Timu
ya Tanzania ya Olimpiki, imewasili kwenye kijiji cha michezo ya
Olimpiki kilichopo Stratford, London, ikitokea kwenye mji wa Bradford.
Timu hiyo ya Tanzania, iliweka kambi ya mazoezi katika Chuo Kikuu cha
Bradford tangu walipowasili nchini Uingereza wiki mbili zilizopita,
ikiwa tayari kuiwakilisha Taifa katika michezo hiyo ya Olimpiki 2012.
Timu hiyo ilipokelewa na Balozi wa Tanzania, nchini Uingereza,
Mheshimiwa Peter Kallaghe na maofisa wengine wa Ubalozi na kusindikizwa
moja kwa moja kwenye kijiji cha michezo hiyo kilichopo Stratford, ikiwa
tayari kwa maandalizi na ufunguzi rasmi wa michezo hiyo utakaofanyika
siku ya Ijumaa 27/07/2012 hapa London.

Pichani,
Balozi wa Tanzania, Mheshimiwa Peter Kallaghe akiwa pamoja na
Wanamichezo hao watakaoiwakilisha Taifa mwaka huu katika Michezo hiyo ya
Olimpiki nchini Uingereza.

No comments:
Post a Comment