EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, November 14, 2012

Ndesamburo azungumzia afya yake.

Daniel Mjema, Moshi
MBUNGE wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo (Chadema), amethibitisha kuwa anaumwa na anapatiwa matibabu nchini Uingereza.

Hata hivyo, amesema hadi jana alikuwa anaendelea vizuri na anasubiri uamuzi wa daktari wake kumruhusu atoke hospitalini. Ndesamburo alitoa kauli hiyo alipokuwa anazungumza na gazeti hili juzi usiku.

“Ni kweli naumwa, lakini sijazidiwa hata kidogo si hata wewe (mwandishi) si unanisikia ninaongea na wewe vizuri kabisa ningekuwa nimezidiwa tusingeongea hivi,” alisema Ndesamburo.

Mbunge huyo amewatoa hofu wananchi wa Jimbo lake kuwa afya yake ni imara baada ya kupatiwa matibabu na mara madaktari wake watakapomruhusu atarejea nchini.

Hata hivyo, Ndesamburo hakuweka wazi ugonjwa unaomsumbua, lakini akisisitiza kuwa suala la kuumwa kwa binadamu ni la kawaida na kwamba hali yake kwa sasa ni nzuri.

Wakati Ndesamburo akithibitisha kuugua, Katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema jana alilijia juu gazeti hili akihoji sababu za kuandika habari ya kuumwa kwa Ndesamburo.

Hata baada ya mwandishi kumweleza katibu huyo Ndesamburo ni kiongozi wa umma hivyo watu wake wanapaswa kufahamu alipo, bado aliendelea kuhoji kwa nini iliandikwa akisema habari hiyo ilikuwa na agenda ya kisiasa nyuma yake.

Ndesamburo hajaonekana katika jukwaa la siasa kwa karibu mwezi mmoja sasa, hali iliyotafsiriwa ndiyo iliyochochea baadhi ya watu kuvumisha kuwa hali yake ni mbaya.

Mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, hakuhudhuria vikao vya Bunge lililomalizika Ijumaa kutokana na kuwapo kwake nje ya nchi.

Mkurugenzi wa Idara ya Shughuli za Bunge, John Joel aliliambia gazeti hili jana kwamba ofisi ya Bunge ina taarifa kuhusu Ndesamburo kwenda kumwona daktari wake nje ya nchi, kwa ajili ya uangalizi wa kawaida, lakini siyo kwamba alikuwa mgonjwa sana.

“Ofisi ya Bunge ina taarifa kwamba Mheshimiwa Ndesamburo alikwenda nje ya nchi kumwona daktari, maana aliwahi kutibiwa huko na alikuwa ameambiwa kwenda tena huko, kwa hiyo siyo kwamba yuko mahututi ni uangalizi wa kawaida wa afya yake,” alisema Joel.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate