Askofu Moses Kulola enzi za uhai wake.
Askofu Mkuu wa Kanisa la E.A.G.T na mhubiri wa kimataifa wa siku
nyingi, Moses Kulola amefariki dunia. Askofu Moses Kulola amefariki leo.
Mtoto wa Askofu Kulola, ambaye naye pia ni mhubiri wa kimataifa na
mchungaji wa kanisa la EAGT Lumala mpya, Mch. Daniel Moses Kulola
amethibitisha taarifa hizo kupitia katika akaunti yake ya Facebook. Kwa
kuandika hivi: "WATU WA MUNGU SALAAM, NINA SALAAM ZA MAJONZI. BABA YANGU
MZEE KULOLA AMEFARIKI MUDA SIYO MREFU."
Hivi karibuni marehemu alilipotiwa kulazwa katika hospitali ya
Bugando iliyopo mkoani Mwanza kwa matibabu kutokana na matatizo ya
kiafya yaliyokuwa yanamkabili lakini Agosti 22 mwaka huu mwanaye Mch.
Daniel Moses Kulola alieleza kuwa baba yake karuhusiwa baada ya kupata
nafuu.
MUNGU AILAZE ROHO YA ASKOFU KULOLA MAHALI PEMA PEPONI. AMEN
MUNGU AILAZE ROHO YA ASKOFU KULOLA MAHALI PEMA PEPONI. AMEN
Wana wa Mungu, tunasikitika katika hili mzee wetu amemaliza safari yake. Imefanya huduma ya Injili kwa kipindi chote cha maisha yake, alikuwa ni baba wa imani kwa watumishi wengi. Mungu aitie nguvu katika katika utumishi huu na pia familia kwa ujumla wake
ReplyDelete