Baadhi ya wabunge wa CHADEMA, wamehusishwa na mauaji ya Mwenyekiti wa
Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wa Kata ya Ndago wilayani Iramba mkoani
Singida, Yohana Mpinga (30).
Akizungumza bungeni jana, Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba alisema kabla ya mauaji hayo anayoona yalipangwa, alitishiwa kuuawa kwa kutumiwa ujumbe mfupi wa simu na wabunge hao kutokana na mijadala yake bungeni.
Nchemba alitoa madai hayo alipoomba Mwongozo wa Spika akitumia Kanuni ya Bunge ya 47 inayohusu kusitishwa kwa shughuli za Bunge ili kujadili jambo la dharura la Taifa.
Sehemu ya ujumbe huo ambao Spika wa Bunge, Anne Makinda alimzuia kuusoma, unamtaka Mwigulu asijifanye anajua, kwani mwenzake Chacha Wangwe (Marehemu Mbunge wa Tarime) alijifanya anajua na “sasa yuko wapi?” Ujumbe mwingine ulimwambia kuwa skafu ya Bendera ya Taifa anayovaa shingoni, itageuka sanda yake.
Akiomba Mwongozo huo, Nchemba alisema kutokana na tukio la kinyama lililotokea jimboni mwake juzi la kuuawa kwa Mpinga na watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa CHADEMA, aliomba Bunge liahirishwe ili suala hilo lijadiliwe kwa kina.
“Naomba tuahirishe Bunge tujadili suala hili, kwa kuwa inaonesha kilichotokea kilipangwa, nilipokea SMS (ujumbe mfupi) katika simu yangu za kunitishia kuuawa kutokana na mijadala ninayochangia bungeni na namba za walionitumia SMS zimebainika kuwa ni za wabunge wa CHADEMA,” alisema Mwigulu.
Alisema namba za simu zilizokuwa zikitumika kumtumia ujumbe huo mfupi alizipeleka Polisi na tayari wabunge hao waliomtishia maisha wamebainika majina yao na hatua zaidi zitachukuliwa.
Pamoja na kukataa kutaja majina ya wabunge hao, Nchemba nje ya Bunge alionesha ujumbe mfupi aliotumiwa ambao unasema:

- “Hivi wewe unajiamini nini? Kwa nini unatusonga hivyo? Unadhani nchi hii ni ya CCM milele? “Utajutia kimbele mbele chako. Unadhani ni wewe tu unayejua sana? Ukabila kwenye chama chetu unakuhusu nini, hata kama ni kweli, kwa nini kututia aibu?”
- “Hata ufanyeje, 2015 tunaingia Ikulu na mjengoni tutajaa, Wangwe alijifanya kujua kama wewe leo yuko wapi?”
- “Bendera unayovaa kila siku shingoni itageuka sanda yako. Kila mtu ana haki ya kuvutia kwake, lakini wewe umezidi. Hatuwezi kuitema keki tuliyokwishaionja”.
- “Fahari yako leo, itageuka kilio kwako. Utatutambua.”
Hata hivyo, Spika Anne Makinda alimkatisha Nchemba asiwataje kwa majina wabunge hao waliomtumia ujumbe mfupi wa kutishia kumwua na kumtaka aiachie Polisi ishughulike na jambo hilo, ambapo pia aliukataa Mwongozo wa kuahirisha kikao.
via gazeti la HabariLeo
No comments:
Post a Comment