
MWIGIZAJI zao la Maisha Plus, Upendo Mushi ‘Pendo wa Maisha Plus’ amemwagana na mpenzi wake ambaye ni Mtangazaji wa Runinga ya Clouds, Nickson George.


Wawili hao waliodumu penzini kwa miezi kadhaa iliyopita, juzikati wamemwagana huku kila mmoja akimhukumu mwenzake kuwa mkosaji. Alipoulizwa Nickson bila kufafanua sababu alisema Pendo ndiyo chanzo cha yote.Pendo naye alipotafutwa, alifunguka: “Aah! We acha tu, Nick (Nickson) anajiona sana, nimeona bora tusiumizane kichwa achukue ustaarabu wake na mimi nifanye yanayonihusu.”
No comments:
Post a Comment