EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, July 24, 2012

Mavuno ya kusema "...ni wafanyakazi wa kawaida tu!" huko Mahospitalini ndiyo haya...

Pamoja na mgomo wa madaktari uliotikisa nchi kutajwa kuwa umemalizika, huduma katika hospitali kubwa nchini zikiwamo Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Mifupa (MOI) bado si za kudhirisha, gazeti la MWANANCHI limebaini.

Kuzorata kwa huduma hizo kunatajwa kuwa ni kutokana na ukimya uliopo kwa sasa baina ya serikali na  wataalamu  hao  ambao mara kadhaa wameomba kurejea katika meza ya majadiliano na serikali hata baada ya kurejea kazini.

Kwa muda mrefu wataalamu hao walikuwa kwenye mgomo wakishinikiza serikali kutekeleza madai yao, lakini mgomo huo umetulizwa kwa serikali kuwatimua madaktari waliokuwa kazini kwa vitendo (Interns) na kusitisha usajili kwa ambao idadi yao imefikia zaidi ya 380.

Miongoni mwa majibu ya serikali  kwa madaktari hao yaliyotolewa baada ya vikao sita vya kamati iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete kushughulikia madai yao ni kuwa wataalamu hao ni wafanyakazi wa kawaida kama watumishi wengine wa umma na hivyo taratibu za madai yao zingeshughulikiwa kwa kufuata taratibu za kawaida.

Mmoja wa maofisa katika Hosptali ya Taifa ya Muhimbili aliyezungumza kwa sharti la jina lake kutotajwa gazetini, alisema majibu hayo yamedhoofisha utendaji kazi wa wataalamu hao ambao kwa sasa wanaondoka kwenye maeneo ya kazi mara tu muda  wakazi unapomalizika.

“Awali wataalamu hao walikuwa wanafanya kazi bila kujali muda wa kuondoka kazini, lakini sasa muda ukiisha hata kama alikuwa hajamaliza kutembelea wagonjwa anaondoka kwenye kituo cha kazi na ukihoji anakuambia naye  ni mfanyakazi wa kawaida kama ilivyo kwa wafanya kazi wa sekta nyingine za watumishi wa umma,” alisema ofisa huyo ambaye siyo daktari kitaaluma.

Baadhi ya madaktari bingwa walipohojiwa na gazeti la MWANANCHI  walibainisha kuzorota  kwa huduma hizo, huku wakitaja sababu kubwa kuwa ni idadi ya watumishi wachache baada ya wenzao kufukuzwa kazi na pia kutokuwa na majibu ya kuridhisha juu ya madai yao.

“Madaktari walio katika mafunzo hufanya kazi kubwa, kutokuwapo kwao kunasababisha pengo katika utendaji kazi wa kila siku,” alisema Mmoja wa madaktari hao na kuongeza: “Pia na sisi tumeambiwa ni sawa na wafanyakazi wengine walio katika sekta za utumishi wa umma, tufanya kazi kama wao na muda unapoisha tutaondoka kwenye vituo vya kazi hata kama kutakuwa na mahitaji mengine ya kitaalamu,” alisema mmoja wa madaktari hao kutoka MNH.

Alipoulizwa juu ya kuzorota kwa huduma hizo Katibu wa Jumuiya ya Madaktari Dkt. Edwin Chitage alitaja sababu mojawapo kuwa  idadi ya madaktari waliofukuzwa na kusitishwa usajili katika hospitali za umma ni kubwa.

Dkt. Chitage alitaja baadhi ya hospitali kubwa alizodai kuathiriwa na tukio hilo la kufukuzwa kazi kwa madaktari kuwa ni MNH, Hospitali ya Rufaa Mbeya, Bugando (Mwanza), KCMC (Moshi) na Hospitali ya Rufaa Dodoma.

Dkt. Chitage alibainisha kuwa huduma katika hospitali zote kubwa zilizokumbwa na mgogoro bado hazijarejea katika hali ya kawaida na hiyo ni kutokana na idadi ndogo ya madaktari waliobaki pamoja na kutokuwa na majibu sahihi juu ya madai yao waliyowasilisha serikalini.

Naye Katibu Mkuu wa (MAT) Dkt. Rodrick Kabangila alisema inasikitisha kuona serikali imekaa kimya licha ya jitahadi zilizofanywa na chama hicho za kutaka kukutana katika meza ya majadiliano.

Wakati serikali ikiwa kimya juu ya mgogoro huo kwa sasa, viongozi wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) na Jumuiya ya Madaktari na Madaktari waliofukuzwa na kusimamishwa jana walikutana  Dar es Salaam kujadili mustakabli wao.

Katibu wa Jumuiya hiyo Dkt. Chitage alilihalikisha gazeti la MWANANCHI juu ya kufanyika kwa  mkutano huo ambapo alisema mapendekezo yatakayotokana na mkutano yatasambazwa  kwenye vyombo vya habari.
Geofrey Nyang’oro,
MWANANCHI.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate