EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, May 23, 2015

UKILAZIMISHA SANA PENZI JIANDAE KUTESEKA!

NiJumamosi nyingine tunakutana katika uwanja wetu wa  Love Story. Kama kawaida waungwana tunakutana hapa kupeana mawili matatu yahusuyo maisha ya uhusiano. Baada ya kupata darasa la kumpa moyo wako wote halafu ukaambulia maumivu tulilojadili wiki iliyopita, wiki hii tunakuja na mada nyingine nzuri kama inavyojieleza hapo juu.
Kwenye ulimwengu huu wa wapendanao, licha ya kuwepo kwa wale ‘wanaoinjoi’ mapenzi lakini wapo wale wanaoteseka. Wanateseka kwa sababu ya kupenda. Mtu anampenda mwenzake lakini kutokana na sababu anazozijua anayependwa, hathamini tu penzi la mwenzake.
Yule ambaye hathamini penzi huwa anakuwa na sababu zake. Zinaweza kuwa za msingi au zisiwe na msingi. Anaweza kuwa hathamini kwa sababu ana mchumba wake mwingine kama si mke au mume. Hiyo ni sababu ya msingi lakini awe ameisema mapema kabla safari ya uhusiano haijafika mbali.
Anaweza kuwa hathamini kwa sababu hayuko tayari wakati huo kuishi na mtu. Anachoamini yeye ni kwamba muda wake wa kuwa ‘serious’ na mapenzi bado haujafika. Hiyo si sababu ya msingi sana lakini wapo watu wa aina hiyo.
Kwa makusudi kabisa mtu anaamua kucheza na akili ya mwenzake kwa kujifanya ana penzi la dhati kumbe moyoni ana lake jambo. Mtu wa aina hiyo huwa hawezi kudumu muda mrefu na mwenzake kwani uongo siku zote haujifichi, utadhihirika tu!
Kuna mwingine anaweza kuwa na wewe kwa sababu tu ya maslahi. Anajifanya anakupenda kumbe moyoni anakuwa na lake jambo. Utafika wakati atakapotimiza anachokihitaji basi atamuoa au kuolewa na mtu anayemtaka.
Bahati mbaya sana, katika aina ya watu ambao wanacheza na mioyo ya watu, upande wa wanaotendewa huwa haujui lolote. Watu hao wanacheza na mioyo ya wenzao kwa kipindi fulani halafu baadaye wanakuja kufanya maamuzi mengine.
Tena mbaya zaidi kwa sababu wanakuwa wanakuwa tayari wamedumu penzini kwa muda mrefu, wanaamua kuanza visa vya hapa na pale ili kutafuta sababu ya kuanza kujiengua. Ataanza kupunguza spidi ya penzi. Kama alikuwa na kawaida ya kuuliza umeamkaje, anaweza akapitisha hata siku mbili au tatu hajafanya hivyo.

Upande wa pili mwenzake anaanza kuteseka. Kwa sababu alishawekeza nguvu kubwa penzini, alishajiwekea matarajio yake kwamba penzi lao litafika kwenye hatua ya ndoa na kudumu zaidi kumbe mwenzake hana mpango huo.
Kwa sababu alikuwa na penzi la kweli, hayupo tayari kukupoteza. Ataanza kulazimisha kwa namna yoyote atetee penzi lake. Atapambana kwa kila namna lakini zaidi atakayoyapata ni maumivu. Kila atakalolifanya kwake litakuwa ni mateso.
Kinachotakiwa kufanywa na wewe unayeteseka kwanza, unatakiwa kuyakubali mateso na kuyaona ya kawaida.
Yachukulie kama ni sehemu ya changamoto za maisha na kuanza kutafuta suluhu ya haraka ili moyo wako usiumie zaidi.
Kama umeshafanya kila liwezekanalo ukaona bado hakuelewi, huna sababu ya kuanza kunung’unika. Tuliza akili yako na ikiwezekana tafuta vitu vya tofauti ufanye ambavyo vitakufanya uondoke kwenye mawazo hayo.
Usitumie muda mwingi kuwaza umbali wa safari yenu mliyopitia maana kwa mtu aliyeamua kufanya yake hawezi kutambua maumivu utakayoyapata. Kwa nini uumie moyoni kwa kulilia penzi ambalo mwenzako halithamini hata chembe? Kwa nini uumie kwa mtu ambaye hajawahi na hatarajii kuthamini penzi lako? Kwa nini uumie kwa mtu ambaye tayari ana chaguo lake? Achana naye.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate