Global Publishers & General Enterprises LTD, kampuni inayoendelea kukua katika tasnia ya habari nchini, kwa mwaka 2014 ina nafasi za kazi za uandishi mahiri wa habari kwa wenye elimu, ujuzi na sifa zifuatazo:
ELIMU NA SIFA:
Wanahitajika waandishi mahiri wenye elimu ya Degree, Advanced Diploma au Diploma ya uandishi wa habari, wenye ufahamu wa kutosha kuhusu masuala ya habari za michezo na burudani ndani na nje ya Tanzania.
Kwa wasiokuwa na ujuzi lakini wenye vipaji, elimu ya kutosha na mapenzi ya dhati na tasnia ya uandishi, watapewa nafasi ya kujifunza ili kujipatia uzoefu.
Aidha, mtarajiwa awe kijana aliye tayari kuanza kufanyakazi wakati wowote. Awe anajua kutumia kompyuta. Awe na uwezo wa kufanyakazi bila kusimamiwa, mwenye ubunifu, aliyetayari kufanya kazi usiku na mchana. Mwenye kumiliki na uwezo wa kutumia kamera ana nafasi nzuri ya kuchaguliwa kwanza.
Mwisho:
Kama unafikiri unakidhi vipengele vyote vilivyoainishwa hapo juu, tuma barua yako ya maombi ya kazi haraka, iliyoandikwa kwa mkono wako ukiambatanisha na maelezo yako ya kikazi (CV) na nakala ya cheti/vyeti
vyako, kwa:
MENEJA MKUU
S.L.P 7534
DAR ES SALAAM
Wasilisha mwenyewe ofisini kwetu, Sinza Bamaga (Nyuma ya TSN
Petrol Station). Simu: 2773356/7. Mwisho wa kupokea maombi ni
Januari 15, 2014.
No comments:
Post a Comment