Mashabiki wa Simba,
leo wamemtembezea kichapo mama mmoja aliyekuwa amevalia jezi ya timu ya
taifa ya Tanzania, Taifa Stars yenye nembo ya Shirikisho la Soka la
Tanzania (TFF), kosa kukaa kwenye jukwaa walilokuwa wamekaa wao.
Haikuweza kufahamika mara moja, mashabiki wa Simba wana bifu na TFF au hawapendi timu ya taifa.
Mama huyo alikimbizwa huku akipewa kichapo hadi kutokwa damu, kabla ya kuokolewa na Polisi waliomteremsha jukwaani.
Aliporwa vitu vyake kama pochi na kadhalika. Baadaye akiwa amekwishaokolewa na askari, ndipo msamaria mwema mmoja, albino akamuokotea baadhi ya vitu na kuwakabidhi askari.
Huwezi kulipa jina lingine tukio lile, zaidi ya udhalilishaji wa kijinsia. Alikuwa anatia huruma mama huyo wakati anahangaika kujitoa kwenye kundi la mashabiki wa kiuma wa Simba, iliyofungwa 3-1 na Azam leo katika Robo Fainali ya Kombe la Kagame.

No comments:
Post a Comment