EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, October 22, 2013

CHOMBEZO:KITANDA CHA MAMA MWENYE NYUMBA...MWANZO MPAKA MWISHO.

“Mke wangu, kila siku namwona huyu kijana mchafuchafu anakuja kuokota chupa tupu hapa, ina maana tuna chupa tupu kila siku?”

“Siyo hivyo mume wangu, we hujamfuatilia tu, anakuja kila baada ya siku tano. Tumsaidie mume wangu, si unamwona kijana mwenyewe maskini huyu,” alisema mama Joy huku macho yake yote yakimwangalia yule kijana mwokota makopo…

“Awe anakuja mchana basi, usiku kama huu hapa nje, mimi naweza kumchapa risasi nikidhani mwizi. Si unaona hata mavazi yake? Kwanza haogi huyu, hata harufu anatoa
“Mume wangu usimkufuru Mungu, sisi kupewa uwezo ni matakwa yake, hakuna binadamu ambaye akipewa nafasi ya kuchagua maisha bora na duni, atasema anataka duni.”

“Mimi sijafika huko, ila nasema awe anakuja mchana tu  si usiku kama huu.”

“Sawa mume wangu,” alisema mama.

Hayo yalitendeka  wakati baba Joy akiegesha gari mahali pake kisha akashuka na kuanza kutembea mkononi ameshika brifkesi yake.

Siku hiyo, baba Joy alikuwa kama amevaa Kinaijeria f’lani.

Mama Joy alimpokesa mumewe brifkesi kisha akamwacha apite ili yeye amfuate kwa nyuma. Wakati mumewe anaingia, mama Joy aligeuka kumwangalia mwokota chupa tupu ambaye kwa muda huo alikuwa amebeba fukp la ‘salfeti’ begani.

Mama Joy alimwonesgha ishara kwamba aondoke haraka sana kwa vile mumewe amerudi. Kijana wa watu, alitoka getini kwa kuruhusiwa na mlinzi.

“Unasikia mama Joy,” baba Joy alianza kusema tena akiwa amekaa kwenye sofa kubwa…

“Abee…”

“Mimi sipendi watu wawe wanaingiaingia humu ndani hovyo. Tena nadhani iko haja ya sehemu ya kutupia taka niijenge nje ili watu wasipate sababu ya kuingia ndani…

“Wewe kijana mchafuchafu vile, si lazima pia atakuwa mwizi..?”

“Nimekuelewa baba Joy, hataingia tena usiku ikitokea itakuwa mchana.”

“Iwe hivyo, sitaki kumwona tena usiku. Kwanza wewe ni mke wa mtu, mnachekeanachekea kwa sababu gani?”

“Basi mume wangu jamani, nimekuelewa.”

Mzee huyo aliondoka kwenda kazini, mkewe mama Joy alisiama nje kwa muda mrefu, alipotaka kugeuka kurudi ndani, kwa mbali alimwona mwanaume akitokea. Mgongoni alibeba furushi…

“Au yule?” alisema moyoni. Alisubiri kwa muda ili amwone kwa karibu, lakini hakuwa yeye.

Nusu saa baada ya kuingia ndani, kengele ya geti kubwa ililia…

“Mh! Si yeye huyo?” alijihoji mama Joy akiamini aliyebonyeza kengele ni mzoa taka. Japokuwa alijua mlinzi atashughulikia, lakini aliamua kutoka mwenyewe kuelekea getini ambapo alimkuta mlinzi anasukuma geti kubwa.

 “Nani amepiga kengele?” mama Joy aliuliza…

“Sijamjua ni nani?” mlinzi alijibu huku akiendelea kusukuma geti, likawa wazi…

“Shikamoo mama,” mzoa taka alisalimia akiwa anatabasamu...

“Hujambo wewe?” mama Joy alijibu hivyo badala ya kusema marhaba. Na tangu mzoa taka huyo ameanza kuingia ndani ya nyumba hiyo kuchukua taka, kila akimsalimia shikamoo mama Joy anajibiwa hujambo wewe au asante kijana…

“Sijamboo, shikamoo…”

“Asante…askari, funga geti…”

“Sawa. Huyu mzoa taka aingie..?”

“Aingie ndiyo. Akishaingia funga geti.”

Mzoa taka aliingia hadi ndani, akamkaribia mama Joy ambaye naye alimkaribisha hadi kwenye sehemu yenye taka.

Mlinzi aliwakodolea macho. Kilichomshangaza zaidi ni kauli ya baba Joy kwamba hataki kumwona mlinzi huyo nyumbani kwake…

“Sasa mbona amemuingiza tena leo? Halafu kuna siri nzito mimi naiona kati ya mama na huyu mzoa taka, maana mama akiamkiwa shikamoo hatakagi kuitika marhaba,” mlinzi aliwaza.

Mama Joy alimfikisha mzoa taka kwenye pipa la taka ambalo lilijengwa vizuri ndani ya nyumba hiyo…

“Jana mwenzangu mzee alikasirika sana,” alianza kusema mama Joy…

“Hata mimi kama nilimwona. Niliogopa sana…”

“Yeye anasema hataki kuona unaingia humu ndani usiku. Akasema atalitoa hili pipa na kulijengea nje huko.”

“Kwa hiyo akinikuta saa hizi humu ndani kwake si ataniua?”

“Hawezi, ingawa ana bastola…”

“Mama mimi nakwenda, kumbe mumeo ana bastola..!”

“Hawezi kukuua, alisema hataki uingie usiku, ‘asa kwani saa hizi ni usiku?” alisema mama Joy huku akimsogelea mzoa taka huyo na kumshikashika kidevuni. Alizikuna ndevu zake chache…

“Una ooo nzuri kijana, sema tu hutaki kuitunza…”

“Una macho mazuri, madogoooo, sema tu unayashindisha juani mpaka yanakuwa mekundu, au unavuta bangi..?”

“Sivuti bangi mama…”

“Una midomo mizuri, minene halafu myeusi, naipenda.” Hapo mama Joy vidole vyake vilikuwa vikicheza kwenye midomo ya mzoa taka huyo ambaye alionekana hajapiga mswaki…

“Halafu kifua chako kimetuna vizuri sana, mi nakipenda, unafanyaga mazoezi  nini?”

“Nina muda huo mama, labda kimetuna chenyewe tu.”

Mama Joy alimvutia kwake mzoa take, akamgusanisha na kifua chake huku akizidi kummwagia sifa kibao…

“Halafu kifua chako kina joto zuri…”

“Asante mama…”

“Halafu masikio yako yamekaa vizuri kwa kushikwashikwa,” mama Joy akamshika masikio mzoa taka huyo…

“Mama unanitekenya lakini…”

“Kweli..?”

“Kweli tena…”

“Nakutekenya nikifanyaje?”

“Hivyo unavyonishikashika masikio…”

“Yaani hivi,” alisema mama Joy akiendelea kumshikashika sehemu hizo, mzoa taka akachachamaa mwili, akatupa furushi lake chini.

Kutokana na maisha yake ya kifukara ambapo kula, kulala kwake  kwa kubahatisha, mzoa taka hakuwa akipata mademu, kwa hiyo mama Joy kumfanyia ‘utani’ ule wa kimahaba kwake ilikuwa kama mtende ulioota kwenye jangwa…

“Unajua mwenzio naumia mama, kwani nini kimetokea mpaka leo unafanya hivi..?”

“Kijana tulia, kwani siku zote hukuona kama nimekupenda sana mwenzio..?”

“Aaah! Mama wewe mke wa mtu, mimi siwezi, naogopa na sitaki.”

Mama Joy alijua kauli ya mzoa taka huyo ya kugoma inaweza kuzua matatizo makubwa kwamba atamtangaza, akaamua kumbaka.

Kwanza, aliangalia kulia na kushoto, alipoona hakuna mtu na mlinzi hawezi kufika, alimshika mzoa taka na kumlaza chini kwenye nyasi za bustani, akamvua suruali, akamvua ‘kufuli’ kisha yeye akavua zake na kuanza kujihudumia kwa raha zake…

“Mama…”

“Abee…”

“Mumeo ana bastola lakini…”

“Wala isikutishe, ha…ha…wezi kuja…”

“Akija je?”

“Ni…nisi…kie mi…mi…”


Kwa kuwa walikuwa wanaiba, mama Joy alijitahidi kupiga mashuti ya kasi ili apate goli la ushindi. Hakukuwa na mbwembwe, madoido wala manjonjo, mama Joy akafika juu ya mlima na kutangaza ushindi.

Aliamka na kumsimamisha mzoa taka ambaye bado alikuwa hoi kwa ‘mzuka’ ingawa naye alishabanjua dafu lake moja, lakini bado alikuwa anataka tena…

“Simama basi.”

Mzoa taka alisimama…

“Vaa…”

Mzoa taka alivaa nguo zake, akaendelea kusimama…

“Chukua matakataka yako, mimi nakuja sasa hivi,” alisema mama Joy huku akienda ndani.

Mzoa taka alijishangaa kwa jinsi alivyobaki na harufu ya pafyumu ya mama Joy…

“Mmm…ananukia vizuri, sijui kajimwagia nini mwilini?”

Baada ya dakika mbili tu, mama Joy alirudi, akampa mzoa taka shilingi elfu hamsini, nyekundu tupu…

“Hizi ukanunue suruali nzuri, shati zuri, viatu, chup*** na kisha uoge uwe mzuri zaidi ya hapa, sawa kijana wangu?”

“Asante sana mama, sawa.”

Mzoa taka aliweka pesa mfukoni, akabeba furushi lake na kutoka.

Getini, mlinzi alimtupia jicho baya mzoa taka…

“Hivi wewe kijana, huko mitaani hakuna matakataka hadi uje hapa?”

“Sasa kwani yako?”

“Jibu swali wewe, acha ujeuri, nitakuwa sikufungulii…”

“Usifungue tuone kama nitakuwa siingii…”

“Utaingia kwa njia gani?”

“Pana nini hapo getini..?” mama Joy aliuliza kutokea mbali karibu na mlango mkubwa wa kuingilia ndani…

“Si huyu hapa,” alisema mzoa taka…

“Anasemaje?”

“Mama namtania tu huyu ni mtani wangu. Teh! Teeh! Teeeh!”

Mama Joy aliingia ndani. Mwili wote ulikuwa ukinuka jasho la mzoa taka. Mbaya zaidi alimchafua hadi  nguo aliyovaa…

“Daaah! Yataka moyo kuwa na mpenzi kama huyu,” alisema moyoni mama Joy, mara honi ya gari mlangoni ikalia…



“Mh! Siyo mume wangu kweli huyo?”

“Na kama ni mume wangu si ajabu amemuona mzoa taka,” aliwaza mama Joy huku akikimbilia chumbani, akachukua taulo kisha akakimbilia bafuni ambako alioga kwanza.

Alipotoka alimkuta mumewe amekaa sebuleni. Mama Joy alitetemeka sana…

“Vi…pi mwenzetu?”

Baba Joy alimkazia macho mkewe bila kumjibu kitu halafu akaangalia kwenye tivii ambayo ilikuwa haijawashwa…

“Baba Joy.”

Baba Joy alimwangalia mkewe kama ishara ya ‘nakusikiliza ongea’. Lakini mama Joy alipoona hali ile, hakuongeza neno, alipitiliza chumbani…

“Mh! Hapa kuna ishu, lazima.”

Licha ya kujikausha kwa taulo lakini aliendelea kuhisi ananuka uchafu aliogusishwa na mzoa taka. Alivaa gauni simpo, akatoka hadi mlango mkubwa, akatumbukiza miguu kwenye sendozi, akaelekea getini…

“Mlinzi…”

“Naam mama…”

“Baba Joy alipoingia alisemaje?”

“Hajasema kitu, amepiga honi tu kisha akaingia.”

“Ulimwamkia?”

“Ndiyo mama.”

“Akaitikiaje?”

“Kha! Mama kwani wewe nikikuamkiaga huwa unaniitikiaje?”

“We mshe** nini? Nakuuliza swali na wewe unanijibu swali…”

“Alisema marhaba, nikamuuliza mbona umewahi kurudi? Akasema amechoka sana…”

“Mlinzi fungua geti haraka,” sauti ya baba Joy ilisikika kwa kishindo na vile ilikuwa nzito na nene ndiyo kabisa.

Baba Joy aliingia kwenye gari, likarudi ‘rivasi’ na kugeuza kisha likatoka ndani bila kuaga mtu. Mlinzi alifunga geti nyuma ya baba Joy…

“Mlinzi,” mama Joy aliita…

“Naam mama…”

“Hebu njoo huku ndani,” mama Joy alisema huku akianza kutembea. Alipofika sebuleni, alikaa mkao wa hasira.

Mlinzi aliingia…

“Nifunge mlango mama..?”

“Wa nini..?”

“Nilikuwa nauliza tu…”

“Hebu kaa hapo.”

Mlinzi naye alianza kutetemeka, alihisi kibarua kimeingia mdudu mbaya…

“We mlinzi si una namba ya mume wangu..?”

“Ndiyo…”

“Simu yako iko wapi?”

“Kule kwenye kibanda changu.”

“Nenda kailete haraka sana.”

Mlinzi alisimama na kutoka.  Mama Joy aliwaza mengi kichwani mwake wakati anamsubiri mlinzi…

“Huyu lazima alimpigia simu mume wangu, akamwambia mzoa taka amekuja, maana jana si alisikia baba Joy alivyokuwa akikataza watu kuingia? Lakini yeye alisema hataki watu waingie usiku, sasa kwani saa hizi usiku?”

“Halafu ni kweli itakuwa yeye maana hawapatani tangu zamani. Hata leo yenyewe pale getini si walibalulana kidogo. Atakuwa yeye tu. Baba Joy alikuja akidhani atamkuta mzoa taka, bahati nzuri kashaondoka.”

Mara, mlinzi aliingia…

“Iko wapi?”

“Hii hapa.”

Mama Joy aliipokea simu hiyo na kusachi namba zilizopiga kwa siku hiyo, hakukuwa na namba zilizopiga wala kupigwa…

“We unan’tania siyo..?”

“Hata kidogo mama…”

“Ina maana hii simu yako hujapiga simu wala kupigiwa..?”

“Leo kuna wakati nilitoa laini. Kwa hiyo kuna uwezekano namba zote zilizopigwa na nilizopiga zimefutika zenyewe.”

Mama Joy alikubaliana na hilo, lakini alijua mlinzi alifanya hivyo makusudi. Yaani alipomwambia akachukue simu, mlinzi alipofika alitoa laini au alifuta namba zote ili kupoteza ushahidi kama alimpigia baba Joy…

“Haya nenda,” alisema mama Joy. Mlinzi alisimama, akaondoka bila kuaga.

Nyuma, mama Joy alianza kufikiria vitu vyake…

“Huyu mlinzi atakuwa adui wangu kwa mzoa taka. Kama anaweza kumpigia simu mume wangu kumwambia kuna mwanaume ameingia ni tatizo, tena kubwa sana.

“Kinachoonekana, baada ya mume wangu kurudi alimwambia ameshatoka ndiyo maana hata alipoingia ndani alifikia sebuleni. Tena mbaya sasa amekuta mi natoka kuoga, si ndiyo hatari zaidi?

“Sasa hapa nifanyeje? Maana kama kutokea limetokea. Nikisema nimchongee chochote kwa mume wangu atajua natengeneza bifu kwa sababu anatoa siri zangu na mzoa taka, dawa yake hapa moja tu…” alisema moyoni mama Joy kisha akabetua vidole, akasimama, akaingia ndani…

“Asumta,” alimwita mwanamke anayefanya kazi ndani ya nyumba yake…

“Abee…”

“Kaniitie mlinzi.”

Asumta alitoka nje hadi kwa mlinzi, tena kwenye kibanda chake…

“Fuko unaitwa na bosi wa kike.”

“He! Leo mama yangu umetoka nje, ajabu!”

“Unaitwa huko.”

Asumta na mlinzi huyo waliongozana hadi ndani, Asumta akawa anapita, mlinzi akabaki sebuleni…

“Asumta…”

“Abee bosi…”

“Endelea na kazi zako, mimi nina maongezi na Fuko…”

“Sawa bosi,” Asumta aliitika huku akiinamisha kichwa kama ishara ya utii.

Mama Joy alisimama, akamfuata mlinzi kwenye kochi alipokaa, akapiga magoti chini yake na kumshika mapajani…

“Niambie ukweli. Ulimpigia mume wangu simu kumwambia..?”

“Kumwambia nini?”

“Kwamba mzoa taka ameingia..?”

“Lini? Leo?”

“Leo ndiyo.”

“Hapana, sijampigia.”

“Fuko…”

“Naam mama…”

“Usinifiche,” alisema mama Joy huku akimshikashika sehemu mbalimbali za mwili mpaka kwenye flaizi ya suruali…

“Si…sija…m…mmmpigia,” mlinzi alianza kupagawa na lile zoezi la kushikwashikwa sehemu za mwili…

“Ma…ma…ma…hu…huko s…siii…ko…”

“Sema ukweli wewe. Kwanza huku ndiko. Uli…ulimpigia simu baba Joy..?” alisema mama Joy huku akizidisha kumhamasisha mlinzi wake huyo kwa kuendelea kumshika sehemu mbalimbali za mwili wake…

“Siiii…sija…sijampigia mama…kwe…kweli tena.”

Mama Joy naye alianza kupagawa, alianza kuangusha ‘malalamiko’ ya mahaba huku akifumba na kufumbua macho yake makubwa kama golori.

Sasa ukimya ulitawala, wote walikuwa wakifanya mambo yao kwa vitendo huku wakiwa wamechanganyikiwa kwa mahaba.

Mama Joy akiwa bado amepiga magoti, alimsimamisha mlinzi kisha na yeye akasimama na kusogea naye mpaka kwenye kochi kubwa.

Mama Joy alijitupa, akamvuta mlinzi, naye akajitupa tii. Hapakuwa na simile, mahaba yalitawala, yakapamba moto. Mama Joy aligawa raha kwa mlinzi. Maswali kama, ‘ulimpigia simu baba Joy’ yakaisha yakabaki manung’uniko ya mapenzi.

Mpenzi, mahabuba wangu, sweetheart, wa rohoni zikawa ndiyo kauli kutoka kwenye kinywa cha mama Joy.

Alipofanikiwa kuvunja dafu tu, mama Joy akaanza kutoa maonyo…

“Usije ukamwambia mtu lakini…”

“Sa…sawa,” alijibu mlinzi…

“Nihakikishie…”

“Kweli si…sitasema…”

“Ukisema je?”

“Nifukuze kazi…”

“Shauri zako, utafukuzwa kweli.”

Mara, mlinzi alianza kupiga kelele za ‘furaha’ za kufika mwisho wa kilele cha mlima…

“Usipige kelele sana basi, hausigeli atatusikia, atajua, akijua atasema,” mama Joy alisema akiwa amemmiliki kifuani mlinzi wake huyo huku akimkaribisha kwenye kilele cha furaha…

“Sa…sawa…” alisema mlinzi huku akizidi kupiga kelele. Ilibidi mama Joy amuwekee kiganja kwenye midomo ili sauti isitoke…

“Nimekwambia usipige kelele husikii, unataka kunitafutia matatizo siyo?” alihoji mama Joy huku kiganja bado kikiwa kwenye midomo ya mlinzi. Wakati huo mlinzi alipunguza kelele kwani alishasimama kileleni kwenye mlima wa maraha.

Alitoka haraka kwenye kifua cha bosi wake, akavaa sawasawa huku akiona aibu kwa mbali…

“Ukiwa mtulivu utafaidi vingi kutoka kwangu, ukiwa hujatulia kazi itaota mbawa. Umesikia  mpenzi wangu?”

“Nitakuwa mtulivu ili nifaidi. Lakini mzee si atajua..?”

“Utamwambia wewe..?”

“Mimi siwezi. Lakini wanasemaga wasomi wanajua mambo mengi.”

“Hawezi kujua kama hataambiwa.”

“Yule mzoa taka je?”

“Mzoa taka hakuhusu wewe, nyamaza. Na ole wako uzungumzie kuhusu mzoa taka.”

“Sitamzungumzia.”

“Haya nenda kazini kwako, lakini funga mdomo wako.”

Mlinzi alitoka huku akisemasema maneno anayoyajua mwenyewe.



***

Mama Joy aliingia chumbani kwake kwenda kuoga. Alipomaliza alikwenda kukaa kwenye ‘dressing table’ na kujipodoa vilivyo, pafyumu na manukato mbalimbali ili kuondoa shombo la wanaume hao wasio na hadhi yake.

Alipomaliza, alikwenda jikoni kwa mfanyakazi wake wa ndani na kuongea naye mawili matatu huku akimkazia macho ili aone kama anajua chochote kuhusu kilichotokea…

“Pilipili umeweka za kutosha?”

“Ndiyo bosi…”

“Mchuzi uziwe kama ule wa juzi, umefuata vile nilivyokufundisha?”

“Ndiyo bosi, wala hakuna shaka.”

Mama Joy alijiridhisha kwamba hakuna siri yoyote anayoijua mwanamke huyo.

***

Saa moja jioni, mama Joy alipokea simu kutoka kwa mumewe…

“Nina safari ya Arusha usiku huu. Nakwenda kufanya makubaliano na wale jamaa wa Tanzanite…”

“Mbona ghafla baba Joy..?”

“Imebidi niende…”

“Kwa ndege au gari..?”

“Kwa gari…saa mbili na nusu asubuhi nitakuwa na kikao nao.”

“Haya, safari njema mume wangu…”

“Oke, take care…”

“Usijali mume wangu.”

Mama Joy alikaa sebuleni akijiuliza maswali mengi kuhusu safari hiyo ya ghafla ya mumewe…

“Ni kweli au ananitega?”

“Si ajabu anataka kujifanya amesafiri ili usiku arudi kimyakimya akijua atanifumania na mzoa taka. Amechelewa, kama mtoa siri wake ni mlinzi naye nimemweka mikononi, yuko upande wangu sasa.”

Alitoka nje na kumwita mlinzi…

“We Fuko…”

“Naam bosi…”

“Njoo mara moja.”

Mama Joy alirudi sebuleni, akaa kumsubiri mlinzi. Aliingia muda huohuo…

“Mzee amekupigia simu..?”

“Ndiyo bosi…”

“Amekwambiaje?”

“Amesema nifunge geti kwa kufuli yeye hatarudi, anasafiri na wewe ameshakwambia…”

“Oke, vizuri sana kaendelee na kazi, ikifika saa nne usiku uje hapa sebuleni kuna mambo muhimu tuongee.”

“Sawa bosi.”

Dakika tatu baada ya mlinzi kuondoka, mvua kubwa ilinyesha huku ikiambatana na upepo mkali…

“Mh! Na kaubaridi haka ukipata mwanaume akukumbatie kukupa joto…patanoga,” aliwaza mama Joy huku akijikunyata, akaguna tena baada ya mvua kumwagika zaidi…

“Lakini si nimemwambia Fuko aje saa nne. Leo hakuna kulinda. Atalala na mimi chumbani mpaka asubuhi, loo!”

Kwa mbali akasikia kama sauti ikisema…

“Na mvua hii mumeo si ataghairi kusafiri? Sasa akija na kumkuta mlinzi chumbani unadhani ndoa ipo hapo?”

“Mume wangu hataweza kuingia ndani mpaka afunguliwe  geti, mbaya zaidi mwenyewe amemwambia mlinzi afunge geti kwa kufuli kwa sababu hatarudi tena leo, ana safari ya Arusha,” mama Joy alisema kama anayeijibu ile sauti.

Lakini palepale alipata wazo la kumpigia simu mumewe ili ajifanye anamuonea huruma kwa sababu ya mvua kubwa na safari. Mama Joy aliamini kwa kuongea na mumewe atapata picha kama ameghairi safari au la!

Bahati mbaya simu ilikuwa haipo hewani hata pale alipopiga simu mara tatu hadi tano, baba Joy hakupatikana…

“Kha! Asa huyu vipi?” alijihoji mama Joy akianza kupata wasiwasi kwamba, kweli mumewe anaweza kuzuka ghafla licha ya kwamba hataweza kuingia ndani hadi apige simu lakini atakuwa ameondoa uhondo kati yake na mlinzi.

Saa nne juu ya alama, mlango mkubwa uligongwa, mama Joy akiwa amejilaza sebuleni.

Alitoka kwenye kochi akaenda kufungua…

“Umefunga geti kwa kufuli kweli wewe Fuko?”

“Ndiyo mama…”

“Haya pita, lakini sasa nina wasiwasi na kitu kimoja…”

“Kipi tena mama..?”

“Mvua ni kubwa sana na mzee alisema anasafiri, haiwezekani akaghairi kusafiri, akarudi..?”

“Mh! Lakini hataweza kuingia ndani hadi afunguliwe geti…”

“Nitakwenda kufungua mimi,” alisema mlinzi…

“Sasa ukitoka si atasikia mlango huu ukifunguliwa wakati wewe unatakiwa kukaa kwenye kijumba chako..?”

“Mama, atasikia na mvua hii, labda kama itaacha kunyesha mama.”

Hapo, mlinzi alishaketi, mama Joy naye aliketi lakini kwenye kochi jingine.

Walitulia kwa muda wakitazamana. Mama Joy ndiye aliyekuwa akimwangalia kwa macho ya mahaba mlinzi wake huyo ambapo yeye alikuwa akisikia aibu na kuangalia chini kila mara…

“Sasa?” aliuliza mama Joy…

“Sijui, si uliniita bosi ukasema una mazungumzo muhimu na mimi.”

“Ee, ni kweli. Sasa nataka tukaongelee chumbani kwani mambo yenyewe ni nyeti sana.”

Mlinzi alishtuka kusikia kauli hiyo mpaka ikawa inajirudiarudia kichwani mwake…

“Ee, ni kweli. Sasa nataka tukaongelee chumbani kwani mambo yenyewe ni nyeti sana.”

“Sawa bosi,” alisema mlinzi. Moyoni alijua hakuna cha mambo nyeti wala nini, bosi wake anataka kitu na boksi.

Mwanamke huyo ndiye aliyetangulia kusimama, akamfuata mlinzi, akamshika mkono na kuanza kuondoka naye. Waliingia chumbani ambapo kwa mara ya kwanza na aliamini pengine na ya mwisho kwa yeye kuingia kwenye chumba cha tajiri yake.

Ni kweli alikuwa hafanani na chumba hicho lakini alishatunukiwa na mama mwenye nyumba.

Nje mvua ilikazana kunyesha, kibaridi kilikuwa kikali kiasi kwamba, chumbani hakukuwa na haja ya kuwasha ‘AC’ kama inavyokuwaga wakati wa joto…

“Utaoga?” mama Joy alimuuliza mlinzi wake huku mwili ukimnyevuanyevua kwa hisia za mahaba. Alitamani lisitokee hilo la kwenda kuoga kwani dakika tano mbele kuanza pale kwake ilikuwa ni pigo la kiu yake ya kufanya mapenzi…

“Kuna baridi sana bosi, siwezi kuoga.”

Mama Joy alimshika kwa fujo mlinzi wake na kumwangushia kitandani na nguo zake zikiwa zimeloa mvua chapachapa, miguuni matope, mpaka kinyaa.

Kisha na yeye akavua nguo haraka. Alivua zote akabaki kama alivyozaliwa…

“Njoo baba njoo,” alimwita mlinzi huku yeye akiwa anaelekea ukutani. Mlinzi alishangaa sana kwanini aitwe ukutani badala ya kitandani. Kwanza alisita, ghafla mwanamke huyo akamfuata, akamshika mkono na kumvuta.

Walikwenda hadi kwenye kona ya ukuta. Mama Joy akamchojoa nguo zote huku akimtaka ajisikie yuko huru. Aliamini kama mlinzi huyo atakuwa na wogawoga hatamtosheleza katika huduma ya mapenzi…

“Sawa.”

Mama Joy akaenda kitandani, akatoa godoro na kuliburuza peke yake hadi kwenye kona. Kwa kuwa chumba kilikuwa kikubwa na chenye nafasi ya kutosha, aliliweka pembeni kabisa, akarudia mashuka mawili.

Alitandika mwenyewe shuka moja, jingine akalitupia juu ya godoro kwa ajili ya kujifunuka.

Alimvuta mlinzi, naye akaangukia hapo. Shughuli ilianza. Mama Joy alimwingiza mlinzi wake kwenye shuka na kumwanzishia mechi huku akijisisimua mwenyewe.

Mlinzi alibadilika moyo, akawa kama mwanaume mwingine. Alianza kumchezesha mchakamchaka bosi wake huku wakiwa gubigubi ndani ya shuka zito.

Bosi alikubali, alilalamika sana na kumuahidi mlinzi wake hiyo mabo kibao…

“Fuko…nitahakikisha unaongezewa mshahara…nitahakikisha unabadilishiwa kazi, uje kufanya kazi za huku ndani…nitakuwa nakununulia nguo…”

“Nitashukuru sana mama,” alisema Fuko…

“Kwa sasa sitisha kuniita mama, niiite mkeo…”

“Haya mke wangu…”

“Eee, hapo sawa sasa…”

Mvua ilizidi kunyesha mpaka wenyewe ndani wakaogopa mle chumbani…

“Mh! Mvua kubwa sana mke wangu,” mlinzi alisema bila woga wala kumung’unya maneno kwenye kinywa chake chenye harufu ya sigara…

“Nikumbatie zaidi, mi naogopa mume wangu,” alisema mama Joy huku na yeye mwenyewe akimkumbatia sana mlinzi wake huyo.

Fuko alitii agizo, aliongeza kumbana mwanamke huyo mpaka mwisho wa uwezo wake. Mama Joy alitangaza kuvunjia dafu lake hapo lakini wakati akijilegeza kwa zoezi hilo simu yake ikaita na kumtoa kwenye stimu…

“Siyo baba Joy huyo kweli?” alisema mama Joy huku akikurupuka kwa fujo pale kwenye godoro…



Aliifuata simu na kuiweka sikioni, lakibi ilikata. Alipoangalia namba na mpigaji ni mumewe, alipompigia ikawa haipatikani tena…

“Khaa! Sasa huyu mbona ananiweka katika wakati mgumu sana,” alisema mama Joy.

Mlinzi alimfuata na kumdaka, akamrejesha kwenye godoro chini huku akimtaka kumtendea haki kwani ‘gari’ lake lilishaongeza spidi lenyewe…

“Mke wangu nina hali mbaya,” alisema mlinzi…

“Jamani mbona hata mimi mwenyewe,” mama Joy alisema akijiweka sawa. Mpambano mwingine ukaendelea ambapo mwanamke huyo hakuchelewa akatangaza dafu linavunjika, mlinzi naye akapasua la kwake sambamba na mama Joy.

Walibaki kimya kwa muda, kila mmoja alikuwa akihema kwa kasi, wakati mwingine walitazamana kama waliotaka kuchekeana, lakini mama mlinzi aliona aibu.

Simu ya mama Joy iliita tena, akaiwahi, akaiweka sikioni…

“Baba Joy,” aliipokea kwa sauti ya chini kama vile alikuwa hataki mtu mwingine asikie…

“Nimelala ndiyo, umesafiri na mvua hii..?”

“Ooo, pole sana. Basi safari njema,” kusema ‘basi safari njema’, mama Joy alitoa sauti ya juu kuliko alipopokea simu.

Aliweka simu kwenye meza, akamfuata mlinzi na kumwangukia kwa furaha…

“Mume wangu, leo tufaidi mpaka wenyewe tuseme basi.”

“Bosi ameamua kusafiri na mvua?”

“Anasema anakaribia Kibaha Maili Moja.”

Walicheka, wakakumbatiana. Mama Joy akamtoa mlinzi kwenye godoro na kumsimamisha kisha yeye akabeba godoro na kuliweka kitandani…

“Haya! Tulale kwa raha zetu sasa,” alisema mama Joy. Alitangulia kupanda yeye, akamwita mlinzi, lakini naye kabla hajapanda, mama Joy alishuka na kwenda kwenye kabati kubwa la nguo lililomo chumbani humo na kutoa pajama pea moja...

“Vaa hii ya mista, usiku wa leo kuna baridi sana, sawa?” Mlinzi aliidaka pajama hiyo na kuitumbukiza mwilini mwake kisha akapanda kitandani kulala.

Ulikuwa usiku wenye historia kwao, walitumia muda mwingi kukumbatiana ndani ya shuka moja na kila ‘walipochaji’ walicheza ‘mechi’.

Mpaka saa saba usiku, walikuwa wamecheza mechi nne, mama Joy alianza kuwa hoi, lakini mlinzi alitaka kupasha mazoezi ili mechi ziendelee.

“Mume wangu tutaendelea kesho, mimi sasa nimechoka sana,” alisema mama Joy kwa sauti ya tabu. Ni kweli alichoka. Hakuna siku amewahi kuchezeshwa mechi mfululizo kama usiku huo.

Mpaka jua linataoka, wawili hao walikuwa wamelala fofofo, hawajitambui.

Mfanyakazi wa ndani ndiye aliyetangulia kushtuka kwamba, mama mwenye nyumba siku hiyo alikuwa amepitiliza kulala. Na aliligundua hilo baada ya geti kubwa kugongwa kwa nguvu…

“Nani huyo? Halagu mbona mama hajaamka mpaka muda huu?”

Alitoka kwenda getini ambapo alishangaa kutomwona mlinzi huku geti limefungwa kwa kufuli kwa ndani…

“Mh! Pana usalama kweli hapa..?” aliwaza mfanyakazi huyo huku moyo ukianza kupata wasiwasi hasa alipokumbuka kesi nyingi za walinzi kufanya uhalifu na kukimbia.

Alikimbilia ndani, akagonga mlango wa chumba cha bosi wake huyo huku wasiwasi ukizidi kumpanda…

“Lazima kuna tatizo, kwanza mlinzi hayupo halafu mama naye hajaamka, pengine hayupo pia. Si kawaida yake kuwa kimya asubuhi, lazima angefungulia redio,” alisema moyoni.

“Ngo ngo ngooo…” alizidi kugonga, lakini geti kubwa nje nalo liliendelea kugongwa kwa nguvu vilevile.

Mfanyakazi huyo alianza kuamini tajiri yake yupo baada ya kusikia mlio wa simu, akategemea kusikia ikipokelewa na ‘haloo’ lakini ikawa sivyo, ukimya ulitawala.

Alishika kitasa na kukitingisha kwa nguvu huku akiita…

“Bosi…”

“Bosi kuna mgeni…”

Kwa mbali, mama Joy alisikia kutingishwa kwa kitasa cha mlango, akashtuka. Alifikicha macho, akabaini jua lilishaanza kuchomoza, akakurupuka kitandani…

“We Fuko…” mwenye nyumba alimwamsha kwa fujo…

Mlinzi huyo alikurupuka naye huku akifikicha macho kwa nguvu…

“Ha! Jua limetoka, mama yangu. Kama wamekuja wageni nje itakuwaje?”

“Bosi,” aliendelea kuita yule mfanyakazi…

“Kuna nini?” mama Joy alihoji, wakati huohuo simu yake iliita tena, akachanganyikiwa zaidi…

“Mungu wangu…atakuwa nani huyo..?”

Fuko alivaa nguo zake na kufungua mlango ili atoke mbio, akakutana na macho ya mfanyakazi wa ndani…

“Ha!” alihamaki mfanyakazi…

“Ooosh,” mlinzi naye alishutuka akarudi chumbani…

“Sasa wewe unatokaje bila kuniambia, je ukikutana na huyo mama wa kazi itakuwaje?” alihoji mama Joy…

“Siyo nikikutana naye, nimekutana naye kweli, amesimama hapo mlangoni…”

“Kweli..?”

“Kweli bosi.”

Yule mfanyakazi alipokutana na macho ya mlinzi, alitoka mbio kwenda jikoni huku mapigo ya moyo yakimwenda kwa kasi ya ajabu…

“Oo…ooo…”alihema…

“Ina…ina maana…ina maana mama na Fuko ni wapenzi? Hivi ina…inawezekana kweli..?”

Mama Joy alifungua mlango, hakukuta mfanyakazi wale msaidizi wake, akatembea kuelekea jikoni, akasikia mlio wa mfuniko kwenye sufuria, akarudi chumbani mbio…
“Toka sasa, yupo jikoni…”

“Hawezi kuniona..?”

“Nimekwambia yuko jikoni sasa atakuonaje?”

Mlinzi alitoka mbio. Kufika nje akasikia geti kubwa linagongwa, akaweweseka kwanza kabla ya kwenda kumjua anayegonga…

“Siyo bosi huyo…kama ni yeye amerudi saa ngapi? Hajatuona kweli..?”

Alikimbilia getini, alipogundua bado kulikuwa na kufuli, aliingia kwenda banda na kuchukua funguo…

“Ngo ngo ngooo…”

“Nani?”

“Mimi…”

“Wewe nani..?”

“Mzoa taka…”

“Unataka nini, leo hakuna takataka hapa ndani, halafu…”

“Mama je..?”

“Mama gani, we mama yako anaishi humu ndani kwani..?”

“Mama mwenye nyumba…”

“Kwani kama hakuna taka, mama wa nini sasa?”

“Sikiliza bro, mi sioni ni kwanini unanichukia, wewe unapata liziki yako kivyako na mimi napata kivyangu, sasa…”

“Fuko ni nani huyo?” mama Joy alihoji akiwa amesimama mlango mkubwa macho kayaelekeza getini…

“Mzoa taka mama, simi sijui anataka nini mama, kwani leo kuna takataka humu ndani, mimi sijaziona,” alisema sana mlinzi…

“Wewe hujaziona kwani we ndiyo mzalisha taka? Hebu mfungulie.”

Mlinzi alifungua geti haraka sana, mzoa taka akaingia huku akiwa amebeba fuko la Rambo mgongoni…

“Karibu kijana wangu…”

“Asante mama, shikamoo…”

“Asante sana. Karibu pita.”

Mzoa taka alizama ndani ya geti akimfuata mama. Nyuma yake, mlinzi alikuwa akimwangalia kwa jicho baya ile mbaya…

“Mama mi nina wazo,” alisema mlinzi…

“Liweke wazi…”

“Hilo dude la taka lingejengwa nje…”

“Si jukumu lako,” alijibu mama Joy.

Mlinzi aliumia sana moyoni. Aliamini mzoa taka ana jambo na bosi wake, haiwezekani usiku kucha ampe mapenzi motomoto tena kitandani kwa mumewe, kisha asubuhi hiyo aanze kumgeuzia kibao na kuongea naye kama vile siku nyingine za nyuma. Alimezea lakini akaweka kitu moyoni.

Mama Joy alimshika mkono mzoa taka na kwenda naye nyuma ya nyumba ambako kuna dude la taka…

“Hivi kijana wangu unaitwa nani vile..?”

“Kofu…”

“Kofu..?”

“Ndiyo…”

“Kofu nani?”

“Kofu Nduche…”

“Mbona jina lako limefanana sana na la mlinzi wangu yule..?”

“Yeye anaitwa nani?”

“Fuko…”

“Sasa mama Fuko ni sawa na Kofu..?”

“Eee, Fuko ukiigeuza na kuanzia kwa mbele si unapata Kofu…”

“Eee, kweli. Basi ndiyo hivyo.”

Walipofika kwenye dude la taka, mzoa taka alichungulia ndani ya dude na kukutana na taka kidogo sana…

“Leo hamna kitu mama…”

“Wewe shida yako nini, si nakupa hela yako ya kuzolea…au?”

“Sawa,” alisema mzoa taka huku akianza kuingiza sehemu ya mwili kwenye dude hilo kwa lengo la kuchota takataka kidogo zilizokuwepo.

Mama Joy alimsogelea Kofu na kumshika kiuno kisha akamvuta. Jamaa alichomoka, akasimama akimwangalia mwanamke huyo…

“Vipi, leo hutaki?” aliuliza mama Joy huku akiwa amelegea macho kama aliyekula kungu manga…

“Sijui wewe…”

“Mimi niko tayari,” alisema mama Joy…

“Hata mimi, lakini leo nimechoka sana…”

“Umechokeshwa na nini?”

“Sijatia kitu tumboni tangu nimeamka.”

“Hilo tu, twende huku,” mama Joy alimshika mkono mzoa taka na kwenda naye hadi jikoni kwake…

“Kuna nini?”

Mfanyakazi wa ndani akafunua sufuria moja…

“Kuna hili pilau, halafu kuna nyama imeshaiva, ila kwenye friji kuna mikate na maandazi, keki zipo mezani, chapati zipo kwenye hotpot, lakini kama utataka samaki wa kukaanga wapo tayari kwenye friji ni wa kupasha moto tu…”

“Mh! Mwenzetu umetaja vitu vingi hadi nimesahau vya kwanza…mpe huyu maziwa na pilau,” alisema mama Joy. Alijua kwa kazi ya kuzoa taka mchana kutwa na kama toka ameamka hajatia kitu tumboni, alitakiwa chakula kizito kidogo…

“Kaa pale kwenye kiti.”

Mzoa taka alikaa akisubiri kifungua kinywa hicho ambapo moyoni alisema atakula mpaka kukomba sahani na akitoka pale ni mpaka kesho yake, fedha yote ya siku hiyo atakwenda kununulia bangi na kupiga viroba kwa wingi.

Mama Joy alikwenda chumbani kwake, akabadili nguo. Alivaa taulo akaingia bafuni kuoga. Alipotoka, alivaa khanga mbili, moja alijizungusha kupitia kwenye nido zake, nyingine kupitia kiunoni.

Akatoka kwenda jikoni ambako alimkuta mzoa taka yuko katikati ya mlo wa pilau na maziwa kwenye kikombe kikubwa…

“Vipi, changamka upate nguvu…”

“Sawa mama…”

Mama Joy naye alichukua kikombe na kujimiminia maziwa peke yake…

“Nikupe na nini mama?” aliuliza mfanyakazi…

“Hapana, maziwa yanatosha sana.”

Ukimya ulitawala jikoni, mzoa taka alikuwa akiendelea kupata ‘brekfasti’ yake, mama Joy alikuwa bize na maziwa yake huku mfanyakazi naye akijihudumia mwenyewe.

Mzoa taka alitangulia kumaliza kila kitu…

“Hebu muongeze mgeni maziwa na pilau,” alisema mama Joy lakini mzoa taka aligoma. Ilikuwa lazima agome hata kama anavuta bangi. Maana wavuta bangi wanasifika kwa kula sana, lakini pale alipewa maziwa kwenye kombe kubwa, pilau kwenye sinia na si sahani…

“Mimi nimeshiba sana…”

“Ongeza japo kidogo, we mwanaume bwana,” alisema mama Joy…

“Hapana mama, kesho.”

Mama Joy naye alitelekeza kikombe chake chenye maziwa na kutoka na mzoa taka hadi kwenye dude la taka…

“Sasa, si tayari umeshiba?”

“Nimeshiba sasa…teh! Teh! Teh!” alicheka mzoa taka huyo huku jasho jembamba la shibe likimchuruzika kuanzia kichwani.

Mama Joy alimsogelea mpaka akamkumbatia, akampiga busu. Mzoa taka naye akamrudishia kwa busu. Mama Joy akaenda mbele zaidi, akaomba denda licha ya kwamba kinywa cha mzoa taka huyo kilikuwa kikitoa harufu ya sigara.

“Mwee, ulimi wako una kajoto kazuri,” alisema mama Joy huku akimung’unya mate ya mzoa taka huyo ambaye mwenyewe alikuwa akijiuliza ni kwanini mwanamke huyo mwenye mume tajiri ameangukia kwake tena mchafumchafu asiye na thamani mbele za watu.

Aliwaza jinsi wanawake mitaani wanavyomkataa kwa sababu ya uchafu wake na mibangi anayovuta…

“Mm…au mganga wake alimwambia atembee na mwanaume mchafumchacfu nini?” alijihoji mwenyewe.

Mama Joy, licha ya kulala na kuamka na mlinzi wake, lakini muda huo alijikuta akichemka kwa kutaka penzi tena.

Alimshika mzoa taka na kumlaza pembeni ya dude la taka, akamvua nguo, akavua na zake, wakaanza ligi ya mapenzi huku mwanamke huyo akimiminika wingi wa maneno ya mahaba.

Mlinzi, yaani Fuko alihisi kuna kitu kinachoendelea kwenye dude la taka kwa vile toka bosi wake huyo alivyomshika mkono mzoa taka na kuzama naye maeneo hayo hakurejea tena, hakujua kama mzoa taka alipelekwa hadi jikoni akala pilau na maziwa.

Alisukuma geti kulifunga lote kisha akaanza kutembea kuelekea kwenye dude la taka, aliamini atakutana na fumanizi japo akili nyingine ilimwambia endapo atawafumani kweli ajue na kibarua kitakuwa kimeota nyasi.

Upande mwingine alijua hawezi kufukuwa kwa sababu ishu si kikazi ila wivu wa kimapenzi…

“Itakuwa alale na mimi halafu mzoa taka kaja anampapatikia vile, lazima kuna kitu wanakifanya,” alisema moyoni mlinzi.

Alipotokea kwa mbali alianza kuona miguu minne ikiwa imefungana pamoja, akashtuka…

“Si nilisema mimi,” alisema moyoni. Miguu hiyo ilikuwa ikipishanapishana kwa kuingiliana kwa staili mbalimbali. Mlinzi aliweza hata kujua miguu ya mzoa taka ni ipi na ya tajiri yake ni ipi.

Alichofanya, alikimbilia jikoni kwa mfanyakazi wa ndani…

“Dada nanihii, nenda kwenye dude la taka haraka sana ukaone…”

“Kuna nini kwani Fuko..?”

“Nimekwambia we nenda, husikii…”

“Sasa nitakimbilia sehemu kutazama kitu ambacho sikijui, pengine nikikiona nitaogopa je?”

“Shauri zako,” alisema mlinzi na kutoka.

Nyuma, mfanyakazi huyo aliamua kwenda kwenye dude la taka huku akili yake ikiwa haiwazi atakutana na kitu gani.

“Ha..!” alishtuka sana mfanyakazi huyo ambaye kiumri alikuwa amempita mama Joy.

Mama Joy naye alishtuka kusikia hamaki ya mfanyakazi wake, akamsukuma mzoa taka kisha yeye akasimama haraka sana huku akihema kwa kasi…

“Mama…” alisema yule mfanyakazi…

“Mama nini? Unasemaje kwanza?”

Mfanyakazi alikimbilia ndani huku akilia. Kwake yeye kitendo alichokiona alikichukulia kama nuksi au mkosi, pia alihisi kujidhalilisha nafsi kwani hakukitegemea..

“Yaani bosi! Anazini na mtoto mdogo yule! Tena mchafuuu! Mh! Ama kweli dunia imekwisha! Loo!” mfanyakazi huyo alisema hayo moyoni mwake.



***



Mama Joy, baada ya kumwona mfanyakazi wake amekimbia, alihisi heshima kubwa amepata…

“Mimi naona twende chumbani kwangu, hapa wala siko huru, kama ameanza kuja huyu anaweza kutokea mwingine,” mama Joy alimwambia mzoa taka…

“Chumbani mwako! Kitandani?” mzoa taka alishangaa na kumuuliza…

“Kwani kuna nini?”

Wakati mama Joy anamwambia mzoa taka kwani kuna nini, alishamshika mkono na kwenda naye kupita kwenye mlango mdogo wa nyuma ambapo si rahisi kuonwa na mtu.

Mlinzi pale getini alikwenda tena kwa kunyata hadi akafika eneo ambalo kuna nguzo nene, akasimama ili ajipange tena kwenda jirani na dude la taka…

“Safari hii nikiwakuta bado wanazini nawafumania, nitamwambia bosi habari hii nitamwambia mume wake akirudi safari, najua hatataka,” alisema moyoni mlinzi.

Alishangaa sana kutowakuta pale chiji ya dude la taka, akabaki kutumbua macho pima huku akijiuliza ni wapi wawili hao wanaweza kuwa wamekwenda kumalizia kula ‘uraha’ wao…

“Au wamekwenda choo cha nje kule? Haiwezekani! Labda wamekwenda kule nyuma kabisa,” alisema huku akienda nyuma ya nyumba ambako pia hakuwakuta…

“He! Au wameingia ndani kabisa?”

Alikwenda jikoni, akamkuta yule mwanamke wa kazi amekaa kwenye kiti huku akilia…

“Nini tena? Amekufokea?”

“Mh! Siwezi kulia kwa kufokewa na tajiri wangu wa kazi hata siku moja, ila mimi nimemshangaa sana bosi, yule kijana ni mchafu sana halafu sijui anavuta bangi. Lakini eti yeye amelala naye kama mpenzi wake! Unajua sijawahi kusikia achilia mbali kuona,” alilalama mwanamke wa kazi…

“Kwani uliwakutaje?” mlinzi aliuliza…

“Wako ‘kazini’…”

“Walipokuona?”

“Mama akamsukuma yule kijana, halafu akaanza kunijia juu, mimi nikaondoka,” alisema mfanyakazi wa ndani huku akiangaliaangalia nje kwa tahadhari kubwa…

“Mama huyu…”

“Lakini we Fuko, mbona na wewe umelala kwa bosi usiku wa kuamkia leo?”

“Si ndiyo hapo sasa hata mi mwenyewe najiuliza, kwanini alale na mimi halafu alale na mzoa taka? Usikute ni mambo ya kishirikina,” alisema mlinzi…

“Kwani wewe ulikuwaje hadi mkalala kitandani na kuzini?”

“Alinitongoza..!”

“Alikutongoza..?”

“Sasa wewe dada unavyoona mimi naweza kumtongoza huyu bosi, nitaanzia wapi kwanza? Au unadhani mzoa taka alimtongoza? Huyu mama ni mtaalam wa kutongoza, huenda hata mumewe alimtongoza.”



***

Mama Joy alimtumbukiza chumbani kwake mzoa taka ambaye alifikia kushangaashangaa chumba kilivyo kikubwa na vitu vingi…

“Mh! Si nitachafua hapa leo?” ndani ya moyo wake aliamini hivyo…

Alimshika kijana huyo na kumuegemeza kifuani kwake huku akimwambia maneno matamu ya mahaba…

“Mpenzi wangu, nataka nikiachana na wewe leo nisitamani mwanamke mwingine mpaka ipite wiki moja, sawa?”

“Sijakulewa.”

“Nasema hivi, tukipanda kitandani sasa hivi ufanye mambo mazuri sana, nataka tukimaliza leo nisiwe na hamu ya mwanaume mpaka wiki moja ipite.”

“Sawa.”

Mama Joy alimvua nguo mzoa taka na kubaki na ‘kufuli’ tu, kisha akavua na za kwake. Alitangulia kupanda kitandani, mzoa taka akafuatia akiwa na wasiwasi, hamu ya mapenzi hakuwa nayo kama ilivyokuwa kule nje kwani mazingira ya chumba na alivyo yeye vilikuwa vitu viwili tofauti…

“Sijui ananisema mi mchafu sana,” aliwaza…

“Sasa mbona jogoo mwenyewe hawiki, una nini?” aliuliza mama Joy huku akijaribu ‘kumtoa’ jogoo kwenye banda ili aende nje akawike, lakini wapi!

“Kijana, una nini mpenzi wangu, mbona hivi..?”

“Hata mi sijui, lakini tungeenda kule nje kwenye majani ndiyo kuzuri…”

“Mimi nje siwezi, we si umeona hali ilivyokuwa kule nje, kwani tatizo lako nini?”

“Sina uhuru na humu chumbani kwako, kuko kama ikulu bwana…”

“Umewahi kufika ikulu wewe?”

“Si wanasemaga kuzuri sana…”

“Sasa ikulu hakuna wafanyakazi wa kufanya usafi?”

“Mi sijui, lakini bado naogopa sana…”

“Unamuogopa mume wangu..?”

“Hapana, ila ntachafua…”

“Nini..?”

“Mashuka yako, mi sijaoga toka juzi ilee.”

“Wala usijali, mfanyakazi yupo atafua mashuka, we tulale hapahapa, lakini fanya nilivyokwambia, nikomeshe kabisa leo,” alisema mama Joy huku akipeleka mkono kwenye jogoo la mzoa taka huyo.

Kwa mbali, alianza kuwika kwani mzoa taka alihakikishiwa amani yake.



***

Fuko na mfanyakazi wa ndani walitoka kiaina kwenda kuwachungulia wawili hao kule nje, wakawakosa…

“Ha! Watakuwa wamekwenda wapi?” aliuliza mlinzi…

“Hawa wamekwenda chumbani. Hakuna sehemu nyingine wanayoweza kwenda zaidi ya huko,” alijibu mfanyakazi.





***

Baba Joy alikuwa amemaliza mambo yaliyompeleka Arusha, sasa alikuwa amekaa kwenye mgahawa akibadilishana mawazo na wenyeji wake…

“Unajua bwana, mwanamke siku zote anatakiwa kujitambua. Ukikuta mwanamke hajitambui ujue kazi unayo we mwanaume…” alisema mmoja wa wenyeji hao aitwaye Molleli…

“Ni kweli. Wanawake wa sasa wengi hawajijui. Utakuta mwanamke mke wa mtu lakini bado anapenda magenge, anapenda makundi, anataka awe anatoka na marafiki zake. Halafu ogopa sana mke wa mtu akiwa anapenda kuwa na ukaribu na vijana vijana…”

Baba Joy aliguna hapo. Akakumbuka jinsi mkewe alivyo na ukaribu na mzoa taka kiasi cha kumkaribisha ndani kwake hata giza likiwa limeingia.

Palepale alichukua simu yake iliyokuwa mezani na kumpigia simu mlinzi…

“Hujambo Fuko..?”

“Sijambo bosi, shikamoo…”

“Marhaba, mama Joy yupo..?”

“Yupo bosi…”

“Na nani..?”

“Unasema..?”

“Nakuuliza yupo na nani..?”

“Nani mama..?”

“We una akili kweli? Unadhani nakuuliza kuhusu nani..?”

“Nimekujibu bosi, nimesema mama yupo…”

“Yupo na nani..?”

“Unasema?”

Baba Joy alikata simu kwa hasira. Lakini akili ikamwambia kuna kitu ndiyo maana mlinzi anajibu maswali yote kasoro hilo tu! Aliisachi namba ya mkewe, akampigia.



***

Mama Joy alikuwa akimbembeleza mzoa taka akubali kulala kitandani na aondoe mawazo kwani ndiyo yanayomfanya jogoo ashindwe kuwika….

“Haa! Mume wangu huyo anapiga…

“Haloo…”

“Uko wapi wewe..?”

“Nani mimi..?”

“Unaniuiliza swali gani hilo..?”

“Niko nyumbani…”

“Na nani..?”

“Nani mimi..?”

“Mama Joy…”

“Abee…”

Baba Joy alikata simu. Alianza kuhisi kitu kikubwa zaidi. Akampigia mfanyakazi wa ndani…

“Za safari bosi..?”

“Njema, upo nyumbani..?”

“Ndiyo bosi…”

“Mama je..?”

“Yupo bosi…”

“Yupo na nani..?”

“Nani mama..?”

“Hivi nyiye hapo nyumbani pana nini leo..?”

“Kwa nini bosi..?”

“Mbona hammalizi kujibu badala yake mnauliza maswali… nimekuuliza mama je, yupo hapo nyumbani? Badala ya kunijibu unaniuliza na wewe ‘nani mama?’” alifoka baba Joy…

“Samahani sana bosi, mama yupo na mgeni wake…”

“Mgeni gani…?”

“Kijana mmoja hivi…”

“Huyo kijana we unamjua..?”

“Namjua bosi, anakujaga kuzoa taka...”

“Kumbe ni yule mzoa taka siyo?” aliuliza baba Joy huku akisimama kwenda kuongelea pembeni maana aliona pale siri zake zitakuwa nje…

“Ndiyo bosi…”

“Wako wapi muda huu..?”

“Naona wapo…ooooo, wapo sebuleni bosi…”

“Yaani huyo mzoa taka anakaa sebuleni kwangu..!”

Moyoni mfanyakazi huyo alisema…

“Ungejua wako chumbani kabisa, ungepaa na ndege utue Dar ufumanie.”

“Haya, asante sana,” baba Joy akakata simu. Alisimama kwa muda, kisha akampigia tena mfanyakazi huyo…

“Haloo bosi…”

“Sasa sikia, akiwa anatoka huyo mbuzi nibip…”

“Sawa bosi.”

Baada ya kukata simu, mfanyakazi huyo wa ndani alimwangalia mlinzi…

“Unajua bosi amejua..?”

“Hata mimi kaniuliza hivyohivyo. Nilishikwa na kigugumizi kama wewe mwanzo,” alisema mlinzi…

Mzoa taka na mama Joy walitumia dakika kama ishirini kule chumbani. Wakati wanatoka, mama Joy alitangulia mbele akifuatiwa na mzoa taka kwa nyuma.

Walizunguka kwenda kwenye dude la taka, mzoa taka akachukua fuko lake akasindikizwa hadi getini. Alichopewa na mwanamke huyo anakijua mwenyewe.

Mfanyakazi wa ndani alipogundua hilo alimbip baba Joy, naye akapiga haraka...

“Bosi wametoka tayari,” mfanyakazi alisema kwa sauti ya chini sana…

“Mama Joy kamsindikiza mpaka wapi?” baba Joy aliuliza huku akiinua mkono wa kushoto juu na kuutingisha ili aweze kusoma saa…

“Kamfikisha getini tu…”

“Haya, sasa sikia, mimi nitarudi kesho, nikifika mjini sitakuja nyumbani mpaka huyo mwanaharamu aje, kwani si anakujaga kila siku?”

“Ndiyo bosi.”

“Haya, nashukuru sana ee..?”

“Sawa bosi.”

Baada ya kukata simu, mama Joy alitokea jikoni…

“We mbona unaongea kwenye simu kwa kunong’ona sana, unaongea na nani?”



“Shangazi yangu anasema anaumwa sana bosi…”

“Sasa kama shangazi yako anaumwa ndiyo uongee kwa kunong’ona..?”

“Anasema hajisikii vizuri bosi…”

“Khaa! Sasa asipojisikia vizuri yeye ndiyo inakufanya wewe uongee kwa kunong’ona..?”

“Nisamehe mama…”

“Hapa nyumbani kwangu karibu nitawaachisha kazi watu maana nahisi kama mmeanza kunifanyia ushushushu kwenye nyumba yangu, mimi sitaki,” alisema mama Joy akiwa amesimama huku amemshikia kiuno. Akaendelea…

“Unanichimba siyo?”

“Sikuchimbi bosi…”

“Ulikuwa unaongea na nani? Maana najua siyo shangazi yako…”

“Shngazi bosi, kweli tena…”

“Nikikwambia unipe simu nione nitakuta namba ya shangazi yako..?”

“Ngoja mama nikwambie ukweli…”

“Niambie…”

“Kuna mzee mmoja wa nyumba ya tatu hapo, huwa ananitaka. Ndiye amekuwa akinipigia simu kila mara. Sasa hivi amenipigia anasema kama sina kazi niende tukale japo denda, sasa nilikuwa namuuliza denda ni nini..?”

“Sasa ulikuwa unanificha nini..?”

“Nilijua utakasirika bosi…”

“Nikasirikie nini?”

“Utajua kumbe naachaga kazi nakwenda kukutana na wanaume nje.”

“Sasa mi nikasirike nini? Wewe si mtu mzima bwana! Lazima utataka kuguswaguswa, kutekenywatekenywa, kushikwashikwa na kupewa jotojoto,” alisema mama Joy huku akionesha kwa viitendo maneno aliyokuwa akiyasema, mfanyakazi huyo akawa anacheka na nguvu ikaanza kumrudia kwa mbali…

“Au siyo, mimi sina wasiwasi hata nikikuona unaingiza mwanaume ndani, ilimradi baba Joy asijue tu, mimi mzungu bwana,” mama Joy alikazia huku akitoka.

Baada tu ya kuondoka, mfanyakazi huyo alifuta ile namba ya baba Joy kisha akaminya namba za shangazi yake kama alitaka kupiga lakini hakupiga.



***

Mzoa taka alikuwa kijiweni na wachafau wenzake. Mazungmzo yao yalitawaliwa na maneno ya kihuni huku wakichimbana mikwara kibao…

“Jamani masela ee…kuna mke wa mnene mmoja ameiva kwangu ileile…kila siku nikienda kuchukua taka ananipa chombo natumia, ameshaniingia hadi room, yaani yuko sawa ile mbaya.”

Wenzake walimkatalia, yeye akawaapia. Alitumbukiza mkono mfukoni na kutoa elfu hamsini…

“Hii amekata leo baada ya kumwendesha kitandani, mwanamke hasikii, sura yangu inamponesha kichefuchefu.”

Masela wenzake walianza kumsakama walitaka aigawe ile elfu hamsini…

“Mwana mzuka basi, ichanechane hiyo fifte, watu tukaning’nie kwenye sembe.”



***

Mama Joy alitembea hadi kwa mlinzi…

“Hebu fungua geti…”

“Unataka kwenda wapi bosi..?”

“Si juu yako kujua..?”

“Mzee anaweza kuniuliza…”

“Kwani hana simu yangu..?”

“Mbona leo alinipigia mimi…”

“Kuhusu nini..?”

“Aliniuliza kama upo.”

Mama Joy alisimama, akageuza…

“Alikuuliza kama mimi nipo? Ukamjibuje..?”

“Nilimwambia upo, akauliza upo na nani..? sikumjibu…”

“Mh!” aliguna mama Joy, akakumbuka muda ule mumewe alipompigia simu wakati yeye anambembeleza mzoa taka na maongezi yao yakawa hivi…

Anamwambia mzoa taka…

 “Haa! Mume wangu huyo anapiga…Haloo…”

“Uko wapi wewe..?”

“Nani mimi..?”

“Unaniuliza swali gani hilo..?”

“Niko nyumbani…”

“Na nani..?”

“Nani mimi..?”

“Mama Joy…”

“Abee…”

Baba Joy anakata simu.

Mama Joy alianza kuhisi kuna kitu mumewe amekinasa, akahisi kizunguzungu kichwani…

“Fuko hebu sema ukweli wako, hujamwambia nipo na mtu mwingine ndani..?”

“Sikumwambia mama, labda kama aliongea na Helena.” Helena ni yule msaidizi wa kazi za ndani…

“Mh!” aliguna mama Joy, akakumbuka mambo haya…

“We mbona unaongea kwenye simu kwa kunong’ona sana, unaongea na nani?”

“Shangazi yangu anasema anaumwa sana bosi…”

“Sasa kama shangazi yako anaumwa ndiyo uongee kwa kunong’ona..?”

“Anasema hajisikii vizuri bosi…”

“Khaa! Sasa asipojisikia vizuri yeye ndiyo inakufanya wewe uongee kwa kunong’ona..?”

“Nisamehe mama…”

Mama Joy aligeuza, akarudi ndani. Alipitiliza hadi jikoni…

“We dada…”

“Abee bosi…”

“Baba Joy alikupigia simu leo..?”

Mfanyakazi huyo kwanza alisita kujibu, akili ilijipeleleza ili kutafuta je ajibu ni kweli au akatae?

“Hapana bosi…”

“Hebu lete simu yako.”

Helena aliitoa simu haraka sana huku akionesha unyenyekevu wote. Mama Joy alikwenda kwenye namba zilizopigwa, hakuiona ya mumewe, akaenda zilizopiga pia hakuiona, ila aliikuta ile ya shangazi ikiwa ameseviwa kwa jina la ‘Anti Suzy’…

“Oke, nisamehe sana kwa kukagua simu yako, maana kuna mtu ameniambia baba Joy alikupigia…

“Hapana mama, hajanipigia.”

Mama Joy alirudi sebuleni, akakaa kwenye kochi. Aliwaza kidogo, akampigia simu mumewe.

Sauti ya baba Joy ilikuwa nzito kupindukia…

“Haloo…”

“Halo, baba Joy…”

“Nini?”

“Khaa! Asa mbona unapokea simu unaniuliza nini..?”

“Ulitaka nikuulizeje..?”

“Unajua nataka kukwambia nini..?”

“Wewe mwanamke wewe, usiniletee usanii mimi, we endelea tu,” baba Joy alikata simu.

Mama Joy alibaki ameishika simu yake huku mikono ikitetemeka na wasiwasi juu…

“Helena,” kwa mara ya kwanza alimuita kwa jina mfanyakazi wake huyo…

“Abee bosi…”

“Haraka sana.”

Sekunde kadhaa, Helena akawa amefika…

“Kamuite na Fuko.”

Helena alitoka hadi kwa mlinzi…

“Bosi anatuita, lakini usoni kama hayuko sawasawa…”

“Aah! Kakwambiaje kwani?”

“Kwanza we ndiyo ulimwambia mimi nilipigiwa simu na mumewe..?”

“Sikusema hivyo, nilisema labda alikupigia na wewe, nilitumia neno labda.”

“Nyiye,” mama Joy aliwaita akiwa amesimama nje ya mlango mkubwa.

“Tunakuja mama,” alisema mlinzi huku wakitembea kwa kasi kuelekea alikosimama.

Mama Joy alipowaona wamekaribia, aligeuka kutangulia ndani…

“Tumefika mama…”

Mama Joy aligeuka kuwaangalia kisha akakaa kwenye kochi…

“Nani kati yenu ni mnafiki kwangu..?”

Wote wawili waliangaliana kwa nyuso zenyen wasiwasi…

“Nauliza nani kati yenu ni mnafiki kwangu..?” safari hii mama Joy aliongea huku akipandisha sauti juu…

“Labda mwenzangu bosi, mimi siwezi kuwa mnafiki kwako, hata wewe bosi unajua, ningekuwa mnafiki mzee aliponiuliza uko na nani si ningesema upo na mzoa taka na pia ningesema na mimi niliamkia kwako…”

“Wewe Helena ndiyo mnafiki siyo..?”

Mfanyakazi huyo alitulia kwa muda akimkazia macho bosi wake kisha akasema…

“Mimi si mnafiki kwako bosi, ina labda dhamira inakusumbua…”

“Dhamira inanisumbua..?”

“Ndiyo bosi…”

“Una maana gani..?”

“We bosi unajua mwenyewe, sisi na wewe tuko kwa muda gani, lakini leo hii tuje kuanza unafiki kwako ni kweli..?”

Mama Joy alitulia kwa muda akitafakari, kisha akawaambia…

“Ondokeni zenu.”



***

Siku ya pili, Helena alikuwa akinywa chai jikono wakati simu yake ilipoita. Alikimbilia kuangalia kwenye kioo ni nani aliyepiga…

“Mh!” aliguna kwanza. Alikuwa baba Joy…

“Shikamoo bosi…naomba utume meseji hali mbaya sana wenzio huku nyumbani,” alipomaliza kusema akakata simu.

Baba Joy alihema kwa kasi akijiuliza maswali mengi. Alijikuta akiyarudia yale maneno ya mfanyakazi wake wa ndani…

“Shikamoo bosi…naomba utume meseji hali mbaya sana wenzio huku nyumbani…”

“Kunaweza kuwa kumetokea nini?” alijiuliza. Pia akajiuliza atume meseji au asitume?

Baada ya kuwaza na kuwazua kama dakika tano, aliamua kutuma meseji…

“Kuna nini kwani?” baba Joy aliituma meseji hiyo. Akakaa akisubiri majibu…

“Mkeo kama ameshtuka ulivyonipigia simu, lakini hajaonesha kuamini ila kama anataka kuamini. Tuma meseji tu.”

Baba Joy alikaa kwa muda kisha akamtumia meseji…

“Mimi narudi leo, niko njiani hapa tayari. Nitafikia mahali, mzoa taka akija tu, niambie.”

“Sawa bosi wangu.”



***

Baba Joy aliendesha gari kwa kasi huku kichwa chake kikiwa kimejaa mawazo kibao, hasa ya wivu wa mapenzi. Hapo alikuwa akipita Chalinze…

“Iko siku kila kitu kitakuwa wazi,” alisema moyoni.

Mara simu yake iliita, akaangalia kwenye skrini kisha akasonya. Alikuwa mkewe ndiyo maana alisonya, moyoni alitamani namba aibadilishe, badala ya kuwa My Wife, iwe Malaya wa Mjini…

“Nini?” baba Joy aliuliza kwa sauti iliyojaa machugu…

“Khaa! Yaani unapokea simu yangu na kuniuliza nini…”

“Sema unachotaka kuniambia, kama vipi kata simu…”

“Nakuuliza uko wapi kwani?”

“Arusha Mjini…”

“Ha! Hurudi leo..?”

“Kesho,” baba Joy akakata simu.

Mama Joy alihema kwa kasi. Alijua mambo yameharibika, lakini alijipa moyo kwamba Mungu mkubwa!

Kisa cha mama Joy kuulizia hayo, alijua mzoa taka angefika muda wowote ule kwani jana yake alipoondoka alimwambia asikose kuja kesho.

Alitoka hadi getini…

“Fuko…”

“Ndiyo bosi,” Fuko aliitika kwa heshima zote…

“Hakuna mgeni wangu..?”

“Hakuna bo…”

“Ngo ngo ngooo,” geti kubwa liligongwa…

“Labda huyo…”

“Hebu fungua.”

Fuko alifungua geti, macho ya mama Joy yalikuwa makini kutaka kujua ni nani anaingia maana nyumba yake huingia watu wengi…

“Shikamoo mama,” alikuwa mzoa taka bwana!

Siku hiyo alilipuka kwa suruali ya ‘jinsi’ ya mtumba na t-shirt pia ya mtumba iliyoandikwa kifuani I AM NO BODY! Nguo zote hizo alitokelezea nazo bila kuzifua. Ile 50,000 aliyohongwa na mama Joy jana yake ndiyo alifanyia shoping hiyo.

Mama Joy alianza kwa kuachia tabasamu kabla ya kuitikia shikamoo hiyo, alimkazia macho mzoa take…

“Kofu…”

“Naam mama,” mzoa taka aliitika akiwa ameshika fuko mkononi…

“Umependeza sana leo baba…”

“Asante mama.”

Kifupi, mama Joy alitokea kumpenda sana mzoa taka kuliko mlinzi kwa sababu moja kuu. Mzoa taka alikuwa akimbeba mpaka juu ya mlima wakati mlinzi kila alipokuwa akikaribia mlima alishidwa na kurudi nyuma.

Mama Joy alimshika mkono mzoa taka na kwenda naye ndani, sebuleni lakini alipofika mlangoni, mzoa taka huyo aliweka pembeni fuko lake…

“Hebu njoo wewe,” alimuita mfanyakazi wake…

“Hujambo kijana?” mfanyakazi alimsalimia mzoa taka.

“Sijambo, shikamoo.”

“Marahaba…”

“Hebu mpe huyu juisi au maziwa ya moto kama yapo.”



***

Baba Joy alikuwa akipita Mizani ya Kihaba, meseji ya Helena ilipoingia kwenye simu yake…

“Mwenzio mzoa taka ameingia sasa.”

Baba Joy alisukuma mafuta kwa kasi ya ajabu, baadhi ya magari yaliyokuwa yakitoka kwa mbele yake yalipisha pembeni yakiamini kuna tatizo.

Ndani ya dakika ishirini tu, baba Joy alifika nje ya geti la jumba lake la kifahari, akasimama huku mlinzi akiwa hajui kama bosi wake yuko nje. Alimtumia meseji Helena…

“Bado yumo ndani?”

“Yumo. Walikuwa sebuleni, sasa wameenda chumbani kwako wenzio. Da! Mzoa taka bosi yupo kwenye kitanda cha mama mwenye nyumba. We ukifika Dar njoo hadi nyumbani kwako.”

Baba Joy alitamani kupaa. Hakutaka kupiga honi ili afunguliwe geti, akafungua mlango na kushuka.

Alipofika getini alilisukuma. Kwa bahati njema, baada ya mzoa taka kuingia, mlinzi alisahau kulifunga geti hilo kama ilivyo kawaida yake…

“Ha! Shikamoo bosi…mi sihusiki lakini. Halafu tulimwambia mama hakutusikia,” alisema mlinzi.

Baba Joy alimpuuza na kutembea kwa kasi kwenda ndani. Hakushuka na brifkesi wala kitu chochote kile kingine.

Alipofika kwenye mlango mkubwa alishtuka kwanza kwa kuona fuko chafuchafu la mzoa taka.

“Huyu mwanaharamu leo namtoa ubongo, ndiyo dawa pekee,” baba Joy alisema moyoni akiwa sebuleni sasa. Akakumbuka kuwa, aliposhuka alisahau bastola kwenye gari lake, akairudia.

Mlinzi alishangaa sana kumwona bosi wake akitoka mbio…

“Kuna nini bosi, mbona unakimbia hivyo?”

“Shii,” baba Joy alimkataza mlinzi kwa kuweka kidole kwenye midomo.

Sauti ya mlinzi ilimfikia mama Joy kule chumbani, akashtuka kidogo...

“Mh!” aliguna…

“Vipi?” mzoa taka alimuuliza…

“Mlinzi wangu sijui anaongea na nani?”

“Si kuna mama mwingine anafanya kazi ndani kwako…”

“Ee, labda huyo.”

Kwa bahati mbaya sana, mama Joy aliisikia sauti ya mlinzi wake lakini hakujua alichokuwa akikiongea. Aliachana na mambo ya nje kwa mlinzi na kumgeukia mzoa taka…

“Baby wangu, leo itakuwa kama jana..?”

“Kuhusu nini..?”

“Mambo yetu…”

“Yapi..?”

“Aaah! Nataka tukimalizana mimi na wewe nisimfikirie mwanaume mwingine tena leo.”

“Wewe tu, mimi mbona niko poa wangu.”

Mama Joy alimshika mzoa taka, akamvutia kwake na kumuomba denda kwa ishara. Lakini ghafla machale kama yalimcheza, alichukua simu ya mezani na kupiga getini…

“Halo getini hapa, Fuko naongea…”

“Nimesikia sauti yako ja juu sana, ulikuwa unaongea na nani?”

“Siyo mimi mama,” mlinzi alijibu…

“Una uhakika..?”

“Ndiyo bosi.”

Mama Joy akakata simu.



***

Baba Joy alisukuma geti, akazama akiwa na bastola mkononi…

“Ili aniheshimu lazima nimbandue jicho la kushoto,” alisema moyoni baba Joy.



***

Mama Joy na mzoa taka wake, walizama katika denda kiasi kwamba, walikuwa wakichuruzisha mate. Muhemko wa mama Joy ndiyo uliosababisha mzoa take asimcheleweshe, akamshika na kumpindulia kitandani sasa…

“Waooo,” alisema mama Joy akijifanya anasikia raha.



***

Baba Joy alijiuma kidole akakunja uso. Alikumbuka mlango wa gari haukufungwa na ndani mlikuwa na fedha nyingi sana zikiwa waziwazi, akageuza na kutoka.

Wakati anatoma alibamiza mlango mkubwa wa sebuleni hali iliyomfanya mkewe, mama Joy agundue kuwa kuna mtu ama ameingia sebuleni kwake au ametoka.

“Na lazima mtu huyo atakuwa si mlinzi, maana mlinzi hawezi kuingia sebuleni kwangu bila ya ruksa,” alisema moyoni mama Joy, akatoka kitandani, akachukua khanga na kujifunga maana tayari alishavua nguo na kubaki kama alivyoingia duniani kwa mara ya kwanza…

“Kama ni mlinzi leo atanitambua. Ina maana kuwa na yeye kwa siku moja tu ndiyo ameshapata tiketi ya kufanya anavyotaka?”

Alipofika sebuleni, alishtuka kumwona mume wake akiingia getini tena akiwa kasi…

“Ooh! Mungu wangu nimekwisha mimi,” alisema mama Joy na kukimbilia chumbani. Alimkusanya mzoa taka na nguo zake na kumvuta kutoka naye hadi jikoni ambako mfanyakazi alikuwepo akiendelea na shughuli zake.

Mfanyakazi huyo alijifanya ameshtuka sana kuliona tukio hilo, lakini alikuwa analijua litakuwepo tu.

Mama Joy baada ya kumtelekeza mzoa take jikoni alirudi chumbani haraka, akaweka shuka vizuri na kujifanya amekaa.

Mlango ulisikumwa kwa nguvu, baba Joy akazama ndani huku akihema kwa kasi ya ajabu…

“Yuko wapi?” ndiyo swali alilomuanza nalo mkewe…

“Yuko wapi nani?”

“Huyo mzoa taka wako…”

“Mzoa taka wangu! Yupi huyo?” mama Joy alijibalaguza ingawa ukweli alikuwa akiujua. Alikuwa akitetemeka maana mumewe alishika bastola.



***

Kule jikoni, Helena alihisi mambo yataharibika zaidi kwa ndoa ya mabosi wake, alichofanya, alimchukua mzoa taka kumpeleka nje kwa njia ya uani.

Mlinzi getini alitaka kulipua bomu, lakini Helena akamuwahi…

“Unataka kusema nini, wewe je, hujawahi kulala kwa mama? Sema na mimi nikusemee.”

Mzoa taka alipitishwa, akasepa zake akiacha lile fuko chafu la takataka.



***

“Mimi si mwendawazimu eti niulizie nani halafu pasiwepo mtu, nina ushahidi wote kwamba yupo,” alisema baba Joy huku akiinama kwa lengo la kuchungulia chini ya kitanda…

Mama Joy alibaki kimya kwani aliamini kuingiza maneno mengi kusha aende akamnase jikoni angewamaliza wote, hata yeye.

Baba Joy alipoona mvunguni mwa kitanda hola, alilifuata kabati la nguo, akafungua humo, lakini hamkuwa na kitu, akaenda chooni ambako pia hakuona kitu.

Alitoka kwa hasira akimwacha mkewe chumbani hadi jikoni, hola. Akaenda kwenye vyumba vinne vya wageni, hamna kitu. Akenda chumbani kwa mfanyakazi…

“Si kawaida yangu kuingia humu lakini leo nimelazimika,” alisema baba Joy akitoka. Aliamua kwenda uani kwa nyuma ambapo ili afike huko lazima apitie jikoni, akakutana na Helena akiwa anaingia kutoka kumsindikiza mzoa taka…

“Hujambo..?”

“Sijambo bosi, habari za safari..?”

“Nzuri, mbona sijamwona..?”

“Hayupo ndani..?”

“Sijamwona, nimekuja hadi chumbani kwako lakini hamna kitu.”

“Kha! Atakuwa amekwenda wapi sasa? Aliingia naye lakini.”

“Au uliona vibaya, si ajabu aliingia kuzoa taka na kuondoka zake. Lakini hapana, huyu atakuwemo humuhumu ndani maana mlangoni nimekuta fuko lake chafu, linanuka,” alikandia baba Joy huku akitoka uani ambako pia hakufanikiwa kumwona mzoa taka. Hapo, bado mkononi alishika bastola yake tayari kwa kumtegua shingo mwizi wake.

Baba Joy alikwenda hedi getini…

“Fuko…”

“Yes boss…”

“Kuna mtu katoka baada ya mimi kuingia..?”

“Muda huu..?”

“Ndiyo muda huu…”

“Unataka kusema nini, wewe je, hujawahi kulala kwa mama? Sema na mimi nikusemee.”

Mlinzi alipokumbuka maneno hayo ya Helena, alijikuta akifunga kinywa chake…

“Sijaona mtu bosi…”

“Una uhakika..?”

“Kabisa kabisa bosi wangu…”

“Sasa funga geti, usifungue mtu kuingia wala kutoka hadi nitakaposema mimi.”

”Sawa bosi,” alisema Fuko kwa utii wote huku akimwangalia baba Joy kwa macho ya kuibia. Kama baba Joy angekuwa makini angegundua jambo geni kwenye macho ya Fuko…

“Nikisikia amepita mtu hapa mimi na wewe wewe na mimi.”

“Hapiti mtu bosi, si kuingia si kutoka.”

Baba Joy alikwenda ndani, alikagua kila sehemu ambayo aliamini inaweza kuwa na maficho ya mtu lakini hakuweza kumwona mzoa taka wala muokota makopo.

Alikwenda kwenye ukuta pembeni kabisa kisha akampigia simu Helana.

”Haloo bosi...”

”Helena...”

”Abee bosi...”

”Hivi mzoa taka hakutoka kweli?”

”Mimi sina kumbukumbu nzuri bosi zaidi ya kumwona akiingia.”

”Kutoka hukumwona..?”

”Ukiwa jikoni si rahisi bosi kumwona.”

”Oke sawa, ndani hayupo. Oke kwaheri, lakini asante kwa ushirikiano wako.”

”Sawa bosi wangu.”

Baba Joy alirejea sebuleni akatoa kiti na kukaa nje ya nyumba eneo ambao hakuna mtu anayeweza kuingia ndani kwake kupitia getini nila yeye kumwona kwa macho...

”Chai taayri,” mkewe mama Joy alimwambia…

“Niletee hapahapa.”

Chai ilipelekwa pale nje, mama Joy moyoni alikuwa akichekelea kwani alijiona ni mshindi. Baada ya kumwekea chai mumewe aliingia ndani akaenda jikoni…

“Helena…”

“Abee bosi…”

“Mzoa taka alitoka?”

“Nilimtoa mama, si unasema mi mnafiki, lakini hebu ona wema niliyokutendea…”

“Ulimtoaje?”

“Mpaka getini…”

“Mlinzi hakumuona?”

“Ndiye aliyemfungulia mlango…”

“Akasemaje?”

“Alitaka kumkatalia asitoke ili baba amuone…”

“Sasa, ikawaje?”

“Nilimwambia afanye hivyo halafu mimi niseme hata yeye alipolala na wewe usiku wa juzi…”

“Una uhakika..?”

“Niliwaona mama…”

“Kelele…”

“Basi bosi…”

“Sasa sikia, hakikisha baba Joy hapati taarifa potofu kuhusu mimi na mzoa taka, akikuuliza simamia uongo, mwambie kwamba alikuja akazoa taka na kuondoka zake…”

“Lakini bosi…”

“Lakini nini sasa..?”

“Kuna kitu kimoja hujakijua…”

“Kama..?”

“Fuko la mzoa taka…”

“Limefanyaje?”

“Huna habari..?”

“Ningekuuliza Helena..?”

“Liko mlangoni nje pale…”

“Mh! Kweli..?”

“Hata sasa lipo…”

“Baba Joy ameliona..?”

“Amekaa nalo jirani, si amekaa nje..?”

”Ndiyo... lakini bado uongo utashika nafasi yake, utasema alichukua fuko jingine zuri alipewa na mama.”

”Si mzee atakasirika kutoa fuko jipya zuri kumpa mzoa taka asiyempenda..?”

”Afadhali uovu huo kuliko wa kitandani...”

”Sawa bosi.”



***

Mzoa taka alifika kijiweni akiwa anahema kwa kasi ya ajabu...

”Msela vipi?” msela mwenzake alimuuliza…

“Ni noma, nusu nidakwe…”

“Na nani?”

“Mwenye mji, ye kazuka tu bila mawasiliano na mkewe…”

“We ulikuwa wapi?”

“Si kwenye kitanda…”

“Cha nani..?”

“Cha mama mwenye nyumba, nikazama nikaibuka, nilipofika getini eti ulinzi shirikishi naye anataka kuniwekea wingu, ningemtoa roho ujue, mi sioni noma kulala jela, maisha yenyewe nimeshachoka nayo.”



***

Baba Joy baada ya kumaliza kunywa chai, alimuita mlinzi wake, Fuko…

“Hebu vuta kiti ukae hapa nataka kusema na wewe…”

“Sawa bosi.”

Baada ya mlinzi kukaa, baba Joy alimwangalia kwa macho makubwa kisha akachukia…

“Huu mfuko mchafu ni wa nani..?”

”Mzoa taka bosi...”

”Yuko wapi..?”

”Sijajua bosi...”

”Una maana gani..?”



”Nina maana sijajua aliko kwa sasa...”

“Mimi nahisi kazi imekushinda…”

“Hapana bosi, haijanishinda…”

“Sasa kwanini usijue nani kaingia nani katoka wakati we upo getini...?”

“Nisamehe bosi…”

“Sasa sikia, ili uendelee kuwa kazini nijibu swali langu moja tu…”

“Sawa bosi…”

“Mzoa taka alipoingia alipitia wapi?”

“Pale getini bosi…”

“Alitoka..?”

“Sijamuona bosi…”

”Sasa nakupa kazi, mimi nitaangalia geti, wewe nenda ndani, zunguka kote hakikisha unampata mzoa taka kisha mlete hapa kwangu, sawa?”

”Sawa bosi.”

Mlinzi Fuko alikwenda ndani, alianza kwa kufikia jikoni ambako alimkuta Helena...

”Leo balaa,” alianza kwa kusema...

”Balaa kivipi?”

”Sai bosi...”

”Bosi gani..?”

”Mwanaume...”

”Kafanyaje?”

”Mh! Eti kaniambia niingie huku ndani, nimtafute mzoa taka kila sehemi hadi nimpate kisha nimpeleke kwake...”

”Ah! Hilo tu...”

”Unasema hilo tu sasa nitampataje?”

”We zuga huku wee, kisha nenda kamwambie hujamuona, unahisi ulipokuwa ndani yeye katumia mwanya huo kutoka getini...”

”Mh! Unajua yeye yuko wapi?”

”Si sebuleni..?”

”Nani kasema, amekaa getini. Kasema anashika nafasi yangu ili mtu asiingie wala kutoka.”

Mara, mama Joy alitokea jikoni...

”Fuko unafanyaje hapa..?”

”Bosi kuna tatizo kubwa...”

”Ni tatizo gani linakufanya uache lindo na kuja kukaa hapa, geti unamwachia nani?”

”Getini yuko bosi...”

”Yuko bosi! Una maanisha baba Joy..?”

”Ndiyo bosi...”

”Kwanini..?”

”Aliniita, akaniuliza kama nilimwona mzoa taka akiingia, nikamjibu ndiyo, akaniuliza nilimwona akitoka? Nikamjibu sijamwona, ndiyo akasema nimtafute humu ndani hadi nimpate, yeye amekaa getini kuchukua nafasi yangu.”

Mama Joy alivuta pumzi, akawa mambo mengi. Aliwaza kuwa, mlinzi wake alikuwa sahihi au si sahihi kumjibu mumewe kwamba, mzoa taka aliingia...

”Lakini si alishajua aliingia, sasa labda kwenye kutoka, angemjibuje, alimuona akitoka au hajamuona...?”

”Oke, wewe rudi, mwambie Helena amekwambia mlinzi alitoka...”

”Hapana bosi, hata mimi nilimwambia sijamwona akitoka...”

”Alikuuliza saa ngapi?”

”Muda si mrefu bosi...”

”Alikuja jikoni..?”

”Ndiyo bosi.”

”Mh! Baba Joy naye kwa kubana...”

”Ni kweli bosi, amekubana sana, huna ujanja,” alisema mlinzi huku akicheka hali iliyomkera sana mama Joy...

”Kwako ni furaha na amani au?” mama Joy alimuuliza Fuko...

”Hapana bosi, unajua mzee amechezwa na machale na inabidi utengeneze sana ili asiendelee kukuchunguza, ni hatari kwako...”

”Umeyatoa wapi maneno hayo..?”

”Ni mawazo yangu tu bosi...teh! Teh! Teh!”

Mama Joy alitoka kwa kasi na kwenda chumbani kwake. Kule nyuma, Helena na Fuko walijiuliza...

”Sasa bosi anapoondoka na hasira anategemea nini? Yeye ndiyo alitakiwa kushauri nini kifanyike ili kuondoa hii hali,” alisema Fuko...

”Sasa ndiyo imetokea wewe tafuta njia...”

”Sina njia, labda nisaidie wazo.”

Helena alitulia kwa muda kisha akasema...

”Sikia, mfuate bosi getini, mwambie umekagua kila mahali hujamwona mzoa taka. Lakini una wasiwasi na chumbani kwake maana ni huko tu ndiko hujafika...”

”Mh! Je, kama na yeye akienda na kukagua kila mahali huko chumbani, hata chini ya kitanda, kabatini, chooni, bafuni kote asipomwona mzoa taka si atajua amepita getini..?”

”Mwambie kuna wakati mama alikutuma dawa ya meno, labda alitumia muda huo wa kukutuma kumtoa mzoa taka...”

”Eee, sawasawa, hapo nakubaliana na wewe,” alisema mlinzi na kutoka jikoni. Alirudi getini...

”Yuko wapi mzoa taka, fuko lake chafu bado liko hapa na wewe nimekwambia lazima umlete kwangu,” baba Joy alisema...

”Bosi, nimemsaka kila mahali lakini wapi! Nina wasiwasi na chumbani kwako kwa sababu ndiko mahali pekee sijafika...”

”Chumbani nilimtafuta hadi ndani ya kabati la nguo, hayupo. Bado kesi iko kwako. Lazima alipita hapa getini, je alipitaje?”

”Ee bosi nina wasiwasi na jambo moja...”

”Lipi hilo..?”

”Labda alipita wakati bosi mdogo aliponituma dawa ya meno dukani.”

”Alikutuma dawa ya meno?”

”Ndiyo bosi...”

”Ulitumia dakika ngapi kwenda na kurudi?”

”Kama kumi bosi, maduka ya kule chini karibu na barabara.”

Baba Joy alitingisha kichwa kama kukubaliana na maneno ya Fuko...

”Oke...sawa, ni nimekuelewa vizuri, endelea na kazi,” alisema baba  Joy.

Alisimama mlango mkubwa na kumwita mkewe...

”Mama Joy...”

”Abee.”

Sekunde kadhaa mbele, mama Joy alisimama mbele ya mumewe...

”Abee...”

”Hili fuko la taka hapa chafuchafu vipi?”

Mama Joy hakujibu kitu, alilifuata, akainama kuliokota na kuondoka nalo. Wakati anaondoka, baba Joy alimtupia macho mwanzo mwisho, akabetua vidole na kuzama ndani.



***

Asubuhi iliyofuata, baba Joy aliondoka kwenda ofisini kwake kama kawaida. Alikuwa na ahadi za kibiashara kama tano baada ya kuwa Arusha.

Nyuma, mama Joy alioga, akajipodoa vizuri sana na kutoka hadi getini...

”Fungua geti,” alimwamuru Fuko...

”Sawa bosi,” mlinzi alifungua geti kwa wasiwasi huku akikumbuka alivyomchongea mwanamke huyo kwa mumewe jana yake kwamba anahisi alimtoa mzoa taka jana yake alipomtuma dukanu kununua dawa ya mswaki.

Baada ya geti kuwa wazi, mama Joy alitoka nje na kusimama akiangaza kulia na kushoto...

”Sijui kijana wangu mzoa taka atakuja au ndiyo ameingiwa na woga? Angekuja japo nimwone kwa macho tu...nakapenda katoto kale...kanayajua mambo.”



***

Baada tu ya kufika ofisini, baba Joy alimuuliza sekretari wake mambo mawili matatu kama yalitokea wakati amekwenda Arusha...

”Yule mzungu wa Adams Company alikuja, pia wale Wahindi wa Singapore wamefika jana, watakuja leo. Mambo mengine bosi yapo kwenye infile zako bosi...”

”Oke,” baba Joy alipitiliza hadi mezani kwake, ila anakaa tu akakumbuka kitu...

”Hivi, yule Fuko aliniambia kuhusu kununua dawa ya meno, wakati napiga mswaki asubuhi ile dawa ilikuwa mpya au ya zamani? Mbona kama sikumbuki kitu chochote pale,” alisema moyoni baba Joy.

Alisita kwanza kufanya jambo lolote lile na kuwaza kuhusu hilo la dawa ya meno...

”Noo! Pale hapakuwa na dawa mpya, ingawa sina uhakika na hili, oke, nitalifanyia kazi.



***

Mama Joy alisimama nje akiangaza kulia, kushoto na sehemu nyingine mbalimbali za eneo alilosimama...

”Sijui kama ataweza kuja tena kwangu, maana jana aliponea kwenye tundu la sindano. Na angekutwa na baba Joy hakiyamungu angemtoa sikio na risasi, mi baba Joy namfahamu vizuri sana yule mwanaume, ana hasira kama mkizi,” alisema moyoni mama Joy.

Alihisi mwili ukimnyevunyevua hasa akizingatia kuwa, jana yake akiwa katka hatua za mwisho za ’kutibiwa’ na mzoa taka ndipo mumewe alipoingia. Halafu mbaya zaidi, usiku baba Joy hakumgusa...

”Mh! Akija atagonga geti bwana,” alisema moyoni mama Joy na kuanza kuingia ndani. Lakini kabla hajazama, kwa mbali kulia kwake alimwona mwanaume anakuja, akasita, akarudi ili kumsubiria. Kwa bahati mbaya hakuwa mzoa taka, lakini alikuwa kijana wa palepale mtaani, ni nyumba ya tano tu kutoka nyumbani kwake...

”Hujambo Bonny..?”

”Sijambo, shikamoo mama Joy...”

”Asante, unakwenda wapi..?”

”Kule kwa mzee Mdenga na Madi...”

”Kufanya nini..?”

”Nimeutwa na baba...”

”Halafi siku hizi  Bonny mbona unajazia hivyo, unafanya mazoezi nini..?”

”Eee, nanyanyua vyuma siku hizi mama Joy...”

”Huko kwa Mdenga na Madi unarudi muda gani?”

”Sasa hivi...”

”Basi ukirudi pitia hapa tuongee kitu...”

”Sawa mama Joy.”

Bonny alitembea akiwaza kuhusu kauli ya mwanamke huyo, hasa ya kumwambia akirudi apitie kwake amwambie kitu...

 ”Huko kwa Mdenga na Madi unarudi muda gani?”

”Sasa hivi...”

”Basi ukirudi pitia hapa tuongee kitu.”

 Bonny aliyarejea mazungumzo yale huku akiwa hajui ni ya nini. Yeye alizaliwa mtaani hapo, lakini mpaka kufikia umri alionao hajawahi kuingia kwenye nyumba hiyo. Siku moja tu aliishia getini akiwa anaongea na Joy mwenyewe ambaye kwa wakati huo alikuwa shuleni sekondari ya boding...

”Tutaona nikirudi,” alisema moyoni hivyo na kuendelea na safari yake.



***

”Mama leo mbona safari za nje ni nyingi?” mlinzi alimuuliza mama Joy...

”We mume wangu..?”

”Kwani kukuuliza lazima niwe mumeo..?”

”Sasa kibali unapata wapi..?”

”Siku ile chumbani kwako si ulisema nikuite mke wangu na wewe ukaniita mume wangu, nilijua bado kibali kinafanya kazi...”

”Fuko umechoka kazi siyo..?”

”Hapana bosi...”

”Sasa ujasiri huo unaupata wapi?”

”Bosi nilikuuliza nikiwa na maana, nilijiua labda unatoka kumwangalia mzoa taka...”

”Wewe anakuhusu nini mzoa taka,” mama Joy alimkatisha...

”Nilitaka kukwambia alikuja asubuhi sana leo, nikamwambia mzee bado yumo ndani ajaribu baadaye.”

Mama Joy aliyekuwa akitembea kuelekea ndani, alisimama, akageuza na kuanza kutabasamu...

”Fuko...”

”Ndiyo bosi...”

”Ni kweli..?”

”Kweli bosi...”

”Kwa hiyo atarudi..?”

”Alisema saa tano...”

”Ngo ngo ngooo,” geti liligongwa...

”Ni yeye nini? Hebu mfungulie.”

Mlinzi alikwenda kufungua geti, lakini huyo aliyefunguliwa hakuingia, aliulizia kwa nje kiasi kwamba, mama Joy hakumwona...

”Marhaba hujambo...eee yupo....nimwambie nani?” mlinzi alijibizana na huyo mtu aliyegonga geti. Akamgeukia mama Joy...

”Bosi kuna kijana anaitwa Bonny anakuulizia wewe...”

”Mwingize apite. Karibu sana Bonny...”

”Asante sana mama Joy.”

Mama Joy alinyoosha mkono na kuushika mkono wa Bonny na kuanza kutembea naye kuelekea ndani...

”Hivi mama alirudi ile safari yake ya China..?” aliuliza mama Joy...

”Alirudi lakini amekwenda tena.”

Kule nyuma, mlinzi aliwatumbulia macho na kutingisha kichwa...

”Bosi bwana, sasa huyu kijana naye sijui amemtoa wapi? Na sijui ana shida naye gani?”

Mama Joy na Bonny walifikia sebuleni, Bonny alipokaa, mama Joy alikwenda jikoni kwanza, aliporudi naye akakaa kwenye sofa lilelile alilokaa Bonny...

”Niambie kijana wangu, chuo ulimaliza vile..?”

”Bado mwaka mmoja...”

”Sasa mbona uko hapa?”

”Nimefuata ada...”

”Mh! Ada shilingi ngapi kwani?”

”Iliyobaki ni laki mbili, sasa wakati nakwenda baba si alikuwa Marekani na mama China, baba amerudi jana, nadhani kesho nitaondoka...”

”Oke, sasa na mimi hapo kwenye laki mbili nitakuchangia shilingi laki moja, umesikia..?”

Bonny alifurahi sana si kwa sababu attachangiwa ada kwani baba yake ana uwezo sana, ila alijua kwenye bajeti yake ya shule atakuwa na laki moja ya ziada kwa hiyo akiwa chuo ataweza kwenda klabu na masela wenzake...

”Sawa mama Joy...”

”Nikupe sasa hivi au..?”

”Hata sasa hivi maana nadhani kesho asubuhi ndiyo naondoka, hatutaonana tena.”

Mama Joy alimwangalia kwa macho ya mlegezo huku akijilambalamba ulimi kama mtu anayeonja chumvi kwenye mapishi...

”Njoo uchukue,” alisema mama Joy akisimama, Bonny naye akasimama na kumfuata mwanamke huyo hadi kwenye mlango wa chumbani, akasimama...

”Ingia tu Bonny...”

”Hapana mama Joy, si vizuri niingie chumbani kwa baba...”

”Hamna neno Bonny, ingia tu.”

”Mama panatosha hapa...”

”Noo bwana, ingia, nitakupa laki mbili zote,” mama Joy alichombezea, Bonny akalainika, akazama chumbani. Mama Joy akafunga mlango nyuma ya Bonny huku akivua nguo chapchap...

”Bonny umejazia vizuri sana hakuna haja ya kupoteza muda, tufanye kweli, wala usione aibu haya mambo ya kawaida sana hapa duniani,” alisema mwanamke huyo akiwa ameshavua nguo zote.

Bonny aliweka kiganja cha mkono kwenye uso wake ili kuficha macho yake yasimwone mwanamke huyo ambaye kiuhalisia ni sawasawa na mama yake mzazi, mama Bonny...

”Bonny njoo sasa, tafadhali njoo kitandani, we mwanaume bwana, tena kijana rijali kabisa, ona ulivyo na kifua cha mazoezi, teh..! Teh..! Teh..! Teh..!  Bonny bwana...”

Bonny alijikuta akivutiwa na shilingi laki mbili, badala ya kuyaangalia mapenzi kwa mama Joy alivuta picha ya matanuzi atakapokuwa chuoni, alimsogelea mama Joy...

”Jamani, ona kifua chako kijana, kimejengeka vizuri sana, unafanya mazoezi gani Bonny?”

”Ya kunyanyua vyuma mama Joy...”

“Tu basi..?”

“Tu basi.”

Mama Joy alimvutia kifuani kwake, akamkumbatia wakiwa wamesimama wakitazamana. Ilifika mahali, mama Joy akapenyeza mkono ndani ya kifua cha Bonny na kuanza kukipapasapapasa huku akisema…

“Garden love hizo, daa kijana wewe bwana, girlfriend wako anafaidi sana eee..?”

Bonny alitamani kumwambia ampe sasa hizo laki mbili badala ya kupoteza muda…

“Anafaidi kawaida tu, si sana…”

“Acha bwana, mmh! Ona kazi, angalia ulivyo mpana…”

“Mama Joy…”

“Niambie kijana mtanashati…”

“Hizo laki mbili vipi?”

“Utapata wala usiwe na wasiwasi, hutaki kupumzika kidogo kwanza..?”

“Kupumzikaje..?”

“Kitandani…”

“Haa! Mimi mama Joy nipumzike kwenye kitanda chako..?”

“Kwani kuna nini, si kitanda cha mama mwenye nyumba.”

Mara mlango uligongwa…”

“Nani..?”

“Mimi,” aliitikia mlinzi…

“Unasemaje?” mama Joy alimuuliza baada ya kufungua mlango. Hakuwa na shaka kwamba aliyegonga ni mumewe kwa sababu alijua hawezi kutoka ofisini baada ya kutokuwepo kwa siku mbili…

“Mzoa taka amekuja bosi, nimwambieje?”

“Mwingize ndani, anisubiri kule nyuma kwenye dude la taka.”

Mama Joy alifunga mlango kwa nguvu, akamrudia Bonny…

“Sasa mpenzi wangu wakati wa kukupa zile laki mbili umefika, umesikia..?”

“Nashukuru sana.”

Mama Joy aliliendea kabati lake la nguo na kutoa laki mbili, Bonny akaziona…

“Hizi hapa.”

Lakini kabla ya kumpa alimshika na kumvutia kwake, wakagongana vifua, mama Joy akatumia nafasi hiyo tena kumwomba denda Bonny, kijana kinywa kikafunguka na kukaa wazi, ulimi wa mwanamke huyo ukapita zake na kuanza kutalii huku ukitoa joto la mahaba…

“Mmm…” aliguna mama Joy, akaguna sana, Bonny akajikuta mikono yake ikimshika mama Joy kwenye mabega na kumvutia kwake, wakakumbatiana kwa sana…

“Mmmm…” Bonny aliiga kama mama Joy. Wakiwa wanaendelea na kulana denda, Bonny alifanikiwa kuziona zile laki mbili kwenye mkono wa kulia wa mama Joy, hapo akazidi kusisimka. Alianza kuamini kwamba, kama atamshikilia mwanamke huyo atakuwa msaada wake mkubwa kila akirudi toka chuo.

Miguu yao ilichoka kusimama, wakajikuta wakiangukia kitandani. Bonny hakujali umama, akamvua nguo lakini zake hakutaka kuvua, akamchezesha gwaride la haraka.

Mama Joy alimsifia sana Bonny, akamwambia anapenda aone kifua chake kikiwa kazini kinafananaje, Bonny akashuka kitandani na kuvua nguo zote, wakabaki walivyozaliwa. Gwaride likaendelea.

Mama Joy alipata ushindi wa kwanza na wa pili huku alipokuwa akiusaka wa tatu, akauupata sambamba na kijana huyo.



***

Jikono mlinzi na Helena walikuwa wakimteta bosi wao huyo…

“Kwanini amekuwa hivi siku hizi? Zamani hakuwa hivi…”

“Ooo, we unajuaje, niulize mimi ninaye shinda ndani, we si unawaona wageni wakiingia na kutoka tu,” alisema Helena, akaongeza…

“Tena nadhani we umeanza kubaini hilo baada ya kupewa nafasi ya kula tunda, lakini huyu mwanamke hajatulia hata kidogo, ni mzinzi mkubwa, sijui anajisikiaje? Hana aibu wala haya, ameumbwa vibaya…”

“Mh! Kwa kweli, pengine malezi ya kwao, maana kuna watu wamelelewa vibaya katika maisha na ndiyo wanaokuwa na tabia hii…”

“Kulelewa vibaya kivipi, ina maana wazazi wake walikuwa wakimwambia awe mzinzi..?”

“Hapana, utakuta mzazi hajali bintiye akitoka na kurudi hata saa sita usiku, unadhani anakuwa wapi kama si kwa wanaume..?”

“Ni kweli lakini.”

Mara, walisikia mlango wa chumbani ukifunguliwa, mlinzo akakimbia kurudi kwenye lindo lake…

“Bosi amesema nenda kamsubiri kwenye dude la taka, lakini ujue mzee mwenye nyumba yupo hapa mjini…”

“Yupo ndani..?”

“Nimekwambia yupo mjini, hujui Kiswahili..?”

“Sasa mbona unawake kaka..?”

“Lazima niwake, iko siku moja utanaswa kama mwizi wewe, malaya wa kiume we…”

“Kha! Bosi hayo matusi yanatokea wapi tena?”

“Acha wewe, ondoa kelele zako hapa, ala!”

“Usinikoromee, we nyanda wa geti tu, huna tofauti na mimi, tena afadhali mimi Napata nafasi wa kuja kujirusha na bosi wako…”

“Nani hajajirusha naye?”

“Ina maana hata wewe tayari..?”

“Achilia mbali mimi, hivi saa hizi yuko ndani na kijana naye anajirusha kama wewe na mimi.”

Mara, mama Joy na Bonny alitokea na kuwakuta mlinzi na mzoa take wamesimama getini…

“Nyie vipi hapo..?”

“Hakuna kitu bosi, nilikuwa namwelekeza huyu aende kwenye dude la takataka kama ulivyosema…”

“Mama,” mzoa taka aliita…

“Unasemaje kijana wangu..?”

“Huyo nani..?”

“We unamtakia nini?”

“Mh! Isije kuwa kama mimi..?”

“Kama wewe kivipi..?”

“Mpenzi wako…”

“Ha!” alihamaki Bonny kumsikia mzoa taka akisema maneno yenye dalili kwamba ni mpenzi wa mwanamke huyo…

“Usijali sana Bonny, huyu kijana anakujaga kuzoa takataka humu ndani kwangu…”

“Pii…piii,” honi ya gari ililia getini…

“Nani huyo?” aliuliza mama Joy…

“Bosi, si wote tuko ndani?” alijibu mlinzi huku akikimbilia geti dogo kwanza…

Alifungua na kuchungulia nje, akaliona gari la baba Joy…

“Bosi…bosi mzee kaja…”

“Pipii…piii…”

“Mh! Hebu fungua, hakuna jinsi,” alisema mama Joy. Mzoa taka baada ya kusikia mwenye gari nje ni mume wa yule mwanamke, alitimua mbio kuelekea kwenye dude la taka, akazamisha fuko lake kwenye dude lile  kisha na yeye akapanda na kuzama bila kujali harufu.

Geti lilifunguliwa, baba Joy akaingia na gari mpaka kwenye sehemu anayoegesha, akashuka akiwa amekazia macho Bonny…

“Shikamoo baba Joy…”

“Marhaba Bonny, hujambo bwana…”

“Sijambo…”

“Za siku..?”

“Nzuri…”

“Upom, sijakuona siku nyingi, siku hizi nasikia upo chuo aliniambia mzee wako…”

“Eee, nipo chuo.”

“Sawa, karibu sana.”

“Asante, nilikuja kusalimia sasa naondoka,” alisema Bonny lakini kwa sauti ya kutetemeka kwa wasiwasi…

“Ni vizuri, umekuwa baba sasa, naona hata sauti imeanza kutoka ya kutetemeka.”

Baada ya Bonny kuondoka na geti kufungwa, baba Joy alimkazia macho mkewe…

“Kuna fundi atakuja kuchukua gari hili akatengeneze…Fuko fungua geti nataka kutoka na hilo gari analolitumia mama Joy.”

Geti lilifunguliwa, baba Joy akahamishia vitu vyake, hasa brifkesi kwenye gari jingine aina ya Land Cruiser V8 na kuondoka zake bila kuongeza kitu kwa mkewe wala mlinzi…

“Fuko funga geti,” alisema mama Joy. Aliondoka na kumfuata mzoa taka kule alikokimbilia ambapo hakumuona. Alishindwa kumuita kwa jina kwa sababu alishamsahau jina…

“Huyu atakuwa amekwenda wapi?”

Mzoa taka kule ndani ya dude la taka alisikia dalili za mtu kutembeatembea, aliwaza ni mume wa mwanamke anayefanya naye mapenzi. Na alijua anamsaka yeye, sasa ili kujilinda aliinua kichwa kidogo na kuchungulia…

“Ah!” alijikuta akishangaa hivyo baada ya kumwona mama Joy…

“Siii,” alimwita maana alikuwa amempa mgongo akielekea kona nyingine ya nyumba.

Mama Joy aligeuka na kumwona mzoa taka, akaachia tabasamu laini…

“Wewe umezamaje humo ndani..?”

“Nimezama tu mwenyewe, si unajua tena kujiokoa…”

“Haya toka tuongee sasa, maana pale ulimuulizia yule kijana ni nani, yule kijana anaitwa Bonny, ni kijana wa nyumba ya tatu tu hapo mbele, familia yake na familia yangu ni kama marafiki wakubwa sana, alikuja kunisalimia,” alisema mama Joy baada ya mzoa taka kutoka katika dude la kuzolea taka…

“Mbona mlinzi wako alisema yeye ni kama mimi…”

“Yule mlinzi hana akili nzuri, sisi wenyewe tumemgundua baada ya kuanza kazi, hapa tulipo tunatafuta mlinzi mwingine,” mama Joy aliamua kumsilibia Fuko akiamini hata yeye Fuko maneno yake alilenga kumharibia.

Mama Joy kwa wakati huo hakuwa anahitaji penzi, Bonny alishamgalaza kila mahali, mwili ulikuwa umechoka kama mtu aliyetoka kufanya mazoezi ya viungo…

“Kwa hiyo sasa?” aliuliza mzoa taka…

“We zoa taka zako nenda uje kesho, mimi nataka kulala sasa, mwili wote unauma.”

“Unauma kwa sababu gani..?”

“Mzee wako usiku alinikamua sana…”’

“Siyo yule kijana..?”

“Nimekwambia yule kijana ni mtoto wa jirani, hujaamini tu…”

“Sawa, lakini sasa mimi leo nimekuja nina shida moja…”

“Shida gani..?”

“Nataka kupanga chumba Manzese…”

“Kwa hiyo unataka pesa za pango..?”

“Eee…”

“Tena itakuwa afadhali, kule nikija tunajificha zetu. Ni shilingi ngapi?”

“Elfu sitini…”

“Kwa siku moja?” aliuliza kwa mshangao mama Joy…

“Hapana, kwa miezi sita…”

“He! Ina maana kuna wenye nyumba wanaochukua kodi ya miezi sita..?”

“Manzese wapo wengi, kama huyu ninayekwambia.”

Mama Joy alimtaka mzoa taka asuburi palepale alipo. Aliingia ndani na kutoka na shilingi laki moja na elfu ishirini…

“Hizi ni kwa ajili ya mwaka mmoja…”

“Eh! Atakubali..?”

“Ina maana huwa hawakubali kupokea fedha ya mwaka mzima, ajabu!”

Mzoa taka alizipokea, akaondoka akiahidi kurudi na majibu kesho yake.



***

Usiku wa siku hiyo, mama Joy na mumewe wakiwa kitandani, mazungumzo yao yalikuwa hivi…

“Mama Joy…”

“Abee,” mama Joy licha ya kuitika lakini pia mapigo ya moyo wake yalikwenda kwa kasi, haikuwa kawaida ya mumewe kumwita hivyo usiku wakiwa wamelala.

Hata pale ilipotokea mume anataka haki yake ya tendo la ndoa alimshika mahali na kumwonesha ishara kwamba alitakiwa kugeukia upande wa pili sasa…

“Hivi unavyoamini wewe ni mke wa mtu..?”

“Naamini hivyo, kwani vipi baba Joy…”

“Mimi siamini…”

“Kwa kutumia kigezo gani..?”

“Leo sitakamwabia natumia kigezo gani, ila kesho au keshokutwa nitakwambia na utakijua tu.”

Mama Joy alionesha dalili za kumdharau mume wake, akageukia ukutani na kunyamaza kimya.

Baba Joy alilala akiangalia juu, yaani chali, viganja vya mikono aliviweka kwenye mto na kuegemeza kisogo chake hapo.

Alikuwa akiamini mkewe ana uhusiano na mzoa taka na aliendelea kuamini kwamba, jana yake aliporudi kutoka Arusha kijana huyo alifichwa au alitolewa nje ya nyumba hiyo kwa staili ya kikomandoo…

“Lakini kama ni hivyo, tatizo liko getini, lazima…”

“Dawa hapa ni moja tu, kumwaga ‘mapesa’, nimmwagie pesa mlinzi, nimmwagie pesa Helana, wao ndiyo watakuwa wakinipa hatua kwa hatua kwa sababu lazima wanajua,”  aliwaza moyoni mwake baba Joy, hata alipopitiwa na usingizi hakujua zaidi ya kujikuta ameamka kumekucha lakini akiwa amechoka sana...

“Leo lazima kila kitu kiwe wazi,” alisema akitoka chumbani akiwa na pajama mpaka jikoni ambako alimkuta Helena akifanya usafi…

“Hujambo Helena…”

“Sijambo bosi, umeamkaje?”

“Mimi mzima. Eee, nina shida na wewe, lakini iwe siri ya sisi wawili…”

“Ipi tena hiyo bosi?” aliuliza Helena. Akilini aliwaza kwamba, neno litakalotoka kwenye kinywa cha baba Joy ni…

“Mimi nimetokea kukupenda sana, sasa kwa sababu mama Joy analeta mambo ya kijinga naomba sana uwe mpenzi wangu, lakini tufanye kwa siri.”

Lakini kilichotoka kinywani mwa baba Joy ni hiki…

“Najua mzoa taka bado anaingia…na najua kwamba anapoingia wewe huwa unaona kwa macho yako. Sasa nataka nikupe pesa, lengo langu akiingia tu, unibip kwa simu, sawa?”

“Sawa bosi, lini…?”

“Leo, kesho, keshokutwa, yaani akija tu…”

“Sawa bosi…”

“Unataka shilingi ngapi?” baba Joy alimuuliza Helena huku akiwa amemkazia jicho la kusikiliza…

“Mh! Bosi, mimi nadhani angalia wewe mwenyewe kiasi utakachotaka kunipa sawa tu kwangu.”

“Oke, nikiwa natoka kwenda kazini nitakupa mzigo wako.”

“Sawa bosi.”

Baba Joy aliondoka hadi getini…

“Fuko…”

“Shikamoo bosi…”

“Achana na shikamoo, nataka tuongee…”

“Sawa bosi…”

“Naamini mzoa taka anapoingia wewe huwa unakuwa getini?”

“Ni kweli bosi, lakini…”

“Sitaki kujitetea, subiri nimalize ninachotaka kuongea…”

“Sawa bosi…”

“Nitakupa pesa, ninachotaka ni kwamba, akiingia tu, unanibipu…”

“Tena leo lazima atakuja bosi…”

“Una uhakika..?”

“Ndiyo bosi…”

“Oke, basi mimi nitakapotoka, nitajifanya nakwenda ofisini, lakini sitafika huko, nitakuwa jirani tu…”

“Sawa bosi.”

Baba Joy alirejea ndani, chumbani, akaenda kuoga. Wakati anaoga mama Joy aliamka na kutoka. Alianzia jikoni na baadaye uani. Alikuwa hajui hili wala lile…

“Nimemmisi mzoa taka wangu. Kale kakijana sijui kanatumia mzizi, nakapenda sana kuliko mlinzi. Ila Bonny yeye ana mwili wa mazoezi, amevimbavimba vizuri…teh… teh… teh teh!”

Baba Joy alipomaliza kujiandaa, alitoka mkononi ameshika brifkesi yake. Alianzia jikoni kwa Helena. Alipofika, aliweka brifkesi juu ya kabati na kulifungua, akatoa shilingi laki mbili…

“Kamata hizi Helena, nataka kazi nzuri…”

“Jamani bosi, asante sana, kazi njema,” alisema Helena huku akipokea kwa kuonesha dalili ya kupiga magoti.

Baada ya baba Joy kuondoka, mama Joy alitokea jikoni…

“Nimekusikia ukisema jamani bosi, asante sana, kazi njema, ni kitu gani amekupa?”

Helena alipigwa butwaa, akawaza haraka na kupata jibu kwamba, kama hakukiona alichopewa, hakuna haja ya kumtajia…

“Hajanipa kitu…”

“Sasa ulikuwa unashukuru nini..?”

“Alikuwa ameniaga kwamba anakwenda kazini nibaki salama ndiyo na mimi nikamwambia asante kazi njema.”

Mama Joy alitaka kukubali japo hakutoa sauti, akatoka kwenda mbele ya nyumba. Ile anatokea, akaona mkono wa mumewe ukitoka kama kushikana na mlinzi…

“Khaa! Toka lini baba Joy akasalimiana na mlinzi kwa kushikana mikono?” alijihoji mama Joy, naye akawa anaelekea usawa uleule. Alifika wakati mumewe akiwa ameshatoka na geti limeshafungwa na mlinzi…

“Leo baba Joy amekusalimia kwa kukupa mkono?”

“Ndiyo bosi…”

“Au alikuwa anakupa kitu?”

“Sijakiona bosi…”

“Hujakiona kinini?”

“Hicho kitu ulichosema alinipa.”

Mama Joy akaona kama anaongea na chizi, akarudi zake ndani na kuendelea na shughuli nyingine za kifamilia.

Mlinzi aliingia ndani ya kibanda chake na kuzihesabu zile pesa alizopewa na bosi wake…

“Kumi, ishirini, thelathini, aro…baini, haaamsiniii, sitini, sabini, themanini…” mlinzi alihesabu hadi alipokoma kwenye noti ya mwisho akiwa anatamka laki mbili…

“Duuu, ole wake aje leo mzoa taka, kitamnukia. Hii ndiyo mipango ya mjini bwana, kula na wewe uliwe, ala!” alisema kwa sauti mlinzi licha ya kwamba alikuwa pake yake.

Mara simu ya getini ilipigwa kutokea ndani, akaiwahi kuipokea…

“Haloo…”

“Fuko, akija mzoa taka mlete ndani moja kwa moja…”

“Sawasawa bosi.” Simu ikakata…

“Imekula kwako leo, utakiona cha mtema kuni,” mlinzi alisema moyoni.

Mpaka inatimu saa sita na nusu, mzoa taka alikuwa hajatokea. Na kwa usongo siku hiyo, kila mara mlinzi alikuwa akitoka getini na kuangaza kulia na kushoto.

Saa saba, baba Joy alimpigia simu Helena lakini hakuipokea kwa sababu mama Joy alikuwa beneti…

“We simu yako si inaita, kwa nini hupokei?”

“Ni msumbufu mtu mwenyewe…”

“Ni nani kwani?”

“Ni mtoto wa baba’angu mkubwa.”

Baba Joy alipoona simu ya Helena haipokelewi akampigia mlinzi wake…

“Bosi, mzoa taka hajatokea…”

“Ngo ngo ngooo,” geti liligongwa…

“Hebu subiri, geti linagongwa si ajabu yeye,” alisema mlinzi na kukata simu. Alikwenda kwenye geti dogo na kufungua akachungulia nje…

“Karibu bwana mzoa taka, karibu sana,” siku hiyo mlinzi alimchangamkia sana kuliko siku nyingine yoyote ile…

“Asante sana, nimekuja…”

“Eee, najua umekuja, demu wako alisema ukija nikupeleke mpaka ndani…”

“Demu wangu?”

“Aaa, sasa kwani bosi wangu si demu wako…”

“Acha hizo wewe, ingia twende,” Fuko alisema na kumshika mkono kwenda naye. Alipomfikisha ndani, mlinzi alirudi mbio getini na kuchukua simu yake kumpigia baba Joy…

“Simu unayoipiga kwa sasa haipatikani, tafadhali jaribu tena baadaye,” simu ilijibu hivyo. Alirudia na kurudia lakini majibu yakawa hayohayo.

Mara, Helena alitua getini.

“Fuko…”

“Naam…”

“Una namba nyingine ya bosi…?”

“Sina, unamtafuta..?”

“Sikiliza, aliniambia akija mzoa taka nimpigie simu, yeye hatakuwa mbali na maeneo haya, sasa simpati…”

“Hata mimi hivyohivyo, wewe alikupa na ‘hela’..?”

“Kwani wewe hajakupa hela..?”

“We nijibu kwanza mimi na mimi nitakujibu wewe…”

“Hamna, nijibu kwanza wewe,” alisema Fuko.

Wakati wao wakibishana kama walipewa fedha au la, mama Joy na mzoa taka walikuwa chumbani, walikaa kitandani wakisema wanaongea mambo yao…

“Mpenzi, chumba kimepatikana…”

“Wapi..?”

“Kule maeneo ya nanihi, si mbali sana…”

“Bonge la chumba. Simenti chumba chote, kikubwa kama uwanja wa mpira, halafu bei ya ubwete…”

“Ngoja kwanza, una maana mimi nitaweza kuja na gari nikaegesha mahali..?”

“Mh! mh! Mwenye nyumba anaweza kutengeneza pakingi ana nafasi kubwa…”



***

Baba Joy alikuwa amekaa kwenye mgahawa mmoja mpya. Hauna watu wengi na uko mtaa wa pili kutoka nyumbani kwake. Simu yake iliisha chaji na alikuwa akipigania kuchajiwa na mwenye mgahawa huo…

“Chaja ya pini ndigo ilikuwepo mzee, sijui nani kaichukua? We Benadi…” Benadi ni mhudumu wa mgahawa huo…

“Nani kachukua chaja ya pini ndogo..?”

“Sifahamu bosi, muulize Malinda jana alikuwa analalamika simu yake haina chaji,” alijibu Benadi.

Baba Joy alitoka mbio hadi nyumba ya pili baada ya mgahawa huo. Nyumba ambayo hakuna anayemjua…

“Jamani hodi…”

“Karibu,” binti mmoja, mweupe, mnene kiasi alitoka na kumwangalia kwa tabasamu mzee huyo…

“Karibu sana…”

“Asante…”

“Shikamoo…”

“Marhaba, shida yangu chaja, nipo kwenye mgahawa huo na kuna mtu wa muhimu sana natakiwa kumpigia, simu imeisha chaji.”

Yule binti alinyoosha mkono ili aipokee simu hiyo huku akisema…

“Au ulitaka chaja ukachajie hapo mgahawani..?”

“Ndiyo maana yangu, itakuwa si mbaya sana,” baba Joy alisema huku akionesha dalili za kuchanganyikiwa. Alimini kuwa, endapo ataiacha simu yake pale ndani akipigiwa na Helena au Fuko hatajua.

Yule binti aligeuka kurudi ndani akimaanisha anakwenda kuchukua chaja. Baada ya muda alirejea…

“Hii, si utairudisha mwenyewe..?”

“Usajali binti, nitairudisha mimi mwenyewe, nakushukuru sana binti yangu…”

“Usijali baba.”

Baba Joy alitoka haraka na chaja hiyo hadi kwenye ule mgahawa…

“Ee bwana nimebahatisha chaja, naomba nichomekee kwenye soketi yenu basi.”

Chaja ilipokelewa, ikapelekwa kwenye soketi huku baba Joy akiwa amerudi kwenye kiti alichokaa na kuendelea  kunywa soda yake.



***

Mama Joy na mzoa taka waliongea mengi kuhusu chumba cha kijana huyo, alimuahidi kumnunulia godoro, kitanda, kabati la ngu, meza, redio, tivii na kapeti kubwa chini…

“Lakini nakuonya, usije ukakifanya chumba cha kuingiza malaya wako…”

“Haitawezekana mupenzi, mimi nakupenda wewe, kama hivi unaniwezesha, unanitengenezea maisha…”

“Hapo umesema, mimi sitaki kabisa mwanamuem malayamalaya.”

Mama Joy aliposema hataki wanaume malayamalaya, mzoa taka alitamani kusema…

“Mbona we malaya tu.”

Mama Joy akijua muda unakwenda, alianza kwa kumshikashika mzoa taka sehemu mbalimbali za mwili…

“Sasa kijana ukiwa unajua tutakutana uwage unaoga hata kidogo jamani…”

“Leo dawasa walizuia maji…”

“Uwe unajitahidi kuhifadhi, sawa?”

“Sawa mupenzi…”

“Halafu mi sitaki uwe unaniita mupenzi, we ita mpenzi tu nitakuelewa,” alisema mama Joy huku akiendelea kumshikashika kijana huyo, mwili ulimsisimka, damu zilimtembea kwa kasi, akaanza kuhisi kuzimiazimia kwa raha na yeye akapeleka mkono kwenye ‘nido’ la kulia la mwanamke huyo, mama Joy akaruka kidogo...

“Wao, umejuaje kijana wangu. Hapo uliposhika ndipo penye transifoma,” alisema mama Joy.



***

Helena aliamua kuweka wazi kwa Fuko akiamini hata yeye amekatiwa kitu kidogo chake…

“Mimi alinipa hela, lakini hapa hoja si hela bali ni kumpata bosi ili tumwambie mzoa taka yumo chumbani mwako, tena kitandani,” alisema Helena…

“Ni kweli, ana simu mbili, lakini ile simu moja sijui inatumia namba gani?” alisema mlinzi. Walipiga plani ya kwenda kwa mama Joy ili wakaombe namba lakini wakaona haiwezekani…

“Atakuuliza unataka namba yake hii ya nini? Halafu tena mfano akikupa halafu mumewe akarudi sasa hivi na kumfumania si atajua ni sisi kwa sababu tuliomba namba…”

“Ni kweli, itakuwa ngumu, sasa tufanyeje?”

“Mh! tuendelee kumpigia, itakuwa simu imeisha chaji, akiwasha tu tutampata tutamwambia…”

“Au tumtumie meseji, wewe mtumie na mimi ili akifungua simu na kukutana nazo atajua kumbe tulimtafuta wote.”



***

Kule kwenye mgahawa, mara muuza mgahawa alitokea akiwa ameshika ile chaja aliyokwenda nayo baba Jy pale…

“Bwana vipi, tayari mara hii?” baba Joy aliuliza akiwa na uso wa shauku…

“Mzee hii chaja kumbe ni ya pini kubwa, sijui itakuwaje?”

“Haa!” baba Joy alihamaki, picha ya mzoa taka na mkewe mama Joy ilimwingia hivihivi anaona kwa sababu tu ya kukosa mawasiliano…

“Ile simu ingekuwa nzima ningeitumia, sasa…”



***

Kule chumbani, mama Joy na mzoa taka mchakato ulikolea kupita kawaida. Mapenzi yalikuwa motomoto, kila sehemu ya kitanda ilitoa mlio wa masikitiko kwa kulemewa na uzito wa walio juu.

Mzoa taka alijituma kuliko jana na juzi. Mama Joy alikuwa mtu wa ‘kulalamika’ tu kama yuko na mumewe. Hakujali kwamba baba Joy angeweza kurejea nyumbani hapo ghafla na kuwanasa.

Mlinzi, baada ya kumkosa baba Joy kwenye simu alifanya doria. Alikuwa akienda ndani na kusimama kwenye mlanngo wa mama Joy kisha kurudi getini. Kuna wakati alipokuwa amesimama hapo mlangoni, Helena naye alitokea…

“Bado wapo?”

“Bado, tena bosi anapiga kelele sana, huyu mwanamke anatafuta matatizo,” alisema mlinzi.



***

“Basi jamani nawaombeni nipe simu yenu mi niweke laini yangu mara moja, kuna mtu nataka kuwasiliana naye dakika moja tu,” baba Joy alimwambia yule mwenye mgahawa ambaye naye alitoa laini na kumpatia simu yake.

Baba Joy aliweka laini kwenye simu hiyo na palepale meseji zikaanza kumiminika kwa wingi.

Mapigo ya moyo yalimwenda kwa kasi huku akiwa kama anazisoma meseji hizo kwa hisia kabla ya kuzifungua…

“Bosi hupatikani kwenye simu, umezima. Mzoa taka ndani ya nyumba hapa.” Hiyo ilikuwa meseji kutoka kwa Helena…

“Bosi, mwizi wako keshaingia sasa, kazi kwako ukichelewa utamaliziwa uhondo wote ohooo.” Huyo alikuwa mlinzi.

Baba Joy hakutaka kupoteza muda kwa kusoma meseji nyingine, alimpigia Helena…

“Bosi yumo bado yumo chumbani,” alisema Helena.

Baba Joy alikata simu. Kwa machungu na maumivu ya wivu alijikuta akitaka kuondoka na simu ya watu…

“Sasa mzee wangu mbona unaondoka na simu halafu hii chaja vipi, umeazimia wapi? Soda pia hujalipa mzee wangu.”

“Ooo, sorry. Chaja ya nyumba ya pili hapo, simu yako hii, samahani kwa kutolipa,” alisema baba Joy huku akitoa noti ya shilingi elfu kumi ambayo hakusubiria chenji.

Aliingia ndani ya gari lake na kuondoka kwa kasi kuelekea nyumbani kwake. Barabarani nusura agonge magari mengine. Akili yake ilikuwa haimwambii nini cha kufanya baada ya kufika huko…

“Hivi nikiwakuta laivu niwafanyaje? Niwaue wote, nimuuze yule mshenzi, niwatoa nje na kuwatembeza uchi au? Nitajua hukohuko,” alisema moyoni baba Joy. Hapo alikuwa akikata kona kuingia barabara inayoelekea kwake.

Alipofika getini hakutaka kupiga honi. Aliegesha gari na kushuka akiacha mlango wazi.

Bahati njema kwake alikuta geti liko wazi, akazama ndani na kumwona mlinzi akitokea ndani…

“Bosi wapo chumbani,” mlinzi alimwambia kwa sauti ndogo. Baba Joy alisimama kwanza na kukumbuka bastola ameiacha kwenye gari. Alirudi mbio, akaichukua na kwenda ndani. Alitembea kwa mwendo wa kunyata wakati anaukaribia mlango wa chumbani.

Ulikuwa wakati mgumu sana kwake, mapigo ya moyo yalimwenda kwa kasi zaidi, hakauwa akiamini kama kweli mkewe, tena wa ndoa anaweza kufanya tendo lile.

Baba Joy aliamini akigonga mlango kwa nguvu linaweza kutokea lolote, hivyo aliamua kugonga polepole…

“Ngo ngo ngooo…”

Kule chumbani, mama Joy hakusikia mlango ukigongwa, lakini mzoa taka wake alisikia…

“Mmm…mlango unagongwa mupenzi…”

“Mlango unagongwa! Kweli..?”

“Ngo…ngo…ngo…”

“Nani?” mama Joy aliulizia kwa ndani tena akitumia sauti yenye hasira ya kero.

Baba Joy alishika kitasa na kukichezesha juu na chini mara kadhaa…

“We nani? Helena.”

Jiko halikuwa mbali sana, baba Joy akaenda kumchukua Helena…

“Akiuliza nani, mwambie mimi. Nataka ajue ni wewe kisha aje kufungua akutana na macho yangu,” alisema baba Joy. Kwa kiherehere, mlinzi naye alichomoka kwenye lindo lake na kwenda ndani kujua kulikoni, wakakutana wote watatu pale mlangoni…

“Ngo ngo ngo,” aligonga tena baba Joy…

“Helena…”

“Abee bosi…”

“Unasemaje…?”

“Nina shida bosi…”

“Shida gani, kila kitu si kipo..?”

“Mwambie kuna wageni,” baba Joy alijikaza kiume, alimnong’oneza Helena…

“Kuna wageni mama, ndiyo maana nimekuja kukugongea…”

“Kuna wageniu..?”

“Ndiyo…”

“Wametokea wapi..?”

“Mimi sijui…”

“Wanaume wanawake..?”

“Mchanganyiko.”

Mama Joy aliacha maswali, ilimaanisha anatoka kitandani ili kutoka kwenda sebuleni.

Mara, mlango ulisikika ukifunguliwa kwa ndani…

“Hao ni wageni gani wanaokuja bila…haaa! Mungu wangu eee,” mama Joy hakumalizia kusema baada ya kufungua mlango na kukutana na sura ya mumewe, mlinzi na Helena…

“Rudi chumbani, malaya mkubwa wewe…unawezaje kufanya uchafu huu. Mbuzi we,” alifoka baba Joy huku akimsukuma mama Joy ambaye aliangukia ndani…

“Wewe mbwa wewe,” alisema baba Joy akiwa amemnyooshea bastola mzoa taka…

“Mzee samahani mzeee, usinie mzee wangu. Samahani sana mzee.”

“Wewe unachotakuwa kukifanya ni kusali sala yako ya mwisho na si vinginevyo. Afadhali niwaue na mimi nikafungwe ndiyo itakuwa furaha yangu kubwa, wanyama nyinyi.”

Mzoa taka aliachia haja ndogo pale kitandani. Mama Joy alipoteza fahamu, mlinzi alimkejeli mzoa taka…

“Nilikwambia bwana, acha mali za bosi wangu hukutaka kunisikia, unaona sasa yamekukutana makubwa mchafu kunuka we…” 

“Mzee nisamehe mimi sawa na mtoto wako wa kumzaa,” alisema mzoa taka baada ya kumwona baba Joy kaielekeza bastola uswa wake…

“Mzee wangu nisamehe mimi ni mtoto wako mzee…”

“Wewe ni mtoto wangu nilizaa na mama yako yupi? Na kama ni mwanangu iweje ulale na mama yako..?”

“Ni shetani tu.”

Baba Joy alijizuia sana. Ilibaki kidogo tu amlipue kwa bastola, lakini alipowaza kuhusu mali zake, utajiri wake akasikia uchungu nazo. Alijua akifanya hivyo atakwenda kuishia jela. Akasikia sauti ikisema masikioni mwake…

“Unadhani ukienda jela nani atasimamia maliz zako?”

“Dawa ya hili tukio ni moja tu, fukuza mke, oa mwingine, Mungu atakusaidia.”

Baba Joy alijikuta akiganda na silaha yake huku akimkazia macho mzoa take. Bado akaendelea kusikia sauti ikisema:

“Kijana ana tatizo gani? Unadhani ana ubavu wa kumtongoza mkeo kweli? Lazima mke kaanza yeye. Kwanza ulishamkataza kuwa na mazoea na huyo kijana kwa hiyo ilitakiwa yeye ndiyo awe na heshima.”

Aliingiza bastola kwenye sehemu ya nyuma ya suruali kwa juu upande wa kulia kisha akasema…

“Simama kijana.”

Mzoa taka alisimama huku akitetemeka…

“Lakini bosi huyu dawa yake ilikuwa kumlipua tu,” alisema mzee. Baba Joy alimgeukia mlinzi na kumwambia…

“Nenda kazini kwako.”

“Sawa bosi.”

Lakini kabla mlinzi hajatoka, alimwambia abaki hadi atakapomruhusu. Mlinzi akabaki amesimama. Baba Joy aliamini kumruhusu mlinzi wake kuondoka katika mazingira kama yale si vizuri, alijua mzoa taka anaweza kufanya lolote lile akamzidi nguvu na hata kutumia bastola yake kumwangamiza maana bado kijana ana nguvu nyingi.

“Helena,” aliita…

“Abee bosi…”

“Lete maji kwenye ndoo.”

“Sawa bosi.”

Baada ya dakika mbili Helena aliingiza maji kwenye ndoo ya plastiki huku akiwa anaangazangaza huku na kule.

“Mmwagie maji mama Joy.”

Helena alimwagia maji yote ya kwenye ndoo kisha akaondoka haraka kama mtu ambaye hakupenda kukiona kile chumba kutokana na heshima.

Mara, mama Joy alishtuka. Alikohoa kwa mbali kisha akakaa…

“Kuna nin?” aliuliza lakini hakuna aliyemjibu. Wote, mpaka mzoa taka walikuwa wakimwangalia tu.

“Ah! Mume wangu baba Joy nisamehe sana mwenzio. Nisamehe mume wangu. Mungu ameamua kuniumbua jamani. Nilijiona mimi bado msichana wa kufanya mmambo haya kumbe nilikosea sana. Nisamehe sana baba Joy.”

Baba Joy hakujibu kitu, alibaki kimya akiwaangalia wote kwa zamu. Lakini alishangaa sana kumwona mzoa taka akimwangalia mlinzi kwa macho yaliyojaa hasira…

“Wewe mbona unamwangalia huyu vibaya sana..?”

“Naye ana madhambi yake kama mimi…”

“Kama yapi..?”

“Niliwahi kusikia anatembea na mkeo.”

Baba Joy alimgeukia mlinzi…

“Ni kweli habari hizi?”

Mlinzi badala ya kujitetea alibaki ameshika kifua huku akitetemeka…

“Basi labda angeulizwa mama mwenyewe ni kwanini amekuwa na tabia hiyo..?”

“Tabia gani..?”

“Ya kututongoza wanaume wa chini yake…”

“Kwa hiyo kumbe ni kweli siyo..?”

“Mi haikuwa lengo langu bosi, mama mwenyewe.”

Baba Joy aliishiwa nguvu, miguu ilikataa kusimama, akabaki ameduwaa tu. Baada ya muda akaita…

“Helena.” Sauti ilikuwa nzito sana tena inakwaruzakwaruza…

“Bee bosi.”

Helena alifika, baba Joy akiwa amekunja sura kama siimba akamwangalia Helena…

“Unajua nini kuhusu mama Joy na Fuko..?”

“Ah! Bosi, ninachojua mimi ni hicho ulichosikia wewe…”

“Unajua mimi nimesikia nini..?”

“Si kwamba wamewahi kulala wote usiku kucha au?”

Baba Joy pamoja na uanaume wake, aliangukia upande wenye bastola na kupoteza fahamu.

Alikuja kuzindukia hospitalini akiwa ametundikiwa dripu ya maji. Alipindua kichwa kulia na kushoto na kubaini alizungukwa na mama Joy, Helena na mtoto wa kaka yake aitwaye Metro na mkewe mama Simon. Pia kulikuwa na wanawake watatu ambao yeye hakuwajua kwa sura na wala aliiyewapeleka pale…

“Unajisikiaje kwa sasa?” Metro alimuuliza…

“Mwili umechoka sana.  Ni muda gani umepita tangu nimeletwa hapa?” baba Joy aliuliza…

“Mmmh! Kama masaa mawili,” alijibu Metro…

“Baba pole sana,” alisema mama Simon…

“Asante sana mwanangu.”

Katika salamu hizo, mama Joy hakawahi kusalimia hata kutoa pole. Si kwamba alikuwa amekasirika bali alikuwa anaogopa. Macho ya baba Joy yalipokutana na mama Joy akasema…

“Wewe sitaki kukuona kabisa.”

“Usiseme hivyo baba Joy…”

“Nimesema sitaki kukuona…”

“Mama ungeondoka,” alisema Metro. Ilibidi mama Joy na wale wanawake waondoka na ndipo ilipojulikana kumbe alikwenda naye yeye…

“Nyumbani kukoje Helena..?”

“Nimefunga geti bosi…”

“Fuko yuko wapi..?”

“Ulipoanguka na yeye akakimbia…”

“Mzoa taka..?”

“Yeye pia bosi…”

“We Metro umepataje habari..?”

“Mama mdogo alinipigia simu.”

Baba Joy aliendelea vizuri, lakini alilala mpaka kesho yake mchana ndipo akaruhusiwa kurudi nyumbani kwake. Aliondoka na gari la Metro na mke wa Metro akiwemo Helena.

Ile wanafika getini tu, teski ilisimama, akashuka Joyce ambaye ndiye msababishaji wa jina la mama Joy, baba Joy. Alionekana mnyonge sana, uso ulijaa hasira pia. Alikaribishwa ndani na Metro…

“Za shule mdogo wangu..?”

“Nzuri kama Metro, shikamoo…”

“Marhaba, pole na safari…”

“Nimepoa.”

Baada ya kufika sebuleni, Joy alikumbana na mama yake…

“Karibu sana mwanangu,” alisema mama Joy akinyoosha mikono ili kumkumbatia…

“Noo mama, noo! Sitaki karibu yako wala sitaki unisemeshe…”

“Khaa! Kwa nini sasa..?”

“Unajua kwa nini…?”

“Mi sijui…”

“Mama niache,” alisema Joy na kupitiliza hadi chumbani kwake kwanza, kisha akatoka sebuleni…

“Kaka Metro baba yuko wapi?”

“Chumbani.”

Joy alikwenda chumbani, akasukuma mlango na kuzama ndani huku akianza kulia…

“Pole baba angu…pole baba.”

Baba Joy alipomwona mwanaye akilia na yeye alianza kulia huku akisema amepoa na ujio wake umemfariji sana.

Joy alikaa pembeni ya kitanda na kumuuliza baba yake kama chanzo cha tatizo lake ni mama kama alivyoambiwa na kaka yake, Metro…

“Ni yeye kweli mwanangu…”

“Sasa itakuwaje baba..?”

“Mama yako umefikia mahali pa kutoa uamuzi wangu mimi kama mume. Wewe tulia ila ajiandae kwa lolote lile.”

Mara, mama Joy aliingia chumbani…

“Sasa wewe Joy unapojifanya unakataa kunisalimia mimi mama yako mzazi maana yake nini? Hujui kama naweza kukuachia laana kubwa..?”

“Mama huwezi, hata maandiko yanasema laana pasipo sababu haimpati mtu…mimi sina tatizo la kulaaniwa, ila wewe ndiye baba anaweza kukulaani kwa ulichomfanyia, naamini yeye hajawahi kukufanyia hata siku moja.”

Mama Joy alijikuta akikaa chini kabisa huku akihema kwa kasi…

“Tena mama hii ni aibu kubwa kwako, unadhani mimi nitajifunza nini kutoka kwako? Nashukuru kwa kunilea hadi kufikia umri huu, lakini sijawahi kufikiria kama katika ndoa yangu nitakuja kumsaliti mume wangu…”

“Haya, labda tuseme shetani ana nguvu, lakini mama nguvu za shetani ndiyo hadi unamleta mwanaume ndani ya chumba chako cha ndoa..?”

“Joyce, unajua hutakiwi kuyasema hayo kwa mama yako..?”

“Najua, lakini wewe umesababisha. Ningesemaje kama ungekuwa mwaminifu kwa baba..?”

“Labda nikurekebishe hapo mwanangu Joy, si kuingiza mwanaume, bali ni wanaume?”

“Haya sasa mama…ndiyo unasema nakosea kukusema. We nitakusema tu, niwe navunja maadili au sivunji, hali hii sitakaa na kuifumbia macho hata siku moja.”

Mama Joy alitoka ndani ya chumba kile na kumwacha mumewe na binti yao, Joyce wakiwa wanaendelea na mazungumzo.



***

Siku saba baada ya tukio lile la aibu, Joy akiwa amesharudi shuleni lakini bila maelewano mazuri na mama yake, siku hiyo baba Joy aliporudi nyumbani kutoka kazini alikuwa ametangulizana na mwanadada mmoja wa miaka kama 37, getini walikaribishwa na mlinzi mpya aliyeitwa Kidevu…

“Mama Joy yupo?”

“Yupo bosi wangu,” alisema mlinzi wakati baba Joy akipita na gari.

“Karibu sana Vivian,” baba Joy alimwambia mwanamke huyo.

Waliongozana kuelekea ndani, sebuleni alikaa mama Joy akiangalia…

“Karibuni..karibu mgeni,” alisema mama Joy. Baba Joy hakuitika kukaribishwa huko lakini Vivian aliitika kwa adabu.

Mama Joy hakujua nini kinaendelea kwani tangu aliponaswa katika fumanizi na mzoa taka na baba Joy kupoteza fahamu, hakuwahi kutamkiwa jambo lolote na mumewe.

Macho yake yalikuwa kwa Vivian, kwani alikuwa mwanamke mrembo, mzuri katika kila sifa ya kuitwa mwanamke mzuri. Alikuwa na midomo minene, macho ya mviringo, pua iliyochongeka kiasi na shingo yenye kujitosheleza kwa cheni.

Siku hiyo alivaa gauni la kitenge lakini lilimwonesha alivyo na umbo nambari nane kwa kukatika kiunoni. Miguu yake ilikuwa rahisi kudhani ameongezea na udongo ili kujenga shepu ya duara kama ya chupa ya bia.

Swali kubwa kwa mama Joy ni juu ya mwanamke huyo ambaye wakati anaingia sebuleni visigino vya viatu vyake virefu alivyovaa vilikuwa vikitoa mlio wa kushtua na kumfanya yeyote kuwa makini kumwangalia…

“Vivian karibu kiti,” alisema baba Joy huku akimwonesha kochi kwa mkono. Baada ya Vivian kukaa, baba Joy naye akakaa…

“Mama Joy,” alianza kusema baba Joy…

“Abee mume wangu…”

“Achana na neno mume wangu. Huyu binti umemuona?”

“Ndiyo…”

“Huyu ni sekretari wangu mpya niliyekwambia siku zile kwamba wa mwanzo aliondoka, aliyekuja ni huyu, anaitwa Vivian…”

“Sawa, karibu sana Vivian…”

“Asante sana…”

“Huyu nimekaa naye kwa siku tatu nzima, nambembeleza awe mke wangu mwingine baada ya wewe kukosa uaminifu katika ndoa, mwishowe amekubaliana na mimi…lakini sijawahi kufanya naye mapenzi…”

“Baba Joy…”

“Sitaki useme jambo, nimeamua na ndiyo dawa yako. Sasa, uamuzi ni wako, ukubali kukaa naye au uondoke ukaishi unakokujua wewe. Kwanza kuwepo kwake kutakusaidia sana, maana utaweza kuwaleta wanaume wako bila wasiwasi kama zamani, hilo ndilo nililotaka kulisema mpaka nikaja naye…”

“Baba Joy…”

“Shii, sitaki kusikia. Huyu Vivian anakuwa mke wangu mwingine, kabla ya kuishi nitakwenda kwao kwa ajili ya kujitambulisha na kulipa mahari …Vivian njoo nikuoneshe chumba chako,” alisema baba Joy huku akisimama na kumshika mkono Vivian.

Vivian alisimama, akamfuata baba Joy huku mapigo ya moyo yakimwenda kwa kasi…

“Mh! Mbona mama mwenyewe anaonekana anaujua ushirikina, nitadumu kweli? Mi nitamwomba anipangishie nyumba mahali,” Vivian alisema moyoni lakini baba Joy akawa kama amelijua hilo…

“Sikia Vivian, huyu mwanamke asikutishe, hana lolote. Hana cha uchawi wala nguvu ya kupigana. Wewe utaishi kwa amani tu.”

“Mh! Unanihakikishia hilo?”

“Wala usijali. Mi ndiyo najua kila kitu.”

Wakiwa kwenye chumba ambacho angeishi Vivian, mama Joy aliingia…

“Baba Joy mimi nimekubali kuishi na mke mwenzangu na pia nimeamua kubadilika tabia, kuanzia sasa hutasikia lolote baya…”

“Hata usingekubali, angeishi tu. Mimi ndiyo niliyeamua. Nashukuru kwa kujielewa. Ila nakushauri uende shuleni kwa mwanao Joyce akajue hayo mabadiliko yako.”

MWISHO.

2 comments:

  1. mambo Irene. mimi huwa napenda sana kutemebelea blog yako has napenda hadithi zako katika kipengele cha Chombezo. lakini huwa unachukua muda mrefu sana kuendeleza chombezo hadi kuna wakati unaweza ukasoma sehemu ya 8 kwa mfano, utakapoishia unaweza kuchukua hata mwezi mzima kuleta sehemu ya 9. unakata stimu sana madam usifanye hivyo. tunachoka kusoma mabifu kwenye mablog mengine. tunaamua kujisomea hadith kwako na kwa Adella. Adella naye kama ansoma hii zile fupifupi vipi madam? NAWAPENDA SANA. MDAU WENU lady D.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kuhusu Hadith I hii kusema ule ukweli haina mpangilio mzuri wa kuendana na Maisha kwani Hadith I natakiwa ipangiliwe viema na kwenda sambamba na maisha ya kweli. Hata kama mama Joy anapenda kufanya uzinzi na vijana wadogo au watu wakubwa wa lika Lake na hapa pia ni Mke wa Tajili huwezi kuwa unafanya mapenzi na kuhonga Malaki ya Pesa bila hata mumeo kukuuliza hakiba ya Pesa Nyumba ikoje au kama pesa zimepungua ndani ya nyumba mumeo atakuuliza tu kwa mama Joy ni mama wa nyumba I hafanyikazi ila kazi anavyofanya ni uzinzi na kuhonga vijana. Hata kama wananyumba ya Kifahali mtu huwezi fanya mapenzi nje kwenye Nyasi karibu na sehemu ya kutupa uchafu na khali kwamba mfanyakazi wa ndani ya nyumba Helena anaweza kutoka wakati wowote ule kutupa ukoko na uchafu mwingine akawaona. Hidith I hii hauleti maana kabisa kwa kile muelekeo wake kwani hata kama mama Joy ni mzinzi wa na na gani kwani yeye kaumbwa na na gani mpaka kufika kutotosheka na Sex ya usiku mzima ya Mlizi wa Gate Kufu na Asubuhi alipokuja kijana mtupa taka Fuko na pia kufanya naye mapenzi Asubuhi iliyofuuta? Sikuipenda kabisa Hadith hii kwani haina mpako kabisa.

      Delete

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate