanisogelea na kusimama
sambamba na mwenzake.
“Sasa
mnataka nikafanye kazi gani na nyinyi, ya maajabu kama nyinyi?”
“Eee,
ndiyo,” walijibu wote.
“Mnatoka
wapi?”
Mmoja
wao akajibu:
“Tunatoka
kwa Mungu.”
“Yupi?”
Niliwauliza huku nikiwa nataka kusema ‘kwa jina la baba na la mwana…lakini
wakaniwahi wao kwa kusema:
“Mungu
kama wako, ametutuma kwako, amesema unatakiwa kupata nguvu ambayo na sisi
tunayo, kwa hiyo na sisi tunakupa nguvu hii, POKEA!”
Waliposema
‘pokea’ walinigusa kwa pamoja kwenye paji la uso, nikaanguka chini na kupoteza
fahamu.
Nilipokuja
kuzinduka, nilikuwa katikati ya pori lenye miti minene, mirefu na matawi yakiwa
juu sana .
Nililala
kwenye nyasi, pembeni yangu nilizungukwa na watu wengi ambao niliwaona miguu
tu. Kwa haraka haraka nilihesabu miguu ile na kupata idadi ya ishirini na sita,
ina maana watu waliosimama walikuwa kumi na watatu.
Niliinuka
ili kukaa, lakini mmoja wa wale watu alinizuia nisikae, niendelee kulala,
nikatii kwa vitendo na kurudi kujilaza majanini.
Ghafla
nikasikia sauti nzito, yenye tetemeko.
“Umetakiwa
kupokea nguvu ya kwetu,” ilisema ile sauti.
Yakapigwa
makofi pale, halafu ukafuatia ukimya wa muda mrefu kama vile nililala peke
yangu bila kuwepo mtu mwingine.
“Simama,”
ile sauti ilisema kwa haraka na kwa amri.
Nilijikuta
nasimama lakini nikiwa ndani ya ofisi yangu. Nilijiangalia na kujiona niko kama
nilivyovaa awali, kila kitu ndani ya ofisi kilikuwa sawasawa, hakuna hata kitu
kimoja kilichoharibika au kutokuwepo.
Hofu
ikaniingia kuhusu waumini wangu nje, kwamba kama walikuja wakakuta mazingira
yenye utata wataelewaje?
Niliusogelea
mlango na kushika kitasa, nikaufungua polepole na kuangalia nje. Hakukuwa na
muumini hata mmoja, hata mtoto.
“Khaaa!”
Nilishangaa.
“Ina
maana nimetumia muda mwingi sana ?” Nilijiuliza.
Niliangalia
saa ya ukutani na kugundua kuwa, wakati namaliza ibada ilikuwa saa nne na nusu,
muda ule naangalia saa ilikuwa saa saba mchana, ina maana kuingia kwa wale
watu, kupoteza fahamu hadi kuzinduka ilipita saa tatu?!
Mlango
uligongwa, akaingia mtu mmoja, simfahamu. Nilimkaribisha, akakaa kwenye fomu.
“Nikusaidie?”
“Ee
baba, mimi nimekuja uniombee,” alisema akijiweka sawasawa.
“Nikuombee
nini?”
“Uniombee
naumwa.”
“Unaumwa
nini?”
“Huwa
nikilala usiku naona watu wanakuja kunikaba.”
“Unaona
au unaota?”
“Naona,
wakati mwingine huwa napiga kelele kwa kuwaogopa.”
“Wewe
ni muumini wangu?”
“Hapana,
nasali mjini.”
“Sasa
kwanini usiende kwa mtumishi wa Mungu wa kanisa lako?”
“Ameshaniombea
sana lakini hakuna mafanikio.”
“Sasa
unaamini nini kuja kwangu, kuna mafanikio?”
“Naamini
yapo mtumishi.”
Nilihisi
ni miongoni mwa wale watu walionijia na kunifanyia maajabu yao , lakini sijui
ni nini, kwani ghafla nilijawa na ujasiri wa kutoogopa lolote na kuamua kumwombea
kweli.
Nilisimama,
nikamtaka yeye apige magoti kisha nikamwekea mkono wangu wa kulia kichwani
kwake na kuomba sana mpaka akaanguka chini.
Alipokuja
kusimama, akasema anajisikia mwepesi, ana imani amepona kabisa.
“Usijali,
nenda kwa amani lakini jilinde na dhambi.”
“Sawa
Padri.”
Alipoondoka
tu, mzee mmoja, aliyevaa shuka jeusi kuzunguka kiuno, chini akiwa hana kiatu
wala sendoz, pekupeku, ju mabega wazi, mkononi alishika mkia wa mnyama,
alisimama mbele yangu bila kujua aliingiaje?
“Karibu
mzee wangu,” nilimkaribisha kwa ujasiri mkubwa sana , moyoni sikuwa na hofu
wala wasiwasi.
Pamoja na kuvaa kiajabu kama vile, lakini nilimwona kama mtu wa
kawaida sana kwangu.
“Fumba
kiganja cha mkononi,” aliniambia kwa amri.
Nikajikuta
nafumba bila kuhoji yeye ni nani na ametoka wapi na kaja kwangu kufanya nini.
“Fumbua.”
Nilipofumbua,
unga mweusi ulikijaza kiganja changu.
“Jipake
kidogo usoni.”
Nilijipaka
kidogo huku nikiwa nimeinama kuangalia chini.
“Unaona
nini?”
“Sioni
kitu.”
“Haya,
hiyo dawa ndiyo tunayotumia kufanyia kazi, tunapotoka usiku kwenda kazini kila
mmoja anakuwa na dawa hiyo, ndiyo inayosaidia watu wasituone…
“Fumba
kiganja.”
Nikafumba.
“Fumbua.”
Nilipofumbua,
sikuona ile dawa, kiganja kilikuwa cheupe kama mwanzo.
“Fumba
tena kiganja.”
Nikafumba…
“Fumbua.”
Nilipofumbua
mkononi, nusu kulikuwa na unga unga wa kijani nusu unga unga mweusi.
“Chota
huo unga kisha changanya.”
Nilitii,
kisha akaniambia nijipake kidogo usoni, nikafanya hivyo na kujikuta nakuwa
mwepesi kuliko kawaida ya siku zote.
“Unaona
nini?”
“Najiona
mwepesi sana .”
“Unaweza
kujaribu kupaa?”
“Nijaribu?”
“Jaribu
basi.”
Niliinua
mikono kama vile ndege anavyoinua mabawa, taratibu nilijiona napaa juu huku
miguu ikiiacha ardhi taratibu bila ridhaa yangu.
“Unaonaje?”
“Napaa
sasa.”
“Shusha
mikono.”
Niliishusha,
taratibu miguu ikakanyaga ardhi na kusimama kama mwanzo.
Baada
ya hapo yule mtu akapotea machoni pangu na kuniacha nikiwa na maswali kibao.
Nilijiweka
sawa, nikafunga madirisha ili kutoka, nikafunga mlango na kuondoka kabisa
katika eneo la ofisi.
Nilikwenda
kwenye makazi yangu, lakini kwa wakati huo nilijihisi mnyonge sana , mwili
ulikuwa hauna nguvu, macho hayaoni vizuri mbele na miguu mizito.
*
* *
Saa
saba za usiku, nilishtuka kutoka usingizini baada ya kushikwa na kuvutwa kidole
cha mguu wa kulia na mtu. Kulikuwa na giza kwa hiyo sikujua nani alifanya zoezi
lile.
Swichi
ya kuwashia taa haikuwa mbali na nilipolala, nikaiwasha chapchap, chumba
kilipojaa mwanga sikuona kitu, nikaendelea kulala.
Baada
ya muda nikawa katika ndoto.
“Wewe
Padri, unadhani utafanya kazi mpaka lini?”
“Mungu
apende,” nilijibu.
“Je,
asipopenda?”
“Atapenda
tu.”
“Kwanini
unafanya kazi lakini huna nguvu.”
“Nguvu
gani?”
“Ya
kiroho.”
“Kwa
sababu bado.”
“Bado
nini?”
“Wakati
wa kuwa na nguvu.”
“Ni
sasa.”
“Kwa
maana ipi?”
“Njoo.”
Nilimfuata
huyo mtu, akanishika na kunivuta hadi mahali, akasimama na kuniambia.
“Nenda
kaingie kwenye kanisa lile.”
Mbele
yangu kulikuwa na kanisa, nikaenda kuingia.
Lilikuwa
kanisa langu, waumini wangu, wake kwa waume wengine wamekaa wengine wamesimama.
Walikuwa wengi sana.
Mimi
nikapita hadi mbele kwenye madhabahu na kusimama pale.
“Wale
wenye matatizo waje niwaombee.”
Karibu
kanisa zima walipita mbele kuombewa.
Ule
wingi wao, nikaanza kuogopa kwamba nitaweza kweli?
Wa
kwanza nikamwekea mikono juu kichwani na kumwombea, pale pale aliposimama
akaanza kupiga kelele na kuanguka chini kisha akasimama akiwa amepona na
kurukaruka huku akimtukuza Mungu wake.
Inaendelea!!!!!!!!!!!!!!!! Usikae mbali na Irene Mwamfupe Ndauka pande hizi.
----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
PADRI MLA NYAMA ZA WATU-04
“Hee, hee nimekuwa mzima sasa.”
“Nenda usitende dhambi tena, sawa?”
“Sawa.”
Niliombea karibu kanisa zima, nilipomaliza nikawa natoka huku napigiwa makofi na waumini waliokuwa wamesimama kulia na kushoto kwangu.
“Padiri Padiri Padiri,” walisema wakipiga makofi, pwa pwa pwa.
Kufika nje, nikakutana na yule mtu aliyenichukua nyumbani.
“Umefanikiwa?”
“ Sana ,” nilimjibu.
“Umekubali?”
“Nini?”
“Kwamba wakati wa kuwa na nguvu ya kiroho ni sasa?”
“Nimekubali.”
“Haya, sasa twende kwa aliyekupa nguvu.”
“Kwa Mungu?”
“Wetu sisi.”
Tuliongozana hadi kwenye mti mmoja mkubwa, mrefu sana kwenda juu.
Chini walikaa watu wengi wakiwa kama wapo kwenye maongezi.
Kilichonishangaza miongoni mwa hao watu walikuwepo waumini wangu wa kanisani.
“Afadhali umekuja faza.”
“Faza nimefurahi sana kukuona.”
“Faza karibu sana .”
Wale waumini wangu wote walinikaribisha kwa furaha, amani na upendo wa hali ya juu.
Nilikaa sehemu ambayo kulikuwa na nafasi ya mtu mmoja, yule mtu niliyekwenda naye sikumwona tena alikopotelea.
“Bwaba umekuja huku, uko tayari kwa lolote?” Aliniuliza mzee wa kanisani ambaye sikuwa na mazoea naye.
“Kwani hapa ni wapi?” Nilihoji.
“Hapa ni kwa wachawi.”
“Wachawi!”
“Eee, umekuja kwa wachawi, kazini kwetu, karibu.”
Alipomaliza kusema, alikaa chini, akasimama sasa yule mzee ambaye siku ile kanisani walipoingia wale watu wawili wa ajabu, yeye alikaa katikati yao .
“Eee, nina kila sababu ya kujisifu kwa kupewa heshima hii ya kumkuza kazini mtu mkubwa kama huyu,” alisema yule mzee.
Yakapigwa makofi kwa muda wa dakika tano nzima huku yule mzee akiwa amesimama tu akisubiri yaishe ili aendelee kuongea.
Lakini kwa jinsi nilivyokuwa namwangalia mimi, alikuwa anaongea kwa kujiamini sana na hakuonekana kujali kama mimi ni kiongozi wake wa kiroho.
“Kwa hiyo kuanzia leo mtumishi utakuwa chini yangu ukizitii na kuzifuata amri zangu, sawa bwana mdogo?”
Nilimjibu kwa sauti ya unyonge sana :
“Sawa.”
Pale pale alitembea kuelekea nilikokuwa mimi, akaniwekea mkono kichwani.
***
Wiki moja ilikatika toka hayo yatokee, lakini hakukuwa na jipya jingine, sikuwahi kumwona mtu mwingine akinijia nyumbani wala kanisani ninapokuwa nafanya kazi za Mungu.
Lakini siku hiyo, nikiwa nimelala majira ya saa saba usiku, nilishtuka ghafla. Nikatupa macho mlangoni. Kwa sababu ya giza sikuona vizuri, ila dalili ya kama kitasa cha mlango kikifunguliwa.Nilinyoosha mkono hadi kwenye taa ya kitandani (bed switch) nikawasha kwa umakini sana ili mlio wa swichi usisikike.
Kitasa kikawa kinakaribia chini, lakini kikanata kwa muda. Nadhaani ni baada ya mimi kuwasha taa.
Hali hiyo ilinifanya nitoke kitandani na kusimama katikati ya chumba huku macho yote yakiwa kwenye kile kitasa mlangoni.
Huku taa ikiwa bado inawaka, kitasa kiliendelea kwenda chini, yaani kufunguka, lakini ilionekana aliyekuwa anakifungua yupo makini sana kwani kwa kukitazama haraka tu ilikuwa vigumu kujua kitasa kinafunguka kwa kwenda chini.Mara mlango ukaanza kusukumwa polepole na mimi nilisimama nikaza macho kujua nani aliyekuwa akifanya kazi ile. Wazo kwamba ni mwizi sikuwa nalo kwani nawajua wezi, wao ni papara au kushtukiza.
Mlango uliendelea kusukumwa mpaka ukawa wazi wote, yaani kama kuna mtu alisimama
kwenye korido angeona chumbani, lakini cha kushangaza hakukuwa na binadamu wala kiumbe chochote nyuma ya mlango.
Nilipotaka kuuliza nani mwenzangu, nikasikia sauti ya mtu kukohoa kwa kujibana. Halafu nikasikia mlio wa viatu, ko! Ko! Ko! Ko! Ukisikika kuingia ndani ya chumba, nikarukia kusimama pembeni kwani niliamini aliyekuwa akiingia angeweza kunikumba.
Mlio wa viatu kutembea uliposimama ukafuata mlio wa kufunguliwa kwa dirisha la chumba, na kweli likawa linafunguka hadi mwisho, halafu pazia ikawa inakunjwa na kufungwa katikati kama vile mkunjaji alitaka upepo uingie kwa vizuri.
Baada ya hapo, nikiwa nimesimama pembeni, mlio wa viatu ukatembea kwa mwendo ule ule wa ko! Ko! Ko hadi ukutani kwenye swichi, ghafla nikasikia tap na giza likatanda. Ina maana huyo mtu alizima taa.
Halafu mlio wa viatu ukaendelea tena hadi usawa wa kitanda, ukakwamba pale. Giza likiwa limetanda, nikasikia hali ya mtu anayepanda kitandani kwani kitanda kilitoa mlio Fulani na baadaye, kama baada ya dakika moja ikasikika sauti ya mtu kukoroma.
Niliamini ni uonevu usiokuwa na maana kwangu kwani sikuwa na kosa la kunifanya nishindwe kulala na kulala mtu mwingine, nilikasirika sana . Nikatembea kijeuri hadi ukutani na kuwasha taa.
Ile inawaka tu, ile swichi ya kitandani ikasikika ikizimika, tap! Kukawa giza tena.
Niliifuata kwa fujo ile swichi ya kitandani, nikaiwasha na macho yangu yakakimbilia moja kwa moja kitandani. Mtu mnene, mrefu alikuwa amejifunika shuka huku akiwa amenyoosha miguu na anaangalia juu, yaani amelala chali.
“Wewe ni nani?” Nilimuuliza bila woga.
“Ndiyo jina lako au msafiri unakwenda mahali?”
“Siendi popote.”
“Khaa! Sasa hapa kwako?”
“Hapana.”
“Sasa kwanini umefungua mlango bila hodi na umepanda kitandani kulala bila ridhaa yangu?”
“Nisamehe sana .”
“Basi ondoka.”----------------------------------------------------
PADRI MLA NYAMA ZA WATU-05
Kauli yangu hiyo haikupata jibu zaidi ya mlio wa kukoroma kusikika kama mwanzo.
Nilimsogelea yule mtu pale kitandani kwa lengo la kumfunua shuka na kumwona vizuri. Niliishika shuka kwenye ncha moja, nikaifunua kwa nguvu…
“Ha ha ha ha ha ha!” Alicheka sana yule mtu huku akitoka kitandani na kuficha uso kwa mkono mmoja.
Nilijitahidi sana kuhakikisha namwona uso yule mtu, lakini na yeye alikuwa akawa anaangalia ukutani huku akiendeelea na kicheko chake.
“Wewe ni nani?” Nilimuuliza kwa ukali kidogo.
“Ha ha ha ha! Msafiri bwana, si nilikwambia!”
“Umetumwa?”
“Hapana.”
“Umekuja tu mwenyewe?”
“Ha ha ha ha! Eee!”
Kusema ule ukweli nilichanganyikiwa, kwani sasa nikawa sijui ukweli upo wapi, kila ninachomuuliza ananijibu kinyume na matarajio yangu.
“Basi mimi naomba uondoke humu chumbani kwangu,” nilimwamuru.
“Ha ha ha ha ha! Sawa,” alisema akielekea mlangoni na kutoka kweli lakini nikiwa sijafanikiwa kuona sura. Kwa hiyo mpaka hapo nikawa sijui ni nani yule.
Alipovuka tu ukuta wa chumba changu, nikajikuta napata wasiwasi na woga tofauti na mwanzo alipoingia.
Nilifunga mlango ili nipande kitandani kulala, lakini kabla sijapanda, nikasikia vishindo ti ti titi! Watu kama sita walisimama katikati ya chumba changu.
“Mtumishi wa Mungu vipi? Habari za kulala?”
“Salama.”
“Aaa, tumetumwa kwako.”
“Na nani?”
“Aaa, vaa miwani yako kwanza kisha utuangalie vizuri.”
Nilipeleka mkono kwenye stuli ndogo iliyokuwa pembeni ya kitanda na kuchukua miwani, nikaivaa na kuwaangalia.
Walikuwa tofauti na nilivyowaona wakati wanatua. Walikuwa wamevaa viguo vyeusi (kaniki) kukatisha kiunoni kwenda chini ya mapaja, kila mmoja alionekana amekasirika na hana utani na usoni walipaka vitu vyeupe, kama si unga, basi chokaa.
“Unatuona vizuri sasa?”
“Ndiyo.”
“Basi ndivyo tulivyo, toa miwani.”
Nilipotoa tu, walirejea na kuwa kama walivyotua, wamevaa kawaida.
“Unatakiwa kuhudhuria mateso ya waumini wako usiku wa sasa,” mmoja wao aliniambia, wengine wakatingisha vichwa kama ishara ya kukubaliana na maneno ya mwenzao.
“Wapi?”
“Katika kila nyumba yenye muumini au waumini wako.”
“Ni mateso ya aina gani?”
“Utajua huko huko na huna hiyari katika hili, kwani ulishapata baraka zote za uchawi.”
Nilijikuta nasimama, naanza kutembea kuwafuata kutoka nje mpaka uwanjani mbele ya nyumba, wakaanza kutengeneza duara na mimi nikawa mmoja wa wanaduara.
Mmoja akapeleka mikono na kuwashika wa kulia na kushoto kwake, wengine wakafanya hivyo mpaka mimi. Tukawa tumekamatana mikono. Yule aliyeanza kushika, akainama kama dalili ya kusujudia, wengine wakafuatia na mimi pia, kufumba na kufumbua, tukajikuta tukipaa juu na kutua chini ya mti mkubwa wa Mvule. Sikumbuki tulitumia dakika ngapi kuwa angani na kushuka.
Milio ya ngoma iliyotawala pale ilinifanya niamini kuwa, kweli nilikuwa katikati ya maskani ya kichawi.
“Bila kupoteza muda sasa tunaingia mitaani, hasa kwenye nyumba za waumini wa kanisa ambalo padri wao tunaye kwenye kundi letu na kufanya kazi ya kuwatesa, sawa?” Sauti nzito, iliyokuwa ikisikika na kitetemeshi ilisema.
Nilipomwangalia msemaji huyo, ni mzee mmoja aliyekuwa amevaa kanzu ndefu nyeusi, juu, yaani kichwani alivaa pembe za mnyama, mkononi alishika mkia, pia wa mnyama.
“Sawa,” wenzangu waliitikia kwa sauti ya juu.
Kifupi mimi nilikuwa sijui kitu chochote. Nilikuwa sijui watafanyaje huko kwenye kutesa watu, sijui nani atakayeteswa, kama ni waumini wote pia sikujua. Ila, mzee mmoja alinifuata na kuniambia:
“Tuondoke mimi na wewe.”
Nikawa namfuata hadi kando kando ya ule mti mkubwa, akasimama ghafla hadi nikamkumba.
Kufumba na kufumbua, tulitua nje ya nyumba ya muumini wangu mmoja ambaye anamiliki mashine ya kusaga na trekta moja.
“Haa! Hapa si kwa..?”
Kabla sijamaliza kusema, yule mzee akaniambia kwa kunikatisha:
“Ulisikia tulivyoambiwa kule?”
“Kwamba?”
“Tunawatesa akina nani?”
“Waumini wangu.”
“Sasa unauliza nini?” Alinijibu huku akitembea kwa kurukaruka kwa mguu mmoja.
Alipoona mimi nimezubaa akanifuata:
“Jipige kifuani kwa mkono.”
Nikafanye hivyo.
“Hapo sawa sasa, nifuate mimi kwa kila hatua mpaka ndani na kuanza kazi, sawa?” Aliniuliza.
Tulikwenda hadi kwenye mlango mkubwa, nikadhani atagonga ili tufunguliwe, kumbe sivyo bwana.
“Kila ninachofanya mimi na wewe unaniiga, sawa?” Aliniambia akinigeukia, kwani nilikuwa nimesimama nyuma yake.
“Sawa.”
“Haya tunaanza sasa.”
Alijipiga tena kifua na mimi nikajipiga. Kufumba na kufumbua tukawa ndani, sebuleni.
“Sasa niigize kwa kila kitu.”
“Sawa,” nilimjibu kwa sauti ya chini kama ile aliyoitumia yeye kuniambia.
Alitembea kwa kurukaruka kwa mguu mmoja, huku mguu wa pili ukiwa unaning’inia tu. Kwa mimi nilivyoona, hakukuwa na sababu yoyote ya kutembea vile, ila kwa kichawi nadhani ni sawa na ni kawaida kwao.
Na mimi niliruka ruka kwa mguu mmoja huku mwingine ukining’inia hadi kwenye mlango wa kuingia kwenye vyumba, yule mzee akasimama, lakini kwa mguu mmoja.
Tulisimama vile mpaka mimi nikabadili msimamo, nikatumia mguu mwingine maana nilichoka sana .
Ghafla akaweka mguu mwingine chini huku akigeukageuka kuniangalia.
“Sasa tunaingia chumbani kwa baba mwenye nyumba, sawa?”
“Sawa.”
“Una swali lolote kabla hatujaingia?” Aliniuliza.
“Ndiyo.”
“Enhe, lipi hilo ?”
“Haaa…”
“Uliza haraka.”
“Sawa, hatutaonekana?”
“Wapi?”
“Tunakokwenda.”
“Kwani si nimekwambia kila kitu unaigiza kwangu?”
“Kabla sijaigiza je?”
“Hatutaonekana.”
“Basi, swali langu ni hilo tu.”
“Kwa hiyo huna swali jingine?”
“Sina na wala sitakuwa nalo.”
“Oke nifuate.”
“Niko nyuma yako.”
Aliinua mikono juu, akapiga makofi na mimi nikafanya hivyo hivyo. Kufumba na kufumbua tukawa tumesimama katikati ya chumba.
Yule mzee akanigeukia, akaniangalia lakini hakusema kitu. Mdomo akauangalizia juu na kufanya tendo kama anapuliza moto, na mimi nikafanya hivyo hivyo. Akamsogelea mzee mwenye nyumba aliyekuwa amelala usingizi mzito wa chali, akamkalia tumboni huku akijisotesha kuanzia kiunoni kwenda kifuani na kurudi.
Mimi nikawa mtazamaji tu, lakini yule mzee akaniangalia na kunipa ishara kwamba na mimi nimpandie mke wa yule mwenye nyumba ambaye alikuwa amelala kitanda kingine na mtoto mdogo kama wa mwaka mmoja.
Nilipanda bila kujiuliza maswali kwanini napanda, nikajisotesha kama alivyokuwa akifanya yule mzee, lakini nilipotua macho usoni kwa yule mama ambaye naye alilala chali, nikamjua kuwa ni muumini wangu mzuri pale kanisani.
Kusema ule ukweli niliumia sana moyoni, nikajihisi ni mtenda dhambi nisiyestahili msamaha wa aina yoyote ile.
Lakini ilinibidi niendelee tu na kazi niliyokuwa naifanya kwani ni jukumu ambalo nilishalivalia njuga sikuwa na budi kulimaliza sawasawa na safari yetu ya kuingia ndani ya nyumba ile.
Mara yule mzee alishuka kutoka kwenye tumbo la yule mzee mwenye nyumba huku akinifanyia ishara ya mimi pia kushuka.
Tulishuka wote, tukasimama tukiangaliana. Mara mwenzangu akaufuata ukuta sehemu ya kichwani ya yule mzee, akasimama na kumwinamia kisha akapeleka mkono hadi jirani na shingo yake na kuukunja kama vile ameshika shingo na kumkaba.
Yule mwenye nyumba akawa anarusharusha miguu kama anayeitafuta pumzi baada ya kuziba kwa pua na kinywa, huku akisema maneno yasiyojulikana:
“Mmmh! Mmmmmm! Mmm!”
Alivyokuwa akiendelea kubana mkono ndivyo na yule mtu alivyokuwa akizidi kulalamika, sasa akapeleka mikono kwenye koo lake na kujishika huku akizidi kulalamika.
Alichofanya yule mchawi, akawa anambana huku mkono mmoja anafanya kama anamtisha kwa ngumi ya uso yule mzee. Alipokuja kumwachia, akasimama pembeni yake kisha yule mtu mwenye nyumba akashituka kutoka usingizini na kukaa huku akikohoa sana .
“Mungu wangu, Mungu weee! Ooo! Mama,” alisema akiendelea kushika koo lake.
Akamwita mkewe kwa sauti ya juu, naye akashituka na kumuuliza kulikoni:
“Kuna nini mume wangu?”
“Nimekabwa vibaya sana .”
“Na nani?”
“Najua ni wachawi tu hao.”
“Umejuaje?”
“Wamenishika koo kwa kunikaba kisha wakanigiga ngumi za uso. Kwani huoni kama umevimba?”
“Nini?”
“Uso wangu?”
“Hata, ila macho kama mekundu.”
“Ni hao hao lakini mmoja kama nimemwona.”
“Unamjua?”
“ Kama namjua.”
“Ni nani?”
“ Kama ..!”
“Vipi tena mume wangu?”
“Tumbo nalo kama limejaa, ooo linauma sasa, wachawi hao mke wangu.”
Mara mkewe naye akaanza kulia huku akishika tumbo lake na kulalamikia.
Moyoni nilitamani sana yule mzee atokee ili akabiliane na zile tuhuma zile ambazo mimi zilinifika shingoni na niliingiwa na kinyongo na kazi ile ya kichawi ambapo awali niliambiwa hakuna ambaye angeweza kutuona wakati tukiwa kwenye matukio yetu.
“Eee Bwana niepushe na aibu hii, sirudii tena mimi, nimeshajirekebisha,” nilisali kimoyomoyo peke yangu pale mbele ya madhabahu. Nikajikuta nakohoa pia bila sababu.
Ghafla mzee mwingine akanyoosha kidole, wakawa wawili sasa. Lakini pia wakati yule akiendelea kuongea na vile vidole viwili vikiwa juu, mke wa yule mzee aliyekuwa akiongea naye akanyoosha kidole.
“Mbaya zaidi, watu waliotuingilia kutufanyia hivyo huwezi kuamini ukiambiwa, hii ni aibu kwa kanisa na pia ni kufa kiroho. Mungu hawezi kuuvumilia ubaya huu.”
Wakati anazidi kubomoa, mimi haja ndogo ilinibana, nikawa navumilia tu.
Nilitamani ardhi ipasuke, mimi niingie ndani mwake na nisionekane tena maishani mwangu. Mwili ulinitetemeka, akili ikanipotea, nikawa sijui niamue nini.
“Hali ikiwa hivi kuna siku humu huku kanisani watu watashikania mapanga kutoana damu, hakiyanani vile.”
Yule mzee alipomaliza kusema hayo, akaa ghafla kama vile alishikwa na kukalishwa kwa nguvu.
Nikataka kusema muda umekwisha, lakini mzee mmoja kati ya wale walionyoosha vidole alisimama hata bila kuruhisiwa, alipoona mwenzake amekaa tu.
“Nashukuru sana na mimi kwa kupata muda huu. Zamani uchawi hapa kanisani ulikuwa ni msemo tu, si kitu ambacho kinatingisha, lakini mimi nina habari kwamba, sasa uchawi umo ndani kabisa ya hili kanisa, tena washiriki ukitajiwa majina unaweza kubisha hadi unaanguka chini.
“Mimi kama nitapata baraka za waumini wenzangu niko tayari nitaje majina, lakini nilindwe.”
Nilimwangalia vizuri yule mzee nikamwona kama ametumwa, kwani wakati anaongea, hakuwa ananiangalia mimi, wala mtu mwingine, alaiinama tu huku akibwabwaja.
“Sema.”
“Wataje.”
“Waweke wazi bwana.”
“Tutajie.”
“Tuambie.”
Hayo yalikuwa maneno ya waumini wa kanisa lile ambayo yalinichanganya kabisa. Baadhi ya waumini wakawa wanainama kunong’onezana huku wakiniangalia kwa kuniibiaibia.
“Niwataje?” Yule mzee aliuliza tena kwa sauti ya juu.
“Watajeeee.”
Wakati huo, yule mzee mwingie na yule mke wa yule wa kwanza, vidole vyao vilikuwa bado juu wakiomba nafasi ya wao kuongea.
“Eti niwataje?”
Inaendelea!!!!!!!!!!!!!!!! Usikae mbali na Irene Mwamfupe Ndauka pande hizi.
makala yako ya ukwel dada
ReplyDeleteSante Mohamed!
ReplyDeleteStory nzuri sana lakin mbna inajirudia huku chini
DeletePart two hiyo hapo
ReplyDelete