EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, October 21, 2012

BANDARI DAR MABINGWA INTER-PORTS GAMES.


Wachezaji wa timu ya Bandari ya Dar es Salaam wakiwa na vikombe vya ushindi wao mara baada ya kuibuka washindi wa jumla wa michezo ya Bandari inter-ports games iliyofanyika jijini Mwanza hivi karibuni.
-Yang’ara na kuibuka na vikombe vingi
Na Mwaandishi Wetu
Bandari ya Dar es Salaam imeibuka na ushindi wa jumla katika michezo ya inter-ports games ambayo imefanyika jijini Mwanza hivi karibuni na kufungwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mh. Baraka Konisaga.
Wachezaji wa timu ya Makao Makuu wakiwa na vikombe vya ushindi wa michezo ya Bandari inter-ports games iliyofanyika jijini Mwanza hivi karibuni.
Michezo hiyo imefanyika jijini huko kwa muda wa siku tano ambapo zaidi ya wanamichezo 400 wafanyakazi wa Bandari walishiriki michezo mbalimbali kama vile mpira wa miguu, pete, kikapu, riadha, bao na kuvuta kamba.
Akizungumza kabla ya kukabidhi vikombe na zawadi nyingine kwa wanamichezo hao, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana aliwaasa wanabandari kuendelea kushiriki michezo kwa ajili ya kujenga afya zao lakini kubwa zaidi kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwa ufanisi.
“Leo isiwe mwisho wa kushiriki michezo endeleeni kushiriki ili kuoboresha afya zenu lakini pia niwashauri kutekeleza majukumu yenu kwa ufanisi na mkumbuke kwamba mmepewa dhamana kubwa na taifa lenu hivyo ni wajibu wenu kufanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu mkubwa,”amesema Konisaga.
Katika michezo hiyo Bandari ya Dar es Salaam iliibuka na vikombe vingi zaidi ambapo katika soka waliibuka washindi wa kwanza kwa kujinyakulia alama nyingi huku nafasi ya pili ikichukuliwa na MakaoMakuu.
Kwa upande wa mpira wa pete mshindi ni Bandari ya Dar es Salaam na nafasi ya pili ilinyakuliwa na Bandari ya Tanga. Katika mchezo wa kikapu nafasi ya kwanza ilikwenda Makao Makuu wakati Bandari Tanga wakinyakua nafasi ya pili.
Nafasi ya kwanza ya mchezo wa kuvuta kamba wanaume ilikwenda kwa Bandari ya Dar es Salaam na nafasi ya pili ilinyakuliwa na Bandari ya Tanga. Mchezo wa kamba wanawake nafasi ya kwanza ilikwenda kwa Bandari ya Dar es Salaam na Bandari ya Tanga ilishika nafasi ya pili.
Kwa upande wa riadha Bandari ya Dar es Salaam iliibuka tena kidedea huku Bandari ya Tanga ikishika nafasi ya pili. Kwa upande wa wakimbiaji mita mia moja kwa wanawake medali ya dhahabu ilikwenda kwa mkimbiaji kutoka Makao Makuu, medali ya fedhailikwenda kwa mkimbiaji wa Bandari ya Tanga na mshindi wa tatu alikuwa mkibiaji kutoka Bandari ya Dar es Salaam aliyeibuka na medali ya shaba.
Kwa upande wa wakimbiaji wa mita mia moja wanaume medali ya dhahabu ilichukuliwa na mkimbiaji wa Bandari ya Dar es Salaam, fedha mkimbiaji wa Bandari ya Dar es Salaam na shaba ilikwenda kwa mkimbiaji kutoka Bandari za Maziwa (Mwanza, Kigoma na Kyela).
Kwa upande wa mita mia nne wanawake dhabau ilikwenda Bandari ya Dar es Salaam, fedha ilikwenda Bandari ya Dar es Salaam na shaba ilikwenda kwa mkimbiaji wa Makao Makuu. Kwa upande wa mita mia nne wanaume dhahabu ilikwenda Tanga, fedha ilikwenda Makao Makuu na shaba ilinyakuliwa na Bandari ya Dar es Salaam.
Kwa upande wa mchezo mkongwe na wa jadi maarufu kama bao, Bandari ya Dar es Salaam iliibuka tena na ushindi wakati nafasi ya pili ilikwenda kwa Bandari ya Tanga.Kwa upande wa wachezaji bora wa kila mchezo, mlinda mlango mahiri wa timu ya Mtwara, Douglas Bahati aliibuka mshindi.
Kwa upande wa mchezo wa mpira wa pete, Matalena Mhagama ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa aliibuka kidedea na nafasi ya kwanza. Kwa upande wa timu bora ya kuvuta kamba Makao Makuu waliibuka na ushindi huku Bandari ya Mtwara ikiibuka na ushindi wa timu bora ya kuvuta kamba wanaume.
Mchezaji bora wa riadha ni Lucy Kyoma kutoka Bandari ya Dar es Salaam. Bandari zilizoshiriki katika michezo hiyo ni pamoja na Bandari Dar es Salaam, Mtwara, Tanga, Mwanza, Kyela, Kigoma na Makao Makuu yenyewe. Michezo hiyo hufanyika mara moja kila mwaka kwa kuwashirikisha wanabandari na hufanyika mara moja kwa kila kituo.
Mkuuwa Wilaya ya Nyamagana, Mh. Baraka Konisaga akikabidhi kikombe cha ushindi wa kwanza kwa mwakilishi wa washindi wa kwanza wa mpira wa kikapu, Kisanta kutoka Makao Makuu ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania mara baada kukamilika kwa michezo ya inter-ports iliyofanyika jijini Mwanza hivi karibuni.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mh. Baraka Konisaga akikabidhi kikombe cha ushindi kwanza wa michezo ya inter-ports, kapteni wa timu ya mpira wa pete, Judith Ilunda kutoka Bandari ya Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mh. Baraka Konisaga akikabidhi kikombe cha ushindi kwanza wa michezo ya inter-ports, kapteni wa timu ya mpira wa miguu, Vitalis Salila wa Bandari ya Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mh. Baraka Konisaga akizungumza na wanamichezo wakati wa kuhitimisha michezo ya Bandari inter-ports games ambayo ilifanyika hivi karibuni jijini Mwanza katika viwanja vya CCM Kirumba. Kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Madeni Kipande akiwana maafisa wengine wa juu wa TPA.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mh. Baraka Konisaga akikabidhi kikombe cha ushindi kwa mwakilishi wa Bandari ya Dar es Salaam ambao waliibuka na ushindi huo mbele ya bandari nyingine wakati wa michezo ya Bandari inter-ports games ambayo ilifanyika hivi karibuni jijini Mwanza katika viwanja vya CCM Kirumba.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate