EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, July 23, 2012

Ajali ya MV Skagit: Waziri Zanzibar ajiuzulu

PictureDondoo za taarifa hii:  
Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano wa Zanzibar, Hamad Masoud Hamad (CUF) amejiuzulu wadhifa wake baada ya shinikizo la kumtaka kufanya hivyo kutokana na ajali mbili za meli zilizoua mamia ya watu angali kiongozi wa Wizara inayosimamia usafiri wa majini. 
Meli ya MV Skagit, MV Kalama pacha wa MV Skagit iliyopata ajali na kuua watu, imezuiliwa kufanya safari zozote za abiria kwa kuwa haina kibali cha kuiwezesha kufanya hivyo baada ya kubainika kuwa uwezo wake ni kusafiri umbali wa kilomita 7 tu.
Katibu mkuu wa Wizara ya Nishati amesema hakutakuwa na mgao wa umeme kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kwa kuwa kuna hazina ya maji ya kutosha kuzalisha nishati hiyo hadi mwezi Disemba 2012.

Bofya kifute cha pleya ili kusikiliza taarifa nzima.ya TBC

Taarifa zaidi kuhusu kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri, Hamad 
Taarifa ya Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee ilisema tayari Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohammed Shein amekubali ombi la Waziri Hamad Masoud kujiuzulu.

“Tarehe 20 Julai, 2012 Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Mheshimiwa Hamad Masoud Hamad alimuandikia barua Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein ya kumuomba ajiuzulu kufuatia ajali ya kuzama kwa meli ya MV Skagit iliyotokea Julai 18, 2012,” ilisema taarifa ya Dkt. Mzee.


Kufuatia kujiuzulu kwa waziri huyo, Rais Dkt. Shein amemteua Mwakilishi wa Jimbo la Ziwani (CUF) Rashid Seif Suleiman kuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano, “Kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano, Rais amemteua Rashid Seif Suleiman kuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano,” taarifa ya Ikulu ilisema.


Uteuzi wa Waziri mpya wa Miundombinu na Mawasiliano umeanza Julai 23 mwaka huu.


Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF Taifa, Profesa Ibrahim Harouna Lipumba amesema hatua ya kujiuzulu aliyoichukua Waziri Hamad inaonesha uwajibikaji wa Kisiasa na Kiserikali kwa viongozi wa chama hicho.

Amesema mfano wa kiongozi huyo kujiuzulu unafaa kuigwa na wakuu wa taasisi za ukozi ambazo zimeonekana kuzorota katika shughuli za ukozi wakati meli hiyo ilipozama

Hata hivyo, Prof. Lipumba amesema hatua ya  kujiuzulu Masoud haimaanishi kuwa anahusika moja kwa moja na uzembe wa ajali hiyo, lakini kwa kiongozi wa kisiasa inapotokea hali kama hiyo katika taasisi zilizoko chini yake anapaswa kuwajibika kwa kujiuzulu.

Katika mahojiano na Sauti ya Amerika, Waziri Masoud alisema amechukua uamuzi wa kuwajibika kisiasa kwa sababu ajali ya meli hiyo imetokana na hitilafu au utendaji mbaya katika Wizara yake.

Bwana Masoud alisema ingawa yeye hakuwa mtendaji katika operesheni za meli hiyo au usafiri wa baharini, bado anawajibika kama Waziri katika Wizara inayosimamia shughuli hizo.

Alipoulizwa kama ana habari endapo kuna watendaji wengine ambao watajiuzulu au kuwajibishwa, Masoud alisema hayo yatatokana na ripoti atakayopelekewa waziri na tume iliyoundwa kuchunguza ajali hiyo.
Wakati huo huo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohammed Shein ameunda Tume ya kuchunguza ajali ya kuzama kwa meli ya MV Skagit.

Mwenyekiti wa Tume hiyo ni Jaji Abdulhakim Ameir Issa, wajumbe ni Meja Jenerali S.S. Omar, COMDR. Hassan Mussa Mzee, Kapteni Abdulla Yussuf Jumbe, Kaptein Abdulla Juma Abdulla, Salum Taoufiq, Kaptein Hatibu Katandula, Bi. Mkali Fauster Ngowo, Ali Omar Chengo na Shaaban Ramadhan Abdalla Katibu wa Tume.



No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate