Laurent Samatta
Habari ya mjini kwa sasa ni Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani
unaotarajiwa kufanyika Oktoba, 2015 ambapo Watanzania wote watatumia
haki yao ya msingi ya kupiga kura, kuwachagua viongozi wanaowataka.
Showbiz Plus imewatafuta wasanii wa tasnia tofauti Bongo na kuwauliza
mtazamo wao juu ya uchaguzi huo na hali ya upepo wa kisiasa Bongo
ambapo wamefunguka kama ifuatavyo:
MRISHO MPOTO ‘MJOMBA’
Mkali huyu wa kughani na tungo za Kiswahili, yeye amefunguka:
“Kwanza kabisa uchaguzi umegawanyika sehemu mbili, kuna viongozi ambao
wanahitaji madaraka na kuna wengine wanahitaji kufanya biashara.
“Vilevile hata wapiga kura nao wapo wanaojiandaa kufanya biashara kwa
kujua kwamba wakimpigia kura kiongozi fulani, watanufaika na kitu
fulani, tofauti na zamani ambapo utii na nidhamu kwa viongozi na wapiga
kura ulikuwa mkubwa.“Sasa hivi hata wasanii nao wanafanya biashara kwa
kutazama mgombea gani ana fedha ndiyo wanaenda kumfanyia kampeni, kwa
hali hii tutegemee kuwa uchaguzi utakuwa wa kibiashara na si kutafuta
kiongozi bora kwa taifa.”
EMMANUEL ELIBARIKI ‘NAY WA MITEGO’
Msanii huyu wa Bongo Fleva ameeleza mtazamo wake kuelekea uchaguzi mkuu:
“Uchaguzi wa mwaka huu unaweza kuwa mgumu sana kwa sababu watu
wameelimika tofauti na zamani ambapo watu walikuwa wanafanya mambo bila
kujielewa. Vijana na watu wengine wameelimika na kujua kiongozi gani
anafaa na nani hafai.“Ule ujanja wa kusema baadhi ya vyama vitaiba kura
nadhani hilo litakuwa gumu sana mwaka huu kwani kila mtu anapiga kura
akiwa anajua haki zake za msingi.”
KHADIJA KOPA ‘MALKIA’
Malkia huyu wa mipasho,
ambaye pia ana uelewa mkubwa kwenye mambo yanayohusu siasa alisema: “Kwa
kweli mi naona mwaka huu utakuwa mzuri kwa upande wa wanawake kwa
sababu katiba inayopendekezwa ikipitishwa kutakuwa na usawa katika kila
nafasi ya uongozi kati ya wanaume na wanawake.
“Nawasihi wanawake kama wapo wanaoweza kuongoza nafasi mbalimbali
wajitokeze kupigania nafasi hizo kuanzia urais, ubunge mpaka udiwani.
Naamini tutaweza kufika mahali ambapo na sisi tutajivunia kuwa na
viongozi wengi wanawake.”
KULWA KIKUMBA ‘DUDE’
Msanii huyu wa filamu
alisema “Mtazamo wangu kwa kweli mi naona uchanguzi wa mwaka huu utakuwa
mgumu kuliko changuzi zote zilizowahi kutokea ndani ya taifa hili, kwa
sababu watu wengi wameamka na wanajua nini wanafanya.
“Lakini pia wananchi wanaanza kuwakataa baadhi ya vigogo wanaokuja
mtaani kwa mbwembwe na baada ya kupata kile wanachokitaka wanakimbia na
kujali maslahi yao binafsi, kwa hali hii baadhi ya vigogo wataanguka
sana kwenye nafasi zao, tumeona kwenye Serikali za Mitaa mambo
yalivyokuwa, tusubiri lakini uchanguzi utakuwa mgumu sana, vijana wengi
walikuwa hawapigi kura lakini sasa wamejua maana halisi ya kura zao”.
AMINI MWINYIMKUU
Msanii huyu wa muziki wa Bongo
Fleva naye alifunguka: “Uchaguzi wa mwaka huu mimi naona utakuwa mzuri
kwa sababu kila chama kina mashabiki na wapenzi wake na kikubwa ambacho
kinaonekana ni kwamba wananchi wengi wameelewa nini maana ya kupiga kura
kwa lengo la kupata viongozi ambao wataleta maendeleo ndani ya taifa
letu.”
AMRI ATHUMANI ‘KING MAJUTO’
Mkali huyu wa komedi
Bongo, naye alikuwa na mawazo yake: “Mwaka huu uchaguzi utakuwa wa raha
na starehe maana tunahitaji kiongozi bora na kama inavyojulikana kwamba
CCM ni chama kizuri hivyo kila kitu kitakuwa sawa na watu watafurahi,
nadhani kila jambo halitakuwa gumu katika kufanikisha hili kuanzia ngazi
ya urais, ubunge na hata udiwani.
BABY MADAHA
Mwanadada huyu anayefanya poa kwenye
gemu la Bongo Fleva, alifunguka: “Naamini kuwa katika uchaguzi wa mwaka
huu bado nafasi ya wanawake kwenye urais itakuwa ni ndogo lakini kwa
upande wa nafasi za ubunge na udiwani wanaweza kufanya vizuri zaidi na
watu wakashangaa kuona viti vingi vikichukuliwa na wanawake wenye kiu ya
kuleta maendeleo ndani ya taifa letu. Mi naamini wanawake tunaweza.”
EMMA-NUEL SIMWINGA ‘IZZO BUSINESS’
Mkali huyu wa
Bongo Fleva kutoka Nyanda za Juu Kusini, mkoani Mbeya, naye amefungukia
uchaguzi mkuu kwa kueleza kuwa anaamini uchaguzi wa mwaka huu utakuwa
wa amani na utulivu.
“Kuhusu mambo mengine kama vurugu na machafuko, hivyo havina nafasi kabisa,” alisema.
Friday, February 27, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
HABARI MBALIMBALI
‘Dk. Cheni’
‘Sharo Milionea
‘Thea’
African Women
AGNESS MASOGANGE
AK CLASSIC COSMETICS
ALI KIBA
Amanda Poshy
Ant
ANT LULU
Ashley Toto
Aunt Ezekiel
Aunty Ezekiel
AUNTY LULU
Azam Fc
Baby Madaha
BAHATI BUKUKU
Barnaba
BATULI
BBA
Beauty of the day
Belle 9
BI KIDUDE
BIBI BOMBA
Big Brother
Big Brother Africa
Bill Gates
BINTI KIZIWI
BOB JUNIOR
Bodi ya Filamu
Bongo Movie
Bongo Movies
CCM
CHADEMA
Chombezo
Christina Shusho
Chuchu hans.
Clouds Media Group
Club Bilicanas
DAR LIVE
DAVINA
Dayna Nyange
Diamond
Dida
Diva Loveness Love
Dj Ommy Crazy wa Maisha Club
DOGO JANJA
DOKI
DR.CHENI
DSTV
Dude
Dully Sykes
EBSS 2013
Elizabeth Michael
Epiq Bongo Star Search (EBSS)
ESHA BUHETI
Ester Bulaya
Feza Kessy
FIESTA 2014
Flaviana Matata
FLORA MBASHA
FLORA MVUNGI
Francis Cheka
GARDNER
GLOAL PUBLISHERS
GLOBAL TV ONLINE
H. BABA
Halima Mdee
HAMISA
Happy birthday
Hemedi
Hemedy Suleiman
HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE
Hoyce Temu
Huddah Monroe
HUSINA
IRENE PAUL
Irene Uyoya
ISABELLA
J film 4 life
Jack Chuz
JACK PATRICK
Jacob Steven ‘JB’
Jacqueline Dustan
JACQUELINE WOLPER
Jaji Khamis 'Kashi'
Jay Dee
JENNIFER KYAKA (ODAMA)
JIDE
JINI KABULA
JK
JO
Johari
Jokate Mwigelo ‘Kidot’.
JOTI
Joyce Kiria
Joyce Kiwia
JUX
K-LYNN
KADINDA
kaja
Kajala Masanja
Kapotive Star Singers
KATUNI
Kemmy
Kero Zetu
KHADIJA OMAR KOPA
KIKWETUKWETU
KILI MUSIC AWARDS
KOLETA
Lady Jay Dee
Lady Jaydee
Lake Oil
LAVEDA
Linah Sanga
Linex
Lisa Jensen
Loveness Diva
Lucy Francis Komba
Lulu
M2 The P
MABILIONEA
Madam Rita
MADELA
Magazeti
Mahusiano
Maimartha Jesse
MAINDA
MAISHA
Makala
Malkia Elizabeth
MAMTEI
MANDELA
MARIAM ISMAIL
Masanja Mkandamizaji
Mashindano ya Miss Tanzania
Matangazo
Matonya
MaxMalipo
MAYA
MELLIS EDWARD
MENINAH
MGOSI MKOLONI
Mh Halima Mdee
mic
Michezo
MILLEN HAPPINESS MAGESE
MISS CHANG'OMBE
MISS DAR CITY CENTER
Miss East Africa
MISS REDD'S IRINGA 2013
MISS TANGA 2013.
MISS TANZANIA 2014
Miss Tanzania mwaka 2011
MISS TEMEKE 2014
MISS USTAWI
MISS UTALII TANZANIA 2012/13
Miss vyuo vikuu 2013
MKALA
MREMBO HUDDAH
Mrisho Mpoto
Mrisho Ngassa
MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES.
MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013
Mtitu
muziki
Mwana FA
MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14
Mzee Majuto
Nancy Sumari
Nani Mtani Jembe?
NAPE
Nassoro ‘Nora’
Natasha
Nay wa Mitego
Necta
Nelly Kamwelu
NEY WA MITEGO
Nisha
NSSF;Zantel
Nyamwela
NYimbo
Nyota yako
OBAMA TANZANIA
OMMY DIMPOZ
P FUNK
PAM D
Peniel Mgilwa ‘Penny’
PETIT MAN
Profesa Jay
Q - CHILA
Q Boy
Q Chilla
QUEEN DARLEEN
RACHEL NDAUKA
RAIS KIKWETE
Rais Kikwete.
Rasimu Ya Katiba TZ
Ray
Ray C
Redd’s Miss IFM
REDD'S MISS KAGERA 2013
REDD'S MISS TZ
REDDS MISS TANZANIA 2014
Redds Miss wa Mikoa
REHEMA FABIAN
RICHIE RICHIE
Rihanna
ROSE MUHANDO
Rose Ndauka
Ruge Mutahaba.
SABASABA 2013
Saida Karoli
Saikolojia
Sajeti
SAJUKI
Sandra
SHAA
Shamsa Ford
Sheikh Ponda
Shilole
Sintah
Siwema
Skin Tricks
Snura Mushi
Spika Makinda
staa
Staa Wetu
Stella Mwangi
STYLE ZA NYWELE
Taifa Stars
Tamasha la matumaini
TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013
Tangazo
TANZANIA
TEGO
TENGENEZA WEBSITE NA BLOG
TID
Tundaman
Tupo wangapi?
TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14
Twanga Pepeta
USA PAGEANT 2014
VAI
Wastara
WEMA
WEMA SEPETU
Yanga
Yanga Bingwa 2013
YOUNG D
Yvonne Cherry ‘Monalisa’
Z Anton.
Zari
Zito kabwe
No comments:
Post a Comment