“Wakili Tundu Lissu amenituhumu kuwa nimehongwa magari 2
na mheshimiwa Nimrod Mkono. Mimi ninamiliki gari moja mbili, freelnder
ninayotumia Dar Es Salaam na Toyota Carina ninayotumia jimboni. Tuhuma
hii haimo katika tuhuma nilizotuhumiwa nazo na kuandikiwa na chama ili
kujibu. Kama Tundu lissu anadhani tuhuma hii ana ushahidi nayo wa
kutosha aiongeze kwenye tuhuma walizoniandikia ili niweze kujitetea
kwenye vikao, vinginevyo ni mipasho tu. Nawapa changamoto Tundu lissu na
wenzake kama wana tuhuma Mpya dhidi yangu waniandikie kwa mujibu wa
taratibu. Tuhuma nilizo nazo hivi sasa na ambazo nimezikatia rufaa
katika Baraza Kuu zinahusu mkakati wa kugombea uenyekiti Taifa na kutaka
mahesabu ya chama yakaguliwe na CAG.”
Aliandika Zitto Zuberi Kabwe katika ukurasa wake wa Facebook Haya yametokea baada ya Mbunge huyu wa Kigoma kudai vyama vikaguliwe mahesabu kwa mjibu wa sheria za nchi na utaratibu wa utawala bora hali iliyopelekea kupigwa vita kuanzia ndani ya chama chake mwenyewe mpaka chama tawala cha Mapinduzi.Baada ya waandishi kuhoji juu ya tuhuma zinazomkabili alijibu
“…… Jibu langu ni jepesi sana, tuhuma hizo hazipo katika mashtaka dhidi yangu waliyoniandikia wao wenyewe na kunitaka nijibu mbele ya kamati kuu. Kama wanaona tuhuma hizo zina uzito waandike nitoe Maelezo yangu kama mashtaka mapya. Waitishe Baraza Kuu la chama ili lisikie rufaa yangu vinginevyo wakae kimya maana uzushi na kubwabwaja hautawasaidia.
Malicious people are simply manipulative and survive of short term basis. Inspiring people look long term.”
Na baada ya kusema hayo aliamua kupasua jipu na kusema yafuatayo;
My take: Kwa namna mambo yanavyokwenda kwani Zitto anaendelea kkutoa siri nzito zinazohusisha chama chake na chama tawala anaweza akatolewa muhanga kwa kufanywa kitu kibaya.Awe mwangalifu katika kipindi hiki hasa anapotoa tuhuma hizi zinazoenda kukisambaratisha chama na kukiua.
No comments:
Post a Comment