LUIS Suares amekuwa mwiba mkali kwa Chelsea baada ya kuisawazishia bao Liverpool katika mchezo mkali wa jana usiku wa Ligi Kuu ya Uingereza na kuikosesha Chelsea pointi 3 muhimu.

Chelsea iliyokuwa nyumbani ilitangulia kwa bao la John Terry dakika ya 20 lililodumu hadi dakika ya 73.
Kwa matokeo hayo Chelsea imesogezwa hadi nafasi ya tatu ikiipisha Manchester City iliyovuna ushini wa bao 2-1 dhidi ya Totenham Spurs huku nafasi ya kwanza ikiendelea kushikiliwa na Manchester United.
Kufuatia bao hilo la Suares, kocha wa Liverpool Brendan Rodgersameendelea kusisitiza kuwa hata kubali kushuhudia mchezaji huyo akiuzwa katika dirisha dogo la usajili.
Aidha katika mchezo huo Chelsea ilimpoteza nahodha wake John Terry aliyeumia dakika 35 baada ya kugongana na Suares na nafasi kuchukuliwa na Cahil.
Mchezo mwingine ulichezwa jumapili hii ni kati ya Newcastle iliyokubali kipigo cha 1-0 nyumbani dhidi ya West Ham

No comments:
Post a Comment