EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, February 22, 2013

CHAZ BABA ACHUMBIA KWA MIL.1.9

RAIS wa Bendi ya Muziki wa Dansi ya Mashujaa, Charles Gabriel Mbwana ‘Chaz Baba’ amemchumbia demu mmoja aitwaye Rehema Sospeter Marwa.
Charles Gabriel Mbwana ‘Chaz Baba’ akiwa na mchumba wake Rehema Sospeter Marwa.
Akizungumza na mwandishi wetu, Chaz Baba alisema kuwa, amefikia uamuzi huo baada ya kubaini kuwa, Rehema ndiye mwanamke sahihi anayestahili kuingia naye kwenye ndoa.
“Kwa kifupi Jumapili iliyopita nilishamtolea mahari Rehema na huyo ndiye shemeji yenu. Nilitakiwa kutoa shilingi 1,900,000, nikalipa nusu na siku chache zijazo nitamalizia ili niweze kufunga ndoa,” alisema Chaz Baba.

GARI LA KANUMBA LAMSHINDA DK. CHENI


 Chanzo cha habari na Global Publishers

GARI la aliyekuwa staa wa filamu Bongo Steven Kanumba aina ya Toyota Land Cruiser V 8, imeelezwa linapigwa bei na limeshindikana kuuzika kwa sababu ya bei kuwa kubwa ukilinganisha na hali ya mkoko wenyewe ilivyo kwa sasa.
  
Marehemu Steven Kanumba akiwa jirani na gari lake aina ya Toyota Land Cruiser V 8 enzi za uhai wake.
Habari za ndani kutoka kwa chanzo chetu zinasema kwamba, mteja aliyekuwa akitegemewa zaidi ni msanii maarufu nchini, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ ambaye baada ya kutajiwa bei alipewa kwa ajili ya kulifanyia majaribio.
CHANZO KINATIRIRIKA
Kwa sharti la kutochorwa jina lake gazetini chanzo hicho kilitiririka kuwa, si kweli kuwa Dk. Cheni alipewa lile gari ili alitumie kwa muda kufanya vifaa visiharibike bali alikuwa akilijaribu.

MIMI NA ADAM JUMA TUKO SAFI – TUNDAMAN

NYOTA wa muziki wa Kizazi Kipya ‘Bongo Fleva’, Tundaman amefurahi kumalizika kwa hali iliyokuwa ikimkosesha raha, ya mtayarishaji mahiri wa video, Adam Juma kumwekea kinyongo.
Kinyongo cha Adam Juma kwa Tunda, kilikuja baada ya nyota huyo kuamua kuirudia video ya kibao chake cha ‘Demu Sio’ nchini Kenya, kwa madai kuwa awali haikurekodiwa kiubunifu.

Waliofeli wapanga kuandamana kumng’oa Kawambwa

WAKATI mjadala wa kushuka kwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa kidato cha nne ukiendelea nchini, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, amemtaka Rais Jakaya Kikwete kuunda tume kuchunguza na kutoa mapendekezo ya mfumo bora wa elimu nchini.

Alisema kwa hali ilivyo sasa mtu mmoja hawezi kujifungia ofisini peke yake na kuja na mfumo wa kuboresha sekta ya elimu utakaokidhi matakwa ya jamii.
Lowassa alitoa kauli hiyo jana wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika ofisini kwake, jijini Dar es Salaam.

Ingawa hakutaka kuzungumzia hoja ya mbunge wa kuteuliwa na Rais, James Mbatia (NCCR- Mageuzi), aliyetaka Bunge liunde kamati kuchunguza udhaifu katika sekta ya elimu na hoja hiyo kutupwa, Lowassa alisema hakuna sababu ya kubishana kama tuna mitaala au la, lakini jambo la msingi ni kuhakikisha tunapata sababu za matokeo mabaya ya wanafunzi wa kidato cha nne.

“Sitaki kuzungumzia mjadala wa bungeni huyo anasema hatuna mitaala, serikali inasema tunayo, hoja ya msingi zaidi ni kuangalia hii mitaala ni sahihi, inatufaa? Mfumo wetu wa elimu ni mzuri?” alisema Lowassa na kuongeza kuwa tume itakuja na majibu kama mitaala yetu ni sahihi na kama inatufaa au la.
Akitolea mfano, Lowassa wakati wa uongozi wa Mwalimu Nyerere, Waziri wa Elimu wakati huo, marehemu Jakson Makweta, aliunda tume kuchunguza mfumo wa elimu na ilikuja na majibu mazuri yaliyofaa kwa wakati ule na sasa tunahitaji tume nyingine kuja na majibu ya wakati uliopo.

WEMA SEPETU SIJAOLEWA JAMANI, ANAYETAKA KUNIOA AJITOKEZE

MLIMBWENDE wa Tanzania mwaka 2006 ambaye pia ni staa wa sinema za Bongo, Wema Sepetu ameibuka na kusema kuwa, hajaolewa hivyo anayetaka kumuoa ruksa kujitokeza, Amani limemnasa sauti.
 
Wema aliyasema hayo kwa paparazi wetu juzi baada ya kubanwa kuhusu madai kuwa ameolewa ambapo alisema hayupo katika ndoa na mwanaume yeyote yule kama watu wengine wanavyoamini.
Mahojiano kati ya Wema na paparazi wetu kwa njia ya simu yalikuwa kama ifuatavyo:
 
Paparazi: Mambo vipi Wema?
 
Wema: (Kwa sauti ya ukali kidogo) Poa, nani wewe mwenzangu?
 
Paparazi: Mimi ni mwandishi wa Global Publishers hapa…
 
Wema: (Anashusha sauti) Ooo, unasemaje?

WIMBO wa Fulani wa Rich One waanza kutesa

WIMBO unaokwenda kwa jina la ‘Fulani’ ambao umeimbwa na mkali wa muziki huo, Richard Shauri ‘Rich One’ umeanza kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.

Akizungumza  jijini Dar es Salaam jana, Rich One alisema, katika kazi hiyo ameshirikiana vema na wakali wa muziki huo, Inspector Haroun na Juma Nature.
Rich One, aliwataka mashabiki wake waendelee kumpa sapoti katika kazi zake kama ilivyokuwa awali, ikiwa ni pamoja na video ya kazi hiyo.

“Namshukuru Mungu, kazi hii imepokewa vizuri na mashabiki, naamini uwepo wa wakongwe niliowashirikisha, umenipa sapoti kubwa katika wimbo huo,” alisema Rich One.
Alisema kwa sasa amejipanga kufanya vizuri katika soko na amerudi kivingine kwa ajili ya kuwapa burudani mashabiki wake.
Msanii huyo alisema kazi hiyo aliifanya katika studio maarufu ya Halisi Records ya jijini la Dar es Salaam.

‘Uamsho Ifutwe’

TAASISI ya Utawala Bora Tanzania (CEGODETA), imeiomba serikali kukipiga marufuku kikundi cha Uamsho na jumuia ya kimataifa itangaze kuwa ni kikundi hatari.

Kauli hiyo ilitolewa na mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo, Thomas Ngawaiya, kufuatia kuzuka kwa matukio ya mauaji na uharibifu wa mali kwa mgongo wa dini huko visiwani Zanzibar, huku kikundi hicho kikihusishwa kwa ukaribu.

“Kwa kuzingatia hilo CEGODETA, tunaunga mkono tamko lililotolewa na Rais Jakaya Kikwete kwamba uchunguzi wa kina ufanyike ambao utashirikisha mashirika ya nje na wote wanaohusika na mauajji hayo pamoja na wanaofadhili watu wao wachukuliwe hatua za kisheria ili kukata mzizi wa fitina,” alisema.

Ngawaiya aliwatahadharisha Watanzania kutokubali kugawanywa kwa misingi ya dini, ambazo zimeangamiza maisha ya watu wengi katika nchi za Kiislamu duniani.
“Mabomu yamewahi kuua mamia ya watu huko Kenya, Uganda na Sudan kwa sababu ya udini, hadi leo vurugu hizo za mauaji zinaendelea huko kwa kasi.

“Kama Watanzania tusipokuwa makini mambo yaliyotokea kwenye nchi hizo yaweza kutokea hapa kwetu, kwa asiyejua kufa mwambie akatazame kaburi,” alisema.
Aidha aliitaka serikali itoe ulinzi wa kutosha kwa makanisa na viongozi wote wa Kikristo huko Zanzibar, sambamba na bara, pia kwa misikiti na viongozi wa misikiti wanaotishiwa maisha.

Kinara vurugu za kidini huyu hapa..Polisi watangaza bingo atakayesaidia kumpata

KINARA wa vurugu za kidini zinazoibuka kila siku ya Ijumaa jijini Dar es Salaam, amejulikana.

Kinara huyo ametajwa kuwa ni Sheikh Issa Kondo Bungo ambaye amekuwa akitafutwa na polisi kwa muda mrefu bila mafanikio.

Habari kutoka ndani ya Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, zilisema kuwa Sheikh Bungo anadaiwa kuhusika na matukio kadhaa makubwa ya vurugu za kidini, zilizotokea kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam.

Duru za kipolisi zilitaja baadhi ya matukio ambayo Sheikh Bungo anadaiwa kuhusika nayo kuwa ni pamoja na tukio la kuchoma moto kanisa la TAG la Mbagala, baada ya mtoto (jina limehifadhiwa), kukojolea Qur’an.

Tukio la kukojolea kitabu hicho lilitokea Oktoba 10 katika eneo la Chamazi saa 10 jioni wakati watoto hao wakiwa katika ‘kijiwe’ chao cha kuchezea mpira.
Vurugu hizo zilisababisha kuvunjwa kwa vioo vya magari, madirisha ya makanisa pamoja na kuibwa kwa vifaa vya kwaya katika makanisa hayo ambayo ni ya Anglikana, Wasabato na Pentekoste.

WEMA ISSAC ABRAHAMU SEPETU AMFUMANIA BABAY MADAHA NA MME WAKE


MSANII wa filamu na muziki Bongo, Baby Joseph Madaha hivi karibuni alinaswa nyumbani kwa kigogo anayetoka na Wema, Clement.
Kwa mujibu wa chanzo kilichoomba hifadhi ya jina lake, tukio hilo lilitokea hivi karibuni ambapo staa huyo wa filamu na muziki alionekana akiingia kwa usafiri wa teksi nyumbani kwa kigogo huyo anayeishi maeneo ya Mwananyamala-Gereji, Dar.
Baada ya kujiridhisha na maelezo ya sosi huyo, mapaparazi wetu walimtafuta Baby Madaha ili kujua ukweli wa jambo hilo.

“Kweli nilikwenda hapo (kwa Clement), mimi sijui kama niliyeenda kuonana naye ni bwana wa Wema kwa sababu sijawahi kumuona naye na nilimfuata kwa ajili ya kuzungumza mambo ya kikazi,” alisema Baby Madaha

BILIONEA WA SIMBA "MALKIA NYUKI"AKINUKISHA,AWATUPIA VIRAGO MAKOCHA WA SIMBA,JULIO KAMATA TIMU

Malkia wa Nyuki, Rahma Al Kharoos akizungumza jana

Na Mahmoud Zubeiry

MFADHILI wa Simba SC, Rahma Al Kharoos amesema kwamba timu hiyo kwa sasa haistahili kufundishwa na kocha kutoka nje, kwa sababu haina wachezaji wataalamu na wenye ubora na viwango, hivyo amependekeza iwe chini ya mzalendo Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ pekee. 

 
Akizungumza na Waandishi wa Habari jana katika hoteli ya Movenpick, Dar es Salaam, Rahma maarufu kama Malkia wa Nyuki, amesema kwamba kama Simba wanataka kuwa na makocha wa kigeni, basi watafute wachezaji wataalamu na wenye ubora na viwango. 
 
“Unajua ukikaa ukiangalia timu inavyoendelea ya Simba, tofauti na uwezo wake na kocha kutoka nje, sawa sawa na mtoto wa shule ya vidudu, unampa mwalimu wa chuo kikuu. Kwani sisi hatuna makocha hapa, si tuna makocha,”alisema.

Thursday, February 21, 2013

WEMA SEPETU SI WA KITOTO OFISI YAKE NI MOTO WA KUOTEA MBALI



SI OFISI ya kitoto, ni ofisi ya bab kubwa iliyokwenda shule ikiwa imepambwa kwa fanicha na mashine za kisasa.
Naam hiyo ndio ofisi ya Wema Sepetu, mlimbwende na muigizaji nyota wa filamu, ni ofisi itakayobeba kazi zake za kila siku kupitia kampuni yake ya Endless Fame Film.
Akizungumza na waandishi wa wa habari masaa kadhaa yaliyopita wakati akiitambulisha rasmi kampuni yake, Wema Sepetu alisema Endless Fame Film itajishughulisha na utengenezaji wa filamu pamoja na kuandaa matamasha mbali mbali.
Ofisi za Wema Sepetu zitakazoanza kazi rasmi mwezi ujao zipo Mwananyamala koma koma, Dar es Salaam.Chanzo cha habari saluti5

Sehemu ya kumpuzika wageni

Serikali yalipa Sh400 mili watumishi hewa

SERIKALI imelipa mishahara hewa zaidi ya Sh400 milioni kwa watumishi ambao hawapo kazini Hospitali ya Enduleni, Wilaya ya Ngorongoro, mkoani Arusha kuanzia mwaka 2009 hadi mwaka huu.

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi kwenye hospitali hiyo inayomilikiwa na Kanisa la Katoliki Jimbo la Arusha, umebaini takribani tangu mwaka 2009 hadi sasa, serikali imekuwa ikituma Sh8.2 milioni kila mwezi kulipa watumishi 13 ambao wameacha kazi.

Watumishi hao majina yanahifadhiwa, wanadaiwa kuacha kazi hospitalini hapo kutokana na kuzorota kwa huduma, kulikochangiwa na upungufu wa dawa na kushindwa kulipwa stahiki nyingine.
Hospitali hiyo ambayo ipo ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, imekuwa ikihudumia zaidi ya wakazi 70,000 wa Tarafa ya Ngorongoro kutokana na eneo hilo kutokuwa na hospitali nyingine.

Diamond alia na ‘vibaka’

MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinum’ amewalalamikia watu waliomuibia simu yake na kuvujisha wimbo wake mpya ambao anatarajia kuuachia hivi karibuni.
 
Akielezea jinsi wimbo huo ulivovuja jijini Dar es Salaam jana, Diamond alisema nyimbo zake huwa anazitunza katika simu yake ya mkononi, hivyo mara ilipoibiwa akasikia wimbo huo umeshanza kusikika mtaani.

“Wimbo unaitwa ‘Ukimuona’, ni kati ya nyimbo zangu ambazo zimesimama na zenye maneno fulani ya kuwashika mashabiki, kiukweli mistari imesimama, naandaa video yake, pamoja na kuvuja, nitaitoa hivyo hivyo maana ni bonge la ngoma,” alisema Diamond.

Alisema kazi hiyo ataiachia wiki ijayo na kuwaomba mashabiki wake wakae mkao wa kula, kwani anaamini mistari yake imesimama na ina ujumbe katika jamii.
Diamond kwa sasa anatamba na kibao chake cha ‘Kesho’ ambacho kimeliteka soko la muziki mbali na kuwa na vibao vingi ambavyo vinafanya vizuri.

Waziri achafua hewa mazishi ya Padri Mushi Zanzibar

Waumini wamzomea mbele ya Rais Shein
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud, amechafua hali ya hewa wakati wa mazishi ya Padri Evaristus Mushi, aliyeuawa kwa kupigwa risasi Visiwani Zanzibar.
Hali hiyo iliyosababisha waziri huyo azomewe, ilitokea jana kwenye mazishi ya padri huyo, yaliyofanyika katika makaburi ya watawa, yaliyopo eneo la Kitope, nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Mbele ya Rais wa SMZ, Ali Mohamed Shein, Waziri huyo aliwachefua maelfu ya Wakristo waliofurika kwenye mazishi hayo wakati akitoa salamu za pole kutoka kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).

Katika salamu hizo, waziri huyo alianza vizuri kwa kutoa pole na kwamba serikali imeguswa na kifo hicho na maumivu waliyonayo waumini ndiyo iliyonayo pia serikali.

Lakini wakati akiendelea kutoa salamu hizo, alichafua hali ya hewa kwa kusema kifo cha Padri Mushi kimetokana na mapenzi ya Mwenyezi Mungu.

“Ndugu zangu poleni kwa msiba huu, serikali imeguswa sana na kifo hicho kama ndugu na waumini mlivyoguswa. Hata hivyo hii ni mipango na mapenzi ya Mwenyezi Mungu…”
Kauli hiyo ilisababisha umati wa watu waliofurika katika makaburi hayo kupaza sauti kwa kuzomea na kuikejeli Serikali ya SMZ kwamba kifo hicho hakikutokana na mapenzi ya Mungu.

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate