Wakuu wa Sudan wanasema watu
kadha wamekufa kwenye shambulio lilofanywa na wapiganaji dhidi ya
wanajeshi wa serikali katika eneo la Darfur, magharibi mwa nchi.

Umoja wa wapiganaji - Sudanese Revolutionary Front - ulisema ulifanya shambulio hilo na kuuwa wanajeshi wa serikali na kuteka magari ya jeshi na silaha.
Baadhi ya makundi ya wapiganaji ya Darfur mwaka jana yalitia saini mkataba wa amani na serikali ya Sudan, lakini makundi mengine yanaendelea kupigana.
No comments:
Post a Comment