Askofu
Paschal Willium Kikoti wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda amefariki
dunia usiku wa kuamkia leo katika hosipitali ya rufaa Bugando jijini
Mwanza alikokuwa amelazwa.
Kwa mujibu wa Makamu wa Askofu wa Jimbo la Mpanda, Padri Patrick Kasomo kifo chake kimetokana na ugonjwa wa shinikizo la damu na kwamba mwili wake utawasili kesho alhamisi kwa taratibu za mazishi.Padri Kasomo amesema mazishi wa mwili wa Askofu Kikoki unatarajia kuzikwa siku ya jumamosi wiki hii kwenye kanisa kuu la Mtakatifu Maria mjini Mpanda.
IRENE MWAMFUPE JAMIIBlog inawapa pole wakristu wote, ndugu jamaa na marafiki kwa kifo cha Askofu Kikoti. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Amina
No comments:
Post a Comment